Kuna kitu unachanganya, phenomenon(observable event) na Theory. Gravity ni phenomenon ambayo tunaiobserve in everyday life, mfano ukiruka utarudi chini, ukirusha kitu juu kitarudi chini na mifano mingine mingi inayofanania.
Sasa hiyo observation au effect ikapewa jina la GRAVITY. Kwahy ukisema unakataa gravity maana yake unapinga ukweli kuwa ukiruka haurudi chini, ukirusha kitu juu kitarudi chini.
Kitu ambacho ulipaswa uhoji ni the THEORY behind gravity. Yaani gravity inavyofanya kazi. Newton baada ya kuobserve apple limeanguka na kujiuliza maswali hakuweza kujua the theory behind gravity kwahy yeye akaconclude ni force ya vitu venye uzito. Einstein akaja kutoa mwanga zaidi kuhusu gravity( Einstein theory of general relativity.
Kwahy nikuweke sawa hapo.
Tukija kwenye jibu lako la DENSITY ndo inasababisha vitu vifall nimekuelewa vzr kabisa hujakosea but Kuna kitu kinamiss, kitu Gani? Soma Kwa makini hapa!!👇
Assume umechukua object fulani ukaiweka hewani at some distance from the ground, technically hiyo object lazima itafall si ndio? Of course yes, utasema hiyo object ni more dense than air. Swali la kujiuliza tu kwanini Downward direction ⬇️??
Kumbuka hiyo object kabla haijafall down ilikuwa imezungukwa na Air pande zote(juu, chini, na pembeni) na pande zote hizo Kuna air ambayo ni less dense than hiyo object Sasa swali Bado linabaki ni kitu Gani kinachagua direction ya chini na sio otherwise??