nokwenumuya
JF-Expert Member
- Jun 29, 2019
- 820
- 2,896
Nimepata taarifa toka kwa rafiki yangu zinazo dai kuwa, kuna Watanzania wamepigwa risasi na Polisi wa Kenya mpakani Sirari eneo linaloitwa Kipimo.
Wengine pia wamevunjwa miguu na mikono na wamekimbizwa hospital.
Katika hali ya kushangaza baadhi ya Watanzania waliopigwa risasi wamechukuliwa na askari wa Kenya na kupelekwa eneo la Kehancha huko Kenya katika jitihada za askari wa Kenya kuficha tukio hilo.
CHANZO CHA MGOGORO
Inasemwa kuwa mgogoro ulianza baada ya maafisa wa Kenya kusema kuwa katika mahindi yaliyopimwa asilimia 55 ni mazima na asilimia 45 yana sumu kuvu hivyo wanaenda kuyachoma moto huko Kehancha.
Wafanyabiashara wa Tanzania wakatoa sharti kuwa hayo mahindi basi yachomwe moto huku wakiona jambo ambalo Wakenya walikataa na kuwaambia hawawezi kuwapangia namna ya kuchoma mahindi hayo.
Basi wakaanza kuyapakia kwenye malori kwa nguvu na Watanzania wakagoma ndipo askari wa Kenya wakawafyatulia risasi Watanzania kadhaa na kujeruhi kadhaa na kukimbiza baadhi ya majeruhi.