Siri kubwa kuliko zote kuhusu dunia yetu tambarare

JE Dunia ina umbo gani?


  • Total voters
    710
Jibu number 2 umesema ni mwisho wa uoni ? Yani ukomo wa macho kuona ?? Napinga kwa herufi kubwa sana.

Mimi najua na nafahamu kuwa dunia ni duara ila bado napenda tu kujifanyia research ndogo ndogo....

Kuna siku nmekaa mda mrefu sana pale coco beach...

Nkawa naitizama meli ya mizigo ikiwa inaondoka kuelekea magharibi, ni zile meli kubwa zenye minara mirefu juu,

Ile meli kadri ilivyokua inaenda mbali ilizidi kupotea kwa mtindo wa kutumbukia huku mnara ukibaki vile vile,, Hatimae mnara nao ukaanza kupotea kwa style hiyo hiyo....

Kwa akili ya kawaida tu huo sio ukomo wa macho, Maana ingekua ni ukomo wa macho basi ingepotea nzima nzima kwa pamoja kwa sababu umbali wa meli kiujumla unaenda sambamba na kila kitu chake ikiwemo ule mnara.

Jambo lingine ambalo nmewahi kufanya tafiti nmewahi kukaa kwenye kilima nkawa natazama pande zote nane za dunia,

Yani nlikua naliangalia anga kwa umakini sana kutoka nlipo mpaka mwisho wa ukomo wa macho yangu kwenye hizo pande zote nane ...Ukitizama kwa umakini zaidi unagundua kabisa dunia ni TUFE.
 
Kama hizo nyota ulikua unaziona mda fulani usiku, ungejaribu kuamka masaa 3-5 mbele uangalie kama hizo nyota utaziona tena zikiwa pale pale
Maandishi yanaishi, nilipost 2016, unenirudisha Leo 2024,miaka name!
Nashukuru siyo kwa mawazo Yako ila tahadhari ya Kila ninachokiandika,najua naweza FUTA,ila najua athari zinaweza zisifutike kwa watakaosoma


Nirudi kwa hoja Yako, nimefanya yote, ninapoenda Kilala naziona, nikibanywa haja usiku hata wa manane ni lazima nizione, na hazijawai hama kamwe
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Mkuu,..
1. Shida ni kwamba Hakuna proof kwamba maji yanaweza kustick kwenye round-ball kama hii ➑️🌍....au wewe kipi kinafanya uamini hivyo?

2. Hapo ishu ni uoni Tu,... ndiyo maana ukifika physically sehemu ambayo unahisi ndiyo kuna curve au mteremko hutoona curve au mteremko wowote zaidi ya tambarare.....
3. Mimi naona theory of gravity imetumika kujaribu kuelezea jinsi laws of nature zinavyofanya kazi....so,kwa kuwa ni theory haituzuii kuijadili ukweli wake...mfano tunapaswa Kujiuliza namna gravity inavyopelekea maji yastick kwenye round-ball.
4. Mkuu, kama umenielewa nilisema kwamba eclipse haina uhusiano wowote of whether Dunia ni flattened round-plate au ni round-ball....au ngoja nikuulize, Shape ya dunia inahusiana vipi na eclipse?
Kuhusu hiyo picha kwamba Jua linaakisi kwenye mawingu Kwa chini(at the bottom of the clouds)....., Mkuu, Jua haliwezi kuakisi mawingu Kwa chini. ipo hivi,.... Mwangaza wa jua huwa unavuka mawingu na kupenya kutokea kwa juu., ndiyo maana unaweza kuona mawingu yakionekana kuwa na rangi au kuangaza chini wakati wa jua kutokana na mwanga wa jua kupenya kwenye mawingu na sio kwamba mwanga huo unatokea kupitia chini.....
 
Je, tukifika physically hilo eneo ambalo wewe unasema uliona Meli ikitumbukia.... tutaweza kuona hivyo hivyo?

Mkuu yani umejua kwamba Dunia ni tufe Kwa kuangalia anga? Yani umeangalia anga ndiyo ukaona kwamba Dunia ni tufe la namna hii ➑️🌍?!
Basi sawa ni kipi kilichokufanya ujue Dunia ni tufe Kwa kuangalia anga,...uliona kitu gani?
 
Ni kweli maandishi yanaishi chief.

Okay niendelee na mjadala,

Kuna zile nyota huwa tatu kwa pamoja, Huwa zinaonekana sana kuanzia mida ya saa1 jioni hadi saa4-5 usiku.

Kuna ile nyota huwa inang'aa sana kwa kumeta meta kuliko zote nayo inaonekana mida hiyo nliyotaja hapo.


Emu fanya utafiti wako tena siku ambayo anga lipo clear alafu ulete mrejesho hapa hapa.

( Kama una cm yenye camera nzuri piga picha ya saa1-5 usiku eneo hilo lenye hizo nyota, na upige eneo hilo hilo saa7-10 usiku )

Nmetaja aina hizo za nyota sababu ndio popular, Ukifanya hilo zoezi usisahau kutuletea mrejesho hapa.
 
Poa ,ngoja nifuatilie
 
Je, tukifika physically hilo eneo ambalo wewe unasema uliona Meli ikitumbukia.... tutaweza kuona hivyo hivyo?

Jibu ni Hapana huwezi kuona hivyo ukiwa hapo,

Kuhusu mimi kujua dunia ni tufe kwa kuangalia anga ndio nmejua kupitia hayo na mengine mengi, Na nmetoa msisitizo kuwa ni lazima uwe "makini" lakini vile vile uwe timamu kiakili na mwenye uwezo wa kudadavua jambo kupitia fikra zako.
 
Kwanini huwezi kuona huo mteremko ukiwa hapo?!

Sawa,.. umetumia mbinu gani kudadavua mpaka ukagundua Dunia ni tufe Kwa kupitia anga,.
 
Kwanini huwezi kuona huo mteremko ukiwa hapo?!

Sawa,.. umetumia mbinu gani kudadavua mpaka ukagundua Dunia ni tufe Kwa kupitia anga,.
Kuhusu mteremko ndio hiyo curvature tunazungumzia,

Hauwezi kuona curvature ya Dunia sehemu ulipo kwasababu Dunia ni kubwa..( Imagine size ya bakteria akiwa kwenye mpira ndio wewe ulivyo kwenye hili tufe Dunia )

Mbinu nliyotumia;
Nmetumia uwezo wangu mkubwa wa kufikiri mambo kwa kina,

Ambapo nlipata majibu sawa na wengine ambao nao walifikiri kama mimi na wakatunia nyenzo tofauti tofauti kupata uthibitisho.
 
dunia ni kubwa kuliko juaπŸ˜‚πŸ€£πŸ˜…πŸ˜†πŸ˜
 
Kwahiyo hapo kwenye curvature,... ndiyo umeona Meli inatumbukia?

Curvature ingekuepo,..na kutumbukia huko unakosema wewe..,watu wangeshuhudia,...it's just an illusion from your eyes,...Meli haitumbukii mkuu.
 
dunia ni kubwa kuliko juaπŸ˜‚πŸ€£πŸ˜…πŸ˜†πŸ˜
Jua na Mwezi, kipi kikubwa?
Dunia na Mwezi, kipi kikubwa?

Ukishajibu hayo maswali hapo juu,...Njoo uelezee jinsi Solar eclipse inavyotokea kisha utafaham kwamba probably Jua sio kubwa kama ulivyoaminishwa.

Unlearn to learn.
 
Kwahiyo hapo kwenye curvature,... ndiyo umeona Meli inatumbukia?

Curvature ingekuepo,..na kutumbukia huko unakosema wewe..,watu wangeshuhudia,...it's just an illusion from your eyes,...Meli haitumbukii mkuu.
Jaribu kuelewa nini hasa nmelenga/Kumaanisha kwa kutumia hilo neno "kutumbukia"


Umesema ni Illusion ? Nielezee Ni illusion kivipi na inakuaje hadi inatokea hivyo
 
Jaribu kuelewa nini hasa nmelenga/Kumaanisha kwa kutumia hilo neno "kutumbukia"


Umesema ni Illusion ? Nielezee Ni illusion kivipi na inakuaje hadi inatokea hivyo
Mkuu mbona nimekuelewa vizuri tu,..yaani kwamba kwenye dunia yenye umbo la tufe 🌍.... Baharini kuna specific place(point) ambapo kuna Curve ambayo ndiyo inafanya ukiwa nchi kavu uone kama meli inatumbukia:-

Ndiyo maana nimepinga hiyo argument yako Kwa kuwa inaonekana ni illusion tu ya macho,...kama ingekua ni kweli kuna hiyo curve au mteremko tungejua tu hasa kwa level ya technology ambayo Dunia imefikia Kwa sasa.

Mkuu, kumbuka macho ndiyo hufanya tuone kwamba Jua linachomoza na kuzama(Illusionary)....kumbe kiuhalisia haipo hivyo.
 
Illusion ? kwanini isipotee yote kwa pamoja nsiione kabisa ?

Kama kuona inavyotoweka taratibu ni illusion naomba unielezee vizuri inakuaje mkuu
 
Illusion ? kwanini isipotee yote kwa pamoja nsiione kabisa ?

Kama kuona inavyotoweka taratibu ni illusion naomba unielezee vizuri inakuaje mkuu
Mbona simple,... Ni illusion Kwasababu Meli haitoweki wala kupotea taratibu Bali macho yako ndiyo yamefikia ukomo wa kuona... Macho yangekua na uwezo wala usingeona Meli ikipotea,.tena ungekua na uwezo wa kuiona Meli mpaka inapofika destination yake.
 
Mbona simple,... Ni illusion Kwasababu Meli haitoweki wala kupotea taratibu Bali macho yako ndiyo yamefikia ukomo wa kuona... Macho yangekua na uwezo wala usingeona Meli ikipotea,.tena ungekua na uwezo wa kuiona Meli mpaka inapofika destination yake.
Kwahiyo ukomo wa kuona ndio unaonyesha kitu kikiwa kama kinazama ? [emoji28]

Kwanini object husika ( Meli ) isingepotea kwa kufifia ?? Kama ambavyo tunaona ndege angani ?





Kwanza nkuulize umewahi kushuhudia kama mimi ?? Maana naona utetezi wako unakosa maana kabisa, Nataka nieleweshane hili jambo na mtu ambae alishuhudia kama ilivyo mimi,


Alafu swali lingine hivi unaelewa dhahiri maana ya neno Illusion ?
 
Illusion inatokea pale ambapo unaona kitu/situation tofauti na uhalisia wake ulivyo.

1.Ndiyo, ukomo wa kuona ndio unaosababisha meli kuonekana kama inazama baharini. Meli kiuhalisia haizami kabisa(kushuka as unavyosema ukiamini eneo hilo ndiyo kuna curve), lakini inaonekana hivyo kutokana tu na namna mwanga unavyovunjika angani.... Inashangaza kuona unacheka kuhusu hili mbona ipo scientifically proven kabisa?!

2. Mkuu ipo hivi,... Meli huonekana kama inapotea Kwa kuzama baharini kwa sababu Tu ya refraction ya mwanga. Refraction ni jambo la mwanga kubadilisha mwelekeo wake unapopita kupitia njia mbili tofauti. Katika kesi hii, mwanga unapopita kupitia hewa na maji, mwanga huinama. Hii inasababisha meli kuonekana kama inazama baharini,lakini sivyo.

Ebu jaribu kuchukua kipande cha mti kisha kiweke kwenye ndoo yenye maji,,.Je, Tukio utakaloona kwenye hiyo ndoo ni uhalisia au just illusion mwanga umeyahadaa macho yako?

3. Ndege angani hutokea kufifia kwa sababu ya umbali mrefu na hewa inayosababisha athari ya "blur." So, Meli haiwezi kupotea Kwa kufifia kama Ndege ni situations zinazotofautiana.
a. Kupotea Kwa Meli, kunahusisha vitu vinne umbali mrefu, mwanga, hewa na maji.
b. Kupotea Kwa Ndege kunahusisha vitu vitatu umbali mrefu, mwanga na hewa ambayo inapelekea athari ya Blur"......

4. Yap, nimewahi kushuhudia tukio la namna hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…