Siri kubwa kuliko zote kuhusu dunia yetu tambarare

Siri kubwa kuliko zote kuhusu dunia yetu tambarare

JE Dunia ina umbo gani?


  • Total voters
    710
Mkuu,nianze kusema tu kuwa nasikitika sana baada ya kusoma uzi huu kwa namna watu walivyochangia na wanavyochangia......

Mtoa mada amekuja na kuandika mambo mengi sana namna anavyosema juu ya umbo la dunia na ushahidi ameweka.Ameelezea kuwa yeye anaamini kuwa umbo la dunia ni flat,lakini akasema ni flat ya namna ipi anayoizungumzia.Shida ya kwanza ya watu inaanzia hapa...

Kuna watu wanapoona neno flat basi wanakimbilia kwenye fikra zao namna wanavyofikiria flat,wanafikiria flat kama ya meza tu,hapa ndipo panaponisikitisha kuliko mahala pengine popote pale.Mtoa mada ameelezea kuwa dunia ni flat duara yaani kama cd na michoro ameweka,watu wanakuja kujenga hoja kutoka na fikra za flat ya meza au umbo ambalo soyo duara kabisa.

Kwa kukuthibitishia hili angalia watu wanaojenga hoja kwa kuonesha kuwa mtu anaweza kutoka Dar hadi Sydney kisha akaenda Marekani kisha akarudi Accra na baadaye kurudi Dar.Ukiangalia hoja hii imelalia kwenye fikra za dunia isiyokuwa duara ya namna mleta mada aliyoizungumzia kwenye mada yake maana ukiangalia kwenye hoja za mtoa mada utaona kuwa mtoa mada naye anasema kuwa dunia ni duara lakini siyo mviringo kama tufe bali ni mviringo kama CD.Kwa mviringo huu unaweza kabisa kufanya safari hizo nilizotaja hapo juu bila kuhitajika kurudi nyuma.

Hoja ya watu kuzunguka dunia na kujikuta wamerudia pale pale,hoja hii nayo haishindikani kwenye hoja ya dunia duara ya kama sahani.Ukiangalia utaweza kuona kuwa inawezekana kabisa kuwa mtu akatoka Afrika ya kusini,akapitia Australia kisha akafika Amerika ya kusini kisha akarudi tena alipotoka maana atakuwa amezunguka duara inayosemwa na mtoa mada.Kwa maana hii bado hii haithibitishi kabisa kuwa dunia ni duara kwa maana ya tufe.....

Ameelezea mambo mengi sana pia,miongoni mwa mambo aliyozungumzia ni namna usiku na mchana unavyopatikana,watu hawasomi kabisa majibu na thread yote na unakuta mtu anakuja kurudia hoja ambazo zimeshajibiwa kwa uwazi kabisa na hili ni tatizo jingine,uviovu.Huwezi kujifunza mambo mazito kama haya huku ukiwa mvivu,huwezi na hutaweza kabisa kamwe......

Hoja nyingine ni route za ndege.Mtoa hoja amesema kuhusu hili,watu badala ya kujibu sababu ya ndege kutokuwa na rout hizi wameongeza swali kuwa vipi kuhusu ndege binafsi.Kwanza nafahamu kuwa kuna maswali ambayo ukiulizwa unaweza kuuliza aina fulani ya swali ambalo ukilijibu linaweza kukupa jibu la swali lako,lakini swali hili linaweza kujibu au kutokujibu swali kuu la mtoa mada kwasababu zifuatazo....

1;Hakuna uthibitisho ambao umetolewa hadi sasa wa uwepo wa ndege binafsi zinazokatiza north pole au south pole...

2;Kama kuna huo uwezekano wa ndege binasi kukatiza hapo,ni kwaninio ndege za kibiashara zisipite hapo ili kupunguza umbali mrefu? Kutoka South Afrika hadi Urusi kupitoa Siuth pole na kupitia katikati ya bara la Afrika hadi Geneva kisha Moscow wapi ni karibu?

Kimsingi hoja zote hizi ni mfu na zinaongeza maswali zaidi.Hakuna aliyejisumbua kujibu kuhusu ukweli wa binadamu kwenda mwezini.Hakuna ushahidi wa bibadamu kwenda mwezini....

Suala la meli kitoonekana kwa macho inapokuwa mbali ya macho yako hili mtoa mada amelijibu na ndiyo jibu bora kabisa linaloenezea suala hili.Watu walikuwa wanachukulia suala hili la meli kuzama kuwa ni moja ya ushahidi wa duara ya dunia,hii ikiwa na maana kuwa meli ile inakuwa imeshafika kwenye upande mwingine wa duara ya dunia.Mtoa mada amesema kuwa,kama inakuwa hivyo basi ukichukua kifaa maalum cha kuonea mbali usingeiona meli maana itakuwa iko kwenye upande mwingine wa duara ya dunia.

Mfano mzuri wa jambo hili ni kuchukua kijiti kifupi na ukakichoma kwenye chungwa kwenye upande mmoja kisha ukaligeuza chungwa lile upande mwingine kisha ukaanza kutazama,hutaweza kukiona kijiti kile kwakuwa kitakuwa kwenye upande ambao unazuiwa na muinuko wa chungwa lile hata kama utachukua kifaa cha kuonea mbali.Lakini ukichukua mti ukauchoma chini kwenye barabara iliyonyooka kisha ukaenda umbali wa kilomota 10 ukatazama mti ule hautauona bado lakini hii haimaanishi kuwa huuoni kwakuwa upo kwenye upande wa pili wa dunia bali ni kwasababu macho yako hayaoni tu,ukichukua kifaa utaweza kuuona mti huu.....

Kwa mfano huu ni dhahiri kuwa hoja za dunia duara bado zimegaragazwa kwenye mada hii,leteni nyingine......

Sisi tunajifunza na kuhoji pale ambapo tunaona kuna haja ya kufanya hivyo.......
Mkuu eiyer labda nikuulize swali dogo tu,kwa mfano unasafiri letsay unaelekea kusini bila kukata kona,kwa dunia yako iliyo kama cd mwisho wake ni wapi?kwa dunia iliyo kama cd ni lazima kutakuwa na mwisho,sasa nataka uniambie mwisho wake ni wapi?
 
hiyo th
I agree.....

Kimsingi tunaishi kwenye nyakati za uongo mkuu kuliko wakati mwingine wowote ule.Mimi ninaamini kabisa kuwa kuna mambo mengi sana ni ya uongo,angalau 90% ya mambo ambayo tunadhani tunayajua ni kwamba hatuyajui kabisa.....

Suala hili la umbo la dunia ni suala ambalo huwa naliangalia kwa wasiwasi tangu siku nyingi sana,kitu pekee ambacho ninataka kujua ni sababu ya kudanganya kuhusu uongo huu wa umbo la dunia.Nataka sababu itakayobiridhisha,sababu itakayoingia akilini mwangu.....

Kibaya kabisa,kama ulivyosema kwenye maandiko yako hapo juu ni kwamba,wale ambao tunadhani tunaujua ukweli ndiyo hatuujui kabisa.Kuna jambo moja la kutisha kabisa ambalo nimejifunza katika kipindi hiki hapa duniani,nimejifunza kuwa yale mambo ya kijinga kabisa ndiyo mambo ya kuzingatia kuliko mengine.....

Labda niseme hivi,yale mambo ambayo yanaonekana kuwa ya kipuuzi kwa watu "walioelimika" ndiyo mambo ambayo ni ya msingi zaidi kuliko yale yanayoonekana ni ya "akili". Kuna "watu" wamewafanya binadamu kwua kama mbuzi kabisa na hii ni mbaya zaidi.....

Acha tuendelee kujifunza.....

Hongera sana mkuu kwa mada nzuri sana japokuwa utatukanwa na kuonekana unaishi kwenye zama za giza,usijali iko siku watakuja kukukumbuka.....


Hiyo theory haikuanza hivi hivi, lengo lake ni kuwapoteza watu wasifahamu kuwa dunia iliumbwa na Mungu mkuu. Kwamba hakuna Mungu duniani na hivyo hata biblia sio kitabu cha kuaminiwa kwa vile biblia inasema Yesu akirudi kila jicho litamuona, kwa hiyo kama kila jicho litamuona dunia ikiwa ya duara wakati anarudi watu wanaoishi upande wa pili hawatamuona. Hivyo biblia ni kitabu cha watu wajinga wa dunia. Nadhani hii ni vita kati ya Mungu muumbaji na Lucifer ibilisi Muongo
 
Tatizo lako linaakisi matatizo ya watu wengi sana.......

Unaposoma maandiko halafu ukashindwa kuyaelewa unayatupia maandiko hayo lawama badala ya kuchunguza kama wewe ndiyo hujaelewa na maandiko hayo hayana tatizo kabisa.Ni sawa na wewe uwe umesimama barabarani na jamaa zako wanne ambao wanakuambia kuna gari la rangi ya bluu linapita barabarani na wewe unaendelea kukodoa na hulioni gari hilo,badala ya kufikiria tu kuwa inawezekana macho yako yana matatizo hivyo yanakufanya usilione gari hilo,wewe unakimbilia kusema jamaa zako ni waongo na gari hilo halipo.....

Nimezungumzia dunia flat ya CD,haiwezekani uwe na flat ya namna hiyo halafu kuwe na upande wa pili wa duara.Tatizo nililoliona hapa ni wewe kushindwa kusoma maandiko mengi na kuyaelewa.Kwenye maandiko yangu hapo juu nimezungumzia dunaia duara ya tufe kwa namna tofauti na dunia duara ya CD kwa namna tofauti,nikatoa na mifano. Nadhani mfano wa chungwa ndiyo umekuchanganya kabisa maana niliutoa nikionesha tofauti kati ya duara ya CD na duara ya tufe [chungwa] na uwezekano wa kuuona mti.....

Suala la upande wa pili lilikuwa kwenye duara ya chungwa na siyo duara ya CD.Nilisema mti uliosimikwa kwenye chungwa huwezi kuuona kwenye duara ya chuingwa unapokuwa upande mwingine wa duara ile hata ukitumia chomb cha kuonea mbali lakini, kwenye duara ya CD ambapo hakuna upande wa pili,ukisimika mti kisha ukaenda umbali wa kilomita 10 hutaweza kuuona mti huo pia lakini,ukitumia kifaa cha kuonea mbali unauona.....

Sasa kwa kutumia logic hiyo,meli inapokuwa haionekani kwenye macho yako baada ya kwenda mbali,wale ambao wanasema dunia ni duara ya tufe hudai kuwa unakuwa huioni kwasababu inakuwa imeshapotelea kwenye duara ya dunia hivyo inakuwa kwenye upande mwingine wa duara hiyo.Lakini ukichukua kifaa cha kuonea mbali unaiona meli hiyo.Swali la msingi,je kwanini uione wakati iko kwenye upande mwingine wa duara ya dunia?

Kama dunia ni duara ya tufe usingeweza kuiona meli hiyo na ungeishia kuona maji tu pale yalipopinda lakini ni kinyume chake,meli inaonekana bado na hii inathibitisha kuwa dunia ni flat lakini duara kama CD.Kama vile mti ukiusimika kwenye barabara ya urefu wa kilomota 10,halafu mti ule ukausimika mwanzo wa barabara ile kisha ukaenda umbali huo wa kilomita 10 ukatazama hutaweza kuuona mti ule,hii haimaanishi dunia imepinda kutokana na duara yake kama tufe bali huuoni kwasababu macho yako hayana tu uwezo wa kuona umbali huo.Ukichukua kifaa cha kuonea mbali utauona huo mti bila matatizo yoyote,hii inaonesha kuwa dunia haijapinda bali ni flat.....

Nadhani umenielewa....
Kwa mfano wako huo unataka kuniambia kwamba ukitumia vifaa vya kuona mbali,kama uko mbeya unaweza kuiona dar?na rotation ya jua na mwezi inakuaje kwenye dunia flat yaani jua huwa linazama wapi na hata hivyo dunia ingekuwa ni flat ingefika mahali mtu unakuwa katikati yaani upande mmoja usiku na upande mwingine ni mchana!sasa niambie ishawahi kutokea mtu anakuwa katikati upande mmoja usiku na upande mmoja mchana kwenye dunia ya duara hiki kitu hakiwezekani lakini kwenye flat kinawezekana
 
Angalia live ISS utagundua hayo uliyomeza ni matango pori
 
Na vipi kuhusu kupishana kwa ma saa na siku huku usiku huku mchana au kuna sehem jua hua linajificha???
 
hiyo th



Hiyo theory haikuanza hivi hivi, lengo lake ni kuwapoteza watu wasifahamu kuwa dunia iliumbwa na Mungu mkuu. Kwamba hakuna Mungu duniani na hivyo hata biblia sio kitabu cha kuaminiwa kwa vile biblia inasema Yesu akirudi kila jicho litamuona, kwa hiyo kama kila jicho litamuona dunia ikiwa ya duara wakati anarudi watu wanaoishi upande wa pili hawatamuona. Hivyo biblia ni kitabu cha watu wajinga wa dunia. Nadhani hii ni vita kati ya Mungu muumbaji na Lucifer ibilisi Muongo
Mkuu, umemaliza.
 
Kwa mfano wako huo unataka kuniambia kwamba ukitumia vifaa vya kuona mbali,kama uko mbeya unaweza kuiona dar?na rotation ya jua na mwezi inakuaje kwenye dunia flat yaani jua huwa linazama wapi na hata hivyo dunia ingekuwa ni flat ingefika mahali mtu unakuwa katikati yaani upande mmoja usiku na upande mwingine ni mchana!sasa niambie ishawahi kutokea mtu anakuwa katikati upande mmoja usiku na upande mmoja mchana kwenye dunia ya duara hiki kitu hakiwezekani lakini kwenye flat kinawezekana
Unaona kama hakutakuwa na milima inayokuzuia...

Hiyo hoja yako nyingine imeshajibiwa humu kwenye hii thread,punguza uvivu,soma thread kuna majibu hadi picha inayotembea ipo kuonesha ni namna gani kuna mchana na usiku kwenye dunia flat....
 
Mkuu eiyer labda nikuulize swali dogo tu,kwa mfano unasafiri letsay unaelekea kusini bila kukata kona,kwa dunia yako iliyo kama cd mwisho wake ni wapi?kwa dunia iliyo kama cd ni lazima kutakuwa na mwisho,sasa nataka uniambie mwisho wake ni wapi?
Yote haya yameshajadiliwa kwenye mada hii lakini naona mnaona uvivu kusoma....

Jibu fupi ni kwamba inategemea unaelekea upande upi.Kama unaelekea upande wa South pole utaishia kwenye barafu za kule na hii ni sawa na uelekee north pole...

Kama utaelekea upande tofauti utakuja kuibukia pale pale ulipoanzia safari yako....
 
Yote haya yameshajadiliwa kwenye mada hii lakini naona mnaona uvivu kusoma....

Jibu fupi ni kwamba inategemea unaelekea upande upi.Kama unaelekea upande wa South pole utaishia kwenye barafu za kule na hii ni sawa na uelekee north pole...

Kama utaelekea upande tofauti utakuja kuibukia pale pale ulipoanzia safari yako....
kuna kitu mimi huwa najiuliza lakini sipati jibu...ni jiviii.why ,for the people who know the truth and reality huwa wanaficha mambo??

angalia hata akina Leonado Da vinci,tesla,faraday,mogan,newton na wengine kama Galileo galilei...kwanini walikuwa wanauficha ukweli juu ya siri nzito ya ulimwengu huuu...yani mind you brazaz wanaobisha kuwa dunia iko sijui duara ,yani ukweli ulifichwa ili kila mtu apate kureason the truth behind of everything....

yale yote tunayoyaona ni fiction na delusion as a mirror of reality but not reality...

kuna siri nzito snaa juu ya ukweli wote....mambo mengi sna yamefichwa...

vatcan ina own telescope kubwa ya dunia na ni watu wachache sana wanaoruhusiwa kuingia pale na kuitazama dunia katika 3 dimension state na kisha kutengeneza fiction nyingi snaa juu ya uhalisia ili watu wengi wafe bila kujua ukweli....

lakini pia unapaswa kujiuliza kuwa katika maisha yako ,everythinh can not be put truthly,everything you observe in this universe is half of its truth and reality...

hawawezi weka kila kitu wazi...

vatcan kuna siri nzito snaa pale...

maabara ya dunia ipo pale..na pale wanazalisha genetic editing ,genetic engeneering za hali ya juuu snaa lakini ukweli imefichwa...

vatcan has world and unibersal documents that proves the reality of this universe....

unambiwa hivi Space station ipo chini ya vatcan na kila inachokitoa kinakuwa oposite na ukweli...

kwann vatcan iwe bize kuchunguza mambo ya ulimwengu lakini at the same time wanajificha kutojulikana kuwa wao ndo vinara wa kila kitu lakini wanakomaaa kuwaaminisha watu kuwa mungu yupo..huenda hata uwepo wa shetan na jina mungu ni fiction created kwa lengonla kuwaogopesha watu wasifikilie beyond human nature ili wasiumize akili kiluutafuta ukweli juu ya uumbaji na nguvu inayokontrol kila kitu katika universe hii...

kuna kitu naanza kupata picha juu ya hii kitu...

huenda tunaishi katika ulimwengu ulio na ukweli 100% lakini ukawa imefichwa..

ukitaka kujua kwanini watu wanaojua mambo wanakuwa easily killed or assasinated na highly governing system...??

kuna nini....??

angalia hata akina Leonado da vinci waliuliwa kwa siri sana bada y kuanza kutoa siri nzito za dunia kupitia michoro,angalia mnyama Tesla alikufa kifo cha kutatanisha akadondoka gafla akafa..pale pale wakawahi documents na formula alizokuwa kaandika wakazificha ,unambiwa technology unayoiona sasa hivi ni idea na creativity iliyoachwa na Nicola Tesla...wanachokifanya huwa wanafungua makablasha wanainterprete laws and codes wanaingia kazini wanainvert new things lakini kiukweli everything were hidden to control people...

ukitaka kuamini kuwa mambo mengi ukiyajua ujue kabsa kuwa kuna watu watakutafuta na kukuomba ufanye nao kazi lakinibhapo hapo watakuwa wanachora njama wakuue kabla hujasambaza siri nyinginza dunia...

angalia watu wengi wanaostaafu kufanya kazi kwenye taasiis nyeti wakastaafu tu hawachelewi kupata mitindio ya ubongo au kupooza ubongo kabsaa..
unafikiri ni kwanini....!! they dont want them to expose the reality of the universe...

wakiona wew ni geniuz umeyajua mengi ya ulimwengu huu wanakufanyia kitu kinaitwa ABDUCTION,unarun mental health a kupoteza uwezo wa kukumbuka mengi..

chunguzeni watu wanaostaafu kutoka taasisi za siri ndo mtajua wanapatwa na magonjwa gani....

kwa hiyo mjua kabsaa kuwa there is great secret behind about the power of the universe ,how it regulates its creatures.....
 
Wanasayansi wakikuambia dunia ina umbo la mviringo unawakebehi. Lakini wakivumbua vitu kama internet, computer, na simu za mkononi unatumia huku unachekelea.
Unapenda kusafiri kwa raha kwa gari lako na hata angani kwa ndege lakini ukielezwa kuhusu gravity unasema ni u-Freemason na Illuminati au Jesuit.
Wewe ni kama yule mama mzee wa UK aliekuwa anapenda sana chai huku akipinga kitendo cha mabaharia wa Uingereza kuvuka bahari kwenda India.
Naona ukweli fulani kuhusu kile alichosema Dr Watson kuhusu akili za watu weusi.
 
Mimi nawaambia dunia ni shimo....!
-----
Wala siyo flat. Kulijua hili, ni kupanda vindege vidogo wakati wa clear sky (hakuna mawingu) na kindege hicho kiruke futi zaidi ya elfu 25 katika eneo la bahari. Chungulia dirishani na utazame chini karibu kabisa na usawa wa ndege hiyo. Kisha anza kutazama hapo na kuelekea upande wa upeo wa macho yako kwa msitari fikirishi ulionyooka. Kwa haraka utagundua dunia ni shimo. Tena shimo la mviringo.

Kama ni suala kupiga kura, juu ya post ya kwanza ongeza kipengere kingine cha dunia ni shimo.
 
Mimi nawaambia dunia ni shimo....!
-----
Wala siyo flat. Kulijua hili, ni kupanda vindege vidogo wakati wa clear sky (hakuna mawingu) na kindege hicho kiruke futi zaidi ya elfu 25 katika eneo la bahari. Chungulia dirishani na utazame chini karibu kabisa na usawa wa ndege hiyo. Kisha anza kutazama hapo na kuelekea upande wa upeo wa macho yako kwa msitari fikirishi ulionyooka. Kwa haraka utagundua dunia ni shimo. Tena shimo la mviringo.

Kama ni suala kupiga kura, juu ya post ya kwanza ongeza kipengere kingine cha dunia ni shimo.
Hahahahaa dah
 
Hao watu 25 waliosema dunia ni tambarare nadhani bado wanaishi kwenye conspiracies sana. 😵
 
Kwa mfano wako huo unataka kuniambia kwamba ukitumia vifaa vya kuona mbali,kama uko mbeya unaweza kuiona dar?na rotation ya jua na mwezi inakuaje kwenye dunia flat yaani jua huwa linazama wapi na hata hivyo dunia ingekuwa ni flat ingefika mahali mtu unakuwa katikati yaani upande mmoja usiku na upande mwingine ni mchana!sasa niambie ishawahi kutokea mtu anakuwa katikati upande mmoja usiku na upande mmoja mchana kwenye dunia ya duara hiki kitu hakiwezekani lakini kwenye flat kinawezekana
Nikisimama Skanska Dar maeneo ya tegeta nitumie darubini kali bado zanzibar siioni. Hata nikipanda floor ya juu Kibo complex bado zenji haionekani hata kwa darubini ila something ineresting unaona boat ikitokea kwa chini.
 
Back
Top Bottom