Rais amejisifu kuwa serikali yake imeongeza kima cha chini kwa zaidi ya 60% mpaka kufikia 104,000/-. Tukichukulia mfano wa mwana JF mmoja kuwa mshahara wa Rais ni 9,000,000/-, ina maana kuwa itamchukua mfanyakazi wa serikali wa kima cha chini zaidi ya MIAKA SABA (7) ili kufikia mshahara wa Rais wa mwezi mmoja tu! Binafsi nina amini kuwa mshahara wa Rais ni zaidi ya 9m/- kwa mwezi. Pia huwa Rais hagusi mshahara wake kwa vile kamwe halipi rent, hanunui chakula wala mavazi, halipi bili ya umeme, maji, wala kuweka mafuta kwenye gari na hulipwa poshi nyingi sana na marupurupu lukuki.
Je, Rais kweli ana moral authority kusema 315,000/- ni pesa mingi sana wakati mshahara wake yeye mwenyewe ni SIRI?
WAANDISHI WA HABARI fanyeni kazi yenu. Mtege waziri wa utumishi, waziri wa kazi, waziri wa utawala bora, msemaji wa ikulu, katibu mkuu kiongozi, waziri wa habari au JK mwenyewe kwa kuuliza mshahara wa Rais ni shilingi ngapi? Lazima watakwepa kusema ukweli na hapo iandikwe habari kuwa wakati serikali imekataa nyongeza ya mshahara wa kima cha chini, inafanya siri mshahara wa Rais. Hivi hata Mgaya mwenyewe anajua mshahara wa Rais ni kiasi gani?
JK angekuwa na busara za uongozi angetangaza kupunguza mshahara wake yeye binafsi na wa vigogo wengine wakuu serikalini. Hii isingeathiri kipato chake hata kidogo ila ingempa political capital kubwa sana kwenye mgogoro wake na TUCTA. Ni mtazamo wangu tu!