Saint Anne
JF-Expert Member
- Aug 19, 2018
- 76,039
- 230,142
Hahahah,,,, Ila Kweli.mi naamini ktk rangi yangu asilia Bila kujipaka mirangirangi usoni
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Katika picha hizo wako ni yupi(KAMA UMEOLEWA/UMEOA TAFADHALI USISOME)
Kuna story za kutisha nyingi sana kutoka kwa wanaume, kuhusu kuamka asubuhi na kujikuta wakiwa wamelala kitandani pembeni ya viumbe wasio watambua baada ya kutoa MAKE UP usoni usiku.
Wanawake wengine hutumia pesa nyingi kila mwezi kununua make-up, na sababu kuu ya kutumia make-up kuzidi mipaka ni kutokujiamini kwa jinsi walivyo, hasa uzuri wao sehemu za usoni.
Wanawake ni kama bidhaa. Pindi bidhaa zikiwa sokoni, hua kuna na ushindani mkubwa wa biashara nzuri nzuri kuuzika. Na mtu yoyote aliekua mfanyabiashara atakwambia kua ni "lazima bidhaa kila siku kuifanya yenye mvuto sokoni" ili ipate wanunuzi.
Haina tofauti na wanawake kwa make-up. Ni lazima waongeze uzuri katika muonekano wao ili wavutie, hususan muonekano wa sura, kwasababu ya kumvutia mlengwa maana ndio kitu cha mwanzo hutazama (japo wengine huangalia mizigo).
View attachment 867654
Muonekano wa sura mitaani na sehemu za starehe huongopa, tumeshasikia story nyingi za kutisha kutoka kwa wanaume kuhusiana na kuamka asubuhi na kujikuta pembeni ya kitanda kuna mdada amelala asiemtambua. Najua inatisha kama imeshakukuta.
Mfano wa hizo story:
Kuna jamaa dalali wa magari siku moja alikua Club moja hivi, aliwaona wadada wakiwa wamependeza sana. Baada ya usiku wa furaha tele alimuimbisha dada mmoja na wakawa wanapeleka vyombo (tungi, nyagi, bia) pamoja mpaka wakazima. Alipo amka asubuhi, alichokiona pembeni yake kilikua ni cha kutisha. Ilibidi awapigie sim rafiki zake kuwauliza kama aliondoka na mtu sahihi ama laa.
Mwingine alikutana na dada mmoja mrembo maeneo ya beach, akashusha mistari mpaka dada akaingia kilaini, kisha akamuomba waende kuogelea. Walipo zama baharini, na kisha dada kuchomoka, aliona dada kabadilika rangi (rangi imefifia), kope na nyusi hana, mpaka jamaa akashtuka ni kipi kimemsibu yule dada.
Jamaa mwingine alimuona dada mrembo na kuamua kuongea nae, ilikua mwisho wa mwezi, na alikua anataka kujifyatua kidogo ili mwezi uishe viziri kwake, dada alikubali na wakaamua kwenda hotel. Walipofika chumbani dada aliomba taa izimwe na atoe make-up ili alale kwa amani, jamaa aliridhia. Dada aliingia chooni atoe make-up yake, cha ajabu alitumia muda mrefu sana mpaka jamaa akawa na wasiwasi, aliamua kumfuata na kujua kipi kinaendelea kwa ule ukimya. Alichokutana nacho kilimshtua sana, sura alioikuta haikua ile ya yule dada alieongea nae mwanzo, na hata ile shepu iliomvutia haikuwepo. Alijikuta amepiga kelele kubwa, yule dada alishtuka na kuamua kujifungia kule bafuni. Jamaa akasepa bila kuaga!!!
Mfano wa hayo matukio, ni haya
View attachment 867655
View attachment 867656
View attachment 867657
View attachment 867658
View attachment 867659
Sipingi kua make-up ni muhimu. Huwapa kujiamini kisaikolojia, kuonekana mzuri ni kujihisi mzuri. Ila iwe na mipaka jamani, mungu anawaona!!! Mtatutoa roho zetu ipo sikuView attachment 867660
Duh imekua rangi ya nyumba sasa, [emoji15]
Je kwa mafuta ya taa? Maana hua wanatumia kutolea rangi jeuri inayogoma kutoka mahalaSi nzito. Akisema afute kawaida au atumie maji itakua sio kazi ndogoo
Sasa huyo si akitoa hiyo make-up lazima uzimie utazinduka upo kwenye dripWa mwisho mkuu, mwenye sura mbili[emoji18]
Pole sana Mimi huwa sipendi mwanamke wa mkorogo wala minywele ya maiti napenda naturalKweli kabisa, na ndio maana kanifanya kuandika uzi huu mkuu, ilinitesa nikaamua kutoa ya kifuani
Wangejua kunyoa vipara vya wembe wanavyopendeza basi tu, kitu kina meremeta na jua la saa saba kama taa bulb ya LED.Pole sana Mimi huwa sipendi mwanamke wa mkorogo wala minywele ya maiti napenda natural
Hongera sana anneHahahah,,,, Ila Kweli.mi naamini ktk rangi yangu asilia Bila kujipaka mirangirangi usoni
Nitaujaribu huu[emoji41]View attachment 897896
Soulmate unaweza ukachaguliwa kua "BALOZI/AMBASSADOR" wa Nike. Kama diamond platnumz alivyochagulia kua balozi wa Balleirs na Karanga.Nitaujaribu huu
Soulmate si ndio vizuri ...ili tupate pesaSoulmate unaweza ukachaguliwa kua "BALOZI/AMBASSADOR" wa Nike. Kama diamond platnumz alivyochagulia kua balozi wa Balleirs na Karanga.
Kabisa aisee, kila siku itakua mwendo kukwea chupa za chai angani, na kupiga selfie kukera wachawi.[emoji18][emoji23][emoji23]Soulmate si ndio vizuri ...ili tupate pesa
[emoji23][emoji23]Kabisa aisee, kila siku itakua mwendo kukwea chupa za chai angani, na kupiga selfie kukera wachawi.[emoji18]
Mi najua urembo wa zamani haukuwa na manjonjo ya kuedit sura kama siku hizi, wakongwe kama mimi watakataa kama mama zetu waliwakamata baba zetu kwa make-upIla ndio mama zetu hao, walio wakamata baba zetu masikio mpaka tukazaliwa sisi. [emoji18]
Sina pingamizi hapo mkuuMi najua urembo wa zamani haukuwa na manjonjo ya kuedit sura kama siku hizi, wakongwe kama mimi watakataa kama mama zetu waliwakamata baba zetu kwa make-up
We need your commentNo comment
aiseee 😂😂Kidogo kidogo na wanaume wanaoangalia tamthilia ya sultan wanaanza kuwaunga mkono dada zetu,View attachment 898681View attachment 898683