Siri kubwa kuliko zote kuhusu dunia yetu tambarare

Siri kubwa kuliko zote kuhusu dunia yetu tambarare

JE Dunia ina umbo gani?

  • Total voters
    710
Huku ni kubishana na FACTS. Na whenever there is facts, then science is absolutely related and embended within.
Waafrika kila siku tunalishwa sumu za kimapokeo, sio kwenye dini wala theories na tunavimeza kila mtu kwa mtazamo na upembuzi separately!

Swali la kujiuliza tu ni kwamba kwa nini tuendekeze huu upuuzi wa kupokea, kumeza kisha kubishana?? Je, sisi Waafrika hivi ni kweli bado tu hatuja advance to the extent dat we capable of collecting and organizing facts that will defend our own thoughts?? cant we become perculate and blag for our own creativities??
Tumevishwa ufinyu wa fikra kimatendo na kwa kutafakari.
Afrika bara la weusi. Afrika bara la wajinga.
Mkuu kwa hoja zinazotolewa humu ukizichukulia kama "sample"....Afrika bado sana tu.
 
Mkuu kwa hoja zinazotolewa humu ukizichukulia kama "sample"....Afrika bado sana tu.
Kweli kabisa mkuu.
Unakuta mtu anabishana huku katunisha misuli ya shingo kwa rejea za hawa hawa wazungu.
Ni mara mia mtu ukajikalia kimya tu kuliko kuleta ujuaji mwingi pasipo kufanya tafiti binafsi ama lau kujivunia kwa rejea zilizofanywa na waafrika wenyewe.
 
Kama dini zimeletwa na wazungu kutupumbaza na wakafanikiwa hilo,Je wanashindwa nini kutupumbaza na mambo mengine tofauti na dini?

Maana humu watu wanashindana mi theory tu waliyoimeza hakuna jipya.
 
Aisee unaweza pasuka kichwa
Dunia ni sayari, na kuna sayari nyingi tuu.so kama dunia itakuwa flat,means na sayari zingine zitakuwa flat?
Then dunia inazungukwa na jua,mwenzi,nyota,sayari zingine, vimondo..sasa hii dunia ina nguvu gani ya kuvishikiria vitu vyote hivyo?
Anyway wenzetu wanafikiria kuhamia Mars,wakati cc tunabishana flat or sphere of the earth..
Nadhani wakifanikiwa kuhama dunia hii ndio tutapata ukweli wa huu Uzi.
 
Wewe akili zako sawa na maprofesa uchwara wa kibongi aka lipumba
Yaani unaquote yote hayo ili uandike hivyo mkuu.....??
Kwa nini usireply kwa kawaida au ukamtag huyo mtu unayemtaka
 
Nacho kiamini na kukijua Mimi ni kwamba, dunia sio flat bali ni oval shape. Na dunia ipo stationary centred na jua ndio huzunguka dunia.
 
Hiyo siyo nadharia, ni proven fact! Kwenye dunia tambarare ukianzia safari yako katikati ya hiyo dunia tambarare ukanyoosha usawa wa nusu kipenyo hautarejea ulipotoka, badala yake utafika kwenye UKINGO! Mfano kama unasahani hapo karibu simamisha kijiko katikati ya safari, then anza kukisogeza kuelekea nje.....kijiko hicho hakitarejea kilipotoka, badala yake kitafika ukingoni, huo ukingo wa dunia bapa ndiyo nautaka mimi mnionyeshe au mniambie uko wapi!
Asante.
Ndugu lazima usome kwa kina huu uzi usitangulize kupinga kuhusu sura ya dunia. Tumeambiwa kuwa Kuna ncha ya kaskazin na kusini, ncha zote zimetanda na barafu ukiuliza sababu unaambiwa ziko mbali na jua. Nimesoma Geography Muda ningekuwekea distance from the sun kutoka North and South pole, vile vile distance from the sun kutoka equator. tunaambiwa kuwa ndo sababu za nchi za Africa nyingi hakuna barafu.
Point ya msingi ni hii tunategemea kuwa sayari ya 4 na zinazo endelea baada ya dunia inabidi ziwe na barafu nyingi sana tena zimekuwa covered large area Ardhi ya mchanga inabidi isiwepo kwa sababu distance from the sun iko mbali na sayari ya 4, kama North na South pole ya dunia ina barafu . Fuatilia kwa karibu sana pictures tunazo letewa za kuanzia sayari ya 4 na kuendelea utakuta Kuna Ardhi chombo cha NASA kimetua.
Hivi mtu aliyeko South Africa Cape Town anapotaka kwenda urusi anapita njia Ipi Je anapandisha North ya Africa nahitaj kueleweshwa maana nakumbaka kwenye Raman ya dunia ya usafiri wa Anga sijaona kama Kuna njia ya kupita nyuma kwenye mzingo.
Naombeni tuchunguza usafiri wa ANGA tujuwe dunia ni duara au tambarare Kuna siri kubwa kwenye Anga
 
Kaka moudytunechi hivi unaweza kuniambia sababu hasa ya watu kuficha kiwa Dunia sio flat? Maana haiingii akilini kanisa kuwa wanasayansi wameona dunia ni Tambarare alafu wanaficha, wanaficha nini?

Bendera ya UN imeyaonyesha mabara yote kwa mara moja na ndio maana imeonyesha Dunia kama flat ili yote yawe presented lakini haimaanishi kuwa Dunia kuwa ni tambarare,

Maswali mengine ambayo ningependa nikuulize ni haya,
1: je unamaamini sayari nyingine zote pamoja na Nyota zote likiwemo jua, na mwezi pia kuwa viko tambarare? Au Dunia tu ndio iko tambarare?
2: Kama Sayari zingine haziko Tambarare kwa nini Dunia pekee ndio iko Tambarare?

3: Kwa uelewa wako wa kuwa Dunia iko tambarare unaweza kunipa concept ya usiku na mchana inatokea vipi?

4: Unaweza kunieleza kwa kina inakuwaje sehemu moja ya Dunia inakuwa mchana na nyingine inakuwa Usiku wakati Dunia iko tambarare na Jua ni moja linaloangaza Dunia yote?
Iko hivi, mtoa post ka base ktk theory ya wenye evidence hzo za dunia tambarare, so kumkosoa yeye wala haiwafanyi kuwa mnajua sana, karibia maswali yoooote mliyomuuliza yamejibiwa tena kwa vielelezo vya mahesabu, picha video na mpaka sababu za watu kudanganywa dunia ni duara, na wengi wasioamini hilo mwisho wa siku hukimbia chocho coz utetezi wao unabase darasani so akipewa kitu ambacho hakufundishwa ili asionekane alifundishwa uongo inabidi abishe. Ukitaka kwenda sawa nakupata uelewa wa je ni tambarare au flat inabidi kwanza mtoke ktk nadharia za darasani na tujikite ktk tafakuri za akili zstu ktk machache tunayoweza kuyadadisi, ktk kuthibitisha na kwa yale ya darasani tusiwabishie wataalam ila tuwahoji tukikosa jibu basi tuamini walitudanganya.

Kwanza kw vile humu cc wote tuna elimu ya dunia duara tuliyofundishwa darasani tusikubali kuwa wavivu wakuwa wanafunzi tena wakufundishwa dunia ni tambarare... Then tutashindanisha hoja na wakuaminiwa tutamjuakila mtu na uelewa wake...
So kama haujawahi kupata elimu ya dunia duara na uthibitisho wake huna haja yakumpinga mtoa post coz mwenzako atakuwa ana elimu zote za duara na tambarare kwa kiwango chake,,

www.flatearthsociety.org

www.theflatearthsociety.org

Humo majibu ya maswali yooote yaliyoulizwa na wasioamini dunia ni tambarare mengi yamejibiwa with evidence and calculation... Kama haujui kidhungu kuwa mpole.
 
Ndugu lazima usome kwa kina huu uzi usitangulize kupinga kuhusu sura ya dunia. Tumeambiwa kuwa Kuna ncha ya kaskazin na kusini, ncha zote zimetanda na barafu ukiuliza sababu unaambiwa ziko mbali na jua. Nimesoma Geography Muda ningekuwekea distance from the sun kutoka North and South pole, vile vile distance from the sun kutoka equator. tunaambiwa kuwa ndo sababu za nchi za Africa nyingi hakuna barafu.
Point ya msingi ni hii tunategemea kuwa sayari ya 4 na zinazo endelea baada ya dunia inabidi ziwe na barafu nyingi sana tena zimekuwa covered large area Ardhi ya mchanga inabidi isiwepo kwa sababu distance from the sun iko mbali na sayari ya 4, kama North na South pole ya dunia ina barafu . Fuatilia kwa karibu sana pictures tunazo letewa za kuanzia sayari ya 4 na kuendelea utakuta Kuna Ardhi chombo cha NASA kimetua.
Hivi mtu aliyeko South Africa Cape Town anapotaka kwenda urusi anapita njia Ipi Je anapandisha North ya Africa nahitaj kueleweshwa maana nakumbaka kwenye Raman ya dunia ya usafiri wa Anga sijaona kama Kuna njia ya kupita nyuma kwenye mzingo.
Naombeni tuchunguza usafiri wa ANGA tujuwe dunia ni duara au tambarare Kuna siri kubwa kwenye Anga

hilo la safari za anga IS SOMETHING!! Marekani to Russia ilitakiwa iwe karibu sana, maswali ni magumu!
 
Mkumbuke utambarare usemwao haumaanishi hauko ktk hali ya uduara, na uduara wa dunia unamaanisha mviringo
 
Hua sipendi matusi lakini vitu vingine vinaua kabisa tolerance, hii ni karne ya 21 hatuna muda wa kukaa kuendelea kubishana na vila.za!

Hii article nimeona kwa kurukaruka sana, in short nimetumia sekunde kama 30 tu kuiangalia nikapotezea maana umeandika kitu probably saa nzima ila ni upuuzi mtupu.

Twende sasa kwenye common sense, nitajaribu kutokutumia chochote cha kisayansi pamoja na kua wewe unapinga sayansi ila unakuja kusema evidence yako ni picha iliyochukuliwa na kamera (iliyotokana na sayansi), huna hata idea kamera imetengenezwaje na kwa nini haijaonyesha dunia ikipinda kwenye hizo picha, sababu ninayo ila tusiende huko hutoelewa kwa akili yako.

Akili ya kawaida kabisa, hapa tutaona kama wewe kweli unafikiria au ovyo. Unapochukua maji na kuyaachia yaanguke chini yanajaribu kujiweka kwenye shape gani? Jibu ni jepesi tu, sphere (round) sababu ni ndogo, kila kitu kinajaribu kujivuta pamoja kutengeneza shape yenye area ndogo kuliko zote, huwezi achia maji yaanguke yakatengeneza shape ya box hata siku moja.

Sasa kutokana na nilichokisema, mwezi angani ukiwa full hua unauona kama box au sphere? obvious ni sphere, sababu ni ndogo, upo angani particles zake zimejivuta pamoja kutengeneza shape yenye area ndogo kuliko zote ambayo ni sphere, kama huamini mwezi nao ni sphere basi nenda mirembe ukatibiwe akili au tafuta daktari wa macho. Dunia nayo ipo angani vilevile, unadhani ina nini special cha kuifanya isijaribu kuobey hiyo rule ya kujivuta pamoja kutengeneza sphere alafu iende kujiweka kua flat??

Darubini zipo madukani zinauzwa, chukua moja jaribu kuangalia night sky, itafute venus au mars, zote zipo katika shape ya sphere, unaziona kwa macho yako mawili. Dunia ina nini special yenyewe tu ndiyo iwe flat?

Hujaona watu wanazunguka dunia nzima kwa meli kwa kufuata njia moja tu (forward)?? Ina maana walifika mwishoni kwenye hizo barafu zako alafu wakapita uvunguni kurudi mwanzoni au? Hehe hata aliyevuta bangi hili hawezi kutoliona lipo wazi kabisa.

Nimejaribu kukujibu kwa logic ya kawaida kabisa, kama hadi hiyo hujaielewa basi sina muda wa kubishana na watu wanaopoteza muda kusoma ujinga kwenye internet alafu wanajifanya wanasanyansi huku internet yenyewe wanayotumia imetengenezwa na haohao wanaowabishia. Akili ndogo kujaribu kuendesha akili kubwa. Hehehe siamini umeandika kitabu kizima ukisupport ujinga.
 
OKAY KAMA GRAVITY INASABISHA ORBIT,,,ACCORDING TO GRAVITY SMALL BODIES REVOLVE AROUND BIG BODIES HII INGEKUA KWELI KWANINI MWEZI UNAIZUNGUKA DUNIA NA SIO JUA NIPE MAELEZO YA KISAYANSI TAFADHALI,,,,,,,AKAFU SASA GRAVITY MAANA YAKE NNI HASWA MAANA ME NAJUA WAT GOES UP MUST COME DOWN LAKIN KWENYE MFUMO WA DUARA AMNA UP WALA DOWN MAANA WAT WA RUSSIA WANAPOPAITA JUU NI CHINI KWA WATU WA AUSTRALIA ,,DOES IT MAKE SANSE KWELI,,,,,ALAFU PIA JARIBU KUFIKIRIA RULE YA WATER FINDS ITS OWN LEVEL ALAF UNAMBIE GRAVITY INAYASHIKILIAJE MAJI YOTE ,,,,NA PIA KUMBUKA KUA UKIPANDA JUU YA PUCK UP UKARUKA IKIWA INATEMBEA UTADONDOKA TU SASA NDEGE ZINGEKUA ZINAPAAJE WAKATI DUNIA INAMIZUNGUKO MIWILI NA MIZUNGUKO HIYO YOTE INA SPEED ZAIDI YA MILE ELFU MOJA KWA LISAA HAIWEZEKANI UNLESS GRAVITY INAVUTA MPAKA HEWA NA INAMOVE NA ATMOSPHERE IVI KWELI TUNASHINDWA KUTUMIA MACHO YETU,,,,YAAMINI MACHO YAKO MAANA AMNA KIFAA KINACHOWEZA KUPROJECT KITU KAMA MACHO YAKO
Leo nikwambie!!! macho ni maongo kuliko unavyojua
 
Kitu kinachonifanya niendelee kuamini kuwa dunia ni duara ni usiku na mchana,yaan huku kukiwa usiku nchi zingine kunakuwa mchana........kama dunia ingekuwa flat au nusu duara,jua lingekuwa linafika katikati basi dunia nzima yaan nchi zote ingekuwa mchana lakin hiki ktu hakiwezekan lazma kwingne kuwe usku kwingne mchana,afu UN bendera yao waliitoa hvo ili mabara yote yaonekane vizuri(yaan picha imechukuliwa juu ya dunia na sio pembeni kama picha zingine zinavyoonesha)
Mkuu uko sahihi ila hakuna kitu kama juu, chini au pembeni ya dunia. Sema tu hiyo picha ramani ya UN imechorwa kwa kuiangalia dunia kutoka Canada na Urusi zilipo kisha ikafanywa kuwa tambarare.
 
Hua sipendi matusi lakini vitu vingine vinaua kabisa tolerance, hii ni karne ya 21 hatuna muda wa kukaa kuendelea kubishana na vila.za!

Hii article nimeona kwa kurukaruka sana, in short nimetumia sekunde kama 30 tu kuiangalia nikapotezea maana umeandika kitu probably saa nzima ila ni upuuzi mtupu.

Twende sasa kwenye common sense, nitajaribu kutokutumia chochote cha kisayansi pamoja na kua wewe unapinga sayansi ila unakuja kusema evidence yako ni picha iliyochukuliwa na kamera (iliyotokana na sayansi), huna hata idea kamera imetengenezwaje na kwa nini haijaonyesha dunia ikipinda kwenye hizo picha, sababu ninayo ila tusiende huko hutoelewa kwa akili yako.

Akili ya kawaida kabisa, hapa tutaona kama wewe kweli unafikiria au ovyo. Unapochukua maji na kuyaachia yaanguke chini yanajaribu kujiweka kwenye shape gani? Jibu ni jepesi tu, sphere (round) sababu ni ndogo, kila kitu kinajaribu kujivuta pamoja kutengeneza shape yenye area ndogo kuliko zote, huwezi achia maji yaanguke yakatengeneza shape ya box hata siku moja.

Sasa kutokana na nilichokisema, mwezi angani ukiwa full hua unauona kama box au sphere? obvious ni sphere, sababu ni ndogo, upo angani particles zake zimejivuta pamoja kutengeneza shape yenye area ndogo kuliko zote ambayo ni sphere, kama huamini mwezi nao ni sphere basi nenda mirembe ukatibiwe akili au tafuta daktari wa macho. Dunia nayo ipo angani vilevile, unadhani ina nini special cha kuifanya isijaribu kuobey hiyo rule ya kujivuta pamoja kutengeneza sphere alafu iende kujiweka kua flat??

Darubini zipo madukani zinauzwa, chukua moja jaribu kuangalia night sky, itafute venus au mars, zote zipo katika shape ya sphere, unaziona kwa macho yako mawili. Dunia ina nini special yenyewe tu ndiyo iwe flat?

Nimejaribu kukujibu kwa logic ya kawaida kabisa, kama hadi hiyo hujaielewa basi sina muda wa kubishana na watu wanaopoteza muda kusoma ujinga kwenye internet alafu wanajifanya wanasanyansi huku internet yenyewe wanayotumia imetengenezwa na haohao wanaowabishia. Akili ndogo kujaribu kuendesha akili kubwa. Hehehe siamini umeandika kitabu kizima ukisupport ujinga
Hatubishani ila tunaeleweshana, kati yetu hakuna anayeja sana.

Binafsi sitampinga yeyote zaidi ya kuidadis hoja yake. Sawa kwa wanaposema duni ni tambarare unaelewa utambarare wenyewe ni upi na upo wapi? Hata hao wenye hoja ya dunia tambarare picha za hyo dunia bado huwa na hali ya utufe isipokuwa wanaponga kwa hoja zao kuwa sisi hatupo juu ya dunia mviringo kusema kuna muda nchi nyngne watu wake huwa kichwa chn miguu juu yani tupo juu ya li mpira kuuuubwa.

Wanadai maisha yetu sisi ardhini wote tupo ktk utambarare na htupo juu ya mduara ila ndani ya mduara katika hali ya utambarare mfano unapolikata chungw ktkt sisi tuwe juu ya utambarare unaoonekana chungwani, tukiwa tumezungukwa n nguvu mbalimbali zilizomo ndani yake yani tupo katik syari yenye doom, kama hema la duara hv.

Mwisho wa sik iwe tmbarre iwe duara hakuna tutakachozawadiwa zaidi ya kurutubisha bongo zetu.
 
Hujanishawishi bado sababu
1. Mmarekani akitaka kwenda Russia au Japan anapita zake pacific ambayo iko uwani kwetu huko. Ingekuwa tambarare ingebidi apite Afrika au hapo Mashariki ya kati.

2. Russia na Marekani ni majirani kiasi kwamba unaweza kuvuka na feri tu kutoka russia kwenda hapo Alaska

3. Dunia kuwa na barafu kwenye poles wakati Sayari zingine hakuna barafu hiyo inatrgemea na tabia ya Atmosphere yake. Dunia yenyewe hii atmosphere yake ina tabaka baridi sana kama barafu na tabaka nyingine ya joto kali la luyeyusha hata chuma lakini zimetenganishwa kwa km chache tu.

4. Dunia ni duara ndo maana huko angani kuna ma-satelaiti kibao kuanzia za mawasiliano, navigation, za kijeshi na kadhalika na zote zinaizunguka dunia muda wote.

Kwa ufupi hizo sababu ilizoeleza zote ni CONSPIRACY THEORIES na kama umechagua kuwa brainwashed na kuziamini shauri yako. Changanya mambo ya darasani na Logic pamoja na common sense.
 
Ndugu lazima usome kwa kina huu uzi usitangulize kupinga kuhusu sura ya dunia. Tumeambiwa kuwa Kuna ncha ya kaskazin na kusini, ncha zote zimetanda na barafu ukiuliza sababu unaambiwa ziko mbali na jua. Nimesoma Geography Muda ningekuwekea distance from the sun kutoka North and South pole, vile vile distance from the sun kutoka equator. tunaambiwa kuwa ndo sababu za nchi za Africa nyingi hakuna barafu.
Point ya msingi ni hii tunategemea kuwa sayari ya 4 na zinazo endelea baada ya dunia inabidi ziwe na barafu nyingi sana tena zimekuwa covered large area Ardhi ya mchanga inabidi isiwepo kwa sababu distance from the sun iko mbali na sayari ya 4, kama North na South pole ya dunia ina barafu . Fuatilia kwa karibu sana pictures tunazo letewa za kuanzia sayari ya 4 na kuendelea utakuta Kuna Ardhi chombo cha NASA kimetua.
Hivi mtu aliyeko South Africa Cape Town anapotaka kwenda urusi anapita njia Ipi Je anapandisha North ya Africa nahitaj kueleweshwa maana nakumbaka kwenye Raman ya dunia ya usafiri wa Anga sijaona kama Kuna njia ya kupita nyuma kwenye mzingo.
Naombeni tuchunguza usafiri wa ANGA tujuwe dunia ni duara au tambarare Kuna siri kubwa kwenye Anga
Una tatizo kubwa linakusibu, inaweza kuwa ni la kijamii zaidi.
Nenda kamu wow my wife wako kwanza.
 
Back
Top Bottom