safuher
JF-Expert Member
- Feb 11, 2019
- 11,837
- 17,412
Umeshawahi kujiuliza kwa nini kuna jamaa mke wake unamuona wa kawaida sana lakini wanaishi kwa amani kabisa na wanapendana?
Ni kwa sababu wamekuwa marafiki ndani ya ndoa, siri ya rafiki hata awe mbaya kiasi gani hauwezi kuchagua sura yake akiwa mshkaji ndio mshkaji huyo.
Kuna watu wana marafiki ambao hawataki wenza wao wawe kama marafiki zao. Mtu ana rafiki mlemavu lakini hataki mwenza wake awe mlemavu, Mtu ana rafiki kipofu lakini hataki awe na mwenza kipofu, mtu ana rafiki mzee saana lakini hataki mwenza wake awe mzee.
Hii ni kwa sababu urafiki una nguvu ya kuwaunganisha watu kwa muda mrefu kuliko ngono yenyewe. Lakini pia jiulize kwamba mbona suala la urafiki inawezekana kuwa watu wa jinsia moja wakawa marafiki?
Kuonesha namna ambavyo urafiki una nguvu kubwa ya kuwaunganisha watu na kuwafanya waendelee kuwa wamoja. Mwanandoa mwenzio anapokuwa rafiki yako kuna uwezekano mkubwa sana wa nyinyi kuishi kwa muda mrefu katika ndoa yenu kwa sababu ndoa yenu imeunganishwa na jambo la urafiki ndani yake.
Urafiki una nguvu kuliko ngono ndio maana kuna talaka kwa wanandoa na wala hakuna talaka kwa marafiki. Kwa sababu marafiki hawatengani kwa sababu ya ugomvi bali wanatengana kwa sababu ya umbali ndio maana una washkaji zako wa shule hamjawahi kugombana ila kwa sababu ya umbali una washkaji wengine.
Lakini kwenye ndoa watu hawatengani hivi hivi tu lazima wakorofishane wengi wao ndipo waachane. Ngono unaweza kupata kwa siku moja lakini urafiki hauwezi kupata kwa siku moja. Hivyo mwanandoa usijisahau sana ukahisi kwamba ngono ndio ishu kubwa katika ndoa, bali urafiki hasa ndio jambo kubwa.
Wanandoa msiconcetrate kwenye ngono kwa sababu ngono sio ishu tenconcetrate katika mahusiano mazuri ya urafiki na mkeo. Kinachowatenganisha wanandoa ni mahusiano ya kingono na wala sio mahusiano ya kirafiki. Ngono katika ndoa ni dharura endapo utakuwa na hamu ndipo unamaliza haja zako,ila kuna mambo mengi ya kufanya na kujadili na rafiki yako wa ndoa ukiacha ngono.
Mahusiano yanayotegemea ngono hudumu kwa muda mfupi na kuishia kwenye michepuko,mahusiano yanayounganishwa na urafiki hudumu muda mrefu sana.
Mke/mume wako ndiye rafiki yako.