Siri ya Malkia Elizabeth wa Usikochi (UK), Kanisa Katoliki, Nyerere na Uhuru wa Tanganyika

Siri ya Malkia Elizabeth wa Usikochi (UK), Kanisa Katoliki, Nyerere na Uhuru wa Tanganyika

KWANZA NAOMBA USHAHIDI WA BANDIKO LAKO KWASABABU MEENGI YANAONEKANA NI MAMBO YA KUTUNGWA NA KUNGAUNGA.

PILI SIKUJUA, KUMBE BIBLE INAONGEZWA VIONJO NA MANJONJO KILA KUKICHA KWA BARAKA ZA VIONGOZI WA KANISA???

Askofu Maranta aliletewa mapendekezo
kutoka kwa Attilio Beltramino kassi wa katoliki
aliyehudumu kule Iringa, mapendekezo ya kasisi
huyu yalikuwa ni, Umishonari makao makuu
uruhusu udurufu wa biblia zisomeke kwa makabila
ya wahusika wa eneo, ndani ya biblia hizo
yaongezwe mafundisho ya haki ya kujitambua na
kujitawala wenyewe. Pendekezo hili lilimvutia
sana Maranta hivyo akalipa baraka zake, kwa
hakika lilifanikiwa na ndio lilizaa hisia kali za
mwamko wa kudai uhuru, mfano biblia ya lugha ya
kihehe ilikuwa inaeleza wazi athari za
kutawaliwa.


SASA MPAKA IFIKE MWAKA 2200 BIBLE YAO ITAKUWA NA UHUSIANO WOWOTE NA HII YA SASAHIVI?

NAPATA MASHAKA KAMA HII BIBLE YA SASAHIVI INAUFANANO WOWOTE NA ILE YA MIAKA 2000 ILIYOPITA KWASABABU KWA MUJIBU WA MAELEZO YAKO NIMEGUNDUA KILA NCHI INAO UWEZO WA KUBADILISHA BIBLIA NA KUONGEZA AU KUPUNGUZA INACHOONA KINAFAA.

cc mohamedsaidi kakhtaan Pasco BAK ishmaeel

hizo dini zote ni mipango miji tu ndugu,mungu wa kweli hayupo kwenye hizo dini,sasa hao wanaobadilisha bible wanalijua hilo,na kwa maono ya mbali itawasaidia ku survive,tatizo naliona kwa muamedi, msaafu kaupiga pin ya hatari hakuna kubadilisha kitu,kama waislam watang'ang'ana na huo msaafu bila kufanya mipango miji, mwisho wake utakua mbaya sana dunia imebadilika sana, hivyo vitabu vimepitwa na wakati ni old school,amendment ni lazima, tatizo hapa sijui kama unaona kama ninavyoona mimi, hili nalo ni tatizo
 
Last edited by a moderator:
Wanamajlis JF,
Sahib yangu mmoja hivi punde kaniletea ujumbe kuwa natafutwa barazani.
Natafutwa kwa sababu kuna bandiko la Yericko Nyerere natakiwa nijibu.

Nimelisoma bandiko lakini kwa kweli lazima uwe umepitia kozi inayoitwa,
"Reading Difficulty Passages," kuweza kuielewa khasa maudhui yake ni yepi.

Kuna swali la udugu baina ya House of Windsor na Burito Nyerere wa
Butiama.

Hapa nimemvulia kofia Yericko.
Waingereza wenyewe watachoka.

Mimi mwenyewe nimepwelewa kwa kuwa kujibu kitu kisochoeleweka si mchezo.
In Sha Allah ngoja nijaribu.

Katika utafiti wangu mimi wakati naandika kitabu cha Abdul Sykes ndipo kwa
mara ya kwanza nikakutana na maisha ya Nyerere katika siasa na nafasi ya
Queen Elizabeth katika utawala wa Tanganyika.

Wanamajlis,
Hebu someni hii hapa chini nanyi mpate kuelewa historia ya Nyerere na Queen
Elizabeth
kama nyaraka za Sykes zinavyoeleza:

[TABLE="width: 601"]
[TR]
[TD]"Ally Sykes allowed me to interview him on many occasions in spite of his busy schedules managing his business from his city center office. He allowed me to consult his own private files, personal letters, diaries and other family records. These records were kept in a safe which I was informed remained untouched for over 30 years. Going through the files I was amazed by Ally Sykes' obsession with record keeping. Every piece of paper with information was kept, however trifling it may have seemed during the struggle-a 1954 pencil note from Zuberi Mtemvu to Ally Sykes, informing him of a discussion he had with Nyerere about him and TANU; a 1953 money order receipt from Ally Sykes to Japhet Kirilo during the Meru Land Case; an undated copy of the letter from the TAA to Queen Elizabeth signed by the entire executive (President, Julius Nyerere, Vice-President Abdulwahid Sykes, General Secretary Dome Okochi, Assistant Secretary Dossa Aziz, Treasurer John Rupia, Assistant Treasurer Ally Sykes) congratulating Her Majesty on her coronation; a 1952 letter from Rashid Mfaume Kawawa from Bukoba to Ally Sykes informing him of the political situation in the Lake Region; a 1963 letter from Lady Judith Listowel; letters from Kenneth Kaunda, Julius Nyerere, Kasella Bantu ... the list is endless..."[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Katika utafiti wangu wote kabla ya uhuru hapa ndipo kwa mara ya kwanza nimeshuhudia
mawasiliano kati ya Nyerere na Queen Elizabeth mwaka 1953 na nyaraka hiyo nimeikuta
katika mafaili
ya akina Sykes.

Yericko anaweza labda kuja na ushahidi mwingine unaoonyesha kuwa Nyerere na Queen
Elizabeth
walikuwa wakijuana na wakiwasiliana kabla.

Tuvute subra.
 
Hivi Yeriko ndugu yangu, Ziwa Victoria lipo Kaskazini mwa Tanzania!?
 
Yericko,
Umekosea jina.

Jina lake ni "Edgar" siyo Edger. Mimi nikiwa mwanafunzi St. Joseph's Convent nilikuwa nikimfahamu vyema.

Wakati mwingine anakuja shule na siku nyingine tunamoona pale Parish Hallau St. Joseph's Cathedral. Kabla hujaandika angalau fanya utafiti kidogo vinginevyo unakuwa kichekesho.
 
Wakuu naona Mohamed Said kagoma kuja km yule mbuzi wa msibani. Na ile formula ya dawa ya kumfanya mbuzi awe ----- hatuna. Dah nomaaaaaaa Sana. Jaribuni kumfuata pale kijiweni kwake lumumba teh teh teh teh. Hv viumbe vya aina ya Yericko vinapatikana wapi??????

Mkwaju Ngoma,
Nimefika kaka yangu.

Sikuwa na taarifa kuwa natakiwa majlis.
 
Watanzania kama Yericko Nyerere wapo wengi sana.Wengine ni maprofesa na walimu wa vyuo mbali mbali nchini"Build a church and university to make us a fool" huyu Yericko leo anakana kwamba Biblia ni maneno ya mungu,Pengo unamsikia Yericko? hawa watu kama Yericko na wale wanaojiita Alshabab ndio huvuruga nchini kwa falsafa zao za kishetani.

Mwache babu yako apumzike huko aliko.Atalipwa kwa mema aliyoyatenda na maovu aliyoyatenda.
Tanzania inabidi tuwe makini na makundi/watu wa/yanayoleta falsafa za kishetani.

Ni muhimu sana taifa liongozwe na watu wenye akili si hivyo wakoloni wataendelea kunyonya ubongo na kuacha mafuvu yasiyoweza kufikiri.
 
Mohamed Said

Natilia shaka sana tafiti zako nyingi sana, uliku unajifungia kwenye mlengo mmoja zaidi, nivigumu kuupata ukweli wa jua na mwezi kama kama unatafiti huku umejifungia ndani ya chumba chenye tundu moja juu tu.

Malkia Elizabeth na Julius Nyerere walikuwa wamoja sana, maasi jeshi ya mwaka 1964 ni Malkia aliyekubali ombi la Julius Nyerere na kisha kutuma kikosi maalumu cha Makomandoo waliofanikisha kuzima uasi ule.

Ulishindwa hata kutumia ushahidi huo tu wakubaini usharika kati ya Julius na Malkia?
 
Last edited by a moderator:
peri

Unachanganya mboga kwa jinsi roho inakuuma.Mohamed Said si huwa anaandika mengi huwa mnamuuliza uthibitisho? Kwani mlishwahi uliza uthibitisho km kweli Mkwawa alikuwa mkombozi wa waafrica na si kibaraka wa waarabu dhidi ya waafrica na wamissionary waliokuwa wakipinga utumwa na vita za kishenzi mkwawa ili ateke watu.
 
Last edited by a moderator:
Murua, makini haipepesi macho..inayotofautisha na kutofautisha tofauti tulizo nazo ktk fikra,ktk kujenga na si kubomoa, katika kusaidia na si kusaidiwa, katika kuweka akiba na si kugombania kugawana akiba.
 
Haha unamkaribisha huyu mzee, yeye anajua habari za gerezani na viunga vya ghahawa tu
Inanikumbusha thread iliyorushwa baada ya kelele nyingi sana kuhusu Mabomu ya Olasiti na haswa Pale Soweto Arusha.Kwa muda mfupi sana ile thread ilikata ukimya.Ile thread ilifanya mioyoyo ya watu ikatikisika na pumzi kubadilika.Hii thread ikiachwa na Mods mohamded Said na akina Ritz hawana pa kutokea zaidi ya kudai references.Wakati zao zina jikuuu zenyewe na stori za kijinga sijui nilimuuliza yeye,sijui nilikaa nae, sijui nini na nini...Mohamed Said ni km mwandishi anayekwenda mhoji msajii mchovu au mcheza soka aliyefulia atakvyojidai enzi zao walikuwa wanajua mpira,sijui walikuwa na uzalendo..halfu ukiwauliza walifanikiwa au kulifikisha taifa wapi majibu hutapata..ila usipowauliza utaandika habari yao km ushahidi wa ubora a ukweli wao.
 
Inanikumbusha thread iliyorushwa baada ya kelele nyingi sana kuhusu Mabomu ya Olasiti na haswa Pale Soweto Arusha.Kwa muda mfupi sana ile thread ilikata ukimya.Ile thread ilifanya mioyoyo ya watu ikatikisika na pumzi kubadilika.Hii thread ikiachwa na Mods mohamded Said na akina Ritz hawana pa kutokea zaidi ya kudai references.Wakati zao zina jikuuu zenyewe na stori za kijinga sijui nilimuuliza yeye,sijui nilikaa nae, sijui nini na nini...Mohamed Said ni km mwandishi anayekwenda mhoji msajii mchovu au mcheza soka aliyefulia atakvyojidai enzi zao walikuwa wanajua mpira,sijui walikuwa na uzalendo..halfu ukiwauliza walifanikiwa au kulifikisha taifa wapi majibu hutapata..ila usipowauliza utaandika habari yao km ushahidi wa ubora a ukweli wao.

Nicholas,

Umesema kweli mimi najinukuu mwenyewe.

Nilipata kumwambia mwalimu wangu Chuo Kikuu kuhusu historia ya TANU
na nikamueleza watu waliokuwapo wakati ule chama kinaasisiwa.

Akaniomba rejea.
Nilimjibu kuwa sina rejea ila kauli za wazee wangu.

Nikamwambia kuwa babu yangu Salum Abdallah alihudhuria mikutano yote
ya siri ya kuasisi TANU iliyokuwa ikifanyika Town School, Tabora.

Mikutano hii ilikuwa ikiitishwa pale na Sheikh Abubakar Mwilima ambae alikuwa
mmoja wa walimu pale shuleni.

Hii ilikuwa katika mwezi June 1953.

Nikamfahamisha kuwa mwaka wa 1947 na 1949 babu yangu aliongoza "general
strike."

Nikamfahamisha kuwa yeye ni kati ya wanachama wa mwanzo wa TANU Tabora
na ilipofika 1955 alikuwa rais muasisi wa Tanganyika Railway African Union (TRAU)
Kassanga Tumbo akiwa katibu.

Nikaendelea kumweleza kuwa mwaka 1960 miezi michache kabla Tanganyika
haijapata madaraka babu yangu aliongoza mgomo uliodumu siku 82 na kuvunja
rekodi ya mgomo ulioogozwa na Makhan Singh wa Kenya uliodumu siku 62.

Nikamaliza kwa kumwambia kuwa ikiwa yeye anataka kuamini historia rasmi
ya Chuo Cha Kivukoni sina uwezo wa kumzuia lakini mimi naijua historia ya TANU
kutoka kwenye vinywa vya waasisi wenyewe.

Babu yangu aliwekwa kizuizini mwaka wa 1964 kufuatia maasi ya wanajeshi.
Baada ya kutoka jela hakushiriki tena siasa hadi alipofariki mwaka 1974.

Kwenye maziko yake TANU ilisoma taazia nzuri sana ya kumsifia kwa uzalendo wake
wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika.

Nicholas,
Kama nilivyomueleza mwalimu wangu nawe nakuambia hivyo hivyo kuwa una haki
ya kuamini historia uipendayo.
 
Mkwaju Ngoma,
Nimefika kaka yangu.

Sikuwa na taarifa kuwa natakiwa majlis.
Mzee Mohamed Said.

Huyu Yericko anatafuta credit kutoka kwako siyo level yako kufanya nae minakasha tuliona ule mnakasha uliyopita kumbe mtupu kabisa kwenye masuala ya history.

Nakushauri mmpuuze ndiyo maana umeona watu wengi wamemuachia huu uzi wake.


Shukran.
 
Unachanganya mboga kwa jinsi roho inakuuma.Mohamed Said si huwa anaandika mengi huwa mnamuuliza uthibitisho?Kwani mlishwahi uliza uthibitisho km kweli Mkwawa alikuwa mkombozi wa waafrica na si kibaraka wa waarabu dhidi ya waafrica na wamissionary waliokuwa wakipinga utumwa na vita za kishenzi mkwawa ili ateke watu.

Nicholas,
Nakuunga mkono.
Hapana haja ya kumkatalia Yericko hayo aliyoandika.

Hiyo pia inaweza kuwa ni upande mmoja wa historia ya TANU na bila shaka
itakuwa na mashujaa wake.

Muhimu ni kuangalia "sequence," ya historia hiyo na matokeo yaliyojiri
baina ya kuanzishwa kwa African Association 1929 hadi kuasisiwa kwa TANU
1954.

Je, zipo habari za Kleist Sykes na Dr. Kwegyr Aggrey katika kuasisi African
Association?

Je, zipo taarifa za uongozi wa AA uliokuwa pia ndiyo uongozi wa Al JAmiatul
Islamiyya fi Tanganyika?

Je, Dr. Vedasto Kyaruzi na Abdul Sykes wana mchango wa kubadilisha chama?
Abdillah Schneider Plantan yupo katika juhudi hizi?

Vipi Ramadhani Mashado Plantan alisaidia propaganda kuijenga TANU kupitia gazeti
lake, Zuhra?

Nyerere alikuwa mgeni Dar es Salaam aliweza vipi kufahamika na kuaminika?
Kazi hiyo aliifanya mwenyewe au kulikuwa na watu waliomleta katika "circle?"

Ikiwa historia hiyo ya Yericko haina lolote kuhusu wazalendo hawa kweli nayo ni historia
lakini itakuwa ni historia ya TANU nyingine siyo TANU tunayoijua wengi hasa sisi tuliokulia
Dar es Salaam na wazee wetu walikuwa ndiyo waasisi wa chama hicho.
 
Mzee Mohamed Said.

Huyu Yericko anatafuta credit kutoka kwako siyo level yako kufanya nae minakasha tuliona ule mnakasha uliyopita kumbe mtupu kabisa kwenye masuala ya history.

Nakushauri mmpuuze ndiyo maana umeona watu wengi wamemuachia huu uzi wake.


Shukran.

Carlos...
Nimekusikia.
Nimekuja kwa kuwa jamaa hapa Majlis walikuwa wanasema nimekimbia.
 
Natilia shaka sana tafiti zako nyingi sana, uliku unajifungia kwenye mlengo mmoja zaidi, nivigumu kuupata ukweli wa jua na mwezi kama kama unatafiti huku umejifungia ndani ya chumba chenye tundu moja juu tu.

Malkia Elizabeth na Julius Nyerere walikuwa wamoja sana, maasi jeshi ya mwaka 1964 ni Malkia aliyekubali ombi la Julius Nyerere na kisha kutuma kikosi maalumu cha Makomandoo waliofanikisha kuzima uasi ule.

Ulishindwa hata kutumia ushahidi huo tu wakubaini usharika kati ya Julius na Malkia?

Yericko,
Malkia wa Uingereza haiendeshi serikali.
Fanya utafiti kabla ya kuandika.

Unachekesha watu.
 
Yericko,
Malkia wa Uingereza haiendeshi serikali.
Fanya utafiti kabla ya kuandika.

Unachekesha watu.

Maalim wangu Mohamed Said

Nikweli hujui nafasi ya Malkia wa Cambridge/Uskochi/Muungano wa Kifalme(Uk) au unafanya makusudi?

Jikumbushe hapa chini kidogo,

JARIBIO LA KUPINDUA SERIKALI YA MWALIMU JULIUS NYERERE.



Japo historia haisemi wazi juu ya mambo mengi sana Tanganyika na Tanzania ya leo, lakini Mwalimu Nyerere tangu awe kiongozi wa nchi hii amenusurika mapinduzi MATATU,

Moja ni la mwaka 1964, lapili ni la mwaka 1970 na la mwisho ni la mwaka 1982

Jaribio la kwanza ndilo lilipelekea kuundwa kwa JWTZ na lilizimwa kwamsaada wa Malkia wa Uingereza aliyetuma makomandoo maalumu na wakafanikiwa, Jaribio la pili ndilo lililopelekea kuundwa kwa Usalama wa Taifa na kikosi maalumu cha ulinzi wa Rais,

na jaribio la mwisho ndio lilipelekea kubadili sera ya usalama wa Taifa kwa kuwapandikiza kila kwenye sekta na kuwa kila mtu ni mlinzi wa nchi hii (usalama

Leo nitazungumzia jaribio/uasi wa 20 Januari 1964 na nini hasa ilikuwa chanzo cha uasi ule.

Kuasi kule kwa Wanajeshi Januari/20/1964 (Tanganyika Rifles) wala sio jambo la zamani sana kiasi cha kusema kwamba Historia ile imetupwa na hakuna anayesema ukweli,nilikuwa nahisi Viongozi kama Mwalimu,kawawa na Kambona wangeyaweka katika maandishi mambo yale muhimu ktk Historia ya Nchi yetu kabla hawajatutoka.Hakuna mahali mambo haya yameandikwa na ndio maana Vijana wanaotaka kujua historia ya Nchi yao wanakuja na hizi hear/say

Askari wale wa Tanganyika Rifles waliasi...Miongoni mwa mambo waliyokuwa wanadai ni hali nzuri ya maisha ya askari mtanganyika,mshahara ulikuwa mdogo,hawakupandishwa vyeo na hakukuwa na Watanganyika katika vyeo vya juu ndani ya Jeshi lile.Askari waliasi na kuingia mjini,na wengine walikwenda kwenye Makazi ya Maafisa wa kiingereza (Raia) na kuwashikilia.Waziri wa Ulinzi wakati huo alikuwa Oscar Kambona....Mwalimu na Mzee Kawawa kwa usalama wao walitoroshwa na kwenda kujificha,inasemekana Maficho yao yalikuwa Kigamboni.Waziri wa Ulinzi (Kambona) alijaribu kupita ktk Barracks na kuwaomba askari watulie bila mafanikio.

Hali ile iliendelea kuwa mbaya,na Mwalimu kwa ushauri wa Kambona na Kawawa akaomba msaada kwa Uingereza ili waje waokoe hali ile ambayo ilikuwa inaelekea kuwa mbaya,kufuatia kuasi kwa Askari wetu,askari wa Kenya na Uganda nao waliasi kwa sababu sawa kabisa na za UASI wa Tanganyika Rifles.

Malkia alituma kikosi maalumu cha Askari wa Uingereza ambao walikuwepo ktk ghuba ya Aden,Askari hao walikuja na Meli kubwa ya kivita HMS Centaur ambayo ilikuwa na Makomandoo (45 RM),askari na helikopta. Walifanikiwa kutuliza maasi yale, na Mwalimu na Kawawa wakatoka mafichoni na kuonekana hadharani wakiwa na Waziri wa Ulinzi, ambaye alifanya kazi kubwa bila mafanikio kuwaomba askari(Waliokuwa wananuheshimu sana) waache uasi na madai yao yatafanyiwa kazi.

Ukitaka kupata mambo mengi kuhusu maasi yale pitia kitabu "Dar Mutiny Of 1964" by Christopher MacRae
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom