Siri iliyofichwa kuhusu BIBLIA

Siri iliyofichwa kuhusu BIBLIA

Sawa Mkuu nimeelewa hoja zako!!.

MAJIBU YA MASWALI YAKO NI KAMA IFUATAVYO:

WAANDISHI WOTE WAWILI WAKO SAHIHI KWA ASILIMIA MIA KABISA,UNACHOPASWA KUFAHAMU NI KUWA MWANDISHI WA MATENDO AMEONGEZA HABARI NYINGINE/MPYA.

"HAELEZI HABARI YA KIFO CHA YAKOBO NA MAHALI PA MAZIKO YAKE PEKEE,BALI ANAELEZA PIA KUHUSU VIFO VYA PATRIARCHS(WAZEE) NA MAHALI WALIPOZIKWA"

1:UTOFAUTI WA MAENEO.(MAKPELA NA SHEKEM)

Katika kitabu cha Mwanzo 50: 13 Biblia inaeleza,

"Kwa kuwa wanawe wakamchukua mpaka NCHI YA KANAANI,nao WAKAMZIKA katika PANGO ya shamba la MAKPELA,iliyo mbele ya Mamre,aliyoinunua Ibrahim pamoja na shamba kwa Efron MHITI,pawe milki ya kuzikia"

FAFANUZI: Katika aya hiyo hapo juu sehemu/eneo ambalo Nabii Musa analotaja kuwa mahali alipozikwa YAKOBO ni NCHI YA KANAANI,anaongezea habari kuwa alizikwa katika PANGO la shamba ya MAKPELA

FAHAMU : MAKPELA(Kiebrania: Me'arat ha - makhpela - The cave of double)
Sio jina la mji/kijiji au jiji kama BETHEL,YAFA,KAPERNAUM,GAZA ni jina la PANGO - Lilikokuwa katika shamba ambalo Ibrahim alilinunua pamoja na shamba ili afanye kuwa mahali pa kuzikia Watu wake - JINA LA MAHALI HAPO NI KIRIATH - ARBA/HEBRON.
Rejea,Mwanzo 23: 1 - 9
....."9" ili kwamba anipe PANGO YA MAKPELA iliyo katikati ya shamba lake ...."

-Kisha anamalizia kutaja jina la MTU aliyemuuzia Ibrahim SHAMBA pamoja na PANGO lililo ndani yake kuwa ni Efroni,kutoka Katika kabila yake ni MHITI.

TUKIREJEA:Katika kitabu cha MATENDO : 7:15 - 16,Biblia inaeleza,

"Basi YAKOBO akashuka mpaka Misri;AKAFA YEYE (NA) BABA ZETU;wakachukuliwa mpaka SHEKEM,wakazikwa katika kaburi lile,ambalo Ibrahim alilinunua kwa kima cha fedha kwa wana wa hamori huko SHEKEM"

FAFANUZI:Mkuu Mwandishi wa MATENDO anaelezea habari mbili kwa wakati mmoja( TWO NEWS IN ONE/A SINGLE CONTENT),habari hizo ni;

"Basi YAKOBO akashuka mpaka Misri;AKAFA YEYE........"

1 :KIFO CHA YAKOBO NA MAHALI ALIPOZIKWA - KIRIATH - ARBA/HEBRON/MAKPELA(.Mwandishi anasema;"Katika kaburi lile,ambalo Ibrahim....")

"......NA BABA ZETU..."

2:KIFO CHA BABA ZAKE NA MAHALI WALIPOZIKWA - SHEKEMU
(HAPA SHEKEMU WAMEZIKWA NABII YUSUPH NA WANAWE,NA BAADHI YA WANA WA NABII YAKOBO.HADI LEO PANAITWA;

*QEVER YOSEF(Hebrew)/QABL YUSUF(Arabic). - "Kaburi la Yusuph"

HIVI LEO NI SEHEMU ILIYO KATIKATI YA MLIMA GEZARIMU NA EBEL,UMBALI WA MITA 300 KASKAZINI MWA SHEKEMU/SYKAR.

NOTE/KUMBUKA: KIRIATH - ARBA/ILIPO MAKPELA NA SHEKEMU ZIKO KATIKA WILAYA MOJA - INAYOITWA SAMARIA.

PILI: UMBALI KUTOKA MIJI HII MIWILI SIO KAMA ULIYOELEZA KUWA NI SAWA NA KUTOKA *KIBAHA - GEITA* AMBAPO NI KILOMETRES 850.

BALI NI MILE 50/KM 75 SAWA NA KUTOKA BUNDA - MUSOMA/AU DAR - BAGAMOYO/MVOMERO
((AMBAO NI UMBALI WA KAWAIDA KABISA,IKIWA MIJI IMO NDANI YA WILAYA TU)

MWISHO:Mwandishi wa MATENDO HATAJI KABILA anaposema HAMORI bali anataja JINA LA UBINI/SONS OF HAMORI.

..."16" Ambalo Ibrahim alilinunua kwa kima cha fedha kwa WANA WA HAMORI...."


MLINGANISHO.

-Waandishi wote wanataja YAKOBO alikufa.
-Wote wanakubaliana kuwa alifia MISRI
-Wote wanakubaliana kuwa alizikwa katika kaburi la Ibrahim katika PANGO/MAKPELA
-Mmoja anataja kabila la waliomuuzia Ibrahim shamba kuwa ni MHITI,mwingine anataja jina la ubini(sons of).
-Wote wanakubaliana kuwa watu wa ukoo wa Ibrahim walizikwa mahali/eneo/wilaya/mkoa mmoja kama Ibrahim aliyotaka.
- Mmoja analezea habari za baba zake wengine WALIOZIKWA SHEKEMU(Sio YAKOBO),mwingine hawaelezei.

REJEA;MWANZO 12:6

"ABRAM akapita katikati ya nchi mpaka mahali PATAKATIFU PA SHEKEMU,mpaka mwaloni wa More.Na WAKANAANI siku zile walikaa katika NCHI HIYO.

Natanguliza shukrani Mkuu.
Well narrated
 
Sasa ndugu wewe unataka kilichoandikwa na Mathayo kifanane na Yohana. Umeshaambiwa hii ni injili ya Mathayo na hii ni ya Yohana kwa hiyo ni watu 2 tofauti.

Ebu tuwekee Kitabu cha Daniel kinavyokizana na Kitabu cha Ufunuo kama utapata mstali wakati hivi ndo vitabu vigumu sana
 
Sasa ndugu wewe unataka kilichoandikwa na Mathayo kifanane na Yohana. Umeshaambiwa hii ni injili ya Mathayo na hii ni ya Yohana kwa hiyo ni watu 2 tofauti.

Ebu tuwekee Kitabu cha Daniel kinavyokizana na Kitabu cha Ufunuo kama utapata mstali wakati hivi ndo vitabu vigumu sana
Na ndio maana nikaleta hii thread humu JF sababu kama ww unaona Yohana kukinzana na mathayo sio dili kisa waandishi kutofautiana mbona Book of Enoch au jasher kukinzana na Genesis hiyo hoja ya kwamba waandishi ni tofauti hivyo vitabu lazima vikinzane haikutolewa??

Alafu kingine ni kwamba vitabu vingi vya new testament vilinakili maandiko ya agano jipya na sometimes hata kuinterprete mambo kivyao ilimradi tu kuonesha unabii ulitimia hivyo kukinzana ni kidogo sana ila ukilinganisha old testament kwa old testament au new testament vs new testament kuna mistari zaidi ya 200 inakinzana

Sasa cha kujiuliza kama kuna baadhi ya taarifa zinakinzana mbona vimeachwa kwenye bible alafu sababu hyo ya kukinzana inatumika kwa book of Enoch??

Hapa ndio mzizi wa hoja
 
Bible ndo constitution pamoja na mpungufu yake ukiifuata naamini utaingia kwenye ufalme wa milele
Yes ni kweli unachosema ila sasa swali linabaki kwanini vitabu vingine viliachwa kwa sababu vinakinzana alafu vitabu vingine vinavyokinzana vikabakizwa kwa bible??

Hapa ndio mzizi
 
Napenda kuchukua Fursa hii kuwakaribisha katika chama la watu huru chini ya Utumwa wa mzungu kupitia dini ningependa mfanye tafiti juu ya dini za mababu zetu. Tupate kuamia huko kwa kuwa zilitenda miujiza ya ajabu waliweza kuita mvua ikaja. Tofauti na kina Gwajima wanazidiwa na Jembe na Mshana Jr wa kigoma kwa kuleta radi, vimbunga na Mvua
Safi ....nilikuwa nawaza hivi pia
 
Mimi binafsi Naamini kuwa Biblia ni kitabu kitakatifu kwa sababu yaliyoandikwa kwenye bible tunayishi na tunayaona na yanatongoza kwenye maisha yetuu.
Kabla dini haijaingia Africa mababu zetu walikuwa wanaongozwa na Nini na kukiishi ?

Hatuhitaji biblia Wala Quran kutuongoza kuishi ...
Mtoto anapozaliwa na mama kumuwekea nyonyo anyonye kile kitendo Cha kufyonza maziwa Yale hafundishwi na yeyote
It's all about nature
 
Vitabu vya bibilia havipo kwa ajili ya kila mtu, kila kitabu kipo kwa ajili ya jamii fulani ya watu na kizazi fulani. Waumini wa leo huosoma mambo waliyoambiwa wayahudi kuendana na tamaduni zao na lugha zao na kuzileta kwenye tamaduni zao kwa lugha tofauti na walengwa. Lugha ni utamaduni, tafsiri ni ubatili kwa baadhi ya maneno. Ivyo baadhi ya vitabu tuvisome tu kama riwaya. Vile vyenye ujumbe kwa watu wote (vichache) ndo vituongoze hasa mafundisho ya paulo maana yeye alisafiri mabara yote akifundisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nilikuwa nasubiri mtu agusie hapa kidogo .....Asante kwa kuliona hili mkuu ....
Na kila mtu arudi kwenye asili na tamaduni za mababu zake tu ...
 
Swali jingine tujiulize kwanini vimeondolewa kama biblia ni kitabu tu cha story au sio kitakatifu km wasemavyo wengine?biblia ina siri gani ambayo walitoa hawataki tujue....
 
ukitakata uielewe biblia nilazima uwe na nguvu za roho mtakatifu lkn ukisoma kama gazet la mwananchi Au nipashe n.k, hutaelewa na ukitaka ujibiwe hiyo miswali yako kawaulize wapo watu wana Phd za theology watakujb vzr...Kwanza una hoji nini imani za watu? Pambana na hali yko ndugu.......
Ndio mnapokimbiliaga hapa

Story ya adamu na Eva Kuna manabii wanasema Lile tunda lilikuwa Ni tendo la ngono na wanaendelea kusisitiza Hadi Leo mungu hapendi Hilo tendo maana ni kujitia unajis hata ukifanya na mume ama mkeo (na Kuna namna ya kujitakasa ili uwe msafi according to Bible )

Kuna manabii wengine wanakuambia Lile tunda lilikuwa Ni tunda la kawaida la mtini halihusiani na tendo la ngono
Swali: story ya adamu na Eva Ni ngumu kueleweka kias hicho kujua maana Yake hata Kama unasoma Kama gazeti ? Kama mungu alikuwa Ana mpango wa kutuficha kuwa Hilo tunda lilikuwa Ni Nini why alituficha na ambao alipanga kuwafunulia Ni watu wenye sifa zipi na aliwapa maana ipi hasa anayotaka tuijue ? Kuwa tunda ni tendo la ngono ama Ni tunda Kama tunda la mtini ?
 
Mwanga na giza vilisha umbws maana vimetajwa kabla ya mianga kwa maana jua mwanga mkubwa kwa ajili ya mchana, na mwezi na nyota mianga midogo kwa ajili ya usiku.
Mwanga ulikuja Baada ya kuumbwa jua ,mwezi na nyota ....kabla ya hapo ilikuwepo nuru (according to biblia)
Swali: walijuaje siku imeisha na ku count kuwa Ni siku ya kwanza ama ya pili kwa uwepo wa nuru na Giza pekee kabla jua halijaumbwa ?

Maana tunajua baada ya jua kuwepo ilikuwa rahisi kutambua mchana na usiku ili kuhesabu siku
 
Unaamini ya wana historia waliozaliwa mwaka 1970 wanataka kukupa historia ya biblia iliokusanywa karne ya 3.

Mbinu za shetani kuuvuruga ulimwengu. Wasomi wangekuwa na akili wangeshaipanga hii dunia kuwa mahala bora pa kuishi, ila neno la Mungu leifanya jamii kuwa bora ya kistaarabu. Spati picha bila biblia kama dunia ingekuwa salama
 
Back
Top Bottom