Duniani Kote nchi ni ya Jeshi . Nchi yenye Jeshi Kubwa ndiyo nchi imara. Tanzania hatuoni umuhimu wa majeshi yetu Kwa sababu Mwalimu alikua msomi Halisi wa siasa na jamii na Dunia aliijua vizuri Kwa alikua ni Msomi aliyeelimika Kwa kiwango kikubwa sana. Nyerere hakuwa mjinga alipokua analitumia Jeshi lake kwenye vita za Ukombozi na kusaidia nchi nyingine. Aliwaweka Wanajeshi Bize na mambo ya nje na kuwasaidia majirani. Na hicho ndicho wanachofanya Marekana ni nchi za NATO. Nchi za Kiraia zinapaswa kulitumia Jeshi Kwa umakini mkubwa. Huwezi ukasikia Rais wa Marekani anawakoromea wanajeshi Kwa lugha za kudhalilisha. Hata Kagame analiheshimu sana Jeshi lake ikiwemo Jeshi la Polisi. Huku Afrika na hata Tanzania ni rahisi kusikia Rais au mwanasiasa analidhalilisha Jeshi au Polisi wakati huo huo anategemea kuiba kura Kwa sababu Majeshi yatamlinda. Yani ni Hopeless kabisa.
Jeshi ni serikali Mbadala ndio maana imepewa jukumu la kulinda Katiba Muda wote. Kuna maana kubwa uliyojificha nyuma ya Jukumu Hilo . Wanasiasa UCHWARA HAWAWEZI KUELEWA MAANA YAKE. IPO SIKU AMBAYO HAIPO MBALI WATAJUA MAANA YAKE. Historia Duniani Kote hua inatabia ya kuwapitisha wanadamu kwenye nyakati zinazofanana endapo hawatajifunza Kwa waliowatangulia katika nyakati zinazofanana.
Afrika maendeleo ya pamoja yatatokea Kwa mapinduzi na sio Kwa kugonga meza. Afrika ikiwa na Marais 5O kama Kagame na Museveni na Museveni Hakika Kwa utajiri uliopo tungekua tunauza mtungi wa Gesi KG 15 Kwa sh. 20000 na mafuta Petroli Sh. 1200/- kwa Ltr.
Kutoliheshimu Jeshi na kulipa heshima yake inatokana na matatizo ya nchi jirani.Hali inayopelekea wanajeshi wetu angalau kupata sehemu wanapoweza kwenda kuweka roho zao rehani ili wapate anagalu fedha za kuboresha maisha yao na hivyo kutulia na kuwaachia wanasiasa wa ndani ya nchi zao wakilamba asali na kuwakejeli wanajeshi wao . Hiyo ipo pia Kwa majeshi ya Polisi Afrika wanaachwa kama Kuku wa Kienyeji waishi Kwa rushwa na kubambikia watu Kesi ili waweze kuendesha maisha yao na kusomesha watoto wao ili watoto wao wasije wakarithi matusi na kejeli Toka Kwa wanasiasa kuwa hawajasoma ,hawana uwezo wa kuchanganua mambo ,hawajui kupeleleza, ni wababaishaji,wasumbufu, hawajui Sheria n.k lakini ndio wanaowatumia kuiba kura na kuchafua Hali ya utulivu kisiasa na wakishaingia madarakani wanawakejeli na kuwaona hawana maana yoyote na hawastahili kulipwa mishahara ya kuwafanya waendeshe maisha yao Kwa misingi ya Haki na uadilifu . Matokeo yake ni kuwa na mifumo isiyoeleweka na yenye mikanganyiko mikubwa. CDF ni International Rank na vyeo vingine vyote vya Kijeshi chini yake. Hawatakiwi kuwa watumwa wa kisiasa . Wanapaswa kuwa huru mbali na siasa. Raia mmoja TU ndiye mwenye kauli juu ya Jeshi ,yaani Rais basi mana ana mamlaka ya kumteua CDF na Kumtengua muda wowote. Wengine wote hawana jambo lolote la kiutendaji juu ya Jeshi na hivyo hawana maelekezo yoyote Kwa Jeshi zaidi ya blabla za sijui ilani sijui Nini wakati Jeshi na ilani ni vitu visivyoendania Kwani Jeshi linapaswa kulinda Mipaka ya nchi na Katiba ya nchi hata kama hakuna Rais Wala Chama. Yaani hata ikatokea Serikali yote wakaangamia Kwa baridi Kali au Upepo mkali wa kisulisuki Ukalizoa Jengo la Bunge la Kameruni Bado Jeshi litalinda mipaka ya nchi na Katiba mpaka Hali itakapokaa sawa. Hivyo nakubaliana na wewe kabisa kuwa Jeshi linahitaji kuheshimiwa na kuepuka jambo lolote linaloweza kuwafanya wanasiasa kujiweka juu ya Taratibu za Kijeshi Kwa namna yoyote ndani ya nchi zetu za Afrika.
Ni bahati TU Afrika Kuna nchi zenye Vita kama Kongo ,Sudani,Somalia ,Msumbuji, Burundi n.k. Hali inayowapa fursa baadhi ya wanajeshi wa nchi nyingine kufadhiliwa na Mabeberu wa nchi za magaharibi Kwa kulipwa fedha ili wakalinde kile wanachokiita amani. Hapo wanaopata fursa hiyo wanajipatia nafasi ya kuboresha maisha yao na kuvumilia manyanayaso ya wanasiasa waliojaa dharau na kejeli Kwa kushiba asali na kujiona wao wanajua kila kitu mpaka Medani za kivita Kwa sababu TU ya kuangalia Move za Kina Rambo wanadhani kuwa kumbe inawezekana mtu mmoja akalinda mipaka ya nchi[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Nakuunga mkono hata kama hawatakuelewa lakini Iko siku watakuelewa. Siku Sudani na Kongo wakipata amani akili zitakaa sawa Kwa wanasiasa wa nchi za Kiafrika ,Watajua kuwa hakuna Serikali bila majeshi,hakuna heshima ya mahakama bila Majeshi ,hakuna heshima ya Bunge bila Majeshi. Hakuna amani bila Majeshi. Hakuna kula Bata na starehe bila Majeshi. Watu wamwagilia mioyo yao Kwa sababu Kuna majeshi yanayolinda usalama wa nchi.