mshamba_mwingine
JF-Expert Member
- Jul 23, 2023
- 1,057
- 4,145
Dan Lok ni tapeli. Anatengeneza umaarufu feki ili auzie watu kozi, aliwahi kukamatwa akidai nyumba aliyokodisha ni yake.Nilivyomuelewa huyo jamaa ni Kwamba kitabu ni njia inayotumiwa na watu wengi kupata taarifa ya vitu fulani fulani Ila pia kuna njia nyingi zakupata taarifa ukiachana na Vitabu, huyo Dan Lok anauza kozi za copywritting kwasababu alikua na taarifa Kwamba hiki nikikifanya lazima watu waje wanipe pesa, rejea kwenye huo uzi kwamba matajiri huwa wanatega pesa Kwa kuuza taarifa yaani wanachukua pesa mfukoni mwa watu wanaingiza mfukoni mwao ndicho anachofanya huyo Dan Lok.
Hata huyo jamaa wa Facebook nae tunabaki hapo hapo kwenye taarifa, Mark hakuwa na lengo lakuifanya Facebook iwe ni product ya worldwide ila lengo lilikua ni pale pale havard kwamba watu wawe wanapost profile zao kuchat na kadhalika, na hii hakuifanya tu bali lazima alikaa chini akajiuliza kitu ambacho pale chuoni hakipo na endapo akikifanya kitapendwa na wanafunzi wenzie, kwahiyo kitendo tu chakujiuliza it means unatafuta taarifa iwe kwakusoma vitabu vya projects mbalimbali ambazo tayari zilishawahi kufanyika hapo shuleni au kuuliza maswali na kadhalika.
Na pia unatakiwa ufahamu kwamba taarifa za kwenye vitabu huwa haziji direct kwamfano wewe unataka ufanye uvumbuzi wa jambo fulani ambalo litaleta effect duniani kote basi lazima utachukua vitabu vya vumbuzi mbalimbali zilizowahi kufanyika duniani na kuanza kusoma ili ujue kipi kimeshafanyika then baada ya kujua yaliyowahi kufanyika nawewe unakaa chini unaanza kufigure out like jambo gani ambalo halijawahi kufanyika ila unauhakika ukilifanya lazima watu watalikubali duniani kote... TAARIFA NDIO MSINGI.
Mimi najua vitabu mnavyoongelea hapa ni vitabu vya motivation sijawahi kuona mtu anasoma kitabu cha physics eti anaongeza maarifa😂
Sikatazi watu kusoma vitabu, inaweza kuwa hobby ukapata mitazamo mbalimbali itakayokusaidia kwenye maisha lakini wewe jiulize hao walioandika hivyo vitabu wametoa wapi hayo maarifa kama sio kwenye maisha halisi
Kama unasomaga vitabu vya physics, biology basi sikupingi