Erythrocyte,
Chini ya Kamanda Mbowe hakuna mikakati ya kupeleka mbele mashambulizi yanayoendana na vita iliyopo na wakati na mahitaji ya makamanda wake badala yake makamanda uchwara wanabaki kulia lia kama Bundi !! Mshaambiwa kuwa siasa za CCM ni siasa za kijeshi chini ya dola CCM . Kwa maana kwamba Nchi hii ina wenye dola ;wanaolindwa na Dola na wengine hawalindwi wala dola haipo kwa ajili yao. Hawa ni kama wavamizi. Hawatambuliki na hawana Uhuru na haki sawa na wale wengine.
Dr. Bashirini Hali zenu ameamua kuliangamiza Taifa kwa sababu ya kulinda Neno CCM . Hajui hata hilo neno au Chama hata kikifa kesho watu ni wale wale na wataibukia kwingine na kuendelea na maisha na siasa tena za kistarabu zaidi. Huwezi kulinda jina la Chama kwa kutumia dhulma na kuumia nafsi na uhai wa wananchi ambao ndio walipa kodi.
Kama Dola CCM linategemea kodi za watanzania wote iweje litumie bunduki kunyamazisha haki na Uhuru wa wengine kwa kulinda watawala ambao kiuhalisia ndio wanaofaidika na kodi zetu kwa kiwango kikubwa na familia zao. Kwa nini wasiwaheshimu watu wote kwa kuwa wote wanatoa kodi zao kujenga nchi?
Dr . Bashirini hali zenu amepotoka kwa kuzungumzia kupotea kwa KANU kule Kenya kama vile ni Janga linaloiangamiza Kenya wakati KANU ndio ilikua adui wa wa Kenya namba Moja ;KANU alikua ni adui aliyeimarisha ukatili ,ubaguzi, ukabila ,udini na kila aina ya uovu lakini baada ya kufa hiyo chapa ya KANU Leo hii Kenya wanakua wamoja na wenye uhuru na haki zaidi. Na jambo jema zaidi Mtoto wa Mwasisi wa KANU yupo madarakani na hana Muda wa kuwaua wakenye ili kurejesha KANU iliyowatesa wakenya waliopigania Uhuru wakijua wanatafuta Uhuru kumbe wanataka kujenga Chama badala ya kujenga nchi.
Dr .Bashirini hali zenu nimempunguzia maksi nyingi sana kuanzaia kwenye imani yake na dini aliyoamua kuiasi na kujiona kuwa yeye ndiye mungu wa Tanzania anayeweza kupanga anachotaka mpaka akamfukuza Membe aliyeipigania amani na usalama wa nchi hii kwa uhai wake wote na nguvu zake zote na akili zake zote.
Kutumia mtutu wa Bunduki Kulinda Chama chenye wanachama ambao ni binadamu kama kilivyo kingine ni kumkosea Mungu Mwenye enzi na Muumbaji wa wote. Na siku Mungu akiingilia kati Mitutu ya bunduki haitaweza kuwashinda wasio na bunduki kwani wapo watu wema hata ndani ya CCM na dola lake ambao kwao haki ni agizo la Mwenyezi Mungu na katiba na sheria za nchi yetu.
Kwenye Biblia kuna mtu anaitwa mpinga Kristo mwenye namba 666 ambaye atasambaza misheni zake dunia nzima huku akipitia kwenye uchumi ,biashara na fedha.
Hakuna kununua wala kuuza kama mtu hatakua na chapa ya namba 666.
Huyu Mpinga Kristo alitumia mbinu ya kuweka mikakati ya kuhakikisha mtu hauzi wala kununua bila kuwa na chapa ya namba yake. Yesu aliwahi kusema wana wa Giza katika ulimwengu wao wanatumia Hekima kubwa kuliko wana wa Nuru.
Watanzania wanataka Demokrasia wasipoipata ,wasipoiona ndani ya nchi yao wataitafuta nje ya nchi.
Sent using
Jamii Forums mobile app