Siri nne za mafanikio 2024: Vitu ambavyo matajiri hawawezi kukwambia

Dan Lok ni tapeli. Anatengeneza umaarufu feki ili auzie watu kozi, aliwahi kukamatwa akidai nyumba aliyokodisha ni yake.

Mimi najua vitabu mnavyoongelea hapa ni vitabu vya motivation sijawahi kuona mtu anasoma kitabu cha physics eti anaongeza maarifa😂

Sikatazi watu kusoma vitabu, inaweza kuwa hobby ukapata mitazamo mbalimbali itakayokusaidia kwenye maisha lakini wewe jiulize hao walioandika hivyo vitabu wametoa wapi hayo maarifa kama sio kwenye maisha halisi

Kama unasomaga vitabu vya physics, biology basi sikupingi
 
Mkuu wewe unaongelea elimu au kusoma vitabu??

Naona hapa umechanganya mambo kibao. Unaweza kua na elimu ila usiwe mpenzi wa kusoma vitabu.
Hapo naona unaongelea elimu zaidi na sio kusoma vitabu.

Na kusoma vitabu huwa ni kipaji tu, mwingine akishika tu kitabu usingizi huoo.
Na njia za maarifa zimerahisishwa sana siku hizi, sio kila kitu utapata kwenye vitabu.
 
Basi mimi sikukuelewa vizuri

Huko mitandaoni ukiona wanakuambia usome vitabu watakupendekezea vitabu vyepesi vile vya ushauri wa maisha kama rich dad poor dad na vingine😂 eti vitabadilisha jinsi unavyofikiri

Kweli kabisa kila mtu anasoma vitabu shida anasoma vitabu gani

Na pia kuwa na akili ya kukosoa mambo(inquisitive mind) itakufanya ukue vingi hata nje ya kusoma vitabu
 
Hapa Tanganyika unaweza kukutwa na B7 ndani na husomi vitabu vyovyote.

Achana na vitabu, ni huko nje hapa kwetu ingia kwenye mfumo. Ajira, siasa au biashara na watu walio kwenye mfumo.
 
Kama ni mpenzi wa kusoma vitabu wala hauhitaji mtu wa mtandaoni akuchagulie vitabu mkuu...
 
Ukweli mchungu ni kwamba sisi ni mijitu mivivu sana katika suala zima la kuongeza maarifa kwa njia ya kujisomea vitabu! Ukitaka ugomvi na mtanzania, mwambie asome vitabu!
Swadakta mkuuu...tunapenda short cut mfano utawasikia ukibeti unatoboa lakini tuliosoma statistics hasa kwenye probability tunajua kwamba msingi mkuu ni kwamba mcheze watu 1000 mliwe halafu pesa yenu itumike kulipa watu 10 au 20.....kwenda kwenye maombi kwa manabii feki wa mchango, ambao wanawaambia ili ufanikiwe nunua mafuta/maji/toa ulichonacho etc lakini ili yeye afanikiwe awe na gari eti lazima wote mumchangie ....yaani orodha ni ndefu sanaaa...Mwanaume shababi mwenye siha yake kamilifu na mke na watoto eti anaishi kwa kuwa Chawa mpaka anadhalilika ili arushiwe makombo na anayemfanyia uchawa,na jamii inaona sawa kabisa kwamba ametoboa kweli??? Madhara yake?? Halafu baadae tunawalaumu mabeberu kutuletea ushoga really??
 
Kama ni ivyo utajiri si ungekuwa simple tu! After all tukiwa wote matajiri hainogi
 
Mark aliwaibia watu wawili software ambayo ndio msingi wa facebook
 
Utajiri ni asili..kama huna kamwe hutakuwa hata ufanyaje? ...dan lok ni mwehu tuu...thread nyepesi inapewa hongera haswa..hii ni dalili ya umasikini
 
Matajiri wengi wansoma vitabu baada ya huo utajiri kuupata kwanza
 
Rudia kuusoma tena huo uzi, amekwambia mentor wake ambae ni Dan anaekadiriwa Kuwa na Utajiri wa $80M amefanya utafiti then hizo data kaamua kushare na hao clients wake na katika hao client wake huyo bwana aliyeleta uzi nae yumo ndani.
Noma sana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…