Tofauti ni kwamba mwanzo 50 na matendo saba zinakinzana wapi Yakobo alizikwa maana shechem na macpelah ni kama Kibaha na Geita alafu kabila liliowauzia hayo makaburi yanakinzana mmoja anasema ni kabila la Wahiti mwingine kabila la Hamron ambao yote ni makabila tofauti kabisa kama wasukuma na wachagga ndio maana nikasema kama walikinzana Je kivp wawe wameongozwa na roho takatifu alafu wakinzane ndio hoja yangu imejikita hapo.....
Sawa Mkuu nimeelewa hoja zako!!.
MAJIBU YA MASWALI YAKO NI KAMA IFUATAVYO:
WAANDISHI WOTE WAWILI WAKO SAHIHI KWA ASILIMIA MIA KABISA,UNACHOPASWA KUFAHAMU NI KUWA MWANDISHI WA MATENDO AMEONGEZA HABARI NYINGINE/MPYA.
"HAELEZI HABARI YA KIFO CHA YAKOBO NA MAHALI PA MAZIKO YAKE PEKEE,BALI ANAELEZA PIA KUHUSU VIFO VYA PATRIARCHS(WAZEE) NA MAHALI WALIPOZIKWA"
1:UTOFAUTI WA MAENEO.(MAKPELA NA SHEKEM)
Katika kitabu cha Mwanzo 50: 13 Biblia inaeleza,
"Kwa kuwa wanawe wakamchukua mpaka NCHI YA KANAANI,nao WAKAMZIKA katika PANGO ya shamba la MAKPELA,iliyo mbele ya Mamre,aliyoinunua Ibrahim pamoja na shamba kwa Efron MHITI,pawe milki ya kuzikia"
FAFANUZI: Katika aya hiyo hapo juu sehemu/eneo ambalo Nabii Musa analotaja kuwa mahali alipozikwa YAKOBO ni NCHI YA KANAANI,anaongezea habari kuwa alizikwa katika PANGO la shamba ya MAKPELA
FAHAMU : MAKPELA(Kiebrania: Me'arat ha - makhpela - The cave of double)
Sio jina la mji/kijiji au jiji kama BETHEL,YAFA,KAPERNAUM,GAZA ni jina la PANGO - Lilikokuwa katika shamba ambalo Ibrahim alilinunua pamoja na shamba ili afanye kuwa mahali pa kuzikia Watu wake - JINA LA MAHALI HAPO NI KIRIATH - ARBA/HEBRON.
Rejea,Mwanzo 23: 1 - 9
....."9" ili kwamba anipe PANGO YA MAKPELA iliyo katikati ya shamba lake ...."
-Kisha anamalizia kutaja jina la MTU aliyemuuzia Ibrahim SHAMBA pamoja na PANGO lililo ndani yake kuwa ni Efroni,kutoka Katika kabila yake ni MHITI.
TUKIREJEA:Katika kitabu cha MATENDO : 7:15 - 16,Biblia inaeleza,
"Basi YAKOBO akashuka mpaka Misri;AKAFA YEYE (NA) BABA ZETU;wakachukuliwa mpaka SHEKEM,wakazikwa katika kaburi lile,ambalo Ibrahim alilinunua kwa kima cha fedha kwa wana wa hamori huko SHEKEM"
FAFANUZI:Mkuu Mwandishi wa MATENDO anaelezea habari mbili kwa wakati mmoja( TWO NEWS IN ONE/A SINGLE CONTENT),habari hizo ni;
"Basi YAKOBO akashuka mpaka Misri;AKAFA YEYE........"
1 :KIFO CHA YAKOBO NA MAHALI ALIPOZIKWA - KIRIATH - ARBA/HEBRON/MAKPELA(.Mwandishi anasema;"Katika kaburi lile,ambalo Ibrahim....")
"......NA BABA ZETU..."
2:KIFO CHA BABA ZAKE NA MAHALI WALIPOZIKWA - SHEKEMU
(HAPA SHEKEMU WAMEZIKWA NABII YUSUPH NA WANAWE,NA BAADHI YA WANA WA NABII YAKOBO.HADI LEO PANAITWA;
*QEVER YOSEF(Hebrew)/QABL YUSUF(Arabic). - "Kaburi la Yusuph"
HIVI LEO NI SEHEMU ILIYO KATIKATI YA MLIMA GEZARIMU NA EBEL,UMBALI WA MITA 300 KASKAZINI MWA SHEKEMU/SYKAR.
NOTE/KUMBUKA: KIRIATH - ARBA/ILIPO MAKPELA NA SHEKEMU ZIKO KATIKA WILAYA MOJA - INAYOITWA SAMARIA.
PILI: UMBALI KUTOKA MIJI HII MIWILI SIO KAMA ULIYOELEZA KUWA NI SAWA NA KUTOKA *KIBAHA - GEITA* AMBAPO NI KILOMETRES 850.
BALI NI MILE 50/KM 75 SAWA NA KUTOKA BUNDA - MUSOMA/AU DAR - BAGAMOYO/MVOMERO
((AMBAO NI UMBALI WA KAWAIDA KABISA,IKIWA MIJI IMO NDANI YA WILAYA TU)
MWISHO:Mwandishi wa MATENDO HATAJI KABILA anaposema HAMORI bali anataja JINA LA UBINI/SONS OF HAMORI.
..."16" Ambalo Ibrahim alilinunua kwa kima cha fedha kwa WANA WA HAMORI...."
MLINGANISHO.
-Waandishi wote wanataja YAKOBO alikufa.
-Wote wanakubaliana kuwa alifia MISRI
-Wote wanakubaliana kuwa alizikwa katika kaburi la Ibrahim katika PANGO/MAKPELA
-Mmoja anataja kabila la waliomuuzia Ibrahim shamba kuwa ni MHITI,mwingine anataja jina la ubini(sons of).
-Wote wanakubaliana kuwa watu wa ukoo wa Ibrahim walizikwa mahali/eneo/wilaya/mkoa mmoja kama Ibrahim aliyotaka.
- Mmoja analezea habari za baba zake wengine WALIOZIKWA SHEKEMU(Sio YAKOBO),mwingine hawaelezei.
REJEA;MWANZO 12:6
"ABRAM akapita katikati ya nchi mpaka mahali PATAKATIFU PA SHEKEMU,mpaka mwaloni wa More.Na WAKANAANI siku zile walikaa katika NCHI HIYO.
Natanguliza shukrani Mkuu.