kama kweli unataka kujua ukweli na ushahidi wa dunia tambarare, kitu cha lazima kwako ni kuwa wewe kama wewe kwa akili zako wewe, then kama ulivyofundishwa dunia ni DUARA kama mpira (mviringo) inabidi na hapa uwe tayari kufundishwa kuwa dunia ni DUARA kama sahani (tambarare)
baada ya hapo kwakuzitumia akili zako, utachanganua ipi ni ipi bila kulazimishwa na mtu wala kumkosoa mtu coz hakuna zawadi wala kombe la mshindi wa hoja na hatushindanishi hoja humu, zaidi ya kuujua ukweli kupitia mafundisho tuliyoletewa,
maswali yako na wenzako wengi yapo humu humu kwenye uzi so kama unabishana na maandishi ni ngumu kueleweshwa hata kwa ushahidi unaoutaka. kama umeshindwa kujua usiku na mchana unapatikana vp ktk dunia tambarare... fanya hivi, nenda kalale ukiamka anza tena kuusoma uzi huu kuanzia uzi wenyewe na kila aliyechangia....
NAPENDA KUKUSAIDIA TUU, MSAADA WANGU UPO KATIKA MAJIBU UTAKAYOYAPATA KATIKA MASWALI NINAYOKUPA. ILA KAMA UNAAMINI WE NI MBISHI NA HAUTAKI KUSHINDWA.. KAUSHA!!
SWALI LA KWANZA........ KUJUA KAMA DUNIA NI TAMBARARE AU DUARA MVIRINGO
kabla haujafundishwa kuwa Dunia ni Duara Mviringo, na baada ya kufundishwa hvyo. wewe kama wewe unaionaje, je ni mviringo au tambarare?... nipe ushahidi wako wewe vile unavyoiona, yaani bila kudeal na kitabu chochote kile wala elimu yoyote ile wala video wala picha, JE DUNIA NI DUARA MVIRINGO AU NI TAMBARARE?
SWALI LA PILI..... KUJUA USIKU NA MCHANA.
pamoja na nchi kutofautiana masaa na hali ya usiku na mchana... ni kwanini hakuna nchi zenye utofauti wa MASAA KUMI NA MAWILI...? yaani kama huku kwetu ni saa sita mchana, ni nchi gani itakuwa saa sita usiku? kwanini?
SWALI LA TATU.......... JUU YA KUPATA PICHA INAYOONESHA DUNIA NI TAMBARARE AU MVIRINGO.
angani ni wapi...... je picha unayoipata ukiwa katika ndege... inakuonesha nini.....utambarare au uduara? Kipi kina speed kati ya ndege na dunia?
UKIYAJIBU HAYO TUTAENDELEA KUBADILISHANA UELEWA.
Ila kabla ya yote napenda kukushirikisha kitu kimoja hivi..... hivi haufikirii kuwa kutokana na macho yetu kuwa katika hali ya uduara flani yanaweza kufanya kitu kinachokuwa mbali sana tukione katika hali ya uduara kutokana na kucover eneo kubwa la upeo. ukitumia jicho moja kuangalia na unapotumia macho yote unadhani kwanini haoni picha mbili mbili. maana yangu ni kwamba...... lens za kamera hazina utofauti na mfumo wa lens za macho yetu, ndio maana unachokiona wewe hakitakuwa tofauti na ukipiga picha japo lenzi ni ya duara ila picha itatoka mstatiri, so tufikirie kiundani kama macho yetu yanapofika ukomo wa kuona kwanini yanaform taswira ya uduara. tena hilo duara huwa ni mbele ya upeo na angani tuu ila pembeni na ardhini uduara huwa hatuuoni, huwa ni kwanini, mimi mwenyewe natafuta majibu hayo.
kwa mfano baharini, kweli meli ikiwa inakuja kutoka mbali utaanza kuiona sehemu ya juu kwa macho ila kwa darubini inaonekana yote, (kabla ya kubisha uwe umejaribu zoezi hilo) vile vile ukitazama hiyo meli kwa umbali ule ule uliouiona pindi unaangali mbele, ukiiangalia kwa usawa wa mashariki magharibi napo utaiona yote, ili kunielewa namaanisha meli inaonekanaga nusu mtu anapoiangalia kwa usawa wa mbele, lakini kwa usawa wa pembeni inaonekana yote (pitia picha ya mleta uzi).
So kama macho yetu utengeneza uduara hakuna camera itakayokwenda kinyume na macho yetu. so ushahidi wa camera ni sawa na ushahidi wa macho tuu, kwa hiyo hata watu wa flat earth wakipiga picha uduara utaendelea kuonekana labda wabuni lens zao mpya za camera zisizofanan na lens za macho yetu.
pia kwa speed inayotumiwa na dunia katika kujizungusha hata mimi nitasema hiyo live streaming ya ISS ni uongo labda wawe wameweka slow motion.