Siri ya Kuwa na Amani na Furaha ni Kujifunza Kutojali Baadhi ya Mambo

Siri ya Kuwa na Amani na Furaha ni Kujifunza Kutojali Baadhi ya Mambo

Hii hapa ni law of backwards,inasema hivi kadri utakavyo yachukulia mambo negative ndio utapata mambo positive na kinyume chake ukitaka mambo positive unapata negative
Hapa sijaelewa....Sio kwamba unapokuwa Positive ndio vitu vinakuwa positive na kinyume chake... Na tunasisitizwa alwayas kuwa PISITIVE MINDED PEOPLE?>
 
Hapa sijaelewa....Sio kwamba unapokuwa Positive ndio vitu vinakuwa positive na kinyume chake... Na tunasisitizwa alwayas kuwa PISITIVE MINDED PEOPLE?>
Ndio maana nimesema kuwa tayar kujifunza mambo katika mlengo tofauti kabisa

Hawa hawa motivational speaker huwa wanatupa nafuu ya mda mchache.lkn hawatupi dawa ya kutatua tatizo kwa mda mrefu

Mfano wanakwambia ili uwe na furaha,basi kaa kwenye kioo jitazame na jiambie " nina furaha,nafurahia maisha yangu,najipenda"

Lkn

Hawatuambii tutatue kiini cha tatizo kwanza,hawatuambii tutafute sababu ya sisi kukosa furaha

Ndio maana katika uzi huu utajifunza mambo tofauti,,endelea kunifuatilia
 
Iko hivi tunajua kwamba wote tutakufa au sio,na huenda tuna mda mchache sana wa kuishi,sasa kama hivyo ndivyo kwanini tunajikuta tunajiumiza kwa kuyapa kipaumbele mambo ambayo yanatuumiza wakati hatuna mda wa kutosha hapa duniani


Yani ukiwa unajali kila kinachokutokea katika maisha yako amigo,utaishia kuwa looser,utaishia kutokuwa na furaha,utakuwa na huzuni siku zote,utakuwa mtu wa hovyo sana hapa duniani

Sikia jifunze kuwa na mawazo mazuri na kuwa na hisia nzuri, jifunze kuwaza katika namna ambayo itakufanya ujisikie upo katika ulimwengu wako wa peke yako,yani hakuna kukatishana tamaa,hakuna kudharauliana n hakuna kufuatiliana yani ni wewe na maisha yako

Ukifanikiwa hapo hautajali tena mambo yaliyo nje yako bali utajali zaidi yale yaliyo ndani ya moyo wako ambayo ndio wewe halisi yani wewe haswaa

Ukiwa unajali kila kitu matokeo yake utajihisi kwamba unatakiwa uwe na furaha siku zote,unatakiwa uwe na maisha mazuri siku zote,unatakiwa uheshimiwe siku zote,unatakiwa post zako zisomwe kwa wingi siku zote,kitu ambacho si kweli

Wakati mwingine tunakutana na mambo ambayo yapo nje ya uwezo wetu,kwahiyo tunapaswa kuishi nayo au kuyakubali,kwa namna hiyo pekee ndio tunatambua maana nzima ya maisha

Inaendelea....
Point tupu....
 
Tulipokuwa wadogo tulikuwa tunakutana na mambo mengi mapya kwahiyo tulikuwa tunajali sana mambo hayo,ndio maana mwenzio akiwa na puto jekundu nawe ukiwa na jeupe una lalamika kwanini hukuletewa puto jekundu

Kwahiyo tumekuwa huku tunajali mambo mengi sana katika makuzi yetu

Baada ya kufikisha umri fulani wa ujana,tunaanza kuchagua mambo ambayo yanatupa sana attention,mfano kuwa na muonekano mzuri,kuvaa vizur,kuendesha ndinga kali na mambo kama hayo

Na tunapokuwa watu wazima huwa hatujali mambo mengi sana,kwakuwa tunajua hatuwezi kupona kansa,hatuwezi kwenda mwezini, hatuwezi kuwa na maisha ya kifahari kwakuwa tunatambua kwamba maisha ni zaidi ya utajir kwamba maisha sio kuhusu material things bali maisha ni vile ukijikubali wewe mwenyewe pamoja mazingira yako yanayo kuzunguka
kweli kabisa!!
 
Watu wengi tunapenda matokeo lkn sio process/mchakato,ndio maana ni rahisi mtu kukwambia nataka kuwa na maisha mazuri,nataka kuwa na makazi mazuri na mambo kama hayo

Lakini je,tumejipanga kwa ajili ya mchakato wa kuyafikia hayo tunayo yataka,kuwa tayar kwa mchakato maana yake upo tayar kupambana na changamoto yoyote utakayo kutana nayo mbele yako na utadili nayo bila kujilaumu hata kama utakutana na magumu kiasi gani

Ndio maana swali la msingi la kujiuliza kwa kila mtu je,nipo tayar kupambana na changamoto la hili jambo ninalotaka kufanya?

Mathalani unataka kuoa,je upo tayar kupambana na changamoto za maisha ya ndoa? Wale ambao hawakujiuliza hili swali ndio huwa wa kwanza kuona ndoa chungu ndani ya miezi michache tu tangu wafunge ndoa

Lakini kama ulijiuliza na ulikuwa tayar kupambana na changamoto za ndoa,naamini kabisa mpake leo ndoa yako bado ipo imara,kwasababu haijalishi ni changamoto kiasi gani unakutana nazo lkn kwa kuwa ulikuwa tayar kupambana nazo bado unaendelea kudili nazo kwakuwa matatizo ni sehemu ya maisha ya kila siku

Tusijidanganye katika hii dunia hakuna siku ambayo matatizo yatakwisha,ila matatizo yataendelea kuwepo kwahiyo kikupwa ni kuwa tayar kupambana nayo

Wakati mwingine hatufikii malengo yetu kwakuwa huwa tunapenda matokeo zaidi kuliko mchakato wa kuyafikia hayo malengo,nakumbuka miaka ya nyuma lau ungeniuliza ungetaka ukubwani kufanya kazi gani ningekujibu nataka kuwa "mtangazaji wa redio" ni sio siri nilikuwa navutiwa sana watangazaji kama marehemu Julias Nyei Sanga maarufu Anko J redio Tanzania enzi hizo,nyie jen z hamuwezi kumjua huyu,jen x tunamjua

Nilikuwa pia navutiwa sana na mtangazaji Taji Liundi,mpaka leo naamini kabisa kama ningekuwa mtangazaji basi ningekuwa mtangazaji bora sana,lkn niliamini matokeo ya kuwa mtangazaji bora ila sikuwa tayar kufuata mchakato,ndio maana ndoto yangu ilififia kwa kutoenda hata kusomea uandishi wa habari,lkn nilidhani ningekuwa mtangazaji tu from no where

Hii ni kwasababu sikuwa tayar kupambana na changamoto ya kusomea uandishi wa habari,kwahiyo kwa kila unachotaka kufanya jiulize je,upo tayar kupambana na changamoto iliyopo mbele yako?

Unataka kufanya biashara,je upo tayar kupoteza mtaji na kusimama tena na kuanza upya? Je upo tayar kutake risk?
Upo tayar kutumia mda wako mwingi kupambania biashara yako?

Always be ready to choose your own struggle

Inaend.....
 
WEWE SIO MTU SPECIAL

Hivi umeshawi kukutana na watu ambao wanajifanya wana mambo mengi sana hapa mjini,kuna ambaye yeye hujifanya anajuana na watu mashuhuri hapa town,nimemkumbuka bro wangu mmoja tulioa nyumba moja,huyu bwana ukikaa nae anaweza kujifanya kapiga simu anaogea na mtoto wa mzee wa Msoga,mara sijui anaongea na mfanyabiashara gani mkubwa,yani ili mradi aonekane mtu wa maana hapa town

Watu kama hawa wapo wengi sana na hufanya hivyo ili waonekane ni watu wa maana sana,na watafanya lolote lile ili hadhi yao ibakie pale pale hata kama wanajidanganya wenyewe

Kibaya zaidi wapo radhi kuficha madhaifu yao ili mradi tu wawe juu siku zote au waonekane watu wa maana,ikitokea wamefanikisha jambo fulani hata kwa kusaidiwa na wengine watajisifu sana,na wakifanya makosa basi lawama zote zitapelekwa kwa watu wengine kwamba ndio wamsababisha hayo

Msomaji wangu ngoja nikwambie ukweli,thamani ya mtu inapatikana pale anapo jifanyia tathimini yeye mwenyewe na kugundua madhaifu yake na kisha akayafanyia kazi na kujirekebisha na kuwa mtu bora zaidi

Thamani yako haiji kwa kujipa vyeo feki,au kujipa hadhi usiyokuwa nayo,sana sana unazidi kujishushia heshima,huyo bro wangu yani sometime anatega simu inapiga alarm kama mlio wa simu halafu kisha anajifanya anaongea na papaa gani sijui,yani haishiwi drama,na wallah kama hujamjua mbona unaingia king,na madem anawatafuna sana tu hadi marafiki wa mkewe kawatembezea sana,lkn je mwisho wa siku ana fanikisha nini katika maisha?

Sisi tunao mjua ingawa mwenyewe hajui kama tunamjua tunaishia kumradharau,yani yeye kukupiga sound kwamba atakukutanisha na Abdul ni jambo dogo tu dah wacha nicheke mie hahaha!

Inaend...
 
KILA MTU ANATAKA KUWA SHUJAA


Tekinolojia imetatua changamoto ya uchumi lakini imeleta shida kubwa sana na mvurugano katika jamii yetu katika zama hizi

Wale ambao hufanya mambo ambayo sio ya kawaida au ambayo yamepita kawaida ndio huwa mashujaa katika television,magazeti na mitandao ya kijamii,hao ndio hutrend na kuwa sehemu ya habar ya mjini


Tekinolojia inatufanya wote sasa tutake kutrend walau nasi tupate majina hapa mjini na hivyo kutuvuruga na kutufanya tupagawe,mfano kuna ambao wanaoga barabarani na kushoot clip zao na kweli wanatrend,kuna ambao huko ughaibuni wanaenda mashuleni na kuwapiga risasi wanafunzi risasi na wanatrend,na mambo kadha wa kadha

Kwahiyo kila mtu anapambana atoke vipi,saa nyingine tunafanya mambo hata ya kututoa utu wetu kwa jina la tekinoloji ili mradi tuwe vioral mitandaoni,na wakati mwengine tunaandika topic au nyuzi ambazo ni kichefu chefu kwakuwa tunajua ndio zinashika akili za watu basi tunaishi nazo,yaani ni kuvurugwa kwa kwenda mbele

Kwahiyo kwa kiasi fulani ingawa tekinolojia imeleta unafuu na wepesi wa mambo mengi lkn inatuvuruga sana,kwasababu tunajali sana baadhi ya mambo ili nasi tutrend

Kibaya zaidi tunajenga jamii ya kutaka kufanya mambo makubwa na ya kipekee kana kwamba maisha ndio yamepangwa kuwa hivyo,yani bila kufanya mambo ambayo sio ya kawaida inakuwa kama hatuiishi vile

Hao ambao wamefanya mambo makubwa na wanaendelea kufanya,walifanya kwa kujiendeleza na kuwa bora zaidi kwakuwa walifanya si kwa kuwa impress watu ila kwa kutaka kupata matokeo bora zaidi

Ila sisi kinyume chake tunataka greatness out of no where,hatuna misingi ya kutufikisha huko ila tunafanya chochote ili mradi nami Etugrul bey nitrend hapa town

Tumekuwa na jamii ambayo haiamini katika average ila katika extraodinary,yani tukiwa wa kawaida bado hatujaishi ila tukiwa zaidi ya kawaida ndio tunaishi,haya ni majanga

Kwa staili hii kwanini tusiwe na stress? Kwanini tusiwe hatuna furaha,kwanini tusiwe na misongo ya mawazo

Unajua kwanini inakuwa hivi?

Kwasababu tunajali sana hata kwa mambo ambayo hayana ulazima

Inaend......
 
Msosi
Pa kulala
Pamba kali
Ba tamu
Bundle

Mie hapo maisha nimemalizaa kabisaa. Yaan mwishoo.
 
THAMANI YA MAUMIVU

Mnamo mwaka 1944 Jeshi la Japan lilikuwa limetawanyika karibia eneo kubwa la Asia,lkn wakati huo huo ndio mambo yalibadilika dhidi yao ,Jeshi la Amerika lilifanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwadhibiti wajapani,na askari wa Japan walikuwa na machaguzi mawili tu ama wauwawe au wawe mateka

Lakini wakati huo huo aliteuliwa lutenanti Hiroo Onoda,huyu kazi yake au mission yake ilikuwa ni kuhakikisha anapunguza nguvu ya jeshi la marekani kwa gharama yoyote ile,na katu asikubali kujisalimisha

Mnamo mwaka 1945 mwezi wa august wakashushiwa bomu la nyuklia katika mji wa Hiroshima na Nagasaki na hapo Japan ilisalimu amri rasmi

Lakini huko katika uwanja wa vita lutenant Onoda alikuwa katika vita vya msituni nchini philiphine katika kisiwa cha Lubang,akiwa na watu wake kama watatu hivi aliendelea kupambana dhidi ya jeshi la Marekani

Yeye hakujua kama vita imeisha,lkn baadae Japan kwa kushirikiana na Marekani wakasambaza vipeperushi kutoa ujumbe kwamba vita imeisha,lkn pamoja na Lutenant Onoda kuona ujumbe huo,yeye aliamini hizo ni njama za Marekani katika kutaka kumdhoofisha,aliamini bado vita inaendelea

Alikuwa anavamia wanakijiji na kupora na kuwaua yeye na vijana wake,karibia miaka 30 huyu mwamba anapambana tu msituni,pamoja na jitihada kufanywa tena kwa kurusha vipeperushi kwamba vita imeisha lkn bado mwamba aliamini huo ni uongo tu,alichojua yeye ni kufanya misheni yake

Baadae akabakia yeye mwenyewe baada ya wenzie kufa,msako ulifanywa sana na majeshi kumtafuta lkn hakupatikana,kukawa na maneno mengi sana juu ya legend huyu huko Japan,hivyo ikampa hamasa kijana mdogo Suzuki ambaye aliacha shule na mapenzi yake makubwa ilikuwa ni kufanya adventure

Hivyo akaamua this time akamtafute huyo legend,kwakuwa kulikuwa na imani kwamba huenda bado yupo hai,akaenda huko kisiwa cha Lubang akiwa hana mbinu zozote za kijeshi wala dhana za kivita wala silaha

Alichofanya ni kuita kwa sauti kubwa "Onoda emperor anahuzunika kwa kutopatikana kwako' na cha kustaajabisha ndani ya siku nne tu Suzuki alimpata lutenant Hiroo Onoda

Watu hawa wakawa marafiki huko msituni, Onoda baada ya kugundua kuwa ni kweli vita ilishakwisha alishangaa na kuhuzunika sana,lakini alisema wala hajutii kwa yalitokea kwasababu alikuwa anatimiza mission yake

Hiroo Onoda akamuuliza sababu gani iliyomfanya kijana mdogo kama Suzuki kwenda msituni kumtafuta yeye, Suzuki akajibu kuwa alikuwa na mission tatu,ya kwanza ni kumtafuta Onoda,ya pili ni kumtafuta Panda na tatu ni kwenda kumtafuta Snowman/mtu wa barafu huko Himalayas

Kweli huyu dogo aliendelea na adventure yake ambayo huenda baridi kali huko ilikuwa ndio kifo chake

Baada ya Onoda kurudi Japan mwaka 1975 akawa mtu mashuhuri sana,si televisions wala redio stations zote zilikuwa zikimuarika kwa mahojiano ya hapa na pale,na vile vile akachapisha kitabu,pamoja na hayo yote serikali ikampa hela nzuri sana

Lakini Onoda alikuwa na huzuni juu ya maadili ambayo yamebadilika nchini kwake Japan,sasa haikuwa tena ile Japan aliyoipigania na kuwa tayar kufa kwa ajili ya taifa lake,ilikuwa Japan ya kibepari,wanawake wanavaa nusu uchi kama nchi za magharibi

Hili lilimpa huzuni sana hakufurahia tena maisha ya Japana,kwakuwa sio ile Japan ambayo aliipigania,kwake ni afadhali angeendelea kuishi msituni huko Lubang nchini Philiphine kuliko kuona Taifa lake la Japan lilivyobadilika

Mnamo mwaka 1980 akaamua kuhamia kl Brazil na ndiko alikofia huko

Lutenant Hiroo Onoda alijali sana kuhusu Japan ya zamani ambayo alikuwa tayar kufa kwa ajili yake,na hakuwa tayar kuikubali Japan mpya,na huo ndio ukawa mwanzo wa kukosa furaha na kuwa na msongo wa mawazo

Nasi hivyo hivyo huwa kama Lutenant Onoda,huwa tunashindwa kukubali kwamba kuna mambo fulani fulani katika maisha yetu lazima yabadilike,na hatuwezi kuyazuia,tuna option mbili ama tukatae ukweli tuwe na huzuni pamoja na stress au tuuKubali ukweli na kwenda nao sawa na tuwe na furaha

Kazi kwetu

Inaend.....
 
JITAMBUE WEWE BINAFSI


Tuchukue mfano wa kitunguu,kitunguu kina layer mbali mbali au maganda ambayo yamebebana kutoka juu kwenda chini

Na kadri utakavyo zidi kuyatoa ndio kuna uwezekano mkubwa wa kujikuta unatoa machozi

Jambo la kwanza mtu anatakiwa ajue kuhusu hisia zake,ajifahamu anahisia zipi,kadri anavyozidi kujichunguza atazidi kufahamu je hisia hizi ni za furaha au huzuni

Na baada ya kujua hisia zake,mathalani amejitambua kwamba ana husia za huzuni,basi hatua inayofuata anatakiwa ajiulize je hizi hisia zinasababishwa na nini?

Na hapa ndio kwenye mtihani mkubwa,kwa kutojua nini hasa ni sababu ya kuhisi hivi tunavyo hisi basi inakuwa vigumu kutatua changamoto ambayo iko mbele yetu

Usipopata sababu halisi zinazo sababisha huzuni yako tegemea kutotua tatizo na kuendelea kupata huzuni siku zote

Badala yake utakuwa unajiipoza kwa kujipa furaha ya mda mfupi na baadae tatizo liko pale pale

Mfano unasumbuliwa na tamaa ya kutaka hiki na kile,kila fashion mpya ikiingia unataka uende nayo sawa,kuna simu toleo jipya unataka upate,gari toleo jipya unataka uwe nalo

Matokeo yake ukivikosa unakuwa na huzuni,sasa usipojichunguza kwa makini unawe dhani kwamba tatizo la huzuni yako tatizo la kutokuwa na pesa ya kununua product mpya,matokeo yake hata ukipata pesa na kupata vitu hivyo,utafurahi baada ya mda,ila ikija model mpya utakuwa na huzuni tena

Lkn kumbe lau ungejichunguza kwa makini ungejitambua kwamba tatizo au chanzo cha huzuni yako ni HUTOSHEKI NA ULICHO NACHO

Lau ukijua kumbe shida yangu ni kutotosheka na nilicho nacho ndio chanzo cha huzuni yangu,,,litakuja swali la pili,je nifanye nini ili niepukane na tabia hii

Jibu ambalo ni la kudumu la kuondoa huzuni yangu ni KUJIFUNZA KUTHAMINI NILICHO NACHO PAMOJA NA KURIDHIKA NACHO

Hapo utakuwa na amani pamoja na furaha siku zote

So jichunguze na jitafakari na ujitambue

............


TATIZO LA MWANA ROCK STAR

Mwaka 1983 huyu mpiga gita akiwa na band yake ambayo ilikuwa mda si mrefu warekodi album yao ya kwanza,mara ghafla tu bila sababu yoyote anapewa tiketi ya basi na band yake arudi Los Angeles

Akiwa njiani akajiuliza maswali mengi sana kwa nini ameachwa kwenye kikosi,hii ilimuumiza sana,lkn wakati anafika Los Angeles,akawa amemua kitu kimoja,kwamba hakuna huzuni tena ila dawa ni moja tu,kuanzisha band mpya na kuifanya hiyo band iwe kubwa zaidi kuliko hiyo waliyo mtema,na awe maarufu sana,wamuone kwenye tv,na wamsikilize kwenye redio mbali mbali

Kweli alitafuta wapiga wazuri na akaunda band moja inaitwa Legendary Heavy Metal Megadeth,Mungu si Etugrul Bey kweli akafanikiwa kurekodi album yao ya kwanza na wakafanikiwa sana na kushika chat za juu,alipata mpunga wa maana na kuwa mtu famous sana

Mpiga gitaa huyu alijulikana kama Dave Mustaine,aliuza album kama Milioni 25 duniani kote,na ziara mbali mbali duniani


Lakini baadae ikafahamika kwamba kwa miaka mitatu (3) band yake ya zamani ambayo iliuza nakala milioni 180 ambayo inajulikana kama Metalicca ilikuwa imeshika rekodi ya band bora zaidi kwa wakati huo

Hili lilimuumiz sana huyu Dave,kuona band ambayo imefanikiwa zaidi ndiyo iliyo mpiga chini,yani pamoja na mafanikio aliyoyapata na umashuhuri na mpunga mrefu,bado kwake yeye ilikuwa ni failure kubwa

Hapa tunajifunza nini? Je kushindwa unakuchukuliaje?

Je kushindwa kwako ni kwasababu unajifananisha na mtu fulani au hali fulani au kushimdwa kwako kutokana na malengo ambayo umejiwekea na kwa bahati mbaya hujayafikia


No matter what, usijifananishe na mtu yeyote yule hapa duniani kwani utaishiwa kuwa disappointed

See you next time......
 
Ndio maana nimesema kuwa tayar kujifunza mambo katika mlengo tofauti kabisa

Hawa hawa motivational speaker huwa wanatupa nafuu ya mda mchache.lkn hawatupi dawa ya kutatua tatizo kwa mda mrefu

Mfano wanakwambia ili uwe na furaha,basi kaa kwenye kioo jitazame na jiambie " nina furaha,nafurahia maisha yangu,najipenda"

Lkn

Hawatuambii tutatue kiini cha tatizo kwanza,hawatuambii tutafute sababu ya sisi kukosa furaha

Ndio maana katika uzi huu utajifunza mambo tofauti,,endelea kunifuatilia
Uhakika mkuu
 
MAMBO AMBAYO TUMEYAZOEA LAKINI HUTULETEA SHIDA


Q/ Starehe

Starehe ni nzuri lkn huwa inatuletea matatizo mengi sana,kwanza ni rahisi kuipata na rahisi kuifurahia

Ila hutuathiri sana wengi wetu,muulize mtumia madawa ya kulevya yoyote je mwisho wa siku alipata nini? Muulize mwanaume au mwanamke malaya je mwisho wa siku alipata faida gani? Wengi wao hutelekeza familia kwa kuendeleza starehe,wengi hukosa kizazi kwa kutoa sana mimba,wengi hupata maradhi kutokana na athari za pombe na vilevi mbali mbali

Na kibaya zaidi ni product ambayo huwa tunatangaziwa na kuhamasishwa masaa 24,na mwisho wa siku tunaingia kwenye mfumo na kupata madhara kibao




b/ Material success

Watu wengi wanapima utajir au uwezo wao kutokana na kiasi gani cha fedha wanachomiliki,au ni mali ngapi anamiliki,au ni gari ngapi za kifahari anazimiliki

Utafiti unaonyesha kwamba pale mtu anapoweza kupata physical basic needs kama chakula,makazi na mavazi na kadhalika,basi uwiano wa furaha na utajiri huwa karibia na zero

Kama una njaa uko India,ongezeko la dola elfu 10 kwa mwaka litakupa furaha lkn kama upo developed countries ongezeko la dola elfu si chochote kwako,hii maana yake nini? Ina maana unajiumiza mwenyewe kwa kufanya kazi overtime,na wikiend for nothing

Ubaya mwingine wa kuweka sana mkazo kwenye material things kunatufanya kutoyapa kipaumbele mambo mengine yenye thamani katika maisha yetu,kama uaminifu,upendo,kujali,huruma

Pale watu wanapokuwa hawapimi thamani yao kutokana na tabia zao ila kwa kutumia vitu vya kushikika na vya kupita wanakuwa kama wajinga


c/ Tabia ya kuwa Sahihi mda wote

Ubongo wetu sio mashine ambayo ipo sahihi,huwa inafanya makosa,ni mara ngapi tunafanya maamuzi kwa kutumia hisia,tunatabia ya kuwajaji watu,tunakuwa na dhana juu ya mambo mbali mbali tofauti na ukweli halisi

Ukweli ni kwamba watu ambao wanapenda kuwa sahihi kwa kila kitu huwa wanajikosesha nafasi ya kujifunza mambo mapya,wanashindwa kuyaona mambo katika mtazamo mwingine tofauti na wanao uamini wao,watu hao vile vile wanashindwa kujifunza kutokana na makosa yao

Ni vizur zaidi kujifanya hujui na mjinga ili ujinze mambo mengi zaidi.



d/ Kuwa positive muda wote

Kuna watu ambao wanaangalia thamani ya maisha yao kwa kuwa positive mda wote,akikosa kazi anasema walau amepata mda wa kuexplore,mume wake akicheat na dada yake anasema it's okay walau amemjua mumewe ni mtu wa aina gani

Ila kuna wakati maisha yanazingua sana na kitu bora cha kufanya ni kukubaliana na ukweli tu

Kujaribu kuzikwepa negative emotions ni sawa na kuzidi kuleta matatizo zaidi

Wakati mwingine kuwa positive ni njia ya kukwepa ukweli wa mambo na sio suluhisho la kudumu la kutatua matatizo yako


Kuna nyakati watu wanatuuzi,mambo hayaendi sawa na dili zina buma,kwahiyo kuukubali ukweli na kuwa na negative emotions ni kitu cha kawaida kabisa na ndio ubinadamu wetu

Kukataa negative emotions ni kuleta matatizo na hatutopata suluhisho la kudumu

Siri moja nzuri ya negative emotions ni kuiexpress katika namna nzur inayokubalika na jamii na katika namna inayoendana na thamani yako

Kwa mfano value ya Etugrul bey ni kutopenda ugomvi,kwahiyo nitasolve jambo kwa mazungumzo zaidi,na wewe unajua value yako msomaji wangu

Kwa mfano ninapokuwa na hasira naielezea kwa mhusika lkn sichukui hatua ya kurusha ngumi,hasira kama hasira sio tatizo kwakuwa ndio asili tuliyo umbwa nayo,ila kibaya ni kuielekeza hasira katika ugomvi na uharibifu

Kitu cha msingi ni kuwa na maono mazuri ya thamani yetu na furaha itakuja kama matokeo ya kuwa na good value

Tukutane wakati mwingine.....
 
MARA ZOTE HUWA TUNAFANYA MAAMUZI


Leo hii ukilazimishwa kufanya mazoezi na mzazi wako,hakika utaona ni maumivu makubwa na utajihisi unaonewa ingawa ni kwa faida yako mwenyewe

Lakini

Ukiamua kwa hiari yako kufanya hayo mazoezi utajituma na utafurahia kwa kuwa umechagua mwenyewe kufanya hivyo

Kwahiyo siku zote huwa ni watu wenye kufanya maamuzi ya kutafsiri mambo hata kama yametokea nje ya uwezo wetu au maamuzi yetu,mfano ule mfano wa mazoezi,pamoja na kwamba umelazimishwa kufanya na mzazi wako,lkn una maamuzi ya kuyatafsiri kwa namna mbili

Ama utafsir kwamba ni jambo zuri la kiafya ambalo mzazi wako anataka uwe na afya nzuri au utafsiri kwamba ni adhabu kwako

Ebu twende katika mfano wa maisha halisi:

Anaitwa William James,ametoka katika familia bora yenye kujiweza kiuchumi,lkn pamoja na hayo,huyu mwamba alizaliwa akiwa na changamoto nyingi za kiafya

Alikuwa na tatizo la macho ambalo lilimpa upofu wa mda,akawa na matatizo ya kusikia,alikuwa na changomoto ya uti wa mgongo kiasi kwamba wakati mwingine alishindwa kukaa au kutembea kwa siku kadhaa


Alishindwa kuendelea katika masomo,alishindwa kufanya jambo lolote,alionekana lazy katika familia,kibaya zaidi mdogo wake Henry James alikuwa mwandishi wa riwaya alifanya vizur sana katika kazi yake

Mdogo wake Alice James nae alikuwa mwandishi,alifanya vizur na kuishi kwa kutegemea kazi yake

Baba yake na William kwakuwa ana connections na maguru,basi akamfanyia mpango akajiunge na shule ya masomo ya utatibu pale Havard,na akaambiwa kwamba akifeli this time atajijua yeye mwenyewe

Baada ya miaka kadhaa pale Chuoni,alishindwa na kurudi mtaani,akiwa hana hili wala lile,na alikata tamaa na kutaka kujiua kwakuwa alijiona amefeli maisha

Siku moja usiku akiwa anasoma lectures za profesa mmoja,akakutana na somo ambalo linasema lolote linalo mtokea mwanadamu ni kutokana na maamuzi yake

Rejea mfano kule nyuma nilisema ni kwa namna gani tunafanya maamuzi ya kutafsiri matukio kwa yale yanayo tutokea ndio itatufanya tuwajibike kwa namna moja au nyingine

Basi akaamua afanye majaribio ya somo lile,akadhamiria kwamba ataishi kwa mwaka mmoja akiamini kwamba yote yalitokea katika maisha yake lilikuwa ni kosa lake,na baada ya huo mwaka mmoja kama hali haitabadilika basi atakatisha maisha yake

Mwisho wa siku William James alijulikana kama Baba wa Filosofi nchini Marekani,alipewa heshima kama msomi,mwanasaikolojia,mwanafilosa

Alienda kutoa lecture Havard University,na Vyuo mbalimbali Marekani pamoja na Ulaya

Tambua kwamba siku zote huwa tunafanya maamuzi,hata kwa yale mambo ambayo yapo nje ya uwezo ila bado tunafanya maamuzi

Ni kwa kiasi gani utatafsiri yale yanayo kutokea na kuchukua maamuzi ambayo yatakuathiri au laa iko juu yako

Mfano umeachwa na mpenzi wako,una mambo mawili ama uchague kulialia na kupata msongo wa mawazo na kushindwa kufanya majukumu yako ya kila siku

Au

Utafsiri kwamba huyo hakuwa mtu wako wa kudumu alipita kwako akupe uzoefu fulani kisha utakutana na mwenza wa maisha yako

Hapo utaona kwamba always huwa tunafanya maamuzi

.................
 
WAJIBIKA KWA MAKOSA YAKO


Mara nyingi au kama sio mara zote huwa hatupendi kuwajibika kwa makosa yetu ila huwa tunapenda kuwalaumu wengine kwa makosa yetu,kwa kufanya hivyo tunadhani tunajifariji kumbe tunajidhuru wenyewe

Ebu soma mfano huu,bwana Etugrul bey baada ya kuachwa na mpenzi wake ambaye aliamua kuanzisha mahusiano mengine,Etugrul bey alimlaumu sana ex wake kuwa ndio sababu ya kuvunjika kwa uhusiano huo

Na kibaya zaidi akaenda mbali zaidi kumlaumu kwa maumivu ya kuachwa anayoyapata,akamlaumu kwa kukosa furaha,amani na utulivu

Lakini baadae baada ya kukaa chini na kutafakari kwa kina,Etugrul bey akagundua kwamba kumbe hata yeye alichangia sana mahusiano yake kuvunjika,na bahati zaidi hakusoma mapema alama za nyakati au kugundua viashia ambavyo ex wake alivionyesha kuashiria kwamba hakuwa na furaha katika mahusiano hayo

Baada ya Etugrul bey kuchimba na kuchimba zaidi akagundua hakuwa akimjali ex wake kama alivyopaswa kujali,alikuwa na majivuno na hakumpa ex wake attention ambayo alipaswa kumpa,hapo akatambua moja kwa moja kumbe anae ni sababu ya mahusiano hayo kufa

Lkn aligundua kwamba pamoja na kuachwa,ex wake hakuwa ni sababu ya yeye kukosa amani na furaha,hakuwa sababu ya yeye kukosa usingizi usiku na hakuwa sababu ya yeye kuwa na stress

Baada ya kufikiria kwa undani zaidi akajua kwamba pamoja na kuachwa,kumbe ilikuwa ni wajibu wake kufikiri na kuyachukulia mambo katika namna ambayo ingekuwa na manufaa kwake,angechukualia kuachwa huko kama namna moja ya kujifunza na kujua mapungufu yake next time awe mtu bora zaidi

Kwahiyo baada ya kuyajua hayo yote,bwana Etugrul bey ameamua sasa kuwajibika kwa yote yaliyotokea,ameamua kuwa mtu bora zaidi na amejifunza kutoyachukulia mahusiano poa,na atakuwa tayar kuhakikisha makosa ya zamani haya jirudii tena.

Watu wengi huwa tunadhani tunapaswa kuwajibika kwa mafanikio na furaha yetu tu, lakini hatujui kwamba tutapo wajibika kwa matatizo yetu itatupa nafasi ya kujifunza zaidi na kua watu bora,na istoshe matatizo hutuimarisha zaidi

............
 
UNAPOPATA MATATIZO HUWA UNAKIMBIA AU HUWA UNAPAMBANA NAYO


Mwaka 2008 Taliban walichukua utawala wa pakistani kimabavu na kuweka utawala wao wa sheria,ikiwemo kuzuia matangazo ya television,hakuna sinema,hakuna wanawake kutoka nje ya nyumba zao bila kuongozana na mtu wake wa karibu kama baba au kaka

Na istoshe wakazuia wanafunzi wa kike kuendelea na elimu,lakini binti mmoja anaitwa Malala mwenye umri wa miaka 11, yeye alipinga uamuzi huo,na kuamua kuhudhuria shule kama kawaida,na alikuwa mstari wa mbele kupaza sauti na kupigania haki ya watoto wa kike kwenda mashuleni

Mnamo mwaka 2012 akiwa anatoka shule na wenzake,mara paap wakasimamishwa na askari wa taliban,akiwa amebeba silaha au bunduki,na kuwauliza abiria waliokuwa mle ndani ya basi,kwamba nionyesheni Malala

Kwa mshangao mkubwa na ujasiri Malala akajitambulisha mwenyewe,na hapo hapo yule gun man akampiga Malala risasi ya kichwa,na wakasema kwamba kama binti huyo atapona basi watamuua yeye pamoja na baba yake

Lakini kwa neema ya Mwenyezi Mungu alipona na kuendelea na harakati zake kama kawaida,kwa hali ya kawaida tungetegemea angeogopa na kuacha harakati zake,lakini binti wa watu kwa ujasiri mkubwa kabisa,ndio kwanza alipata hamasa na nguvu mpya ya kupigani haki wa wanawake na kuwa msemaji wao

Kutokana na jitihada zake mnamo mwaka 2014 alipata Tuzo ya Nobel na kutambuliwa mchango wake katika jamii

Je wewe ni aina ya watu kama Malala ambao huwa hawa quit pale wanapo kutana na changamoto? Au ndio changamoto kidogo unakata tamaa na kukimbia

Ngoja nikwambie kitu msomaji wangu,hii dunia inahitaji watu ambao wapo strong enough to fight back,watu ambao huwa wanasonga mbele daima na kurudi nyuma kwao ni mwiko

Hata wewe pia unaweza kuwa imara na madhubuti kama Malala.
 
KUWA MAKINI NA KILE UNACHOAMINI

Mwaka 1988 akiwa katika chumba cha matibabu ya kisaikolojia mwandishi wa habar na mwanaharakati wa haki za wanawake Meredith Maran alimshutumu baba yake mzazi kuwa alimnyanyasa kingono

Wakati huo ndio huduma mpya ya repressed therapy ilikuwa imegunduliwa,ni huduma ya kutatua changamoto za kisaikolojia kwa kujaribu kuchambua au kupekenyua kumbukumbu ambazo zimejificha

Sasa iko hivi ubongo wetu huwa hauna jipya zaidi ya kuyafanyia kazi mambo ambayo tayar unayajua au ambayo yameshawahi kukutokea hapo zamani,kwahiyo mambo yoyote mapya ambayo yatakutokea sasa hivi katika maisha yako,basi ubongo wako utajaribu kutafuta data za zamani ambazo zinaendana na uzoefu mpya

Sasa toka awali mwanamama Meredith Maran hakuwa na uzoefu mzuri na baba yake,kwakifupi hawakuwa na mahusiano mazuri katika ukuaji wake

Pili,mahusiano yake na wanaume wake hayakuwa mazuri hivyo alikuwa na kila sababu kuwachukia wanaume

Na kibaya zaidi akiwa mwandishi wa habari alifanya utafiti kuhusiana na unyanyasaji wa watoto wadogo ambao watuhumiwa walikuwa ni wanaume

Na kwa miaka ile ya 1980's kulikuwa na kesi nyingi sana za unyanyasaji wa watoto,lakini kumbe hofu na kumbukumbu ambazo hazikuwa sahihi zilizo sababishwa na aina mpya ya matibabu ya repressed therapy ndio zilisababisha kuibuka kwa imani ambazo sio za kweli kuhusiana na unyanyasaji wa watoto

Ikagundulika kuwa kesi nyingi hazikuwa za kweli na matokeo yake kila mtoto alipofanyiwa hiyo therapy alisema alinyanyaswa kingono,baadae hao wataalamu wa hizo therapy walifungiwa leseni zao na wengine kufungwa kabisa

Tukirudi kwa Meridith Maran akajiingiza kwenye mapenzi ya jinsia moja na mwanamke mwenzake ambaye ni victim wa unyanyazaji wa watoto huko miaka ya nyuma,basi ndio akaathirika vibaya na kuamini Baba yake alimnyanyasa kingono

Ila baadae alikuja kujua amefanya makosa,na wakati huo tayar uharibifu mkubwa ulishatokea katika familia,alitumia karibia miaka miwili kuomba msamaha kwa baba yake na bahati mbaya baba yake alikufa kabla hajamsamehe

Kwahiyo kuwa makini sana na kile unachokiamini huenda sio kweli!
 
KUFELI NDIO MWANZO WA MAFANIKIO

Kufeli ni sehemu ya mchakato wa maisha,ukiona mtu amefanikiwa sana basi ujue alifeli sana

Bahati mbaya tu,huwa hatupewi taarifa za kufeli za walio fanikiwa,lau tungejua upande wa shilingi tungejifunza mengi sana

Ukiona mtu hajafanikiwa kama level uliyofikia wewe basi tambua hakujaribu na kufeli sana,kwani maedeleo yanapatikana kwenye kufeli sana

Lau tukiambiwa huu mtandao wa Jamiiforums umepitia changamoto gani,basi huenda tukawapa big up sana hawa waanzilishi akiwemo founder mwenyewe Melo

Naamini nao walifeli sana mpaka kufanikiwa kuisimamisha hii App mpaka nasi tunatamba nayo,kwahiyo siri ya mafanikio ipo kwenye kufeli zaidi

Kwahiyo usiogope kufeli,haijalishi ni mara ngapi unafeli,kwa kila kosa unalokutana nalo linakupa nafasi ya kujifunza zaidi

Inasemekana yalifanyika makosa 1000 mpaka balbu hii tulinayo inaonekana kama tunavyoiona

Bwana Henry Ford aliwahimiza mafundi wake wapambane karibia mwaka mmoja mpaka wakafanikiwa gari ya silinda sita,kila mafundi wake walipo mwambia mheshimiwa haiwezekani,aliwaambia keep working,na matokeo yake walifanikiwa

Kwahiyo usihuzunike kufeli zaidi bali endelea na mchakato mpaka kielweke
 
Back
Top Bottom