Eng. Zezudu
JF-Expert Member
- Aug 23, 2012
- 8,024
- 11,546
Sijasoma KIV, Unacopy tuipate
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
yote kwa yote mzee THE BOOK OF ENOCH hiki kitabu kingebaki lengo la shetani kuudanganya ulimwengu lisingepita kiurahisi kama ilivyo leo, yaani leo hii kadiri unavyoelimika ndio unazidi kuwa mpuuzi tu. Mfano kwa kitabu cha Enoch upuuzi ufuatao kamwe usingetushika watu na akili zetu;Habari za jioni wana JF mada ya leo pia ni sensitive kidogo maana inagusa imani za watu ila kutokana na kuwepo hitaji la kuweka rekodi sawa nimeona nilete uzi huu ili tujifunze zaidi. Na sababu kubwa ya kuleta uzi huu ni kutokana na mada nazoleta humu nyingi zinatumia pia vitabu nje ya biblia kama source ya taarifa na kumekuwa na wengi wanaokuja na hoja kwamba chochote kilicho nje ya biblia sio kweli yaani quran,midrash,tanakh/torah,zohar,apocrypha,Pseudipigrapha zote ni batili sasa ni kutokana na hoja hiyo imenipelekea kuandaa uzi huu hivyo tuusome kwa makini na tuujadili kwa ustaarabu tu yote kwa yote kujifunza. Nitaugawa uzi huu kwa sehemu mbili ili iwe rahisi kuusoma na ningependa kabla ya kuchangia uusome wote na kuuelewa. Karibuni
View attachment 830330
UTANGULIZI
1. Biblia ni mjumuiko wa vitabu vya manabii walivyoandika kuhifadhi matukio katika historia ya imani yao kwa Mungu na ilikusanywa katika karne ya 3 baada ya Yesu baada ya kuonekana vitabu vya kiimani viko vingi vinakinzana hivyo wakaamua wawe na kitabu kimoja cha kutumika na wote na ilikuwa katika kigiriki na kiebrania. Baada ya karne zaidi ya 10 kupita biblia ya mapema kabisa kutafsiriwa kuingia kwenye kilatin iliyokuwa lugha ya Roma, ilikuwa ''vulgate'' iliyotoholewa kutoka kiebrania na kigiriki kwenda kilatin na padre Jerome karne ya 14 ila tafsiri ya kiingereza ilikuwa king james version karne ya 15 ambayo hata biblia za kiswahili na lugha zingine maelfu zimetoholewa hapo na ambacho wengi hatujui ni kwamba vitabu ambavyo leo tunaviita apocrypha vilikuwepo kwenye KJV ya kwanza ila mataifa mengi yalipotafsiri hayakuvijumuisha hivyo vitabu 14!!! Na leo hii ukivitumia humu JF kujenga hoja utaambiwa ni vya kishetani wakati biblia ya kwanza ya english iliviweka??
Miaka mingi ikapita ndipo yakaja matoleo mengine tofauti ila kwa karne hii biblia inayotambulika kutumika dunia nzima ni NIV yaani New International Version ya 1973, ambayo ilikuja kufanya utafiti na kutumia vyanzo mbalimbali vya nyuma zaidi na kutengeneza tafsiri yake na muhimu hapa tufahamu NIV iligundua makosa kwenye KJV na ikafuta mistari hiyo kwa kigezo kwamba mistari hiyo haikuwepo kwenye vyanzo vya mwanzo ikimaanisha viliongezwa baadae sana. Baadhi ya mistari ilioongezwa na ambayo NIV imeifuta ama kutoitambua Ni Marko 11:26, 15:28,9:44,9:46 Mathayo 23:14,18:11,17:21, Luka 17:36 Yohana 5:3-4, Matendo 8:37 n.k kwa uchache wake ila mingi zaidi iligundulika haikuepo kwenye vyanzo vya mwanzoni kabisa na kwamba vimeongezwa kinyemela.
Simply ikimaanisha biblia ya kiswahili tunayotumia hii ya chama cha biblia iliyotokana na KJV tumepotoshwa?? Je wakristo tumeambiwa haya kanisani?
Je nani mkweli kati ya KJV na NIV??
View attachment 830331
VITABU VILIVYOPUNGUZWA
Baada ya biblia ya nwanzoni kabisa ya kilatin kuwa na vitabu zaidi ya 76 na version zingine hadi 84 kuna vitabu vilitolewa na kina Jerome kwa sababu mbalimbali ikiwemo kughushiwa majina, kutovuviwa na Roho mtakatifu, kukinzana na vitabu vingine vya Biblia,kuandikwa na manabii wa uongo,utata wa maandiko n.k na vitabu hivyo ni kama 4 Maccabees, Assumption of Moses, Ethiopic Book of Enoch (1 Enoch), Slavonic Second Book of Enoch,Book of Jubilees,3 Baruch, Letter of Aristeas,Life of Adam and Eve, Ascension of Isaiah, Psalms of Solomon, Sibylline Oracles, 2 Baruch,Testaments of the Twelve Patriarchs na vinginevyo na hii ndio kitovu cha uzi huu embu basi tuchambue kwa pamoja.
View attachment 830333
TATIZO LA UANDISHI
Kuna hoja zilitolewa kwamba hivi vitabu vilivyoachwa kwenye biblia yaani Pseudipigrapha na Apocrypha mfano book of enoch, Book of Adam & Eve n.k kwamba vilitolewa kwenye biblia sababu kuna utata juu ya waandishi na kwamba kurasa zingine ziliongezwa baadae.... Ila leo hii wanatheolojia wote duniani wanakubali kuwa biblia bado ina pseudipigraphi nyingi mfano Isaya iliandikwa karne 8 kabla ya kristo yaani sura 1-39, ila kipande kuanzia sura 40-55 iliandikwa na mtu ambaye hajatambuliwa mpaka leo huko babeli na sura 56 mpaka 66 imegundulika na wanatheolojia dunia nzima kuwa ziliongezwa baadae yaani miaka mia kadhaa tokea isaya akiandike!!!
Hata jeremia kuanzia sura ya 26 iliongezwa miaka mamia baadae!! Hivyo swali la kujiuliza kwanini basi vitabu vingine vilitolewa kwa hoja hii ilihali biblia bado ina vitabu vyenye kasoro zilezile?? Mfano mingine ni waebrania, Wimbo ulio bora vyote vina utata wa uandishi na mikono zaidi ya miwili imehusika kwa gap la miaka zaidi ya 100!! Je sababu ya kupunguza vitabu vingine kwa kisingizio hiki ni halali au kuna mengine tunafichwa???
Nakihitaji hiki kitabu.yote kwa yote mzee THE BOOK OF ENOCH hiki kitabu kingebaki lengo la shetani kuudanganya ulimwengu lisingepita kiurahisi kama ilivyo leo, yaani leo hii kadiri unavyoelimika ndio unazidi kuwa mpuuzi tu. Mfano kwa kitabu cha Enoch upuuzi ufuatao kamwe usingetushika watu na akili zetu;
1. Kwamba Dunia inazungunguka tena 1000KM/Hr (very nonses to believe) wakati kamwe tangu uzaliwe hujawahi hata kuhisi hatua moja ya mzunguko huo na macho na akili zako zote zinakushuhudia kuwa the world is stationary!!
Book Of Enoch imefafanua wazi sana state ya dunia na universe kwa ujumla kwamba dunia ipo stationary pasipo utata wa kuhoji.
2. Kwamba jua lipo stationary ( Hii ndio highest degree of making us foolish asee) yaani siku zote unalishuhudia jua linavyokata mbuga halafu unasema eti limesimama!!! shetani sio tu ni baba wa uongo lakini pia ni fundi wa kujitengenezea komedi kupitia sisi ili awe anatucheka muda wote wakati anaisubiri adhabu yake. The Book of Enoch imeclarify vizuri tena pasipo utata wa kuuliza swali la nyongeza kwamba, jua liko kwenye motion kuzungunga mduara wa dunia kwa ajili ya ku supply mwanga duniani tu NA WALA JUA SIO CENTER OF SOLAR SYSTEM KAMA TEAM NASA(LIERS) WANAVYOTUDANGANYA NA KISHA KUTUCHEKEA PEMBENI.
3. Kwamba jua lipo mile milion 93 kutoka duniani! (khaaaah) kiuhalisia jua lipo km chache tu kutoka kwenye anga letu na ushahidi ni macho yetu( bila shaka macho yetu hayana lenzi ya kuona mile 93 milion eeeeh)
4.Kwamba dunia ni duara kama tufe, tikiti maji au mpira!! (wanatucheka sana hapa pia) The Book Of Enoch ipo clear kabisa kuwa duania ni flat!! Yeees ni flat, macho akili na hata miguupia inashuhudia kuwa ni juu ya sehemu flat!
5. Kwamba jua ni kubwa kiasi kwamba dunia inaingia kama mara 1000 kwa size ya jua!!! Hahahaha! I hate this kind of fucking science aseee!! The Book of Enoch ime describe vema kabisa kuwa mianga hii miwili, yaani jua na mwezi viko katika same size kasoro moja inatoa mwanga na joto kali wakati mwingine una generate mwanga wake usio na moto taratibu na kisha una extinguish mwenyewe na kugenerate tena. Hii ya kwamba Mwezi unaakisi mwanga kwenye jua kamwe hai make sense na inahitaji nafasi ya kutosha sana kumpanga mtu hadi aamue kukukubalia uongo huu kwa kujilazimisha.
6. Kwamba nyota moja ni kubwa sana kuliko hata dunia, na jua pia ni nyota na kwamba nyota huzaliwa na kufa!!! Yeah The Book Of Enoch imefafanua bila shaka, kwamba nyota ni mianga midogo midogo sana tu ambayo inaning'inia kwenye firmament(anga letu) na kuzunguka pamoja na anga lote.
7. Kwamba mwezini ni somewhere unapoweza kwenda ukashuka ukafanya mambo yako halafu ukarudi!! Nooo, The Book Of Enoch imeu describe Mwezi kuwa mwezi hauna kitu chochote(Yaani sio hard object ambapo mtu anaweza kusimama) bali kitu kinachojaa mwanga taratibu na kisha kufifia na kuzima kabisa na kisha kuanza tena kujaa mwanga upya lakini huku ukiwa kwenye motion kuzunguka mduara wa dunia.
8. Kwamba Antarctika ni bara la saba kwa ukubwa!! Uongo huu ulidumu sana kipindi Mungu hajaruhusu ukweli uanikwe wazi na kila mtu aujue! Najuta kuimba nyimba za kukariri ukubwa wa mabara primary! Antarctika sio bara tena bali ni kingo zilizotufungia mabara na bahari zetu zote.... kitabu fulani Mungu anasema .... nimeiwekea bahari mipaka, wala haitaivuka hata mawimbi yake yakiumuka juu!! yeah ukuta wa antarctica ndio actual boundary ya bahari zote na mabara yote. The Book of Enoch Ime describe hili pia.
9. Kwamba dunia ina nguvu ya uvutano (gravitational Force). Uongo mkubwa mwingine ni huu unaojaribu kuhalalisha kwamba dunia ni duara na linazunguka. Hahahahah hawa jamaa bhana ni sheedah!\
Mengine ni mengi yanayofafanuliwa na book of enoch lakini funga kazi kabisa ni hili:
10. Watu wa awali walikuwa ni blacks, na whites walitokea baada ya fallen angels (watchers) kushuka na kuzini na wanawake wa duniani, kisha kuzaliwa majitu, ambayo mutation yake ikatuletea whites people!! Book Of Enoch inafafanua zaidi kuwa fallen angels (watcher) walikuja na maarifa ya hali ya juu, ya mbinguni ambayo hayakupaswa kuwa sehemu ya maarifa kwa mwanadamu kwakuwa yangemharibu tu. Tazama sas Heavy destructive weapons zinachofanya, na technolijia hizi zinachotufanya! Na tazama jinsi siri hizi za technolojia zinavyomiliwa na wazungu wanaomiliki Wajenzi huru!!
HITIMISHO.
Kwa yote hayo yanayobainishwa na The Book Of Enoch ni dhahili wazi lazima kitabu hiki wangekificha ili ajenda zao ziweze kupita na kuimbwa na wote huku wenyewe wakituchekea pembeni huku wakigonga cheers hasa wanapoona tunakomaa kupongeza kugunduliwa kwa sayari ambazo hazipo in reality bt in CGI tu!
Ndo maana hujalazimishwa kuiaminiBiblia Hii Inayotumika Sasa Ina Contradictions Kibao Ambazo Zinaweza Kukupunguzia Imani Yako.
Kwa Ujumla Huwa Nasema Naamini Kuwa ' Yupo Muumba Wa Ulimwengu Na Vyote Vilivyomo ', Awe Ni Mungu Huyu Wa Kwenye Biblia:Sawa, Awe Ni Mwingine:Sawa. Haya Mambo Ya ' Dini ' Ni Pasua Kichwa Tu.
Kusema Biblia Ni Kitabu Kitakatifu Si Sahihi Hata Kidogo, Ni Sawa Ile Katiba Pendekezwa Kutoka Bunge Maalumu!
PorojoBiblia inajitafsiri yenyewe
Biblia ni ufunuo wa simulizi ya ukombozi upatikanao kwa imani katika Kristo (tazama Luka 24:27, 44-47;
Yoh 5:39). Ingawaje, ufunuo wa Mungu ni jambo la kuendelea—i.e., unajifunua katika Biblia nzima. Kanuni kadhaa hutokana na kweli hii.
1. Maandiko kamwe hayawezi kujipinga.
a. Biblia nzima inakubaliana katika ujumla wake. Kwa hiyo sehemu mbili za maandiko zinazoonekana kupingana zinapochambuliwa vema hugundilika kwamba hazipingani. Sehemu moja ya maandiko inaweza kuboresha nyingine, au kuipa usahihi zaidi lakini haitaipinga.
b. Wakati mwingine kweli mbili au zaidi hufundishwa kwa uwazi katika Biblia, lakini hutokea kukinzana. Kwa mfano Ukuu wa Mungu na wajibu wa mwanadamu ni vigumu kupatana ingawa bado Biblia inafafanua hayo mawili. Katika hali kama hizo kumbuka kwamba Biblia ni mkusanyiko ya kweli za kiungu kwa akili za mwanadamu zenye mipaka. “Wakati kweli mbili au zaidi zinafunazofundishwa kwa uwazi katika Biblia zinakinzana kumbuka kwamba unao ufahamu wenye mipaka. Usiyachukue mafundisho katika hali ya kuzidi kile ambacho Mungu hakusema ile kubaki kuwa sahihi katika ufahamu wako. Mwache Mungu asema alichosema bila kujaribu kumsahihisha au kumfafanua Mungu. Kumbuka yeye ni Mungu na wewe ni mtu. Nyenyekeza moyo wako kirahisi kwa imani na amini alichosema hata kama huwezi kuelewa au hakiendani na ufahamu wako vizuri”.
2. Hatua ya ukombozi kwa pamoja na “shauri zima la Mungu” (Matendo 20:27) ni lazima izingatiwe kwa utaratibu maalumu ili kuelewa kwa usahihi kifungu maalumu cha maneno. Biblia ni kitabu kinachoeleza simulizi moja inayoelezea habari inayokubaliana. Ingawa ukweli wote wa Biblia haujafunuliwa kwa wakati mmoja, lakini ulifunuliwa kwa mwendelezo kwa muda mrefu. AK ni maandalizi ya Injili; Injili zote katika Agano jipya ni udhihirisho wa Injili; Matendo ya Mitume ni upanuzi wa Injili; Nyaraka ni ufafanuzi ya Injili; na Ufunuo ni matumizi ya Injili. Maana kamili ya kifungu chochote cha maneno haiwezi kueleweka vema kama haijazingatia Biblia nzima na hatua ya historia ya ukombozi. “Kusoma Biblia kwa kuzingatia mazingira halisi ya ujumbe kama Neno la Mungu ni lazima kuhusisha maandiko yote yaliyokubaliwa kama mazingira hitimisho ya kifungu husika cha maneno”
MKUU,
MUNGU ALISHAONA JINSI VITABU VYAKE VINAVYOCHEZEWA NA MIKONO YA WAANDISHI....UKIMPA MWANADAMU KAZI YA KUJADILI MAANDIKO JUA SHETANI NAE HATOCHEZA MBALI NAO,LAZIMA ATIE FITINA ZAKE NDIO KAMA HIVYO INAVYOTHIBITISHWA........
MUNGU KWA KULIONA ILO AKALETA KITABU KINGINE NA KUAHIDI KUKILINDA KUTOKA KTK MIKONO YA WAANDISHI.NAAM YAMETIMIA QURAN HATA UTOE "A" INAGUNDULIKA MANA IKO MEMORIZED KTK VICHWA YAN HUMDANGANYI MTU...PIA QURAN HATA IKATAFSIRIWA KTK LUGHA GANI LAZIMA UIAMBATANISHE NA LUGHA YAKE YA ASILI."Hiki ni Kitabu kisichokuwa na shaka ndani yake; ni uwongofu kwa wachamungu"(QURAN 2:2)."Hakika Sisi ndio tulio teremsha Ukumbusho huu, na hakika Sisi ndio tutao ulinda."(QURAN 15:9)
CHAKUZINGATIWA WATU WASOME HISTORIA ZA MAMBO MENGI YAMEFUNIKWA KWA MASLAHI YAAA.......