Siri ya Furaha ya ndoa ni kuishi wanandoa kama marafiki (washkaji) wawili

PESA ndio kila kitu

NADHANI MMEMWELEWA MTAALAM HAPO JUU. Kila mtu ale kadiri ya urefu wa kamba yake; otherwise, soon before 2025, nchi inaweza kupigwa mnada.
 
Kabisa
 
So, PESA inatosha kusolve kila kitu kwenye mahusiano? I mean ukiwa na pesa basi umesha-win mahusiano bora yenye afya?

Pls mama D tena, before uende kwenye majukumu muhimu 🙂
Wanawake wasikuizi bila pesa hayaendi wakuu, na hata kama huyo mwanaume anamaisha ya kawaida ila yupo na mwanamke ujue huyo mwanamke katoka either kwenye maisha ya shida au alikuwa single mother, kwa sikuizi kunakasumba unaenda ukweni kujitambulisha mama/baba mkwe anakuuliza unafanya kazi gani? Na ilitokea kwa kaka yangu hivyo sometimes unaweza jenga urafiki na huyo mwanamke baada ya kumuoa akawa nayeye analeta urafiki kinafiki tu.
 
Utahudumiwa bila ya mwanaume bila pesa? Hizo ni ndoto, haya mwanaume ambaye bdo anatafuta maisha ni masikini tu ambae akipata pesa anahitaji kutafuta mradi fulani maisha yaende.

Ataweza kukuhudimiwa ipasavyo wakati pesa yenyewe ya kubangaiza? Akuhudumie alafu mlale njaa siutalalamika! In short wanawake wengi mnapenda kuolewa kwenye maisha mazuri, na hapo urafiki na huyo mwanaume kutakuwa hamna
 
Mkiwa marafiki hata kusameheana ni rahisi.
 
Hakuna anayedai pesa ila familia inataka kula, kulala, kuvaa.... Majukumu lazima yafanyike kadri ya mahitaji ya kila mwanandoa

Mwanaume ni kichwa na kiongozi wa familia💥
Tell them, mama D .

But, one more question: Ile dhana yetu pendwa ya ^Ham-sea-knee^/50 yenyewe tunaishikiza wapi kwenye hii hoja uliyoisema ya mume kuwa family head?
 
Kwa hiyo upendo mwisho wake ilikuwa karne ya ngapi vile? Au, hivi kuna wanandoa ambao pesa si kipaumbele sana, ila muhimu kwao ni upendo?

I mean, anaweza mume akawa relatively fukara, but then maisha yao ya ndoa yakawa tu na raha bila karaha?
 
But, nani anayependa maisha ya umaskini? Hata Mzee MATONYA new hawezi kuliafiki hilo ^car-bee-sir!^
 
Hapo kwenye muda naona wengi hua tunakosea sana.
Kuna kipindi nilikua nimebanwa sana na majukumu ya kazini, nyumbani nilikua natoka saa 12 alfajiri na kurudi ni saa 3 usiku nimechoka hoi, nikifika home ni kuoga kula na kulala tu.
Nilianza kuona unyonge kwa mke wangu na kupoteza ile furaha na ucheshi wake.
Baada ya kushtukia haya mabadiliko yake nikaamua kujiwekea ratiba hata nikirudi nimechoka na kuchelewa kiasi gani nitenge walau saa moja ya kupiga nae story na kutaniana huku nimempakata.
Hii ilisaidia kurudisha furaha na ucheshi wake wa awali.
 
Furaha ya ndoa ni kila mtu kubeba majukumu yake kwa uaminifu. Kwa maneno mengine: ^Kila mbuzi ale urefu wa kamba yake!^
mama D
Tatizo watu wanajua majukumu ya kumlisha mwenza wako na kumvisha na vitu kama hvyo au kumheshimu, kuhudumia watoto, kushiriki tendo la ndoa kikamilifu na kuweka nyumba ktk hali ya usafi ndo basi mtu kamaliza lakin kuna wakati mwingine wanandoa wanaishi Hakuna kubebishana, kusikilizana, kufarijiana mmoja wenu anapokuwa ktk wakati unaomuumiza yaan mtu akishaleta chakula au yale majukumh common basi anaona kamaliza wakat mume/mke wake anahitaji uwepo wake kwa hali nyingine
 
“It’s a lack of friendship not love that is the cause of marriages to break down”

Inatakiwa

Uweze kujamba mbele ya mtu wako na umwambie kinatema hahahaa

Muweze kupiga umbeya wote mahali popote na kumsimulia mtu wako

Inatakiwa Muwe wasemaji wa Watu mnapokua ndani, jadili nani kafanya nini

Hapo hatatamani hata kuwa na marafiki hao wa kike

Hapo hutatamani kuwa na marafiki wengi wa kiume

Piga umbea hadi wazazi wenu na watoto wenu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…