Kijana nakupa hii toka kwenye kitabu changu kiitwacho vita dhidi ya ugaidi, kitabu kipo chini ya Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania.
NYOTA YA RUMSFELD ILIVYO ANZA KUNGAA NDANI YA REPUBLICAN.
Rumsfeld mtu mwenye umbo dogo na uso wa kijana, rubani wa zamani wa jeshi la maji ambaye hakuonekana umri wake wa miaka 69 kuwa mkubwa katika kipindi cha mgogoro, alikuwa anasubiri amri kutoka kwa Rais huyo kwaajili ya majukumu. Mwanzoni mwa mwaka wakati Rumsfeld alikuwa katika majadiliano kuhusu kuwa waziri wa ulinzi wa Bush alifanya mazungumzo na rais mteule huyo, alimwambia Bush kwamba, wakati kwa miaka minane ya Clinton muundo wa asili uliendelea kuwa ni wa kutumia tahadhari na usalama. Na chaguo la silaha kwa upande wa Clinton lilikuwa ni kombora lenye kuongozwa kwenye lengo.
Rumsfeld alimweleza wazi Bush kwamba iwapo muda ungefika kama ilivyokuja kutokea ukafika kweli kwamba Marekani inakabiliwa na tishio yeye akiwa waziri wa ulinzi angemshauri rais kutumia jeshi. Bush alikuwa amejibu wazi wazi makadirio ya Rumsfeld kwamba hivyo ndivyo hasa alivyokuwa anataka. Rumsfeld aliamini kwamba walikuwa na msimamo wa wazi na wa pamoja. Rumsfeld alikuwa mmoja wa nyota zinazo ngara zaidi ndani ya chama cha Repblican, mnamo miaka ya 1960 na 1970 akiwa na sifa kama za John F. Kennedy mwenye sura nzuri mkakamavu, msomi, mwenye busara, mcheshi na mwenye tabasamu la kudumu. Watu wengi katika chama hicho akiwemo Rumsfeld mwenyewe walikuwa
wanafikiri kwamba njia yake ilikuwa inamwelekeza kwenye urais .Lakini kamwe hakuweza kupata sifa ua umaarufu au sura ya kuwa na msimamo wa ukorofi dhidi ya watu waliokuwa chini yake kikazi. Isitoshe alijikuta akiwa adui wa mmoja wa nyota wa chama hicho aliyekuwa akiibuka, yaani George W. Bush ambaye alikuja kuufikia urais.
Kuibuka kwa Rumsfeld hadi kufika katika ngazi za madaraka ya ndani ni habari inayotokana na mapito magumu, juhudi binasfsi na majungu. Na habari mnamo 1962 akiwa na umri wa miaka 30 zinasema, Rumsfeld alichaguliwa katika vipindi vinne katika baraza la Congress akiwa mwakilishi wa vitongoji vya ufukwe wa kaskazini wa Chicogo ambako alikuwa amekulia, Alijiuzulu kutoka Congress mwaka 1969 na kuwa mkurugenzi wa Ofisi ya Fursa za kiuchumi taasisi yenye kupiga vita umasikini ambayo ilikuwa ni cheo cha uwaziri katika utawala wa Nixon cheo ambacho ni maarufu na chenye kuonekana sana.
Mnamo 1973-74 alikuwa Brussels akiwa balozi wa Marekani katika Umoja wa kujihami wa nchi za Magharibi (NATO) na hivyo kuweza kukwepa kashfa ya Watergate. Kwa mujibu wa kitabu cha simulizi ya maisha ya Nixon, mnamo Julai 1974, Donard Rumsfeld alipiga simu kutoka Brussels akitaka kujiuzulu akiwa balozi wa NATO na arejee kusaidia kazi dhidi ya kufunguliwa mashitaka kwa washirika wake wa zamani. Nixon alijiuzulu mwezi uliofuata na Rumsfeld aliombwa kuwa mwenyekiti wa timu ya kusimamia kipindi cha mpito kabla ya mshirika wake wa zamani Gerad Ford kushika nafasi hiyo. Ford alimwomba Rumsfeld kuwa mnadhimu wa Ikulu lakini Rumsfeld alitaka kubakia NATO. Rumsfeld alikubali wakati Ford alipoahidi kuzipanga upya safu za wafanyakazi na kumpa Rumsfeld madaraka kamili.
Baada ya mwaka mmoja akiwa Ikulu, Ford alimwambia kwamba alikuwa na mpango wa kumwondoa waziri wa ulinzi, James Schlesinger hivyo Rumsfeld angehamia katika wizara ya ulinzi na Mkurugenzi wa CIA William Colby nafasi yake ilikuwa ichukuliwe na George Bush mkubwa ambaye wakati huo alikuwa mwakilishi wa Marekani nchini China. Katika faragha, Rumsfeld alikiita cheo hicho cha China kuwa ni kazi ya ovyo na isiyokuwa na uhusiano wowote na siasa mbele ya nyuso za wamarekani,
Alikuwa anapinga majukumu hayo mapya kwa Bush na yeye mwenyewe, alimwambia Ford kwamba, kuwaweka pembeni watu hao kungesaidia katika kuwatumia wakati wa kampeni ya kugombea urais ikifika. Alisema kwamba wao walikuwa ni watu wawili pekee ambao wangetoa hotuba thabiti za kisiasa katika uchaguzi ambao ungefuatia katika mwaka wa uchaguzi wa 1976. Lakini Rumsfeld alikubali na kuchukua wizara ya Afya. Bush mkubwa alikuwa anaamini kwamba Rumsfeld alikuwa anamwondoa kwa siri kutoka katika CIA ilikummaliza kisiasa. Wakati huo ilionekana kwamba mkuu wa ujasusi na mwenye kupanga njama chafu nchi za nje asingeweza kuwa rais. Rais Ford wakati huo alimpandisha cheo naibu wa Rumsfeld Bw. Dick Cheney kuwa mnadhimu wa Ikulu
Wakati huo pakiwa na manunguniko kuhusu kuingiza siasa katika CIA, baraza la Seneti lilikuwa linakataa kumthibitisha Bush mkubwa kuwa mkurugenzi hadi hapo Ford aahidi kutomchagua kuwa makamu mgombea mwenza wake katika uchaguzi ambao ungefuata, Rumsfeld aliwambia Ford na Cheney kwamba rais asikubali shinikizo la Seneti. Hatimaye Ford na Bush walipata ahadi hiyo kwa Seneti, Rumsfeld alimlaumu Cheney kwa sehemu fulani akimwambia kwa maneno mengi kwamba Umevuruga mambo katika jambo ulilofanya Mnamo katikati ya mwaka uliofuata 1976, paliibuka aina ya upinzani kati ya waziri wa Ulinzi Bush mkubwa na Rumsfeld, Rumsfeld alikuwa amemwomba Bush kuwa mtu mwepesi mwenye kupendelea urafiki na uhusiano na watu wengi katika maoni yake, Bush mkubwa alikuwa anaepuka migongano isiyokuwa yalazima katika maeneo ya Ikulu.
MAJENERALI WAFOKEWA
Hoja za Rumsfeld zilizofuata zilikuwa za ajabu, kila mara alikuwa akinukuu kitabu cha Pearl Habour Warning and Decision kilichoandikwa na Robert Wohlstetter. Alikuwa akiweka msisitizo katika utangulizi wa kitabu hicho ulioandikwa na Thomas Schelling ambaye alikuwa akitoa hoja kwamba tukio la Pearl Harbour lilikuwa ni kosa la kawaida ambalo linaweza kufanywa na serikali. Katika mipango yetu kuna tabia ya kuchanganya mambo mageni na yale ambayo hayawezekani, hatari yenyewe imo katika mapungufu ya matarajio, chuki za kawaida pamoja na hatari kadhaa ambazo huwa za kawaida. Mipango ya Rumsfeld katika kuleta mabadiliko ilikabiliwa na upinzani kadhaa miongoni mwa safu za askari.
Ofisa mmoja mwenye cheo cha nyota nne ambaye alikuwa akifanya naye kazi alimwelekeza Rumsfeld kama jamaa mmoja mjanja ambaye huonyesha sura isiyokuwa yake. Mwingine alimwelezea kwamba iwapo mtu atapingana na Rumsfeld basi ajue hali hiyo ni ya hatari, ofisa huyo alisema. Nilikuwa napanda kwenda katika ofisi ya Rumsfeld katika ghorofa ya tatu na ikitokea tulikuwa hatukubali nilimweleza wazi kwamba nilikuwa sikubaliani naye kuna nyakati alikuwa anafurahia hali hiyo na kuna nyakati alikuwa hafurahii hali hiyo. Kuna nyakati Rumsfeld alikuwa anawafokea majenerali ofisini mwake akiwaambia njoni mtoe maelezo ya mambo ambayo mnayafahamu. Wakati mnazungumza matatizo yalikuwa yanawapata maofisa ambao walikuwa wanatoa
maelezo yasiyokuwa na ufumbuzi thabiti kwa Rumsfeld kwani alitaka kujua walivyofikia maamuzi na sababu kamili za kufanya hivyo. (Kwamujibu wa Colonel G. Dster)
Hali hii iliwachanganya maofisa wa ngazi za juu Na Rumsfeld alikuwa akiwakabili na maswali magumu baadhi ya maswali hayo yalikuwa ni: Ni nini unafahamu kuhusiana na suala hilo?, Unafikiri ninapaswa kukuuliza nini?, Hiyo ndiyo njia pekee ambayo nitaielewa hali halisi. Alikuwa anasema na kuongeza kwamba na hakika hiyo ndiyo njia pekee ambayo na wewe utajifunza mambo! Alionekana kujiamini mno na kutowaamini watu waliokuwa chini yake jeshini akiwa anafanya kazi na kikundi chenye kuwasiliana kwa karibu. Kikundi ambacho washiriki wake wengi wao walikuwa ni raia. Kilikuwa ni kama kioja kwa watu wengine katika jengo hilo, jopo la pamoja la wanadhimu na wakuu wa jeshi la kawaida, jeshi la majini la anga na askari wa miavuli. Rumsfeld hakupenda kuchanganya mambo.
Hakutaka kufanya mambo yasiyotimia alikuwa kila mara anaipanga upya mipango mbali mbali na kuifanyia marekebisho alikuwa anachukia lugha za kijinga Neno Combone lilikuwa daima mdomoni mwa Rumsfeld kila alipokuwa akitaka kupata habari au kufanya jambo fulani alimtumia Steve Cambone mwenye urefu na mwenye utaalamu wa hali ya juu katika mambo ya ulinzi aliyewahi kufanya kazi kwenye tume za ulinzi katika anga za juu za makombora, tume ambayo Rumsfeld alikuwa amewahi kuiongoza Alikuwa ni raia msaidizi maalum kwa waziri huyo na alikuwa kielelezo kikubwa cha uhusiano kati ya Rumsfeld na wafanyakazi wenzake katika wizara ya ulinzi. Combone alikuwa ndiye chombo alichokitumia Rumsfeld katika kuwafikia maofisa wa ngazi za juu jeshini.
Jenerali Henry B. Hugh Shelton, mwenyekiti wa jopo la wanadhimu tangu 1997 hakupendelea sana uongozi mpya wa kiraia ambapo alikuwa akiwajulisha wenzake migongano na Rumsfeld. Katika tukio moja Rumsfeld alipendekeza kwamba Shelton alilazimika kutoa ushauri wake wa kijeshi kwa rais kupitia kwake. Shelton alilazimika kusema kwamba sheria imemfanya kuwa mshauri mkuu wa mambo ya kijeshi kwa rais na aliamini kwamba ushauri wake ni lazima utolewe kwa rais moja kwa moja. Pamoja na mikwaruzo aliyokuwanayo Rumsfeld na maofisa wengine bado waliheshimu kwa akili katika utaalam wake. Jenerali mmoja mwandamizi aliwahi kusema Namheshimu sana kwa umahiri kwamba nimependa unyonge wake ni kutaka kila kitu akifanye Akiwa ameyafahamu mashambulizi dhidi ya kituo cha kimataifa cha biashara, Rumsfeld alikuwa akishughulikia mambo yake ya kila siku habari za kijasusi ofisini mwake zilisema ndege ya tatu iliyokuwa imetekwa ilijibamiza kwenye eneo la magharibi la jengo la makao makuu ya wizara ya ulinzi alihisi kuchanganyikiwa akakimbia kwenda dirishani lakini mahali alipokuwa hakuweza kuelewa hasa kimetokea nini. Alitoka nje na kufuata eneo lililokuwa na moshi uliokuwa ukisambaa angani kutoka mahali ndege hiyo ilipojibamiza
akaanza kushiriki katika kazi ya uokoaji kabla ya ofisa mmoja wa usalama alipomwambia aondoke eneo hilo.
Nakwenda ndani Rumsfeld alisema na haraka akaenda katika kituo cha taifa cha mipango ya kijeshi ambacho ni chumba kimoja kikubwa chenye wafanyakazi wengi. Katika jengo hilo chumba kilikuwa kimejaa moshi hivyo yeye na wenzake walikwenda katika chumba maalum cha mawasiliano kilichokuwa kinaitwa Cables ambapo hewa ilikuwa nzuri kidogo.Jenerali Myers alimtaka Rumsfeled aondoke moshi unazidi kuzagaa kila mahali, alisema kuna watu wengi wanaohangaika kutoa misaada huko hali ni mbaya zaidi kuliko hapa, wengine wasingeweza kuondoka kama Rumsfeld alikuwa bado yupo hapo.
Mnaonaje tukiondoka hapa? Sawa Rumsfeld alisema, lakini akaendelea kufanya kazi. Jeshi ambalo lilionekana kuwa na mipango mbali mbali isiyotegemewa ilikuwa Afghanistan kituo cha Bin laden na mahali penye kutayarishwa mipango yake.Hapakuwa na hati yoyote ambayo ingeweza kusomwa angalau kupata picha yoyote kuhusiana na tukio hilo. Jambo hili halikuwa la kushangaza kwa waziri huyo wa ulinzi. Alimgeukia Myers na kusema, kila nilipotaka kuona mipango kadhaa nimekuwa sifurahi yale niliyokuwa nayaona ni wazi mipango hiyo ni ya zamani na imekuwepo katika makabati ya hati kwa muda mrefu mno, Sijaifurahia hali hiyo bado tuna mambo mengi ya kufanya nabidi kulifahamu hilo, Nafahamu, bwana Myers akajibu.
Chanzo: Kitabu cha Vita dhidi ya Ugaidi kilichoandikwa na
Yericko Nyerere.
About these ads
Occasionally, some of your visitors may see an advertisement here.
Tell me more | Dismiss this message
Share this:
Press This
Twitter
Facebook