Siri kubwa kuliko zote kuhusu dunia yetu tambarare

Siri kubwa kuliko zote kuhusu dunia yetu tambarare

JE Dunia ina umbo gani?

  • Total voters
    710
(Ni Somo Ni pana Mno) bila hilo somo na upana wake katika kuishi ungeathirika na nini? vipi yatokanayo na upana wasomo hilo, yamekurahisishia kuishi au yameongeza ugumu wa wewe kuishi? aliyetaka usome hilo somo mpaka ujue hizo law za universe alikua anatafuta nini kiasi asingekipata kipi kingetokea katika maisha. Yote hayo kwa uwezo wa Muumbaji yalishaumbika ili kusapoti maisha ya kila alichokiumba, ndio maana leo kuna watu wanasifiwa kwa ugunduzi na si kwa uumbaji. maana kila kitu kilikuwepo na walikikuta kipo. sasa shetani kwakutaka sifana wanadamu tumsifu akatumia wafuasi wake walete masomo watu tumuamini yeye kuliko aliyeviumba.

kama unaamini kuna uumbaji wa ulimwengu na vitu vyote vilivyomo basi unapingana na sayansi moja kwa moja. na kama unaamini yatokanayo na sayansi ujue unapingana na uumbaji. Vita ya Muumbaji Na Mgunduzi. Yaani Mungu Na shetani.
ni wazi hujui science haswa ni nini we unjua cosmology na evolution tu ndio sayansi. We unahisi bila math unajenga barabara imara, majengo makubwa unayoyaona unahisi bila math yangesimama vizuri, una soma muda kwa kutumia saa. Unafika unapotaka kwa haraka kwa ajili ya usafiri umevaa nguo nzuri ambazo engineering inehusika , kila hatua kwenye maisha yako imerahisishwa tokana na elimu ya sayansi. We usichukulie theory ya evulotion na cosmology ukahitimisha kuwa sayansi haina faida. Ndio maana nikasema toka mwanzo shetani hajatengeneza elimu ya sayansi yeye anachofanya ni ku manipulate baadhi ya laws
 
Tatizo lako upo kubishana Kutaka Ushindi, ningekujibu hili vizuri tuu.
Swali Langu ni kwanini Unauliza Maswali yatokanayo na elimu ya Dunia mviringo kwa watu wa elimu ya dunia tambarare. Yaani umuulize Mkristo maswali yatokanayo na kitabu cha Kiislam au Kinyume chake. ndivyo ufanyavyo wewe, hapo itakua ni kubishana na si kuelimishana.

maana yangu, soma shape za mwezi zinaelezewaje katika FlatEarth then uje na maswali yatokeayo huko ueleweshwe, maana hapa unataka kujulishwa kitu usichokielewa, LAZIMA UTABISHA

hebu fikilia kwa mfano wa mdogo tu. achana na shuguli za kiofice ambavyo watu wanawasiliana kikazi nchi fulan na nchi ingine kwa masaa ya kikazi inambidi mtu wa nchi ingine awepo ofisini usiku wa manane ili kuendana na mtu wa ofisi ya nchi ingine.

ushawahi kujiuliza kwanin unaangalia mpira unaochezwa nchi za brazil saa 8 hadi 10 za usiku ikiwa kule wanakocheza ni saa 10 jioni?
labda pia useme masaa hayaangalii jua .na useme mwenyewe kama dunia ni duara au tambarale.

vitabu kalibu vyote vya dini ukristo na islam vimeandaliwa kama miongozo ya kuiendesha dunia hasa kisayansi na kiuchumi. hebu fikilia mfano wa kitabu cha mwanzo walipo muongelea kaini na abeli hadi kaini kufukuzwa kwenye nchi aliekua analima ,ikiwa nyie mnaumia kwa abeli kuawa na kumuona kaini ni katili wenzenu wazungu kwa upande wapili wanagundua kunasehemu tulijua tunalima/product na kwa kuhakikisha wametuma wachunguzi kuhakikisha na wamefanikiwa kujua wapi na wamekuja kwenye mabara yetu kuvuna mali za kutosha. nyie bado mnashupaza shingo kumsubili yesu. vitabu kama DANIEL,UFUNUO Nk kalibu vyote hivi vimewekwa na wanajimu na walimu wa astrooloji wa zamani kuelekeza jinsi ya kuiongoza dunia ktk nyanja zote. kulan ndio usiseme.sayansi imezungumzia waziwazi. msisome hivi vitabu kwa lengo la kiiman pekee utakua mwehu.soma kiutafit wa kawaida ila uwe umejua mambo mengi ya kisayasi,kihistoria na kijogorafia ya dunia ndio utaelewa nazungumzia nini.

USIMBEZE MTU ALIEFANYA UTAFITI FULANI NA KUFANYA VITU KWA VITENDO NA AKAFANIKIWA TENA KWA USHAHIDI HALAFU NAWEWE UNAPITA HUMO KUPINGA UKIWA HUNA HATA USHAHIDI ROBO YAKE.

haya umeanza kuleta picha ya mchoro wa dunia ukiwa duara na bado wamekuja na picha ya wazi kabusa ya dunia yako tena miamba wa kisayansi wakiwa kwenye mwezi.hadi maziwa makuu yako unayovua samaki yanaonekana wazi kabisa.
mtu mweusi ni shida sana...!
 
Sasa Mimi muda huo nipo upande Gani mpk niione ndege ipo vertically down?
Je, nipo sourthen? Kama nipo sourthen siwez kuona hivyo Kwa sabab muda huo ndege itakuwa overhead, nikiwa northern siwezi hata kuiona hiyo ndege.
Kama unaamini kuna Camera zinazoweza ku capture Dunia na kuonyesha kwamba ni tufe linalozunguka,...kwanini huoni kwamba inawezekana pia tukapata picha/video inayoonyesha Ndege iki fly down vertically kuelekea destination ambayo ipo chini kwa kuzingatia kwamba Dunia ina umbo la tufe?
 
Mfano nipe jibu Linalothibitisha Dunia, Jua Na Mwezi Havitembei au Vinatembea pindi tuangaliapo kwa Macho.
Nikimaanisha, Je Nikiangalia Nini Nitajua Hivi vitu Vipo katika Mwendo Au Vimesimama.?
Kwa macho huwezi kuthibitisha kuwa Jua au mwezi either vinatembea au havitembei.
 
Kama unaamini kuna Camera zinazoweza ku capture Dunia na kuonyesha kwamba ni tufe linalozunguka,...kwanini huoni kwamba inawezekana pia tukapata picha/video inayoonyesha Ndege iki fly down vertically kuelekea destination ambayo ipo chini kwa kuzingatia kwamba Dunia ina umbo la tufe?
Hivi unatumia akili kufikiri kweli?
Huyo atakaepiga picha atakuwa angle Gani? Juu? Kama atakuwa juu maana yake atakuwa overhead(juu ya ndege) kwahy hapo Hilo swala la down vertically haiwezekani.
Na kama unamaanisha picha kutoka space ambazo ndio zinaonesha Dunia Kwa upana zaidi, huo uwezekano wa kupiga picha mpaka ndege zionekane haupo, hakuna utakachoweza kukiona Duniani ukiwa space.
 
Kwanza kupiga picha au kutopiga picha hakuna umuhimu hapo,..unachotakiwa ni kutuambia na kufahamu kwamba Kama kweli Dunia ni tufe basi Ndege itapaswa iende vertically downward na sio straight-horizontally kuelekea destinations zilizopo below the curve......kitu ambacho hakifanyiki. kwa kuwa Dunia ni flat basi Ndege always utaziona zikipaa Horizontally bila ku bend...

Hiyo ndiyo point ya msingi,..
 
kama unaamini kuna uumbaji wa ulimwengu na vitu vyote vilivyomo basi unapingana na sayansi moja kwa moja. na kama unaamini yatokanayo na sayansi ujue unapingana na uumbaji. Vita ya Muumbaji Na Mgunduzi. Yaani Mungu Na shetani.
We jamaa uchinjwe Xmass😀😀, yaani Ujinga ni kuamini Sayansi inapinga uwepo wa Mungu.
Wakati uhalisia ni kwamba sayansi inafocus na natural world, observation, experimentation, na evidence bila kujali kama hivo vitu vimeumbwa ama la!!

Wakati Vitabu vya Imani kama biblia na Quran vinaelezea uwepo wa nguvu iliyojuu kushinda vyote na iliyoumba vyote vilivyo katika ulimwengu.

Sasa mfano science inaongelea formation ya Dunia inatokana Bing Bang, we unaona hapo imepinga uwepo wa MUNGU? Singularity ilihitaji uwepo wa energy fulani Ili kuwezesha hiyo Bing Bang je kama ndio jinsi alivyoamua kuiumba Dunia hivyo?

Mfano mwingine ni Evolution na chimbuko la binadamu. Science imefanya tafiti zake Kwa kutumia data na mbinu za kisayansi Kwa kuangali mfanano wa DNA structure na mambo mengine.
Sayansi ilibaini Kuna uwezekano mkubwa kuwa binadamu na chimpanzee wanatokana na ancestor mmoja[Hominids Ancestor](common ancestor), na Wala sio kwamba tunatokana na chimpanzee. Sasa hapo imepinga wapi Uwepo wa MUNGU? Je kama Adam na Eva ndo hao Hominids?
 
Kwanza kupiga picha au kutopiga picha hakuna umuhimu hapo,..unachotakiwa ni kutuambia na kufahamu kwamba Kama kweli Dunia ni tufe basi Ndege itapaswa iende vertically downward na sio straight-horizontally kuelekea destinations zilizopo below the curve......kitu ambacho hakifanyiki. kwa kuwa Dunia ni flat basi Ndege always utaziona zikipaa Horizontally bila ku bend...

Hiyo ndiyo point ya msingi,..
Kubend Gani unaongelea hapa? Ulishawahi kuona ndege inatua? Je huwa inatanguliza kichwa kwanza?
 
Ni kweli mmepigwa Knock out,...mpaka leo mmeshindwa kuweka uthibitisho kwamba:-
a. Dunià ni tufe 🌎
b. Dunia inazunguka

Sasa hapo utasema hamjapigwa knock out??!
Hahahaaaa!! Kama tumepigwa knockout why avoiding some basic questions??
 
Back
Top Bottom