Tetesi: Siri ya TANESCO kupandisha umeme kuanzia January ni kulipa deni la IPTL

Hizo hela waliochukua wanajulikana kwanini tulipe watanzania wote? Huenda hata Rais naye sio Mzalendo aiseer
 
I wish waandishi siku moja wamuulize Rais hili suala la Escrow au watu wakaibue tena bungeni
 
Wambeke ata Adrian akija kujibu tuhuma Unafikiri atakubali kwamba ni kweli wamepandisha bill ili kulipa madeni?
Tatizo letu watanzania kiswahili kingi wakati hatujui lolote.
unadhani au unahisi ni nini kilichofanya umeme upande, au vipuri na gharama za uendeshaji zimepanda, na hili kwanini mtukufu halioni na wala sijasikia akiliingilia, wakati tunaoumia ni sisi tuliowapa kura,
 
Nina wasiwasi huenda Hizi pesa chafu huwa zinaingia kwenye mfuko wa chama pendwa hata kampeni huwa zinagharimiwa na hela hizo
 
Pesa wameiba watu wachache wa ccm Leo tunalipishwa wananchi ccm Mungu Anawaona.

Lizaboni,YEHODAYA,Muda wote ,Wakudadavuwa
Si kila unachokiona kipo sahihi. Mengine ni uzushi
 
Hivi hakuna uwezekano wa kuwa na mashirika mengi ya umeme kama yalivyo makampuni ya mitandao ya simu?
Na ccm watapata wapi? pesa za kuchakachulia matokeo ya uchaguzi. Wee unafikiri hizo pesa za kuwalipa wasanii wote wale huwa zinatoka wapi? jiongeze mkuu, pesa huwa zinachukuliwa kwa viini macho vya kushindwa kesi, hapo upo?
 


Bei ya umeme haijapandishwa. Ni kwamba TANESCO walitaka kupandisha bei Ila EWURA ndio waka standardize bei kama inavyoonekana kwenye jedwali.
 
Hivi mikataba ya IPTL na hao dowans ni miaka mingapi? au ndo ile mikataba ya miaka 99. Hivi kwa ajili ya kuzalisha umeme wa dharaula iliyotokana na kukauka kwa maji kwenye mabwawa unahitaji kuingia mkataba wa maelfu ya miaka? Kwa nini wasingeingia mkataba mfupi wa miaka 5 kupisha dharula na wenyewe serikali na tanesco kujipanga kununua mitambo badala ya kukodi kwa mamilioni ya pesa kwa siku. Nafikiri kuna viongozi walifanya huu upuuzi kwa maslahi yao wanayoyajua na wasifikiri wako smart sana kuwabebesha wananchi maskini shida kubwa hivi
 
Kama kumbukumbu zangu ziko sahihi, nakumbuka IPTL walitoa uthibitisho kwamba file hela ni zao; Standard &Chartered hawahusiki n.a. hela za Escrow. Na endapo itatokea Bank hiyo kudai hizo pesa, basi wao watawajibika kwa benki. Imekuwaje Tanesco wanadaiwa tena na benki?
 
Hivi mbona rais hii IPTL hajawahi isemea kitu? Mzee weka hii issue wazi, watz tunaumia
 
Huu ni Ujinga iliopitiliza,
Viongozi, wanasheria na wafanyakazi waliotuingiza kwenye hii mikataba mibovu wako mitaani wanakula Kuku tu kwa mirija, bia kwa uma. Sisi tuliowaamini wao ndio tunataabika. Ifike mahali wananchi wote bila kujali itikadi tuseme enough, yaani imetosha. Hili swala halina Chama, lakini hapa utaona Wazee wa Bk7 wanatetea. Kuna nchi watu waliandamana nchi nzima kisa bei ya Mkate imepanda, sababu kwenye kula huo mkate haijalishi ni chama gani.

Tulidanganywa kua Gesi ikianza kutumika itatatua tatizo la mgao pia itapunguza makali ya bei lakini leo tunaona sio hivyo. Waliotuahidi wapo, na wao wanaendelea kula kuku kwa mrija. Wao kwenye mishahara yao wanapewa na bajeti ya Umeme, ambayo pengine ni karibia au zaidi ya mshahara wa graduate, hivyo hili ongezeko haliwahusu.
 
Hii nchi kuna ahadi nyingi za kupunguza mzigo kwa mwananchi lakini huwa hazitekelezwi
 
Na ccm watapata wapi? pesa za kuchakachulia matokeo ya uchaguzi. Wee unafikiri hizo pesa za kuwalipa wasanii wote wale huwa zinatoka wapi? jiongeze mkuu, pesa huwa zinachukuliwa kwa viini macho vya kushindwa kesi, hapo upo?
Umesahau na mshahara wa Jecha.
 
nasikia Muhongo kazuia hilo ongezeko.
 
Kwa nini serikali isilipe hiyo deni?wananchi hawajaingia huo mkataba,wala hajala hiyo rushwa,sasa unapandisha umeme ili viwanda zisijengwe na bei ya vitu kupanda.
 
Nilisikia Prof Muhongo Alisema Yeye Ni Mtaalam Wa Kugandisha Gas InakuwA Kama Uji Mzito Nadhani Anataka Kutunywesha Huo Uji Sasa
Hahahahahaaaa....

kweli hii nchi ya sizonje ni ya kufikirika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…