Kama Dunia ni Tufe linalozunguka 👉🏼 🌍 kwanini large water bodies kama vile bahari na maziwa yana appear flat and level,......?
Ingekuwa flat ungeona to infinity, hauoni to infinity kwa sababu haipo flat kuna mfano ulipewa wa taa za zanzibar ukiwa kwenye pwani ya dar. Hazionekani ukiwa kwenye pwani ya bahari ila zinaonekana ukiwa juu ya jengo refu.
Na hiyo haitoshi,.....ni kipi kinachoshikilia maji yasimwagike away from Dunia Tufe ikiwa Dunia yenye umbo la namna hiyo inazunguka Kwa Kasi mno.
Je, kuna uthibitisho wowote unaoonyesha namna maji yanavyoshikiliwa kwenye dunia Tufe linalozunguka,... apart from nadharia?
Kinachoshikilia maji yasimwagike ndo hicho hicho kinachoshikilia vitu vyote visimwagike.
Kwa bajeti ya chini ya 100000/- unaweza kufanya experimentation nyumbani kwako zinazoweza kukuonesha ni vipi dunia ingebehave kama ingekua tufe au sahani.
Katika baadhi ya taaluma, kitu kinachoitwa simulation ni muhimu sana hasa kwenye kupunguza cost, kusave time na kuzuia ajali.
Badala ya kutegeneza kitu katika scale yake unategeneza katika small scale, unajifunza kinavyofanya kazi, baada ya hapo unaweza kuscale up. Tabia za dunia zinaweza kuwa simulated kwa bajeti chini ya 100000/-
Gravitational constant, radius ya dunia unaweza hata wewe kuzitafuta kwa kupitia experiment utakazoamua kuzifanya. Jana nimejifunza kuwa hata latitude yako unaweza kuipata kwa measurement pekee.
Nasa sio wagunduzi wa shape ya dunia, shape ya sphere imekuwa ikijulikana tangu miaka 2000 iliyopita, kuna nchi nyingi sana zilizoweza kutoka nje ya dunia au kurusha vifaa nje ya dunia hazina sababu ya msingi ya kuendeleza uongo.
Mkuu nakushauri panga safari ya kwenda Antarctica, kule utapa majibu ya maswali yako.
Ps:
kuna nchi huko ambazo jua halizami kwa miezi kadhaa na likizama halichomozi kwa miezi kadhaa
kuna website huko ambayo inauwezo wa kusema ni nyota zipi zinaweza kuonekana leo kulingana na location yako, eclipses na kadhalika.