Wanamajlis,
Mie nihangaike nini?
Kipi katika uzee huu niliokuwanao kitakuwa kigeni kwangu kinizonge?
Mimi niko hapa
Majlis nasomesha.
Vitabu na "paper" naandika.
Mialiko ya kuzungumza napata kutoka kila kona ndani na nje ya nchi.
Mwezi ulopita BBC World Service wameniomba niwe mmoja wa
wazungumzaji kutoka Tanzania katika kuadhimisha Miaka 100 ya
Vita Kuu Vya Kwanza Vya Dunia.
Hivi majuzi nimetoka Ulaya kwa mwaliko.
Juma lililopita katika Karume Day nimesikika kote kupitia AZAM TV
nikieleza historia ya
Abeid Amani Karume kwa kualikwa.
Karume siku ya mapinduzi alilala kwa mzee wangu hapa Dar es Salaam.
Kaondokea kwetu kwenda kupanda boti ya
Misha Finsilber Kunduchi
ikiendeshwa na
Mzee Shebe kurejea Zanzibar na kuchukua serikali.
Ndani ya boti ile alikuwako pia
Abdallah Kassim Hanga, Mohamed
Abdulrahman Babu na
Ali Mahfoudh.
Utayajuaje haya ikiwa wewe ni mtu wa nje?
Ingia hapa kwa habari zaidi:
http://www.mohammedsaid.com/2015/04/azam-tv-karume-day-abeid-amani-karume.html
Wachapaji vitabu wenye majina yao na wakubwa wanamiminika
kunipa miswada niifanye uhariri.
Magazeti yanagongana kuniomba niwe "columnist," wao kwa kuwa
makala zangu zinauza gazeti.
Watafiti wa historia ya Afrika kutoka sehemu nyingi duniani hawapungui
nyumbani kwangu kwenye "study" yangu.
Hii kweli ni dalili ya mtu anaehangaika?
Nilitoa changamoto.
Aandike kitabu anaeweza kuandika, mmoja mmoja au msaidiane kupinga
kitabu cha
Abdul Sykes.
Sijui ni mwaka wa ngapi sasa hili limeshindikana.
Wapinzani wangu hawajaweza.
Lililowezekana ni kuzomea, kejeli, matusi na kebehi...
Mwisho vikaingia vitisho...
Asubuhi hii nafungua mail katika "academia.edu" katika google
nakuta msg hii kutoka kwa Benjamin Kirby wa Chuo Kikuu cha
Leeds soma ujithibitishie mwenyewe:
https://mail.google.com/mail/u/0/#inbox/14cb56b296552726
Muhimu ni kuwa si kama mimi
Allah kanijaalia akili nyingi kupita
wapizani wangu la hasha.
Mimi nimeweza kuandika haya yote katika historia ya uhuru wa
Tanganyika kwa kuwa waliofanya hayo ni wazee wangu kwa hiyo
naandika kitu ninachokijua siendi maktaba kutafuta.
Ndipo nasema rejea ya historia hii ni sisi tulioitengeneza historia hii.
Hata wanaonipinga ikiwa watajaribu hata kwa uchache sana kuandika
historia za wazee wao watakuwa mabingwa na rejea za historia za
wazee wao.
Nani anaweza kupinga kile unachokijua kuhusu babu yako?
Mtu baki hawezi kuyajua yaliyopitika katika ukoo wako.
Wajaribu wataona kuwa nasema kweli.
Kinachoisikitisha na wakati mwingine nacheka peke yangu kama
mwehu pale mtu mishipa ya shingo imemtoka anasema
Sheikh
Suleiman Takadir na
Zuberi Mtemvu walikuwa wanachama wa
AMNUT.
Kuuliza si ujinga ikiwa hujui jambo si unauliza?
Hivi kweli historia ya TANU imepotezwa kiasi watu hawajui hata
historia ya Uchaguzi Mkuu wa 1958?
Hivi elimu ya mantiki imepotea kiasi hata mtu akielezwa ukweli
kwa ushahidi akili yake imevia hawezi kujua kuwa huo anaoelezwa
ndiyo kweli yenyewe?
Nabandika vitu vingi kwa njia ya "link."
Wapinzani hawagusi chochote katika hii ilm za ziada naiayowawekea.
Wakirejea ni matusi.
Subhanallah.
Ndipo ninapowaambia wengi wa
Wanamajlis wanaonihurumia kwa
kejeli na matusi wakinisihi nisijibu.
Mimi huwaeleza kuwa nina wajibu wa kuwasomesha hawa ndugu
zangu ambao hawakujaaliwa kuipata ilm hii niliyokuwanayo mimi.
Kuna faida gani kusimama Northwestern University, Marekani
nikasomesha ilhali ndugu zangu wako kwenye lindi la ujinga kuhusu
historia ya nchi yao wenyewe?
Hivi sasa naandika kitabu kwa Kiswahili: "Ujinga Katika Usomi wa
Historia ya Tanganyika."
Mijadala yetu hii imenisaidia sana.
Mchapaji kanitia hima niendelee na kazi hii.