Siri ambayo inanifanya nijihisi mzito na kubaki njia panda

Umeshawahi kuambiwa au kusikia siri ambayo endapo ingetoka nje au kujulikana na wahusika ingevuruga au kuharibu kabisa maisha yao? Mimi nitashare yangu ambayo inaniweka mimi na ndugu zangu kwenye wakati mgumu.

Iko hivi:
Binamu yangu ana familia ya siri na anasubiria mke wake afe ili aanze kuishi nao kwa uhuru. Binamu yangu hakua na mahusiano mazuri na mkewe, migogoro isiyoisha, wivu uliopitiliza, kukosekana kwa uaminifu na mengine mengi. Baada ya miaka 20 ya ndoa walikubaliana watengane na kuanza process za awali za talaka. Wana watoto wawili ambao wote wako chuo Dodoma na walipanga wakirudi likizo wawakalishe chini na kuwajulisha kwamba wanatalikiana.

Miezi miwili baada ya kutengana mke wake akagundulika na saratani ya matiti (stage 4 breast cancer), akaanza matibabu Ocean Road na binamu ikabidi arudi nyumbani kumuhudumia na kuwapa sapoti watoto wao kuuguza.

Kisichojulikana nyuma ya pazia ni kwamba, baada ya kutengana, alikutana na mwanamke mwingine akampenda, akaanza mahusiano na kumpachika mimba. Japo anashiriki kwenye kuuguza ila baada ya wiki mbili au tatu anaaga anakwenda safari za kikazi huwa anaenda kukaa kwa yule mwanamke ambaye sasa ana mtoto naye.

Hii situation ina mwaka na nusu sasa na ndugu wachache wa karibu tunajua kinachoendelea ila watoto wake, wakwe na familia ya mke wake mgonjwa hawajui. Kila tukienda kumuona mgonjwa tunamuonea huruma maana hali yake inazidi kuzorota.

Binamu yetu ana huzuni iliyochanganyika na hasira kwa namna maisha yake yalivyovurugika na anavyoshindwa kuwa pamoja na mtoto wake mchanga ambaye kwa sasa ndiyo faraja yake. Mara kwa mara anasema kuwa amechoka kupretend na kudanganya na anasubiri mkewe afe ili apate furaha tena 😢

Tunailinda hii siri japo inatuhuzunisha na tunajua hatuwezi kuruhusu ivuje maana itamuumiza sana mgonjwa na kuharibu uhusianio kati ya binamu yetu na watoto wake wakubwa.

Je, wewe umebeba siri ipi nzito?

PS:

Taarifa za mikoa, idadi ya watoto, hospitali na aina ya ugonjwa siyo halisi, zimebalidishwa kulinda siri 🙃
Kweli walisema hakuna siri ya wawili!
 
umesema siri mara ushatuambia hio nayo sio siri halaf siri gani mnaijua wanafamilia?? siri unabaki nayo rohoni kuna mambo lazima ufukiwe nayo chini, huna kifua cha mbele wala cha nyuma unaonekana huwezi kutunza siri yan friji lako compressor ni mbovu hatari haligandishi
mimi nadhani mleta mada kaleta chai tu

ila sio mbaya, inafundisha na kusisimua.
{26A4AC63-8316-4C89-AA69-97CF8A2851DB}.png.jpg
 
Nilipokuwa form two nilimkuta madam wetu ambaye alikuwa mkuu wa shule/head mistress anakojoa pembezoni mwa barabara aliponiona akashtuka, huku akiwa na aibu iliyochanganyikana na na tabasamu hafifu akasema "we secretarybird njoo tukojoe" nami sikushtuka nikamwambia tu "shikamoo madam".

Yule madam akawa ananipendelea katika Kila jambo pale shuleni mpaka nikamaliza shule, na siri yake sikuitoa, leo ndiyo mara ya Kwanza kuitoa.

Cc: Poor Brain, Monetary doctor, BRAZA CHOGO, underscore itembe.
kuna binam yangu bush nilimkuta anaoga nje, nilimstiri hakulika akawa ananchekeachekea me nipo buyu, tokea siku hiyo hajawahi kuniangalia usoni au basi ngoja nimtunzie siri...
 
Umeshawahi kuambiwa au kusikia siri ambayo endapo ingetoka nje au kujulikana na wahusika ingevuruga au kuharibu kabisa maisha yao? Mimi nitashare yangu ambayo inaniweka mimi na ndugu zangu kwenye wakati mgumu.

Iko hivi:
Binamu yangu ana familia ya siri na anasubiria mke wake afe ili aanze kuishi nao kwa uhuru. Binamu yangu hakua na mahusiano mazuri na mkewe, migogoro isiyoisha, wivu uliopitiliza, kukosekana kwa uaminifu na mengine mengi. Baada ya miaka 20 ya ndoa walikubaliana watengane na kuanza process za awali za talaka. Wana watoto wawili ambao wote wako chuo Dodoma na walipanga wakirudi likizo wawakalishe chini na kuwajulisha kwamba wanatalikiana.

Miezi miwili baada ya kutengana mke wake akagundulika na saratani ya matiti (stage 4 breast cancer), akaanza matibabu Ocean Road na binamu ikabidi arudi nyumbani kumuhudumia na kuwapa sapoti watoto wao kuuguza.

Kisichojulikana nyuma ya pazia ni kwamba, baada ya kutengana, alikutana na mwanamke mwingine akampenda, akaanza mahusiano na kumpachika mimba. Japo anashiriki kwenye kuuguza ila baada ya wiki mbili au tatu anaaga anakwenda safari za kikazi huwa anaenda kukaa kwa yule mwanamke ambaye sasa ana mtoto naye.

Hii situation ina mwaka na nusu sasa na ndugu wachache wa karibu tunajua kinachoendelea ila watoto wake, wakwe na familia ya mke wake mgonjwa hawajui. Kila tukienda kumuona mgonjwa tunamuonea huruma maana hali yake inazidi kuzorota.

Binamu yetu ana huzuni iliyochanganyika na hasira kwa namna maisha yake yalivyovurugika na anavyoshindwa kuwa pamoja na mtoto wake mchanga ambaye kwa sasa ndiyo faraja yake. Mara kwa mara anasema kuwa amechoka kupretend na kudanganya na anasubiri mkewe afe ili apate furaha tena 😢

Tunailinda hii siri japo inatuhuzunisha na tunajua hatuwezi kuruhusu ivuje maana itamuumiza sana mgonjwa na kuharibu uhusianio kati ya binamu yetu na watoto wake wakubwa.

Je, wewe umebeba siri ipi nzito?

PS:

Taarifa za mikoa, idadi ya watoto, hospitali na aina ya ugonjwa siyo halisi, zimebalidishwa kulinda siri 🙃
Kiafrika na unalivyoeleza.

Hii haipaswi kuwa Siri.

Kwanza walishatengana.

Pili, mtoto anatakiwa awajue ndugu zake.
Mengine tuwaachie wazungu
 
Eti anamsubiri afe???
Akianza kufa yeye je....wanaume selfish sana
 
Mimi inanitesa sana hii siri ya huyu kigogo wa idara nyeti hapa mtaani anachapiwa mkewe na kijana dereva wake mpaka mtoto wa mwisho sio wa huyu mzee ni wa huyo dereva wao mpaka sura kamefanana ila sijui why mzee hajastuka muda wote huu dah!
Siyo kwamba bosi hajui.
Dereva kapewa kazi ya ziada na bosi wake. Ya kumlindia heshima, yeye hawezi Tena kutimiza majukumu ya kuijaza dunia.
 
Back
Top Bottom