We jamaa uchinjwe Xmass😀😀, yaani Ujinga ni kuamini Sayansi inapinga uwepo wa Mungu.
Wakati uhalisia ni kwamba sayansi inafocus na natural world, observation, experimentation, na evidence bila kujali kama hivo vitu vimeumbwa ama la!!
Wakati Vitabu vya Imani kama biblia na Quran vinaelezea uwepo wa nguvu iliyojuu kushinda vyote na iliyoumba vyote vilivyo katika ulimwengu.
Sasa mfano science inaongelea formation ya Dunia inatokana Bing Bang, we unaona hapo imepinga uwepo wa MUNGU? Singularity ilihitaji uwepo wa energy fulani Ili kuwezesha hiyo Bing Bang je kama ndio jinsi alivyoamua kuiumba Dunia hivyo?
Mfano mwingine ni Evolution na chimbuko la binadamu. Science imefanya tafiti zake Kwa kutumia data na mbinu za kisayansi Kwa kuangali mfanano wa DNA structure na mambo mengine.
Sayansi ilibaini Kuna uwezekano mkubwa kuwa binadamu na chimpanzee wanatokana na ancestor mmoja[Hominids Ancestor](common ancestor), na Wala sio kwamba tunatokana na chimpanzee. Sasa hapo imepinga wapi Uwepo wa MUNGU? Je kama Adam na Eva ndo hao Hominids?