Siri ya Kuwa na Amani na Furaha ni Kujifunza Kutojali Baadhi ya Mambo

Siri ya Kuwa na Amani na Furaha ni Kujifunza Kutojali Baadhi ya Mambo

Ertugrul Bey

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2020
Posts
14,705
Reaction score
30,041
Screenshot_20250404_192231_Chrome.jpg


Anaitwa Bowiwksi alikuwa anapenda kuwa mwandishi wa vitabu lkn kwa bahati mbaya sana hakuna mchapishaji ambaye alitaka kufanya naye kazi,kazi yake ilikuwa mbaya na hivyo kuwafanya wachapishaji kutopenda kufanya nae kazi

Alikataliwa kwenye vitabu,majarida,machapisho na hata kwa washairi,matokeo yake akaanza kuwa mlevi,mtu wa mademu,mcheza kamali wa kutupwa na tabia zote mbaya alikuwa nazo

Siku moja mchapishaji mdogo katika mtaa wao akaona ebu ngoja ampe nafasi huyu bwana Bowowksi afanye nae kazi

Sasa alitakiwa kuchagua kuacha kazi ya posta ambayo ilikuwa inamuweka mjini au aandike na kubakia hana kitu mfukoni

Huyu bwana akaamua ajaribu bahati yake,kweli akaandika kitabu kuhusu maisha yake ya aibu, na hakuona haya kuanika uchafu wake,kweli bwana baada ya mda mchache akauza kopi nyingi sana za kitabu chake,na ndani ya wiki mbili alichapisha vitabu sita na kuuza kama kopi milioni mbili

Pamoja na kuwa maarufu na mwenye pesa lkn hakubadilisha maisha yake aliendelea na tabia zake zile zile kwasababu hakujali kuhusu watu wana muonaje,aliishi maisha yake

Sibariki vitendo vyake lkn navutiwa na jinsi alivyoamua kuishi maisha yake bila kujali watu watamuonaje

Sisi ambao kila kukicha tunapambana jamii ituone bora,wenye akili na hekima,wenye maisha mazuri,tunaendesha ndinga kali,tuna demu mkali,nyumba nzuri nakadhalika tunaishia kutokuwa na furaha na amani

Kwasababu tunajali sana watu watatuonaje,lkn kiuhalisia tunajiangamiza sisi wenyewe bila kujijua

Upande wa pili kila siku magazeti,vitabu na majarida na mitandao ya kijamii inatuelekeza namna ya kuwa na furaha kana kwamba hatuna furaha,tunaelekezwa namna ya kuimarisha muonekano wetu kana kwamba hatuna muonekano kabisa,tunashauriwa namna ya kuonekana warembo kana kwamba sisi sio warembo

Yaani ili mradi tu ni kutufanya tujione hatufai na hatuvutii,yani lengo lao ni kutufanya tusijikubali na hali zetu,matokeo yake tunakuwa waathirika wa mambo yao

Itaendelea.....

Ni hayo tu!
 
Jinsi tunavyotaka kuwa bora ndio tunajiona hatuko bora kabisa,kadri tunavyotaka kufanikiwa ndio tunazidi kukosa raha kwasababu wakati wewe unapambana kujenga kibanda chako unamuona kijana mdogo kabisa ana mjumba wa maana

Unapotaka kununua usafiri wako wa kukutoa point A na kwenda point B unakutana na madogo wa 2000 wanapush ndinga kali,matokeo yake unaishia kuwa na stress tu

Hii hapa ni law of backwards,inasema hivi kadri utakavyo yachukulia mambo negative ndio utapata mambo positive na kinyume chake ukitaka mambo positive unapata negative

Nataka kusema nini hapa,kubali kwamba uchumi wako ni mdogo na hivyo pambana kwa uwezo wako upate kile unachostahili na sio kile unachotaka

Unataka gari basi nunua gari ya kipato chako na sio gari ya ndoto yako,kwasababu gari ya ndoto yako itakupa stress na matokeo yake utakosa furaha

Usijali hapo yard ya ofisini kwako wenzako wamepaki gari za hadhi gani,we nunua gari unayo imudu na usijali kuhusu wao watakuchukuliaje,ishi maisha yako

Wazee wa zamani hawakujali kama wananukia harufu ya ng'ombe ila kikubwa waliishi maisha yao don't give *** about what people think!

Tambua kadri unavyokuwa na matarajio makubwa ndio kadri unavyozidi kuwa dissapointed

Itaendelea....
 
Watu wa texas wana msemo wao " mbwa mdogo ndio hulia kwa sauti kubwa"

Kwahiyo kama wewe ni tajir je kuna haja gani kuwaambia watu utajiri wako,kama wewe una maisha mazuri unahaja gani watu wajue maisha yako,kama wewe ni mrembo je kuna haja gani utangaze urembo wako

Watu si watakuona tu kwa utajir wako,na kwa urembo wako,kitendo cha kutaka au kujionyesha wewe ni nani kinaonyesha hauna furaha na amani,kwahiyo unataka furaha kupitia watu wengine

Itaendelea
 
Mambo mengi duniani ni strees tupu,cha muhimu ni afya yako na utulivu wa ndani,ili wakati mambo yanoondoa aman na utulivu ndani yako yanapovuma yasikubabaishe,ni kweli watu walio wengi hawana utulivu wa nafsi ndani,wanishia kufanya mambo ili waonekane na jamii ila mioyoni mwao hawana tulizo.
 
Iko hivi tunajua kwamba wote tutakufa au sio,na huenda tuna mda mchache sana wa kuishi,sasa kama hivyo ndivyo kwanini tunajikuta tunajiumiza kwa kuyapa kipaumbele mambo ambayo yanatuumiza wakati hatuna mda wa kutosha hapa duniani


Yani ukiwa unajali kila kinachokutokea katika maisha yako amigo,utaishia kuwa looser,utaishia kutokuwa na furaha,utakuwa na huzuni siku zote,utakuwa mtu wa hovyo sana hapa duniani

Sikia jifunze kuwa na mawazo mazuri na kuwa na hisia nzuri, jifunze kuwaza katika namna ambayo itakufanya ujisikie upo katika ulimwengu wako wa peke yako,yani hakuna kukatishana tamaa,hakuna kudharauliana n hakuna kufuatiliana yani ni wewe na maisha yako

Ukifanikiwa hapo hautajali tena mambo yaliyo nje yako bali utajali zaidi yale yaliyo ndani ya moyo wako ambayo ndio wewe halisi yani wewe haswaa

Ukiwa unajali kila kitu matokeo yake utajihisi kwamba unatakiwa uwe na furaha siku zote,unatakiwa uwe na maisha mazuri siku zote,unatakiwa uheshimiwe siku zote,unatakiwa post zako zisomwe kwa wingi siku zote,kitu ambacho si kweli

Wakati mwingine tunakutana na mambo ambayo yapo nje ya uwezo wetu,kwahiyo tunapaswa kuishi nayo au kuyakubali,kwa namna hiyo pekee ndio tunatambua maana nzima ya maisha

Inaendelea....
 
Kutojali baadhi ya mambo haimaanishi kwamba inakutoa ubinadamu wako bali inakufanya uwe tofauti kidogo na watu wengine

Naam kila mtu kwa namna moja au nyingine huwa anaumizwa kwa kujali sana mambo fulani fulani katika maisha yake,na haya humfanya akose furaha na amani

Sasa wewe kwakujifunza kutoyajali baadhi ya mambo kunakutofautisha na wao,kwakuwa unataka uishi nje ya mipaka ya mitazamo ya watu,unataka kuwa na uhuru wako wa kuishi,unataka kuyaona maisha katika namna ya kipekee kabisa,hautaki kufungwa na mazingira

Yani unataka kuwa wewe halisi na sio mtu ambaye wanakutaka wao uwe wa namna gani,unakataa mitazamo yao na unataka kuwa na mtazamo mpya juu ya nini kile unataka katika maisha yako

.inaendelea....
 
Je wewe ni mtu ambaye huwa unasumbuliwa na vitu vidogo vidogo kama vile remote inashindwa kufanya kazi huwa unapaniki,dish la tv likiyumba huwa unapagawa,au mtu akikuchomekea barabarani huwa unapagawa na kuongea hovyo hata kama aliyekuchomekea hakusikii

Basi jua hauna mambo makubwa yanayo kushughulisha ndio maana unasumbuliwa na vitu na mambo madogo madogo

Inasemwa hivi ubongo ukiwa hauna tatizo la kuushughulisha basi utatafuta tu tatizo lingine la kuushughulisha

Kwahiyo ukiona mambo madogo madogo yanakukosesha raha basi hauna jambo kubwa linalo kushughulisha

Inaendelea...
 
Tulipokuwa wadogo tulikuwa tunakutana na mambo mengi mapya kwahiyo tulikuwa tunajali sana mambo hayo,ndio maana mwenzio akiwa na puto jekundu nawe ukiwa na jeupe una lalamika kwanini hukuletewa puto jekundu

Kwahiyo tumekuwa huku tunajali mambo mengi sana katika makuzi yetu

Baada ya kufikisha umri fulani wa ujana,tunaanza kuchagua mambo ambayo yanatupa sana attention,mfano kuwa na muonekano mzuri,kuvaa vizur,kuendesha ndinga kali na mambo kama hayo

Na tunapokuwa watu wazima huwa hatujali mambo mengi sana,kwakuwa tunajua hatuwezi kupona kansa,hatuwezi kwenda mwezini, hatuwezi kuwa na maisha ya kifahari kwakuwa tunatambua kwamba maisha ni zaidi ya utajir kwamba maisha sio kuhusu material things bali maisha ni vile ukijikubali wewe mwenyewe pamoja mazingira yako yanayo kuzunguka
 
FURAHA NI TATIZO KUBWA

Ngoja nikupe story.moja kwanza halafu tutakuja katika uchambuzi, kuna mfalme mmoja wa jamhuri fulani aliadhamiria kwamba mwanae au prince aishi maisha ya furaha sana na mazuri,hivyo alipanga huyo mwanae asijue shida ni nini

Kwahiyo akaamua kujenga ukuta kuzunguka makazi yake ili mwanae huyo asijue maisha nje ya pale ndani ya kasri,kwahiyo huyo kijana hakuwahi kukutana na wanakijiji au watu wengine nje ya kasri,kwahiyo hakujua kwamba kuna maisha tofauti nje ya kasri

Lkn kadri alivyozidi kuwa mkubwa alikuwa anaboreka na maisha ya raha ambayo amekuwa anayapata ndani ya kasri,hivyo akatamani sana atoke nje ya kasri apate uzoefu mpya

Basi akaongea na mlinzi wake ili amuwezeshe kutoroka na kwenda kuona maisha mengine nje ya kasri

Kweli alifanikiwa kutoka nje ya ukuta wa kasri,na kwenda nje ya kasri,huko ndio akaona kuwa watu wanashida sana,kuna maisha magumu,kuna maradhi,kuna vita na ghasia mbali mbali

Ndo akajua duuh kumbe kuna maisha mengine kabisa tofauti na aliyoyazoe,kwahiyo akawa na hamu sana ya kupata uzoefu mpya,kwahiyo alienda kulala chini,akajaribu kwenda jalalani na kuokota chakuna,kisha akarejea ndani ya kasri,lkn bado alikuwa na hamu sana ya kuzidi kupata uzoefu zaidi

Inaend...........
 
Prince alipotoroka mara ya pili hakurudi tena ndani ya kasri,hivyo akaamua.kuanza maisha mapya na kupata uzoefu mpya,aliishi kwa shida kuna nyakati alikosa kabisa chakula,lala yake ilikuwa mahali pabaya,alipata maradhi na kadhia nyengine mbali mbali

Alikaa huko uswahilini kwa miaka kibao,lkn baadae akaja kuboreka na maisha yale ya hovyo ya ukweli uswahili,ndio akajiuliza hivi maisha hasa yana maana gani?

Maana ukiishi kwa furaha sana nako kuna matatizo na ukiishi kwa dhiki na shida nako kuna matatizo,kwahiyo hakuona ni nini hasa falsafa ya maisha

Maana watu matajiri wanapata shida kutokana na utajir wao na maskini wanapata shida kutokana na umaskini wao,ingawa shida zinatofautiana kati ya kundi moja na kundi lingine

Sasa akaamua kuanzisha falsafa ya maisha ambayo itakuwa tofauti na walau kuleta maana ya maisha katika mlengo mwengine kabisa

Itaend...........
 
Huyu mtu alikuja kuitwa Bhudda,aligundua kwamba maisha ni mchanganyingo wa furaha na huzuni pia,kufanikiwa na kutofaniwa,maradhi na afya,utajir na umaskini,kwa maana haya mambo yote huwezi kuyakwepa kwenye maisha,yapo yalikuwepo na yatakuwepo siku zote na ndio yanafanya maisha yawe na maana

Mfano ingawa maumivu ni kitu kibaya ama yawe ya kimwili au kisaikolojia lkn yana faida na umuhimu wake katika maisha,mfano ukijiumiza kidole chako cha mguu kwa kujigonga kwenye meza au kisturi hapo nyumbani kwako

Lazima kwanza utalalamika na saa nyengine utalaumu hata mpangalio wa hiyo meza au sturi hapo nyumbani kwamba imekaa vibaya,kwa maana ingewekwa kwenye mpangalio mzuri basi huenda usingejiumiza kidole chako

Lakini kwa upande wa pili,hayo maumivu yanakufundisha kitu kimoja kwamba next time uwe makini unapopita hapo ili usijigonge tena,kwa sababu ukijigonga tena mfumo wako wa neva za fahamu utakuhadhibu kwa kukuletea maumivu makali

Sawa na maumivu ya kisaikolojia,kama mpenzi wako au mke wako au mume wako ni kipengele kwako,kwa maana ndoa imekuwa chungu kiasi kwamba hutamani tena ndoa hiyo,basi hayo maumivu yanakufundisha kwamba next time uwe makini kumchagua mtu sahihi ili usirudie kupata matatizo tena ya kihisia au ya kisailkolojia

Kwahiyo kwa kila huzuni au maumivu utakayo kuwa nayo basi nyuma yake kuna somo kubwa na tahadhari kubwa ambayo unafundishwa uichukue ili wakati mwingine uwe sehemu salama zaidi

Kwa kila maradhi ambayo tunakutana nayo hapa duniani basi tunafundishwa tujie chanzo cha maradhi hayo na kuwa makini kuyaepuka ili next time yasije kutudhuru tena


Kwahiyo utaona mambo yote ambayo huwa tunayapitia hapa duniani huwa yana sababu ya kuwepo kwake,kwahiyo haina haja ya kuumizwa sana kufilisika kwako,unafundishwa next time uwe makini na matumizi yako na namna nzuri ya kuendesha biashara au shughuli zako,kwa kila jambo kuna somo kubwa ndani yake

Inaend..........
 
Na tutambue kwamba maisha hapa duniani hayawezi kukosa matatizo hata kidogo,kwasababu ukitatua tatizo moja linakuja lingine,iko hivyo siku zote

FURAHA INATOKANA NA KUTATUA MATATIZO

Ukitatua tatizo moja linakuja tatizo lingine,mfano ukinunua vifaa vya kufanyia mazoezi,basi utaanzisha tatizo lingine la kuamka mapema na kufanya mazoezi,baada ya kufanya mazoezi utakuwa na jasho na huwezi kwenda kwenye shughuli zako namna hiyo,hivyo itabidi utatue tatizo la kunuka jasho kwa kuoga,umeona ni muendelezo wa kutatua matatizo

Mfano wa pili,ukitaka kumfurahisha mke wako kwa kumtoa out labda kila jumamosi,basi utatengeneza tatizo la kutafuta pesa ili ikuwezeshe kumtoa out huyo mpendwa wako,na hata baada ya kufanya hivyo,baada ya mda hiyo sehumu itawaboa utatengeneza tatizo lingine la kutafuta sehemu mpya ili mpate uzoefu mpya,nadhan umeelewa kuwa matatizo hayaishi

Kitu cha muhimu ambacho msomaji wangu unatakiwa ujue ni kwamba huwezi ishi bila matatizo,kibaya ni kutaka usipate matatizo kabisa hilo haliwezekani

Kikubwa ni kuyafurahia matatizo ambayo utakuwa comfortable kuishi nayo na kufurahia kuyatatua,hapo utakuwa umepata furaha ya kweli

Ili tuwe na furaha basi inatakiwa tutatue matatizo,na furaha sio kitu ambacho kipo siku zote kwa maana kama jiwe au sanamu,yani kama lipo basi lipo tu,haipo hivyo furaha ni hali ambayo inatafutwa kwa kutatua matatizo au changamoto mbali mbali

Na wakati mwingine furaha unayopata leo kwa kutatua changamoto fulani ndio itakuwa msingi wa kuzalisha tatizo lingine kesho,mfano umekuwa umekuwa na changamoto ya usafir so ukaamua kununua ndinga yako ikutoe point A na kwenda point B, baada ya kununua gar yako ukapata furaha,lkn kesho yake upo zako town unacruize mara pap umepata ajili,tayar hapo umetengeneza tatizo lingine ambalo hukulitegemea,kwahiyo furaha yako ya kumiliki gari imegeuka na kuwa tatizo lingine

Inaend......
 
HISIA ZINAPEWA UZITO SANA

Hili ni tatizo kubwa,tujue kwamba hisia zipo kwa ajili ya kutupa mrejesho wa mambo na kutufanya tujisikie vizuri kwa kipindi fulani,kwa maana hauta jisikia vizur mda wote

Hisia huwa hazidumu ndio maana unaweza kujisikia vizur sasa hivi lkn baada ya mda fulani ile furaha au hisia za furaha uliyokuwa nayo inapotea,na unaweza ukawa na hisia za huzuni sasa hivi na baaada ya masaa kadhaa hiyo huzuni ikapotea

Na hisia ni kama kiashiria cha kutuambia kitu fulani kiko sawa na kitu hakiko sawa,ambacho hakiko sawa ukitafutie ufumbuzi na ambacho kiko sawa endelea kukiboresha zaidi

Mfano katika mahusiano ,hisia mbaya huwa ni ishara inayo kwambia kwamba haya mahusiano sio mazuri,ndio maana kila mara unapata hisia ambazo hazikupi furaha,maana yake unapewa ujumbe ebu tatua hili tatizo ambalo linakufanya ujisikie huzuni au vibaya katika mahusiano yako

Na hisia nzuri katika mahusiano zinakupa ishara kwamba huu uhusiano ni wa kuupigania kwasababu unakufanya ujisikie vizur,kwahiyo kama ulikuwa unauchukulia poa basi ebu jitahidi kuuboresha zaidi

Kama vile ambavyo unapata maumivu baada ya kidole chako kugusa moto,hayo maumivu yanakwambia next time uwe muangalifu zaidi,na hisia za huzuni zinakwambia just try to fix something chap

Kwahiyo kwakuwa hisia ni zenye kubadilika badilka basi usifanye maamuzi tu kwa kutumia hisia peke yake utafeli amigo,bali fanya maamuzi kwa kutumia akili pia,na kwa kufanya hivyo utafanya maamuzi sahihi siku zote

Anayehitaji kufanya maamuzi kwa hisia tu ni mtoto wa miaka mitatu au mbwa,unajua kwanini kwasababu hawana cha kufanya zaidi ya kushit katika kochi au kitanda

Kwahiyo jua kwamba hisia hubadilika,na haimaanishi kitu kinachokufanya uhisi vibaya sasa hivi ni kibaya,bali unaweza hisi vibaya lkn kitu hicho kikawa kizuri,na unaweza kuwa na hisia fulani juu ya kitu fulani kuwa ni kizuri lkn ukweli wa mambo kitu hicho sio kizuri

Ndio maana inasisitiwa fanya maamuzi kupitia hisia pamoja na reason

Inaend.....
 
JE UPO TAYAR KUPAMBANA NA HALI IPI?

Watu wengi ukiwauliza je unataka mambo gani katika maisha? Watakwambia natak kuwa na kazi nzuri,nyumba nzur,mke mzuri na great sex,na gar nzuri

Lakini

Hakuna hata mmoja ambaye atakwambia nataka kupambana na changamoto fulani katika maisha,kitu ambacho hakikwepeki

Je unataka kuwa na sex body? Upo tayar kutumia mda mwingi gym ili uwe na sex body?

Unataka kuwa na mwanamke mrembo,je upo tayar kupambana na stress zinazotokana na mahusiano hayo?

Unataka kufanya biashara,je upo tayar kupoteza mda mwingi na kujitoa mhanga kwa biashara ambayo hata huna uwakika kama utatoboa?

Unataka kazi nzuri yenye malipo mazuri,je upo tayar kumvumilia boss ambaye anaweza kuyafanya masaa ya kazi mchana kutwa kuwa kama hell?

Je upo tayar kupambana na changamoto?

Inaend....
 
Mambo mengi duniani ni strees tupu,cha muhimu ni afya yako na utulivu wa ndani,ili wakati mambo yanoondoa aman na utulivu ndani yako yanapovuma yasikubabaishe,ni kweli watu walio wengi hawana utulivu wa nafsi ndani,wanishia kufanya mambo ili waonekane na jamii ila mioyoni mwao hawana tulizo.
Muda mwingine ni bora hata kukaa mbali na watu wanaokukera..
 
Back
Top Bottom