Mshangazi dot com
JF-Expert Member
- Nov 19, 2011
- 1,345
- 3,503
Umeshawahi kuambiwa au kusikia siri ambayo endapo ingetoka nje au kujulikana na wahusika ingevuruga au kuharibu kabisa maisha yao? Mimi nitashare yangu ambayo inaniweka mimi na ndugu zangu kwenye wakati mgumu.
Iko hivi:
Binamu yangu ana familia ya siri na anasubiria mke wake afe ili aanze kuishi nao kwa uhuru. Binamu yangu hakua na mahusiano mazuri na mkewe, migogoro isiyoisha, wivu uliopitiliza, kukosekana kwa uaminifu na mengine mengi. Baada ya miaka 20 ya ndoa walikubaliana watengane na kuanza process za awali za talaka. Wana watoto wawili ambao wote wako chuo Dodoma na walipanga wakirudi likizo wawakalishe chini na kuwajulisha kwamba wanatalikiana.
Miezi miwili baada ya kutengana mke wake akagundulika na saratani ya matiti (stage 4 breast cancer), akaanza matibabu Ocean Road na binamu ikabidi arudi nyumbani kumuhudumia na kuwapa sapoti watoto wao kuuguza.
Kisichojulikana nyuma ya pazia ni kwamba, baada ya kutengana, alikutana na mwanamke mwingine akampenda, akaanza mahusiano na kumpachika mimba. Japo anashiriki kwenye kuuguza ila baada ya wiki mbili au tatu anaaga anakwenda safari za kikazi huwa anaenda kukaa kwa yule mwanamke ambaye sasa ana mtoto naye.
Hii situation ina mwaka na nusu sasa na ndugu wachache wa karibu tunajua kinachoendelea ila watoto wake, wakwe na familia ya mke wake mgonjwa hawajui. Kila tukienda kumuona mgonjwa tunamuonea huruma maana hali yake inazidi kuzorota.
Binamu yetu ana huzuni iliyochanganyika na hasira kwa namna maisha yake yalivyovurugika na anavyoshindwa kuwa pamoja na mtoto wake mchanga ambaye kwa sasa ndiyo faraja yake. Mara kwa mara anasema kuwa amechoka kupretend na kudanganya na anasubiri mkewe afe ili apate furaha tena 😢
Tunailinda hii siri japo inatuhuzunisha na tunajua hatuwezi kuruhusu ivuje maana itamuumiza sana mgonjwa na kuharibu uhusianio kati ya binamu yetu na watoto wake wakubwa.
Je, wewe umebeba siri ipi nzito?
PS:
Taarifa za mikoa, idadi ya watoto, hospitali na aina ya ugonjwa siyo halisi, zimebalidishwa kulinda siri 🙃