Siri kubwa kuliko zote kuhusu dunia yetu tambarare

JE Dunia ina umbo gani?


  • Total voters
    710
Na ndo huyohuyo aliesema dunia no tambarare!!
 
Mnijibu hili swali langu
Watu mnaoamini dunia ni mviringo
Hawa wanaoamini dunia duara wamenijibu swali moja na nyie mnijibu
mkuu hapa duniani hakuna MTU aliyeweza kuchimba chini zaidi ya kilometa 15,kwanza sijui utatumia kifaa gani kuna joto kali sana
 

Na mwanga wa blue sio mwisho wa macho yetu kuona labda mimi sijaelewa ulimaanisha nini. Ila ule ni mwanga tu wa jua ambao pia unatuzuia tusione nyota mchana, au wewe unajua mchana nyota huwa zinapotea ndo mana hatuzioni?..

Huna jichanganya mwenyewe tu
Hii ni post nilikutumia lakin wewe ujasoma "" """Yaan wewe ndo umenithibitishia kuwa
wazungu wametudanganya, mwanga wa jua
kuzuia nyota mchana zisionekane? , kwa
akili yangu ya kuzaliwa ukuta unaweza
kunizuia nisione kitu, mlima, majengo,
nyumba Kuna vitu vingi sana, nimekuuliza swali ili ujanijibu upo kimya ...... Mwanga wa
jua ni object? Jibu kama NDIYO AU
HAPANA , mwanga wa jua kama siyo object haiwezi kuzuia nyota mchana tusizione, umesoma physics
ipi iliyokuambia mwanga wa jua mchana
inazuia nyota tusizione, alafu mwanga wa
jua umetuzunguka katika mazingira yetu
Kuna vitu vingi tunaona.
Soma comment zako hapo juu zote mbele, alafu soma jibu langu nlilokupa kwa mara nyingine.
Nimekupa jibu kwa Nini mchana nyota hatuzioni bado unaendelea kuniuliza swali hilo, hauko makini kusoma post neno kwa neno usingeniuliza hiyo post yako juu.
Alafu unanipa link ni Google nisome sababu za nyota mchana kuto kuonekana, umeshindwa kutetea hoja yako kwa kutumia milango ya faham yako, pamoja na kufikiri, kwa hiyo wewe sasa hivi mtu akikuambia Binadamu katokana na nyani kakupa link ugoogle ujilizishe na usome inaonyesha utakubali hiyo dhana kisa umepewa link,,kisa taarifa imepatikan kwenye Google . Wakati kiuhalisia ni uongo. Google wanaandika watu wa kawaida sana.
 
Watu wengi sana wanatoa ushahidi dunia ni duara kuhusu meli kuonekana baharin inakuja nchi kavu. Kwa elimu niliyokuwa nayo sea level inaanzia na sifuri 0 kwa hiyo basi beach zote zilizozunguka mabara yote na visiwa sea level inaanzia sifuri 0. Inamaana kwamba bandari ya dar meli zinapofikia na kuondoka sea level ni 0. Bandari ya Zanzibar sea level ni 0 pale meli zinapofikia na kutoka.
Tuje kuangalia sifa ya maji yaliyopo kwenye sehemu flan either kwenye shimo, beseni, bwawa, kikombe swimming pool Je level ya maji haya yapoje? Kwa macho yangu level ya maji yapo sawa hakuna palipo ongezeka wala kupungua, vile vile haya maji hayawezi kutengeneza shape au sura ya dome, kwa walio soma geography siyo ya kukalili bali kuelewa Kuna feature inaudwa kuto kana na lava. Simple definition DOME is half of a sphere namaanisha nusu duara maji yaliyopo sehemu flan hayawezi kutengeneza hii shape yakiwemo maji ya bahari, ziwa e. t. c.
Tunaendelea kwenye sheet ya geography Kuna maswali unapewa unaunganisha vilele 2 vya milima kwa mstali ulionyooka kutoka point A to point B, unakuta mlima umezungukwa na mistali ya contour. Alafu urefu wa mlima unapimwa kutoka sea level(usawa wa bahari).
Kwa hiyo basi kama Bandar ya dar sea level ni 0 na bandari ya Zanzibar sea level yake ni 0 mstali utakao chora lazima uwe straight line(mstali ulionyooka). Wakati huo huo tumeangalia sifa ya maji yaliyopo sehemu kama bahari, ziwa etc.
Kumbe meli itakayotoka dar kwenda zanzibar, siyo zanzibar tu pekee itakayokwenda kwenye bandari yeyote dunia iwe America, China urusi meli itakuwa. inatembea kwenye maji yaliyo flat mleta mada kaeleza vizuri kabisa kwa Nini unaiona meli kama inaibuka kasema kuwa " inamaana kua dunia inaanza kupinda au ku curve kwa nchi 8 kwa mile moja"
Yupo sahihi kabisa.
Kwenye Geography tumeambiwa kuwa sehemu ya Ardhi iliyo didimia imesababisha kupanda kwa sehemu nyingine ya Ardhi , ime push up land kuja juu, kama milima ingevunjwa na kujazwa kwenye sehemu zilizo didimia basi Ardhi ingekua tambarare hizo ndo theory. Usisahau maji ya bahari kuwa tambarare (flat) + Ardhi(land).
HAYA MNITHIBITISHIE NYIE DUNIA NI DUARA KWA KUANGALIA MAJI YA BAHARI, nategemea maji yenye sea level tofauti.
 
Swali langu limeshindwa kujibiwa
Itabidi na mimi niwe mwana sayansi,

Now my law
Kama dunia ni ya mviringo kama tufe je tukichimba hapa tutatokea nchi nyingine?
Kama vile unapochukua chungwa ukalitoboa kutoka upande kwenda mwingine je tutaweza tokea upande mwingine
 
Ndivyo ilivyo kwa hili swali lako,ila kipenyo chake ni kikubwa sana na kuna joto kali kiasi kwamba kuchimba sidhani kama inawezekana
 
Ndivyo ilivyo kwa hili swali lako,ila kipenyo chake ni kikubwa sana na kuna joto kali kiasi kwamba kuchimba sidhani kama inawezekana
Mkuu kwa mfano kama kuna uwezekano
Tukichimba hapa tutatokea nchi nyingine?

Hii ndio prove ya mwisho kuwa dunia ni ya mviringo
Endapo kama wanasayansi wataprove hii
Basi nitaamini dunia ni ya mviringo
Maana mpaka sasa siamini nadharia yoyote juu ya hili
 
Aha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha kaka shkamooo!!!

Nimeshakupa LIKE yako.
 
Unaweza kutokea nchi nyingine au kwenye maji,bahari.Kuhusu dunia kuwa ni duara wala haina ubishi,technology yote hii bado huamini suala hilo,watu wameenda space wanakaa mwaka 1 wanapiga picha zinaonesha dunia ni duara ila hao wanaosema dunia ni kama meza hawana real photo bali wanatoa michoro tu,hushtki kwa hilo?
 
Kaka Asante. Umenifungua akili yangu.
 
Mkuu hii idea niliyotoa haijawahi kuthibitishwa
 
Mkuu ndiyo maana mie nasema kama kweli mzungu ndiyo katuletea dini ili atupumbaze na akafanikiwa,je tutamuamini vp na mambo mengine hali ya kuwa tayari ana sifa ya uongo.

Yani unakuta mwaafrika anawaona waafrika wenzie wajinga kwa kufuata dini et zimeletwa na wazungu,lakini hapohapo yeye anayoyasoma shule ya wazungu anayaamini bila hata kuyafanyia uchunguzi.
 
Galileo Galilaya aliuwawa na RC kwa kusema dunia ni duara.Halafu then Roman Catholic church walikubali kwamba dunia ni Duara na Galileo Galilei alizikwa tena upya kwa eshima yao ya RC.
Anaitwa Galileo Galilei
 
Taarifa zinaonyesha kuwa hakuna mtu ambaye amefika kwenye mwezi.
Kama hizi ni kweli basi hata hili la dunia kuwa flat linaweza kuwa kweli ( flat muundo wa disc).
1).Lakini je kwa theory hii ya flat earth, lunar eclipse inaelezewa kwa mechanism gani?
2). Inaeleza vip suala la equinox?
3). Inaeleza vip seasons of the year (summer, winter e.tc)?
4). Vip kuhusu nchi hasa zilizopo kwenye poles kama nchi za Scandinavia kuexperience kipindi cha kuwa na long days than nights?
 

Huja nipa jibu kwanini nyota hatuzioni mchana badala yake unaniuliza kama mwanga ni object. Hilo sio jibu hilo ni swali...na hata nikikujibu itadhibitisha nini? Wewe aliekwambia mwanga hauwezi kukuzuia usione mbele ni nani? Unauliza ni physics gani inayosema mwanga unazuia nyota zisionekane ndio mana nimekuwekea hio link usome. Kwenye dunia ya leo kila kitu kipo kwenye internet, unaweza kupata jibu ya swali lako kwenye internet muda wowote ila wewe umeamua kuendelea kubisha kitu ambacho ni wazi huna uelewa nacho. Na hata kama hiyo link imeandikwa na watu wa kawaida kuna tatizo gani? Au wewe aliekwambia dunia ni flat sio mtu wa kawaida? Ni mungu?.....alafu wanasayansi wakisema binadamu ametokana na nyani na wana ushahidi mimi nisiiamini kisa imewekwa Google? Yaani watu wametumia miaka mingi kusoma na kufanya research mimi nije kubisha tu bila kuwa na uelewa wowote...ni sawa na wewe kusema dunia ni flat pamoja na kuwa wanasayansi wanakwambia dunia ni duara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…