Siri nne za mafanikio 2024: Vitu ambavyo matajiri hawawezi kukwambia

Babyloni

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2020
Posts
264
Reaction score
740
Ndugu Msomaji,

Leo Nataka Nikuibie Siri ya MATAJIRI Wengi Ambayo Hawataki Uijue Kuhusu Mafanikio.

Binafsi Siri Hii Nilijifunza 2020 Kutoka Kwa Mentor Wangu Dan Lok.

Kitu Ambacho Kilibadilisha Kabisa Mwelekeo wa Maisha Yangu Mpaka Leo.

Dan Lok Alifanya Utafiti wa Kisiri na Akagundua Kwamba:

"MATAJIRI Wote Unaowajua Wanawekeza Muda Wao na Pesa Zao Nyingi Kwenye Vitu Hivi VINNE:

  1. TAARIFA
  2. EXPOSURE (Kusafiri)
  3. MAZINGIRA
  4. WATU
Kwa Wale Ambao Hawamjui Dan Lok Huyu ni Mjasiriamali na Copywriter Mkubwa Anayeishi Vancouver-Canada.

Forbes Wanamkadiria Kuwa na Utajiri wa $80M.

Ngoja Nielezee Point Moja baada ya Nyingine Hapa Chini:

1. TAARIFA!​

Matajiri Wote Wanajua Kwamba:

Pesa Hazitafutwi Bali ZINATEGWA na Kukusanywa Kutoka Kwenye Mifuko ya Watu Wengine.

Na Kitu Peke Chenye Uwezo wa Kunasa Pesa kama Sumaku Kutoka Kwenye Mifuko ya Watu Wengine ni TAARIFA na Ujuzi.

Ndio Maana Huwezi Kumkuta Tajiri Yupo Busy na Kutafuta Hela kama Masikini.

Matajiri Wote Huwa Wapo Busy Kutafuta TAARIFA Kutoka Kwenye Vyanzo Mbali Mbali Ikiwemo:

  • Vitabu
  • Courses
  • Coaching
  • Mentorship Nk
Hakuna Tajiri Anayewaza Mara Mbili Kuwekeza Kwenye TAARIFA.

...na Ukifanya Utafiti Utakuta Kila Tajiri Ana Shelfu ya Vitabu Nyumbani Kwake...(Bookshelf).

Na Masikini Yeye Ana TV Kubwa na Yupo Busy Kutafuta Hela.

2. EXPOSURE (Kusafiri)​

Hakuna Kitu Chenye Uwezo wa Kubadilisha MINDSET Yako kama Kukiona Kitu Kwa Macho.

Matajiri Wengi Huwa ni Watu wa Kusafiri Mara Kwa Mara Ili Kununua Experience Inayoitwa "EXPOSURE".

Kusafiri ni Mojawapo ya Njia ya Uhakika ya Kujifunza Vitu Kwa Vitendo.

...na Sio Lazima Uende Nje ya Nchi Hata Ndani ya Nchi, Kuna Mikoa Ukienda Huwezi Kuwa Yule Yule.

Kwahiyo:

Nunua Exposure Kwa Gharama Yoyote Ile.

...Hii Pia Inaongeza CONFIDENCE na Kukufanya Ufikiri Kwa Kina Zaidi Kuhusu Biashara na Maisha Kwa Ujumla.

3. MAZINGIRA​

Ukweli Ambao Watu Wengi Hawaujui ni Kwamba:

Sisi ni Zao la Mazingira Yetu Wenyewe.

Mazingira Unayotumia Muda Mwingi Ndio Yatakayokutengeneza Wewe wa Baadae.

Ukisikia Neno MASAKI Unapata Picha ya Watu Gani Wanaoishi Huko?

Ndio Upo Sahihi... ni MATAJIRI.

Kwahiyo:

Sikwambii Ukaishi Masaki Leo Ila...

Kuwa Makini Sana na Mazingira Unayoishi na Kutumia Muda Wako Mwingi Kwasababu Yanakutengeneza Wewe wa Miaka Kadhaa Ijayo.

4. WATU​

Wote Tunajua Kwamba:

Tupo Kwenye Dunia ya Watu...na Watu Ndio Wenye Pesa Sio Vitu.

Na Hapa Sizungumzii Watu kama Watu... Nazungumzia Watu SAHIHI.

Kwasababu...

Sio Kila Mtu ni Sahihi Kwako.

Ukweli Mchungu Kuhusu Watu ni Kwamba:

"Wewe ni Wastani wa Watu 5 Unaotumia Muda Mwingi Kuwa Nao".

Mfano:

Kama Muda Wako Mwingi Unatumia Kukaa na Matajiri 9...

Basi Wewe Utakuwa Tajiri wa 10 Muda Sio Mrefu.

Hivyo Hivyo Pia kama Unatumia Muda Mwingi Kukaa na Masikini Ambao Muda Mwingi Wao ni Kulalamika na Kulaumu Serikali na Kubishana Kuhusu Simba na Yanga...Basi Tegemea Kuwa Masikini Ajaye Pia.

....Na Hii ni FACT!

Kwanini Nakwambia Yote Haya?​

Kwasababu:

Wengi Huwa Tunakuja Kushtuka Wakati Ambao Tayari ni "TOO LATE".

Tafito Zinasema:

"Watu Wengi Wanakujaga Kushtuka Kuhusu Vitu Hivi Wakiwa na Umri wa Miaka 57-69".

Wanaishia Kupata Pressure na Depression na Wengine Hata Kupoteza Maisha.

Wanakuwa Hawana Chochote Cha Kubadilisha Kutokana na Nguvu na MUDA Kuatupa Mkono.

Kwahiyo:

Epuka Kunaswa Kwenye Huo Mtego!

Hakuna Kitu Kinachoumiza Uzeeni kama MAJUTO (Regrets).

Chukua Hatua Sasahivi!

Nina Imani Makala Hii Itaenda Kumgusa Mtu Mahali.

Uwe na Mwanzo Mwema wa Wiki.

Ciao!

Your Cousin,​

Amosi Nyanda
 
Utajiri ni siri.
Screenshot_20240505-132725~2.jpg
 
1. Dan Lok ni tapeli mkubwa. Hilo lipo wazi anaishi kwa kuuza kozi za kufundisha jinsi ya kuwa tajiri

2. Huo ujinga wa kwamba matajiri wanasoma sana vitabu mnautoa wapi? Kwamba Mark alisoma kitabu flani kikamuambia aanzishe facebook?

Yaani maisha ni marahisi kiasi hicho, usome kitabu tu uwe tajiri? Pole sana.

Mimi kapuku ila hapa unatupiga kamba
 
Uzi mzuri sana💥, ila na hitaji kujua umejuaje Siri za matajiri?? Pia, unesema mwenyew kuwa ni vitu ambavyo matajiri hawawez kukwambia so, wewe alie kwambia ni nani??
Au wewe ni Nani??
Tokea nisikie Kuna mtu aliandika kitabu chenye mbinu zote za how to get money then akashindwa kukitoa kitabu hicho kwa kukosa hela ya kuchapisha nachoshwa kabisa nikiwasikia ma motivational speakers Otherwise hio thread angeituma MO au Bakhrhesa
Nakaribisha makasiriko 🤝😎
 
1. Dan Lok ni tapeli mkubwa. Hilo lipo wazi anaishi kwa kuuza kozi za kufundisha jinsi ya kuwa tajiri

2. Huo ujinga wa kwamba matajiri wanasoma sana vitabu mnautoa wapi? Kwamba Mark alisoma kitabu flani kikamuambia aanzishe facebook?

Yaani maisha ni marahisi kiasi hicho, usome kitabu tu uwe tajiri? Pole sana.

Mimi kapuku ila hapa unatupiga kamba
Nilitegemea hii comment kwa sababu mswahili muambie yoootee but isiwe kusoma,yuko tayari hata afungwe jela lakini siyo kuambiwa asome vitabu 50 kwa mwaka mzima. Lakini ukweli utabaki kuwa ukweli maarifa yote yako duniani na yako kwenye vitabu. Mataifa yote yaliyopiga hatua na yenye jamii zenye furaha kama Scandinavian countries wamesoma na wanapenda kusoma.
 
Ukweli mchungu ni kwamba sisi ni mijitu mivivu sana katika suala zima la kuongeza maarifa kwa njia ya kujisomea vitabu! Ukitaka ugomvi na mtanzania, mwambie asome vitabu!
 
Nilitegemea hii comment kwa sababu mswahili muambie yoootee but isiwe kusoma,yuko tayari hata afungwe jela lakini siyo kuambiwa asome vitabu 50 kwa mwaka mzima. Lakini ukweli utabaki kuwa ukweli maarifa yote yako duniani na yako kwenye vitabu. Mataifa yote yaliyopiga hatua na yenye jamii zenye furaha kama Scandinavian countries wamesoma na wanapenda kusoma.
Na mimi nimeuliza hivi; Kuanzisha na kukuza kampuni kisha kujipatia utajiri kunafundishwa kwenye kitabu gani?

Maanake billionaires wapo kwenye 3000 tu, au hicho kitabu kimefichwa?

Matajiri wengi wamezaliwa kwenye familia nzuri/waliweza kujichanganya na watu wenye ushawishi kwa namna flani mfano kusoma vyuo vikubwa nk.

Vitabu ni biashara, havitolewi bure

Unadhani benjamin fernandes wa nala angeweza kupata $40m kwa kusoma sana vitabu badala ya kwenda stanford na harvard?

Kaa chini tu ufuatilie. Utajiri ni aidha uwe na connections, ama uwe mjuzi sana kwenye fani flani(ambapo lazima uende shule)

Kwenda ivy league school tu mfano stanford kunabadilisha maisha ya mtu KABISA. Unakutana na watu wazito mule unafahamiana nao. Unakubalika na makampuni makubwa kikazi. Unakuwa an international citizen.

Pia kuna ile bahati ya kuwa sehemu sahihi wakati sahihi ukifanya kitu sahihi sema haitabiriki mfano netflix alivyoleta movie streaming...

Unavyosema ukanda wa scandinavia wana maisha mazuri kisa wanasoma vitabu, kweli mkuu tunaweza kujadili maendeleo ya nchi kwa hoja ya kusoma vitabu peke yake? kweli? serikali, uchumi havina mchango?

Nimemaliza kufoka sasa.
 
Ndugu Msomaji,

Leo Nataka Nikuibie Siri ya MATAJIRI Wengi Ambayo Hawataki Uijue Kuhusu Mafanikio.

Binafsi Siri Hii Nilijifunza 2020 Kutoka Kwa Mentor Wangu Dan Lok.

Kitu Ambacho Kilibadilisha Kabisa Mwelekeo wa Maisha Yangu Mpaka Leo.

Dan Lok Alifanya Utafiti wa Kisiri na Akagundua Kwamba:

"MATAJIRI Wote Unaowajua Wanawekeza Muda Wao na Pesa Zao Nyingi Kwenye Vitu Hivi VINNE:

  1. TAARIFA
  2. EXPOSURE (Kusafiri)
  3. MAZINGIRA
  4. WATU
Kwa Wale Ambao Hawamjui Dan Lok Huyu ni Mjasiriamali na Copywriter Mkubwa Anayeishi Vancouver-Canada.

Forbes Wanamkadiria Kuwa na Utajiri wa $80M.

Ngoja Nielezee Point Moja baada ya Nyingine Hapa Chini:

1. TAARIFA!​

Matajiri Wote Wanajua Kwamba:

Pesa Hazitafutwi Bali ZINATEGWA na Kukusanywa Kutoka Kwenye Mifuko ya Watu Wengine.

Na Kitu Peke Chenye Uwezo wa Kunasa Pesa kama Sumaku Kutoka Kwenye Mifuko ya Watu Wengine ni TAARIFA na Ujuzi.

Ndio Maana Huwezi Kumkuta Tajiri Yupo Busy na Kutafuta Hela kama Masikini.

Matajiri Wote Huwa Wapo Busy Kutafuta TAARIFA Kutoka Kwenye Vyanzo Mbali Mbali Ikiwemo:

  • Vitabu
  • Courses
  • Coaching
  • Mentorship Nk
Hakuna Tajiri Anayewaza Mara Mbili Kuwekeza Kwenye TAARIFA.

...na Ukifanya Utafiti Utakuta Kila Tajiri Ana Shelfu ya Vitabu Nyumbani Kwake...(Bookshelf).

Na Masikini Yeye Ana TV Kubwa na Yupo Busy Kutafuta Hela.

2. EXPOSURE (Kusafiri)​

Hakuna Kitu Chenye Uwezo wa Kubadilisha MINDSET Yako kama Kukiona Kitu Kwa Macho.

Matajiri Wengi Huwa ni Watu wa Kusafiri Mara Kwa Mara Ili Kununua Experience Inayoitwa "EXPOSURE".

Kusafiri ni Mojawapo ya Njia ya Uhakika ya Kujifunza Vitu Kwa Vitendo.

...na Sio Lazima Uende Nje ya Nchi Hata Ndani ya Nchi, Kuna Mikoa Ukienda Huwezi Kuwa Yule Yule.

Kwahiyo:

Nunua Exposure Kwa Gharama Yoyote Ile.

...Hii Pia Inaongeza CONFIDENCE na Kukufanya Ufikiri Kwa Kina Zaidi Kuhusu Biashara na Maisha Kwa Ujumla.

3. MAZINGIRA​

Ukweli Ambao Watu Wengi Hawaujui ni Kwamba:

Sisi ni Zao la Mazingira Yetu Wenyewe.

Mazingira Unayotumia Muda Mwingi Ndio Yatakayokutengeneza Wewe wa Baadae.

Ukisikia Neno MASAKI Unapata Picha ya Watu Gani Wanaoishi Huko?

Ndio Upo Sahihi... ni MATAJIRI.

Kwahiyo:

Sikwambii Ukaishi Masaki Leo Ila...

Kuwa Makini Sana na Mazingira Unayoishi na Kutumia Muda Wako Mwingi Kwasababu Yanakutengeneza Wewe wa Miaka Kadhaa Ijayo.

4. WATU​

Wote Tunajua Kwamba:

Tupo Kwenye Dunia ya Watu...na Watu Ndio Wenye Pesa Sio Vitu.

Na Hapa Sizungumzii Watu kama Watu... Nazungumzia Watu SAHIHI.

Kwasababu...

Sio Kila Mtu ni Sahihi Kwako.

Ukweli Mchungu Kuhusu Watu ni Kwamba:

"Wewe ni Wastani wa Watu 5 Unaotumia Muda Mwingi Kuwa Nao".

Mfano:

Kama Muda Wako Mwingi Unatumia Kukaa na Matajiri 9...

Basi Wewe Utakuwa Tajiri wa 10 Muda Sio Mrefu.

Hivyo Hivyo Pia kama Unatumia Muda Mwingi Kukaa na Masikini Ambao Muda Mwingi Wao ni Kulalamika na Kulaumu Serikali na Kubishana Kuhusu Simba na Yanga...Basi Tegemea Kuwa Masikini Ajaye Pia.

....Na Hii ni FACT!

Kwanini Nakwambia Yote Haya?​

Kwasababu:

Wengi Huwa Tunakuja Kushtuka Wakati Ambao Tayari ni "TOO LATE".

Tafito Zinasema:

"Watu Wengi Wanakujaga Kushtuka Kuhusu Vitu Hivi Wakiwa na Umri wa Miaka 57-69".

Wanaishia Kupata Pressure na Depression na Wengine Hata Kupoteza Maisha.

Wanakuwa Hawana Chochote Cha Kubadilisha Kutokana na Nguvu na MUDA Kuatupa Mkono.

Kwahiyo:

Epuka Kunaswa Kwenye Huo Mtego!

Hakuna Kitu Kinachoumiza Uzeeni kama MAJUTO (Regrets).

Chukua Hatua Sasahivi!

Nina Imani Makala Hii Itaenda Kumgusa Mtu Mahali.

Uwe na Mwanzo Mwema wa Wiki.

Ciao!

Your Cousin,​

Amosi Nyanda
Sikatai wala sikubali
Ingekuwa KWELI....usingeiweka hapa....
 
Back
Top Bottom