Siri nne za mafanikio 2024: Vitu ambavyo matajiri hawawezi kukwambia

Narudia hakuna jamii zilizoendelea na kustaarabika bila kusoma, hata huyo Nala amesoma vitabu ili kuelewa jinsi ya kuendesha biashara zake. Matajiri wengi wanaajiri experts ambao ni wasomi ili waweze kuwashauri kitaalamu. Ukimuangalia hata Elon Musk vitu vyake vingi vinahitaji akili na kusoma sanaa maana vingi ni science based. Sasa tukirudi kwenye maisha yetu ya kila siku kuanzia kula, kuvaa, kufanya kazi, kilimo, mifugo etc vyote vinefanyiwa tafiti na viko kwenye vitabu. Huna haja ya kusumbua watu kama akina prof Janabi na wengine kupoteza muda kuwaambia daily madhara ya kula hovyo, kunywa pombe hovyo, njia bora za kilimo, kufuga nk vyote hivi viko kwenye vitabu na tafiti mbalimbali. Juzi Mhe Rais akiwa mikoa ya Katavi na Rukwa amekuta tatizo kubwa la utapiamlo wakati mikoa hiyo inaongoza kuzalisha chakula, pia amekuta mahospitalini wanaojifungua ni vitoto miaka 17 , yaani mtoto ana mtoto. Hii yote ni tatizo la elimu, watu hawana maarifa na hawataki kusoma na kujifunza. Ndiyo nikasema huko Scandinavian huwezi kukuta haya mambo kwa sababu jamii imeelimika na inapenda kusoma na kujielimisha zaidi. Hata huko Kenya hawa Gen Z wanaomnyima usingizi Ruto ni wasomi wazuri sana na wanajua their rights.
 
Utajiri unaendana na kufanya mambo yasiyo halali ndiyo maana ni siri. Sasa sijui yeye kajuaje
 
Tuambie matajiri wa Tanzania wanasoma vitabu gani?

Yaani unaanza

1)Mo Dewji,

Vitabu alivyosoma vikampa utajiri


2) Bakhresa
Vitabu vyake alivyosoma vikampa utajiri

3) GSM
.........



Halafu ni kipi kinaanza Kati ya utajiri na kusoma vitabu?


Yaani hao matajiri walianza kuvisoma ndio wakapata utajiri au walipata utajiri ndio wakavisoma?
 
Asante kwa ushauri..

Ila hasa Kariakoo, hatujuwi Wakinga, Wachaga, Machinga wa kila kabila, Watanzania wenzetu wa asili ya Asia na Uarabuni wangapi wesoma vitabu vingapi, kusafiri mpaka wamefanikiwa vile?!
Ila tunakubali, mazingira unayoishi nayoishi, elimu utakapoipata na taarifa yawezekana kuwa sababu ya utajiri wako!
All and all tunakushukuru kwa uzi wako ulivyo debatable! Na ndio maana ya wadau kuja JamiiForums ๐Ÿ‘๐Ÿ‘๐Ÿ‘๐Ÿ‘๐Ÿ‘
 
Hongera coz your copywritting skills inaonekana but I want to ask this, Kwa introverts inakuaje kwenye hiko kipengele Cha watu?.

We know Dan that Asian guy.
 
Rudia kuusoma tena huo uzi, amekwambia mentor wake ambae ni Dan anaekadiriwa Kuwa na Utajiri wa $80M amefanya utafiti then hizo data kaamua kushare na hao clients wake na katika hao client wake huyo bwana aliyeleta uzi nae yumo ndani.
 
Nilivyomuelewa huyo jamaa ni Kwamba kitabu ni njia inayotumiwa na watu wengi kupata taarifa ya vitu fulani fulani Ila pia kuna njia nyingi zakupata taarifa ukiachana na Vitabu, huyo Dan Lok anauza kozi za copywritting kwasababu alikua na taarifa Kwamba hiki nikikifanya lazima watu waje wanipe pesa, rejea kwenye huo uzi kwamba matajiri huwa wanatega pesa Kwa kuuza taarifa yaani wanachukua pesa mfukoni mwa watu wanaingiza mfukoni mwao ndicho anachofanya huyo Dan Lok.

Hata huyo jamaa wa Facebook nae tunabaki hapo hapo kwenye taarifa, Mark hakuwa na lengo lakuifanya Facebook iwe ni product ya worldwide ila lengo lilikua ni pale pale havard kwamba watu wawe wanapost profile zao kuchat na kadhalika, na hii hakuifanya tu bali lazima alikaa chini akajiuliza kitu ambacho pale chuoni hakipo na endapo akikifanya kitapendwa na wanafunzi wenzie, kwahiyo kitendo tu chakujiuliza it means unatafuta taarifa iwe kwakusoma vitabu vya projects mbalimbali ambazo tayari zilishawahi kufanyika hapo shuleni au kuuliza maswali na kadhalika.

Na pia unatakiwa ufahamu kwamba taarifa za kwenye vitabu huwa haziji direct kwamfano wewe unataka ufanye uvumbuzi wa jambo fulani ambalo litaleta effect duniani kote basi lazima utachukua vitabu vya vumbuzi mbalimbali zilizowahi kufanyika duniani na kuanza kusoma ili ujue kipi kimeshafanyika then baada ya kujua yaliyowahi kufanyika nawewe unakaa chini unaanza kufigure out like jambo gani ambalo halijawahi kufanyika ila unauhakika ukilifanya lazima watu watalikubali duniani kote... TAARIFA NDIO MSINGI.
 
Shukran Nyanda
 
Uchumi wa Canada upo juu kuliko Tanzania kwahiyo kuwa tajiri Canada ni rahisi kuliko Tanzania kwasababu kuna mazingira rafiki ya mtu kupata pesa
Canada unaweza kuandika kitabu ukakiweka kwenye mtandao, watu wakanunua hicho kitabu kutoka mataifa mbalimbali kwa paypal na muandishi akapokea pesa kutoka paypal na akaitoa na kuitumia. Tanzania inawezekana kupokea pesa kutoka paypal?
Maisha siyo kusoma vitabu vya kiingereza vya nje kisha uwe tajiri Afrika
 
Inawezekana hizi nondo zote unazijua lakini hata ist huna sasa sijui unakwama wapi john kisomo.............ndio waafrika tumelogwa??........maana haya yote unayajua umeishia kumiliki I phone macho 3 basi sasa shida hiko wapi?
 
Utajiri haupatikani kwa kusoma vitabu vya kiingereza vilivyoandikwa nje kisha uwe tajiri Africa๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜
Uchumi wa Canada ni mkubwa kuliko Tanzania hata mazingira ya kiuchumi Canada ni rafiki ya kuwa tajiri.
Mfano. Mtu anaishi Canada ni programmer, anaweza kutengeneza program au application akaiuza duniani na akapokea pesa kutoka paypal. Hapa Tanzania unaweza kupokea pesa kutoka paypal?
Utajiri haufundishwi kwasababu hata wewe pamoja na kusoma vitabu ukaishia kuwa masikini
 
Upo sahihi ila relevance ndio inakosekana, kiufupi njia za kuwa tajiri Tanzania ziko clear kabisa na miongoni mwa hizo njia kusoma vitabu sio mojawapo. Ntakutajia chache tu.

1.Kuwa na kipaji kikubwa cha sanaa ama michezo hasa mpira na muziki. Kupitia sanaa hizo na mikataba ya matangazo wengi hutajirika.

2.Kujihusisha na shughuli za kisiasa mfano uwe mbunge, waziri n.k kutumia wadhifa huo kujitajirisha.

3.Kujihusisha na biashara mbalimbali ila uwe mzuri kwenye utakatishaji fedha, utapeli, ukwepaji kodi na kutoa rushwa kwa mamlaka mbalimbali.

4.Kufungua makanisa ya kiroho na kutumia nguvu za ziada kuvuta watu kwa miujiza na shuhuda na kuwakamua pesa zao. Kutumiwa na matajiri kutakatisha fedha.

5.Kuanzisha miradi mikubwa na kuvuta investors kwenye mradi kisha kuwatapeli. Mf mr kuku, kilimo cha vanilla, mradi wa nguruwe.

Zipo nyingi ila hizo ni top five models
 
Maskini hujifanya kuwajua sana matajiri kumbe h

Rudia kuusoma tena huo uzi, amekwambia mentor wake ambae ni Dan anaekadiriwa Kuwa na Utajiri wa $80M amefanya utafiti then hizo data kaamua kushare na hao clients wake na katika hao client wake huyo bwana aliyeleta uzi nae yumo ndani.
Ninachojua ni kwamba matajiri hawana muda wa kupiga huo umbea๐Ÿ˜Ž๐Ÿšฎ
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ