Omuchimati
JF-Expert Member
- Aug 23, 2014
- 427
- 202
Dhana ya usaliti ukianzisha haikuachi kamwe labda siku ukiamua kutubu, Seif alimsaliti mzee Jumbe, laana ya usaliti itamwandama mpaka siku atakapoingia kaburini.Kisa cha Prof Ibrahim Haruna Lipumba kutaka kurejelea kiti chake cuf imefichuka. Maalim Seif alipanga kumfuta kabisa uanachama wa chama icho. Ikumbukwe kuwa Prof Ibrahim Lipumba alitangaza kujiuzulu uwenyekiti wa cuf mwaka Jana 2015 lkn aliamua kubaki mwanachama wa kawaida lakini gafla chadema wakashtuka baada ya kugundua kuwa Lipumba bado ananguvu ndani ya chama icho kitendo ambacho kitawazuia kukitumia chama icho ndipo walipomuuzia wazo Maalim Seif kumtimua ktk chama icho Prof Lipumba na Maalim Seif kiafiki wazo hilo ndipo mpango ukaanza kusukwa na ustadi mkubwa na kukabidhiwa kijana machachari wa chama icho Julius Sunday Mtatiro kuwashawishi wanachama wa Cuf bara huku akihadiwa kusaidiwa kifedha kuukwaa uenyekiti cuf na kuna tetesi kuwa alipewa gari na kiongozi mpya wa Cdm. Baada ya Prof Lipumba kunasa mkakati huo ndipo alipoamua kutaka kurejea ktk nafasi yake ili kupimana na nguvu na Maalim Seif. Tetesi zilizopatikana usiku huu zinadai Julius Mtatiro anajiaandaa kuhamia Cdm baada ya mapinduzi yake dhidi ya Lipumba kushindwa kufanikiwa jambo ambalo linamweka ktk wkt mgumu kisiasa ktk chama icho na uwenda akatimuliwa uanachama ndani ya Cuf.