Siri iliyofichwa kuhusu BIBLIA


Hakuna kitu kilichofichwa. Ukisoma nyaraka za Paulo, Petro na Yohana utaona kuwa tangu Kanisa la karne ya kwanza, kuliibuka imani potofu za manabii wa uongo, wakitumia maneno 'roho ya mpinga Kristo'. Hivyo wakati wa kuandika biblia moja, au kukusanya vitabu hasa vile vya Agano la Kale, umakini ulifanyika kuona ni vitabu gani ambavyo havikua na utata wa kiimani. Kwa hiyo walikua sahihi, kwa kuwa baadhi ya vitabu vililenga maisha ya watu wa nyakati zile, na pia tangu Agano la Kale imani potofu ilikuwepo.

Marekani na Ulaya ambao wengi wamekua wapagani, hawawezi kutupotosha kwa elimu zao za Theolojia kuwa kwenye Injili kuna mistari iliyopachikwa kinyemela. Bali katika kutafsiri kutoka lugha za asili, ndipo mapungufu kidogo yalijitokeza, ambayo hayana madhara kwa imani.

Hivyo ndugu yangu, Wikipedia isikupotoshe.
 
Mkuu wikipedia inaingiaje hapa. Tunavyoongea tayari kuna biblia versions 9 na mzee zaidi ni KJV maana ndio ilikuwa ya mwanzoni na mpya zaidi ni NIV (2011) na ndio inadai chanzo cha watafsiri wa KJV ni text receptus waliokuwa nayo 1600 lakini hawa wa NIV waliikuta text receptus ya zamani zaidi kutoka dead sea scrolls ambayo haikuwa na hayo maneno 64,000 na hiyo mistari niliyoorodhesha sasa basi wakasema KJV ilichakachuliwa na ndio leo hii NIV ndio inayotumika zaidi duniani yaani kwenye kila biblia 100 zaidi ya 50 ni NIV ila bible ya kiswahili ilitoholewa kutoka KJV ndio nauliza sasa nani mkweli kati ya KJV na NIV?

Na kama NIV ni mkweli (wanatheolojia 80% wanakiri) je nini hatma ya uhalali wa Biblia kama imewahi kuchakachuliwa

ujibu kwanza hili ambalo halihitaji wikipedia bali uwe na biblia mbili tu ya KJV na NIV ili ujengee hoja
 
Udaku naomaanisha mimi ni kwamba kuna vitabu viliondolewa kwenye biblia kwa sababu havikuwa na usahihi. Mfano hivi leo likitokea tukio kubwa kila mwandishi ataandika anavyoona na pia wengine wataandika kishabiki au kiudaku. Kwahiyo kwenye biblia kuna matukio mengi yalitokea ya kushangaza ambayo yali stajabisha watu kumbuka pia wapenda umbea walikwepo! Embu fikiri bikira anazaa bila kuingiliwa na mwanaume!

Unaweza kuona hiyo siyo habari ndogo kila mtu alielezea. Mfano mzuri humu JF huwezi kuweka kila habari au uongozi wa JF wakiona habari flani haileweki wanaifuta.. Kama JF inakuwa makini na habari zake! Biblia itakuwaje?
 
Kwahiyo unataka kukaa kwenye nafasi ya kumtetea Mungu au!? Mwache Mungu ajitwalie utukufu mwenyewe...
sina na wala sifikirii huo mpango wa kuchukua nafasi yake ila natetea imani kama mitume walivyo tetea.
 
Embu iweke hiyo mistari isije ikawa ni debe tupu..!
Marko 11:26, 15:28,9:44,9:46 Mathayo23:14,18:11,17:21Luka 17:36 Yohana 5:3-4, Matendo 8:37 n.k

Na pia wakadai kuna mistari iliongezewa mfano marko 16 inaishia mstari wa 8 ila 9 hadi 20 ni FEKI???

Pia yohana 7:52 hadi 8:12 wanadai 7:53 hadi 8:11 ilichomekwa hii muhimu sana kaisome utaona kuna ukweli hapo maana mtitiriko wa 7:52 umeendelezwa 8:12

Soma alafu urudi mkuu
 
Uwe unaelewa kidogo mada kabla hujacomments chochote ndugu hakuna mtu aliyekwambia biblia imetungwa mana biblia n mkusanyiko wa vtabu..kinachoongelewa na kujadiliwa kwmb wapo watu ambao wamekaa wanaijua nje ndan biblia na kwsabb zao muhimu wakaamua kutoa baadh y vtabu km vlvyoorodheshwa na vlvyobaki wakaamua kuvipunguza baadh y mistar na kuingiza mistar y kwao na hlo lnawezkana san mana waliyofany hii kaz n watu ambao wanauelewa na wanachokifanya..cku zote kuengeza maandish n rahs zaid kulko kutunga..
 
Ndugu yangu nimesoma luka na Yohana nimegundua yafuatayo kwanza kwenye Yohana 2:1 haijasema siku 3 "baada ya ubatizo" kwamba Yesu alikua huko kana imesema tu siku ya 3,nimesoma Luka sura ya 4 yote inasimulia vile Yesu alibatizwa na kwenda nyikani na mstari wa 14 unasema baada ya hayo alienda galilaya alipofika huko ndo kisa cha kugeuza maji kuwa divai linatokea (maana kana ilikua galilaya.

Ni mji ulio mlimani kaskazini mwa nazareti) nilichojifunza ni nini? Kwamba biblia hapo haijipingi Yohana alikua anaelezea siku ya 3 ya Yesu kuwepo garilaya na si siku ya 3 ya Yesu tokea abatizwe
 
Mimi, ninavyojua Lengo la Maandiko Matakatifu ni kufikisha ujumbe uliotarajiwa wa Mungu kwetu sisi binadamu. Kupitia mafunuo au matendo ya wazi au maneno ya kusikia au hadithi na mifano, Mungu anahitaji kutufikishia amri zake flani ili tuzifuate. Hapa hoja ya Msingi ni Mungu kutufikishia ujumbe wake kama alivyotarajia. Nikitolea mfano wa Agano Jipya, Yesu alikuja duniani na akatuletea maagizo kutoka Mbinguni.

Yale maagizo yaliambatana na Matendo yake alipokuwa hapa duniani.
Waandishi wake akina Matayo, Marko, Luka na Yohana waliandika mafundisho ya Bwana Yesu. Hapo kila mmoja aliandika kwa mda wake kama alivyoshuhudia kwa macho yake mwenyewe. Kila mwandishi aliweza kuweka au kuondoa matukio fulani ambayo yalitendeka na Yesu wakati akifundisha kutegemea alivyo ona inafaa.

Kama akina Marko na Luka wangeandika sawa sawa, mstari hadi mstari, nukta kwa nukta, ushahidi wao ungetia mashaka na ingeonekana kama walikaririshwa kwa pamoja wakati mmoja. Ushahidi mzuri ni ule ambao kila mtu anautoa kwa maelezo yake yanayo pishana ki matukio na shahidi mwingine, lakini ujumbe wa kushuhudia kama mtuhumiwa alitenda kosa unadhibitishwa.

Hivyo basi, pamoja na akina Mathayo kutofautiana ki matukio mahali fulani fulani lakini wote wanaeleza kwa usahihi kabisa ujumbe wa Agano Jipya, kwa mfano.
1. Amri mpya mbili za kumpenda Mungu na Jirani.
2. Mateso, Kifo na Ufufuko wa Bwana wetu Yesu Kristo.
3. Mungu kukutana nasi kwa kupitia nafsi na mwili wa Yesu Kristo.
4. Ubatizo wa Maji na Roho (umuhimu wa kuzaliwa upya kwa mara ya pili)
5. Yesu kuja siku ya mwisho kutufufua wafuasi wake na kwenda kuishi naye Mbinguni milele. NK
Hapa nimetoa mifano michache ili nisiwachoshe wasomaji.
Hivyo basi wandugu wapendwa
Mchakato wa Mungu kuwasiliana na binadamu unapitia matukio mengi sana, kinachotakiwa, ni kufikisha kwa watu ujumbe ukiokusudiwa kwa usahihi.
Kwahiyo Biblia Imeandikwa na watu tena Wakati mwingine Wataalamu mbalimbali waliobobea katika fani mtambuka, hukutana na kujadiri nini kiandikwe na nini kiondolewe ili kuhakikisha UJUMBE ULIOKUSUDIWA NA MUNGU UNAWAFIKIA WALENGWA NA KWA KIASI CHA KUTO KUWACHOSHA.

Hivyo ikisoma Injiri hizo Nne za mwanzo unaona kabisa kutofautiana ki matukia mahali flani flani, na pia aya au sentensi flani kutoonekana kwa mwandishi flani, na kuonekana kwa mwandishi mwingine. Hali kadhalika Biblia kwa ujumla wake Waroma wanatumia vitabu 72 wakivijumuisha na vile vya DEUTROKANONI,

Wanamatengenezo wanatumia vitabu 66 na wameviondoa vile vya Deutrokanoni.
Lakini ukivisoma vyote maudhui yake ni yale yale.
Yanasisitiza Kumpenda Mungu na Kumpenda Jirani.

Hivyo basi Biblia imeandikwa na binadamu na sio Mungu.
Soma Kutoka 34 : 27 - 28. Mungu anamwagiza Musa kuandika kile anachokisikia toka kwake.
Yesu pia alimwagiza Yohana aandike anachokisikia katika mafunuo katika Kisiwa Cha Patmo. Kwenye Ufunuo wa Yohana.
" Kwa malaika wa kanisa lililoko Efeso andika "
2 : 1

Katika Kufasili toka Lugha moja hadi nyingine, waandishi wanapishana Kimazingila, Lugha, Kitamaduni na Kijamii jambo linalopelekea kuathiri Fasili kutoka tamaduni moja kwenda nyingine.
Mfano,
Ukisoma Biblia ya Kinyakyuswa au ya Kihaya, utagundua kuna tofauti ya kisarufi na Biblia ya Kiswahili lakini Maana ipo palepale.
Zinaeleza kwa usahihi kabisa Mpango wa Mungu wa kumuokoa Binadamu.
Cha msingi hapa sio kuangalia hizo tofauti za Kimuundo, na Kisarufi bali Muunganiko wa Kisemantiki (kimaana) ili kujenga dhamira iliyokusudiwa na Mungu kwa wanadamu.
Leo hii tunaona Injiri inahubiriwa, mapepo yanakimbia, wagonjwa wanaponywa, Watu wanaokolewa nk, kwa maombi ya watumishi wa Mungu kupitia mafundisho ya Biblia hiyohiyo inayotofautiana kisarufi mahali flani flani.

Hapa inathibitishwa wazi kuwa NENO la Mungu Limetufikia kwa Usahihi licha ya hizo Minor Errors za kibinadamu (ubinadamu) zinazojitokeza.
Na Hilo Ndilo Lengo Kuu la Neno La Mungu.

Mimi ndivyo nilivyo elewa.
Masahihisho yanakubaliwa

Za Masiku tele, Mheshimia
zitto jr.
 
Tafsiri hizi za watu kubadilishabadilisha Biblia zimekuwepo kwa maelfu ya miaka na mambo mengi wanayoamini atu sasa kwamba ni neno la Mungu kutoka kwenye Biblia, ni tafsiri za watu tu zilizopandiana kwa maelfu ya miaka.

Hayo si maneno yangu mimi mja nisiyejua mengi, ni mawazo ya msomi wa Biblia, Myahudi anayeujua utamaduni wao vilivyo, ambaye kazi yake ni kusoma Biblia na ana Ph.D ya mambo ya Biblia, ambaye kashafundisha mpaka Harvard anaitwa James L Kugel.

Kaandika kitabu kizuri kinaitwa "How To Read The Bible: A Guide To Scriptures, Then Aand Now"

Narudia.

Biblia ni maneno ya watu tu walioandika kuhusu maisha yao.

Si maneno ya Mungu.

Mungu aliyeandikwa katika Biblia hayupo.
 
Hao wanao sema ni watu gani? Ungeweka nahiyo ambayo unasema ipo sahihi ili tufanye ulinganisho.
 
Mzee ni tafsiri gani ya biblia unayotumia? Maana mm nina UV hiyo mathayo 27:44 imesema tu wale wezi haijasema idadi yao ila Luka ndio inasema kuhusu huyo mwizi 1 aliemtukana Yesu contradiction iko wapi hapo sasa?
 
Mkuu nadhani unatamani sana kumjua Mungu lakini hujua pakuanzia! Nami sipendi kukuvunja moyo endelea kuwa nasi pengine mambo ya kakwendea vyema,coz hakuna aliye zaliwa akiwa anajua yote.
 
swali dogo tu wakristo mnijibu
unaweza kunipa historia ya marko,mathayo,luka ,petro na yohana

Can you handle the truth?

No "hidden code", no "secret bloodline", no "arcane wisdom", no "holy grail", in fact, no mystery at all – just the unembellished truth about the greatest fraud in history. Jesus Never Existed reveals a disturbing truth: that the triumph of Christianity was a disaster for humanity – made chillingly ironic by the bogus nature of its central character, superstar and "saviour". Jesus Never Existed is an uncompromising exposure of the counterfeit origins of Christianity and of the evil it has brought to the world. Not a book for those who wish to keep their faith in the cosy bliss of historical ignorance.
 
Mkuu nadhani unatamani sana kumjua Mungu lakini hujua pakuanzia! Nami sipendi kukuvunja moyo endelea kuwa nasi pengine mambo ya kakwendea vyema,coz hakuna aliye zaliwa akiwa anajua yote.
Natamani sana kujua chochote ambacho kina ushawishi. Na kwa nini kina ushawishi.

Imani ya Mungu ina ushawishi sana.

Ushawishi unaotokana na historia ya kihadithi kuliko ukweli.

Ndiyo maana mpaka sasa huwezi kuthibitisha Mungu yupo.

Unaishia kufupisha mjadala kwa kuniambia niendelee kuwa nanyi.

Hiyo habari ya kwamba hakuna aliye zaliwa akiwa anajua yote, inaweza pia kuwa inamaanisha habari ulizojua za kwamba kuna Mungu, ni habari za uongo ambazo hukuzifahamu vizuri, na hapa una nafasi ya kujifunza zaidi.
 
Tafsiri ya Biblia ya “halisi kimsingi” dhidi ya “ulinganifu mtambuka”

Kwa vile ujumbe ni msingi wa kutafuta maana, toleo la Biblia tunayotumia (ikiwa tunatumia toleo

lililotafsiriwa) ni muhimu sana. Kuna nadharia mbili za msingi katika kutafsiri biblia: (1) “halisi kimsingi” kama vile NASB, ESV, NKJV na RSV; na (2) “ulinganifu mtambuka” kama vile NIV, Good News Bible, New Living Traslation, na Contemporary English Version

1. Nadharia iliyopo nyuma ya Tafsiri za Biblia

a. “Halisi kimsingi” hujielekeza katika ngazi ya muundo wa kifungu. Kimsingi wanafanya tafsiri ya lugha (i.e., maamuzi hufanyika kwa kuzingatia maneno [Kiingereza] mazuri zaidi kuelezea maneno ya Kiebrania na ya Kigiriki ya kifungu cha Biblia cha asili)

b. Tafsiri ya “ulinganifu mtambuka” pia hushughulika na muundo lakini hujielekeza katika “wazo” au ngazi ya maana. Huhusika na tafsiri ya maudhui ya kifungu (i.e, tafsiri ya maana ya kitheolojia ya maana ya kifungu cha asili). Hilo husababisha mpangilio na matumizi ya maneno na muundo ambao haufanani na maneno ya asili ya kiebrania na kigiriki, ingawa hakuna awezaye kueleza mabadiliko yamefanywa wapi. Katika kutekeleza, wahariri wa tafsiri ya ulinganifu mtambuka wamefanya tafsiri ya Biblia kwa ajili ya msomaji, ingawa msomaji hawezi kujua wapi lilitokea. NIV na NRSV hazibadiliki kabisa (i.e, inakaribia tafsiri ya maana halisi ya lugha ya asili) kuliko tafsiri za Jerusalem Bible au Good News Bible.

c. .Vifupisho. Kwa upande mwingine wa Tafsiri ya ulinganifu mtambuka (i.e, ikiachana sana na uhalisia) ni vifupisho kama vile Living Biblia. Vifupisho vinatafsiriwa kwa kufuata “ulinganifu mtambuka lakini wakati mwingine huenda mbali kwa kuweka daraja kati ya baadhi ya tofauti za kitamaduni na za kihistoria kati yetu na nyakati za biblia”. Hivyo, “msomaji hupokea tafsiri kiasi Fulani cha theologia ya mtafsiri (na inapaswa ijulikane hivyo)” (Ibid.) Hayo matoleo ni mazuri kwa ajili kutupatia maana halisi na ya msingi katika kupata tafsiri ya kifungu cha Biblia, tahadhari ni lazima ichukuliwe na ni muhimu kulinganishwa na tafsiri za maneno halisi toka lugha ya asili ikiwa zinapatikana.

2. Mapungufu yaliyomo kwenye matumizi ya tafsiri ya ulinganifu mtambuka. Tafsiri zote za ulinganifu mtambuka husumbua “usomaji” wa tafsiri kwa msomaji wa siku za leo akilinganisha na kifungu halisi alichoandika mwandishi. Kibaya zaidi hubadili kabisa kifungu cha asili kwa namna ambayo haiwezi kuvumilika kama ingelifanyika kwa riwaya au tamthiliya. Huwa zinaondoa maneno mengi ya kitheolojia yaliyotumiwa na mwandishi wa asili. Hivyo tafsiri sahihi hufanywa kuwa ngumu zaidi— hususan katika kuelewa tofauti ndogo vichwa vidogo vya kifungu, ukizingatia kwamba maudhui huwa yanapatikana katika baadhi ya maneno, nukuu na dhana, na kulinganisha vifungu vya maneno tofauti tofauti—wakati mtu anapotumia tafsiri ya ulinganifu mtambuka badala ya tafsiri halisi zaidi.

Tafsiri sahihi ya biblia hatimaye ni ile inayotokana na yale aliyosema mwandishi wa asili na si vinginevyo (i.e., “maana ya lugha”), badala ya kile anachowaza mhariri wa siku za leo kuwa ndicho alichomaanisha mwandishi wa asili (i.e., “ maana ya kimaudhi”)
 
Nimejaribu kusoma kile mleta mada anachosema ni siri sijaona kama kuna siri hapo. Kila kitu kipo sawa kabisa na kimenyooka tu. Nafikiri nia yake ni kupigania vitabu ambavyo havipo katika biblia viwepo, lakini sionia akieleza huko viliko vina msaada gani kwake usiokuwepo kwa wengine.

Ninavyofahamu biblia ina siri lakini sii hizi za mtoa posti. Siri zza biblia zipo ndani ya mistari yake na zinasomwa katikati ya hiyo hiyo mistari mfano katika vitabu vya ufunuo kuna mihuri ambayo lugha yake ya kuwakilisha ni ya fumbo kama mpanda farasi, wenye uhai, mnyama, namba 666, kahaba nk.

Hizi ndizo siri za mifano inayohitaji kufunguliwa na kuwa wazi.
Biblia ni kitabu ambacho kina kusudi moja kuu la ukombozi wa manadamu aliye anguka, nalo limeshikamana vilivyo bila kujikanganya licha ya waandishi kutofautiana kwa karibu ya miaka elifu tatu. Sasa mwandishi yeyote akijitokeza na utunzi wake usiovuviwa sii tu kwamba anatengwa bali amejitenga mwenyewe na lile kusudi kamilifu la Mungu.
 
tatizo lako huna taarifa kuwa biblia yako na quran imecopy vitabu vya kale (hususani the book of the dead cha wamisri wa kale)
kama ungejua hilo usingesema biblia na quran havina shaka
kati ya vitabu vichekesho biblia na quran vinaongoza
 
Mkuu ni vizuri kama hujaona contradiction yeyote hapo basi ungenisaidia na hyo mistari mingine iliyobaki mfano hyo story ya wezi pale mslabani mathayo anasema wote walimtukana ila luka anasema mmoja tu ndio alimtukana Yesu ipi ni ipi mkuu

Karibu tuelimishane
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…