Sipendi kuona mume wangu anakosa hela, huwa nampa hela, je inatokea kwa wanandoa wote?

Sipendi kuona mume wangu anakosa hela, huwa nampa hela, je inatokea kwa wanandoa wote?

Habari wapendwa.Naomba kwa wale wanandoa mnisaidie hapa kama ni kawaida kwa wanandoa ama ni nini? .
Namshukuru Mungu tulipata kuoana na mume wangu ,kweli Maisha ni mazuri tunafurahia ndoa yetu na watoto wetu pia. Namshukuru Mungu pia amenipa mume ambaye sio mlevi wala mpenda starehe yaani inshort hela hachezei anafanyia vitu vya maana sana.kuna wakati tulifungua joint account ilivyofika kiwango tulikuwa tunataka tukakubaliana akazitoa na akafanyia kazi nzuri sana kwa uaminifu.Na pia mara nyingi nikiwa na hela ambazo najua sizitumii kwa muda huo nampa anafanyia biashara zake baadaye nikihitaji anazirudisha.

Kabla na baada pia ya kuolewa niko ndoto nyingi ya mimi kufikia level fulani na nilimshirikisha pia na akalifurahia.
Sasa tatizo linakuja kwamba kweli mpaka leo karibia miaka minne sasa hakuna kitu nimefanya katika kuachieve ndoto zangu,nimepiga kihatua kidogo sana,Hela naweka akiba inafikia kabisa kiasi nataka kutimiza malengo yangu but najikuta tu nimempea mume wangu bila yeye kuniambia nimsaidie.yaani niko hivi sipendi kuona mume wangu hana amani au akiwaza wapi apate hela au akiniambia hasara aliyopata katika business smtms nachukua card yangu ya bank naenda kutoa hela zote nampea kwa kumwambia hii hela siko na kazi nayo na naona niweke huko kwa business yako so zitumie tu kule usirudishe. (But lengo langu ni kutaka tu ajisikie vizuri pamoja na hasara aliyoiopata hela nyingine imekuja)Na ukimpa anapeleka pale kwa uaminifu kabisa.
Hela ya matumizi akinipa kweli namrudishia sijui kwanini but naona tu kwanini nichukue hela wakati mahitaji madogomadogo ya nyumbani naweza toa hela na vile bado hatujaanza kusomesha so mahitaji sio mengi si bora hiyo hela aendelee kuizungusha kwa biashara.basi naona tu hivyo na nakuwa na amani.weekend hii ilikuwa nikachukue frame ya kufanyia kabiashara kangu(hili hata sikumwambia kwamba nimeshapata frame) but juzi akaniambia habari ya kiwanja alichokiona mjini sehemu nzuri sana na kina title na alipokuwa anaongea anaonesha kabisa kwamba we real need that land.Hakuniambia toa hela wala nini but mimi "emoj mwenyewe nikamwambia niko na pesa nikaenda bank ninedraw
Hela zote hadi za mtaji wa biashara yangu ninayofanya online nimempea.nimebakiwa tu na 100k za kuniweka hadi mwisho wa mwezi nianze upya kusave .

Wapendwa jamani hii ni kwangu tu ama ni kwa wanandoa wote???.sifanyi chochote kuachieve my dreams but niko na Amani sana ndani ya moyo wangu kwa sababu my husband is so happy napenda tu kumwona anafuraha sitaki kabisa apate stress kisa hela au kisa mambo yake hayaendi vizuri.namuombea sana na pale naweza kutoa pesa natoa sana na pale pa kumencourage namuencourage sana na kwa mimi hakuna kitu mimi nimejifanyia and am happy.hii itakuwa ni nini??? [emoji23][emoji23][emoji23].

Sent using Jamii Forums mobile app

mungu wangu.utakua malaika
 
leo nimeamka na kucheka tu! sijui why nimecheka! ila umesema mwenyew mumeo anaifanyia biashara kwa uaminifu bas we endelea kumpa tu mamy !... ila kwa mie mhenga.... kuna shida sehem...why kila mara alie lie shida kwako!hajawah kukuambia mke wangu mwezi huu tumeingiza faida kias hiki! au ni mm tu sijakuelewa!

anywys umepata mume mtaftaj pambana muongeze kipato huna haja ya kujitenga nae! pls waweza kuja share nasi hapa mwaka 2020 biashara za mumeo km hutojali! am very positive to you my dear emoji!! ili na sisi tulioshindwa kushare biashara na waume zetu tujue tunakosea wapi!

kuhusu wewe kutoarchive ur dreams wala usihofu unaachieve kupitia mgongo wa mumeo kitu ambacho ni afya sana kwa ndoa zetu !hilolisikutie hofu mamy

............nimecheka sana sana .....
demi
Neybright
Heaven Sent
espy
Nalendwa

mkuje mfundwe huku
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Mie hata sijamuelewa eti, kama hakuna shida yoyote na anafuraha na amani sasa anataka ashauriwe nini?
Sanasana nilichoona anataka tuu kusifiwa na wapenda miteremko, sasa mtu kila siku unafanya kazi ya kumuongezea tuu pesa si ujinga huo,
Unaendelea kuongeza pesa alafu profit haiongezeki wooiiiii huo ni upuuzi wa hali ya juu ila yeye aendelee tuu kumuharibu huyo mumewe maana naona shemeji yetu atazidi kuwa na akili mgando
 
Kila mwanaume mwenye mafanikio kuna mwanamke nyuma yake.ndo kama wewe.mko wachache.kama Una Dada yako au Mdogo wako hajaolewa uje pm tuyajenge haha
 
Kila mwanaume atakuona unachokifanya kipo sawa ila kiukweli kuna kiasi cha kumsaidia mwanaume na sio kwa kiwango kama hicho chako.

Punguza roho nzuri ambapo hatakama utakuwa unampa hakikisha wewe kama wewe una akiba yako ya kutosha na sio ya kusema umpe yote halafu usubiri mwezi ugeuke uanze upya kuna leo na kesho mumy emoj.

Wanaume sio viumbe wa kuwaamini kwa 100%.

[emoji124] [emoji124] [emoji124]

emmyta unateleza kias mamy! msome lovebitelol ushauri wake kwa utulivu!... emoji yupo sahihi kumsaidia mumewe si ni mwili 1?/ hiyo akiba yake si ndio anampa mumewe aizungushie kwenye biashara
yaan hapo yeye hela yake anampa mumewe izunguke so hakuna shida kbs kwa hilo!

mwezi mbn sio mkubwa sana ! anaweza tafuta nyingine ikiwa kubwa anampa mue kuendelea kutengeza faida!kuliko kuweka pesa si bora izungushwe tu!
 
Umesema kweli dada mana utumiaji huo sio kabisa sababu endapo itatokea wanapata shida au tatizo linalohitaji pesa na hakutakuwa na njia ya kulitatua zaidi ya kutafuta majirani waende kukopa kumbe lait angekuwa na akiba yake ingeweza kusaidia tatizo na maisha yakaendelea.
kabisa ila nampa hongera
 
Ni wanaume wachache wanafanikiwa bila support ya wake zao. Ndoa nyingi siku hizi zimejaa ubinafsi, sio mume wala mke, wengi ni wabinafsi na umimi umetujaa, ndio maana hata hii thread watakushangaa sana.

Kitu kimoja, akipata faida anakuonyesha na mnanufaika as a family? Je, katika miradi yake/yenu anakushirikisha 100%? Je, investment zenu na nyumba zina hati ya familia au ni kwa jina lake?

Anyway, siku hizi dawati la jinsia lipo macho, huwezi kudhuliumiwa hata likitokea baya.
 
Vipi mafanikio yana ongezeka? au unatoa tu hela, but hongera sana kumbe bado wapo wanawake wenye upendo
 
Ni wanaume wachache wanafanikiwa bila support ya wake zao. Ndoa nyingi siku hizi zimejaa ubinafsi, sio mume wala mke, wengi ni wabinafsi na umimi umetujaa, ndio maana hata hii thread watakushangaa sana.

Kitu kimoja, akipata faida anakuonyesha na mnanufaika as a family? Je, katika miradi yake/yenu anakushirikisha 100%? Je, investment zenu na nyumba zina hati ya familia au ni kwa jina lake?

Anyway, siku hizi dawati la jinsia lipo macho, huwezi kudhuliumiwa hata likitokea baya.

hahahah sasa na ww mkuu unaleta ufukunyuku! faida hyo haihusu km inapatikana au wanapiga marktime... hyo ya kushirikishwa si ndio amesema anampa hela aendelee kuizungusha mkuu! au mie sijaelewa! sasa hapa masuala ya hati za familia yanakujaje mkuu! hayo ya hati we achana nayo mradi bibie she is happy mengine mbwembwe tu!
 
Hongera kwa kuwa na mwenendo huo, unachokifanya ndicho wanandoa wengi wanapaswa kukifanya. Wengi wangependa kuishi aina hiyo ya maisha. Ndoa ni muungano wa watu wawili, hivyo inapaswa kusaidiana na kuwa pamoja wakati wa shida na raha bila kutiliana mashaka. Sio ndoa zote ziko kama unavyofanya wewe, kila wana ndoa wamejiwekea mfumo wa namna wao watakavyoishi kutokana na mila, imani na malezi yao. Unachofanya wewe kwenye ndoa yako kinaweza kifanikiwe au kisifanikiwe kwenye ndoa ya wengine kwa kuwa sisi binadamu tuko tofauti, kwa kipato, kimila, kiimani na malezi. Hivyo, we', endelea kufanya unachofanya ili mradi ndoa yako ina upendo, amani na furaha. Isikusumbue sana kwamba ndoa za wengine zinafanyaje.

Lakini pamoja na maelezo yako inaonekana kuna mashaka na walakini uliojificha ndani mwako; Kwanini useme kwamba; "Sifanyi chochote ku achieve my dreams but niko na amani sana ndani ya moyo wangu". Kama una amani moyoni mwako, na kama ninyi nyote wawili ni mwili mmoja, suala la 'my dreams' linatoka wapi? Nahisi kuna walakini.

Ushauri
Pamoja na nia njema ya kutaka kumsaidia mwenza wako kwa ajili ya familia yenu, bado endelea kuweka dhamira ya kutimiza ndoto zako, na mshirikishe mwenzio namna gani utakavyoweza kutimiza azma hiyo, hili litakuongezea furaha na amani moyoni mwako. Pia, 'akili za kuambiwa changanya na za kwako', sisi binadamu si wakamilifu, ni vema kuchukua tahadhari na kuamini kwamba mwenza wako kweli 'anatenda haki', kwasababu ukija kugundua hali tofauti itakusumbua sana siku za mbeleni hasa katika kujenga tena imani na upendo kwa wengine.
 
Haya wanawake tunaopigana Ku achieve Dreams wakati tumeolewa tujifunze hapa ili tupunguze kelele za ndani ya nyumba. Bila shaka kwa bibie humo ndani kwao hadi shetani anapaogopa,hongera!!

Sent using Jamii Forums mobile app

msome lovebitelol amemshauri hizo dreams waachie wanaume ukishaolewa ni dream tosha kwa mwanamke! kamsome mamy!
 
Hongera kwa kuwa na mwenendo huo, unachokifanya ndicho wanandoa wengi wanapaswa kukifanya. Wengi wangependa kuishi aina hiyo ya maisha. Ndoa ni muungano wa watu wawili, hivyo inapaswa kusaidiana na kuwa pamoja wakati wa shida na raha bila kutiliana mashaka. Sio ndoa zote ziko kama unavyofanya wewe, kila wana ndoa wamejiwekea mfumo wa namna wao watakavyoishi kutokana na mila, imani na malezi yao. Unachofanya wewe kwenye ndoa yako kinaweza kifanikiwe au kisifanikiwe kwenye ndoa ya wengine kwa kuwa sisi binadamu tuko tofauti, kwa kipato, kimila, kiimani na malezi. Hivyo, we', endelea kufanya unachofanya ili mradi ndoa yako ina upendo, amani na furaha. Isikusumbue sana kwamba ndoa za wengine zinafanyaje.

Lakini pamoja na maelezo yako inaonekana kuna mashaka na walakini uliojificha ndani mwako; Kwanini useme kwamba; "Sifanyi chochote ku achieve my dreams but niko na amani sana ndani ya moyo wangu". Kama una amani moyoni mwako, na kama ninyi nyote wawili ni mwili mmoja, suala la 'my dreams' linatoka wapi? Nahisi kuna walakini.

Ushauri
Pamoja na nia njema ya kutaka kumsaidia mwenza wako kwa ajili ya familia yenu, bado endelea kuweka dhamira ya kutimiza ndoto zako, na mshirikishe mwenzio namna gani utakavyoweza kutimiza azma hiyo, hili litakuongezea furaha na amani moyoni mwako. Pia, 'akili za kuambiwa changanya na za kwako', sisi binadamu si wakamilifu, ni vema kuchukua tahadhari na kuamini kwamba mwenza wako kweli 'anatenda haki', kwasababu ukija kugundua hali tofauti itakusumbua sana siku za mbeleni hasa katika kujenga tena imani na upendo kwa wengine.

hahahahhaa leo mie nacheka tu aisee!lol!unauma na kupuliza!...
 
Back
Top Bottom