usizunguke zunguke,..nimesema atupe majibu ya observation yake no matter ana perceive hayo majibu ni kweli au uongo?
Umeelewa?
Unataka majibu gani ?? Sis tushakwambia Earth is sphere
1. Picha zipo
2. Kimvuli cha dunia wakati wa kupatwa kwa mwezi
3. Usiku na mchana, dunia inazunguka hivyo kufanya upande ambao hauangalii jua kuwa usiku labda wewe utuelezee usiku unatokea vipi? Mwanzo ulisema (kutokana na video yako uliyoituma humu) kwamba mwezi unakaa kati kati ya dunia na jua ndo mana inatokea usiku! Sasa tutakuuliza ule mwanga unaoonekana kwenye mwezi ni wa nini, or mwezi ni transparent kwamba miali ya jua kutoka upande mmoja inapita na kutokea upande wa pili??
4. Muonekano wa meli, 5. Kuzama na kuchomoza kwa jua, ukadai ni refraction ya mwanga. Tumekuuliza ni kwa vipi refraction itafanya jua lionekane linazama au kuchomoza (hujatoa jibu mpaka saivi)
6. Last time uliuliza kuhusu reli hapa, nimekupa project kutoka chuo cha st Petersburg urusi walikuwa wanafanya geodetic survey kwenye kudesign hizo reli. Tutakuuliza wewe kwanini waliifanya hiyo survey or unaelewa hata maana ya geodetic survey ni nini? Unless wewe uwe umewahi kudesign reli na ukaona geodetic survey haina maana tutakusikiliza
7. Tumekupa mfano wa wanaorusha satellite, kwasababu kila kitu kwenye uso wa dunia kinazunguka pamoja na dunia, kurusha satellite na kuiweka kwenye orbit husika lazima wairushe uelekeo ule ule wa dunia kwasababu tayari katika uelekeo ule ina speed kutokana na ilikuwa inamove pamoja na dunia, unless umewahi kurusha satellite na ututhibitishie hapa kuwa hakuna haja ya kufanya hivyo ni wanajisumbua. Otherwise zitakuwa tantalila tu
8. Umeuliza kuhusu maji kutomwagika, umejibiwa unataka yamwagike yaende wapi? Kuna kitu gani kingine kinavuta maji strongly kuzidi gravitational pull ya dunia? Au unahisi yanaweza kuanguka bila kuvutwa?
Mpaka sasa hakuna uthibitisho wowote ulioutoa zaidi ya kusema umeona kwa macho, sasa huoni kama wewe ndo hutumii kichwa kufikiria