Siri iliyofichwa kuhusu BIBLIA

Kwa sasa mimi ni mkiristo jina.nashukuru kwa mafunzo mengi yaliyo jaa utashi.pia kuna wakati nimekua nikihoji sana juu ya utendaji wa mungu lakini pia kuhusu sheria za dini zilizipo dunian kwangu mimi zinazingua.kuna wakat huwa nafiri sana kuhusu mungu na ninadhani wenda mungu baad ya mungu kuumba ulimwengu huu aliondoka zake na kuishi kusiko julikana.

hivyo sheria sijui kanuni zote waliweka wanadamu ndio maana wanakinzana.binafs siamini kama kuna maisha baada ya kifo ukifa habari yako imeisha
 
Kwahiyo tatizo ni ukristo au Mungu?
 
Vitabu vilivoondolewa ndo vingewapa Waafrika uwezo wa kufanya vumbhzi kama Wzungu
Hiki kitu nimekisoma Leo sehem mfano ktk gospel of Thomas na Judah vlikuwa vitabanaisha ni jinsi gani mwanadam anaweza kutumia nguvu ya "psychic power" ili aweze kutatua matatzo yake kitu ambacho watu wanoitawala hii dunia wakaona haitakuwa rahisi kuutawala ulimwengu kama haya mambo yatakuwa wazi
 
Jibu hoja iliyoletwa wacha porojo.
 
We jamaa umeongea ukweli mtupu ambao mi nimekuwa nikiupigania kila mara,kina Mwanamalundi walipaswa wawe kwenye vitabu watumike kama vielelezo,lkn leo ni uhuni tu wa Wazungu na Waarabu
 
Kwahiyo tatizo ni ukristo au Mungu?
Tatizo ukristo na uislam mkuu...dini za hovyo sana hizi
...hata Yesu na Mohammad watakuja zikana siku ya kiama,_kinachofundishwa na kuishiwa nowadays kwenye hizo dini mbili sicho walichofundisha hao mitume kabisa..pathetic
 
Tatizo ukristo na uislam mkuu...dini za hovyo sana hizi
...hata Yesu na Mohammad watakuja zikana siku ya kiama,_kinachofundishwa na kuishiwa nowadays kwenye hizo dini mbili sicho walichofundisha hao mitume kabisa..pathetic
Kwani ni hao mitume walifundisha nini na hayo mafundisho yao yanapatikana wapi?
 
Hao wanaotalawa ulimwengu ni akina nani?
 
Hujajibu hoja hata moja ya.mleta mada hata moja umeiga projo tu mwanzo mwisho.
 
Mm siwezi kuongelea kitu ambacho ni totally religious hata kama nimeona weakness. Respect someone's faith
 
Mm siwezi kuongelea kitu ambacho ni totally religious hata kama nimeona weakness. Respect someone's faith
Hapana mkuu Biblia inasema ukristo ni religion of reasoning yaani sio kila kitu kwa kuwa ni imani tu unakimeza ila lazima uhoji maana mafundisho mengi ya kupotosha soma hapa;

1 Yohana 4:1
1 Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani.

Na hii ni shida kubwa sana wakristo wengi kuna vitu wanapotoshwa ila kwa kuwa wana mentality kama yako basi wao bora liende mwisho wa siku wanapotezwa ona kwa mfano manabii feki walivyojaa wanawauzia sabuni,maji,mafuta eti yakawaponye na wao hawawezi kuhoji maskini wanaingizwa mkenge wakiamini ile ni Roho ya Mungu bila kujua ni ya mpinga kristo!!

Kwa staili hii mpaka Yesu anarudi atakuta walioshika imani hawazidi 10 nyie endeleeni tu kukaririshwa bila kuhoji mtakuja kujuta

Yangu macho!!
 
Mkuu zitto junior,

Nimekusoma vizuri na kimsingi uliyoyaandika yanahitaji UPEMBUZI YAKINIFU wa wataalam wa mambo ya scriptures.
Hata hivyo ni muhimu sana kuhoji ili watu wasienende kama kondoo wapelekwao kuchinjwa bali wakiamini, imani yao iendane na ufahamu sahihi wa kile walichokiamini.

Mimi pia hupenda kuhoji kama hawa watu wa Beroya ambao habari zao zimeandikwa katika kitabu cha Matendo 17
10 Mara hao ndugu wakawapeleka Paulo na Sila usiku hata Beroya. Nao walipofika huko wakaingia katika sinagogi la Wayahudi.


11 Watu hawa walikuwa waungwana kuliko wale wa Thesalonike, kwa kuwa walilipokea lile neno kwa uelekevu wa moyo, wakayachunguza maandiko kila siku, waone kwamba mambo hayo ndivyo yalivyo.


12 Basi watu wengi miongoni mwao wakaamini, na wanawake wa Kiyunani wenye cheo, na wanaume si wachache.

Kwa hiyo KUCHUNGUZA maandiko ni busara.

Ahsante sana.
 
Hata hivyo, ni muhimu kuelewa kuwa Biblia iliandikwa na watu tofauti tofauti zaidi ya 40 kwa vipindi na nyakati tofauti na inasadikika iliandikwa hadi kukamilika kwa miaka karibu 1,600!

Kwa wingi huo wa watu na tofauti kubwa sana ya majira na nyakati za kuandikwa kwake haijuzu yawemo makosa madogo madogo (ya kibinadamu) ambayo hata hivyo hayaondoi ukweli kwamba maandishi ya Biblia yamevuviwa na Roho ya Mungu.

Ndio maana wachambuzi wa mambo ya kiimani husema ili usome Biblia na kuelewa kilichoandikwa hata kikusaidie wewe na watu wanaokusiliza, huna budi kuzaliwa kwa uwezo wa yule Roho ambaye aliwavuvia waandishi ili akusaidie kuelewa hata mahali wao walipokosea.

Ahsante.
 
Aisee mkuu nimekuelewa sana umejibu mada kwa busara na kunielewesha vizuri kabisa bila matusi wala kejeli.... sasa wewe ndio great thinker umefanya analysis ya pande zote mbili

Ubarikiwe mkuu
 
Aisee mkuu nimekuelewa sana umejibu mada kwa busara na kunielewesha vizuri kabisa bila matusi wala kejeli.... sasa wewe ndio great thinker umefanya analysis ya pande zote mbili

Ubarikiwe mkuu
Amekujibu kwa busara ipi? Mbona ameshindwa kueleza huyo roho mtakatifu anapatikana vipi ili uwe naye kisha ukisoma biblia uelewe?

Kama amekiri biblia ina makosa kwa nini isirekebishwe na je inamtegemea roho mtakatifu katika kusahihisha makosa yaliyomo kwenye biblia? Makosa ni makosa tu hata aje roho mtakatifu bado hatayafuta makosa hayo.

Kwa taarifa tu ni kwamba roho mtakatifu huwa ni kisingizio cha kufunika uongo wa biblia.......
Asante.
 
Mkuu Malyenge,
Hoja kwamba Roho mtakatifu anapatikana vipi si muhimu hapa na kwa wakati huu na vile vile Biblia iko very clear on how to receive the Holy Spirit.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…