Sipendi kuona mume wangu anakosa hela, huwa nampa hela, je inatokea kwa wanandoa wote?


mungu wangu.utakua malaika
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Mie hata sijamuelewa eti, kama hakuna shida yoyote na anafuraha na amani sasa anataka ashauriwe nini?
Sanasana nilichoona anataka tuu kusifiwa na wapenda miteremko, sasa mtu kila siku unafanya kazi ya kumuongezea tuu pesa si ujinga huo,
Unaendelea kuongeza pesa alafu profit haiongezeki wooiiiii huo ni upuuzi wa hali ya juu ila yeye aendelee tuu kumuharibu huyo mumewe maana naona shemeji yetu atazidi kuwa na akili mgando
 
Kila mwanaume mwenye mafanikio kuna mwanamke nyuma yake.ndo kama wewe.mko wachache.kama Una Dada yako au Mdogo wako hajaolewa uje pm tuyajenge haha
 


emmyta unateleza kias mamy! msome lovebitelol ushauri wake kwa utulivu!... emoji yupo sahihi kumsaidia mumewe si ni mwili 1?/ hiyo akiba yake si ndio anampa mumewe aizungushie kwenye biashara
yaan hapo yeye hela yake anampa mumewe izunguke so hakuna shida kbs kwa hilo!

mwezi mbn sio mkubwa sana ! anaweza tafuta nyingine ikiwa kubwa anampa mue kuendelea kutengeza faida!kuliko kuweka pesa si bora izungushwe tu!
 
kabisa ila nampa hongera
 
Ni wanaume wachache wanafanikiwa bila support ya wake zao. Ndoa nyingi siku hizi zimejaa ubinafsi, sio mume wala mke, wengi ni wabinafsi na umimi umetujaa, ndio maana hata hii thread watakushangaa sana.

Kitu kimoja, akipata faida anakuonyesha na mnanufaika as a family? Je, katika miradi yake/yenu anakushirikisha 100%? Je, investment zenu na nyumba zina hati ya familia au ni kwa jina lake?

Anyway, siku hizi dawati la jinsia lipo macho, huwezi kudhuliumiwa hata likitokea baya.
 
Vipi mafanikio yana ongezeka? au unatoa tu hela, but hongera sana kumbe bado wapo wanawake wenye upendo
 



hahahah sasa na ww mkuu unaleta ufukunyuku! faida hyo haihusu km inapatikana au wanapiga marktime... hyo ya kushirikishwa si ndio amesema anampa hela aendelee kuizungusha mkuu! au mie sijaelewa! sasa hapa masuala ya hati za familia yanakujaje mkuu! hayo ya hati we achana nayo mradi bibie she is happy mengine mbwembwe tu!
 
Hongera kwa kuwa na mwenendo huo, unachokifanya ndicho wanandoa wengi wanapaswa kukifanya. Wengi wangependa kuishi aina hiyo ya maisha. Ndoa ni muungano wa watu wawili, hivyo inapaswa kusaidiana na kuwa pamoja wakati wa shida na raha bila kutiliana mashaka. Sio ndoa zote ziko kama unavyofanya wewe, kila wana ndoa wamejiwekea mfumo wa namna wao watakavyoishi kutokana na mila, imani na malezi yao. Unachofanya wewe kwenye ndoa yako kinaweza kifanikiwe au kisifanikiwe kwenye ndoa ya wengine kwa kuwa sisi binadamu tuko tofauti, kwa kipato, kimila, kiimani na malezi. Hivyo, we', endelea kufanya unachofanya ili mradi ndoa yako ina upendo, amani na furaha. Isikusumbue sana kwamba ndoa za wengine zinafanyaje.

Lakini pamoja na maelezo yako inaonekana kuna mashaka na walakini uliojificha ndani mwako; Kwanini useme kwamba; "Sifanyi chochote ku achieve my dreams but niko na amani sana ndani ya moyo wangu". Kama una amani moyoni mwako, na kama ninyi nyote wawili ni mwili mmoja, suala la 'my dreams' linatoka wapi? Nahisi kuna walakini.

Ushauri
Pamoja na nia njema ya kutaka kumsaidia mwenza wako kwa ajili ya familia yenu, bado endelea kuweka dhamira ya kutimiza ndoto zako, na mshirikishe mwenzio namna gani utakavyoweza kutimiza azma hiyo, hili litakuongezea furaha na amani moyoni mwako. Pia, 'akili za kuambiwa changanya na za kwako', sisi binadamu si wakamilifu, ni vema kuchukua tahadhari na kuamini kwamba mwenza wako kweli 'anatenda haki', kwasababu ukija kugundua hali tofauti itakusumbua sana siku za mbeleni hasa katika kujenga tena imani na upendo kwa wengine.
 
Haya wanawake tunaopigana Ku achieve Dreams wakati tumeolewa tujifunze hapa ili tupunguze kelele za ndani ya nyumba. Bila shaka kwa bibie humo ndani kwao hadi shetani anapaogopa,hongera!!

Sent using Jamii Forums mobile app


msome lovebitelol amemshauri hizo dreams waachie wanaume ukishaolewa ni dream tosha kwa mwanamke! kamsome mamy!
 




hahahahhaa leo mie nacheka tu aisee!lol!unauma na kupuliza!...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…