Tetesi: Siri ya TANESCO kupandisha umeme kuanzia January ni kulipa deni la IPTL

Tetesi: Siri ya TANESCO kupandisha umeme kuanzia January ni kulipa deni la IPTL

Kwanza inaonyesha uko nyuma katika kupata habari lakini so kosa lako, ni uvivu wa kufikiri ambao so ugonjwa wako pekee.
TANESCO haihusiki na kupandisha bei ya Umeme kisheria EWURA ambae ni mdhibiti anatakiwa kufanya tathmini ya bei ya Umeme kila robo mwaka, si hivyo tu lakini nakusaidia hii ni kwa mujibu wa sheria, najua bado huelewi kwa Kuwa umezoea kulishwa vya uongo na kuamini.
Sasa sikiliza IPTL unayoitaja nadhani kwa sababu unaipenda sana lakini haihisiani kabisa na bei ya Umeme.
Halafu nani kakwambia maombi ya TANESCO yatakubaliwa au la!
Bado kuna mchakato utakaohusisha maoni ya wadau na yatasikilizwa

Halafu gharama za Umeme nakukumbusha zilishuka mwezi April kwa 1.6 na TANESCO hiyo unayoilaumu ndiyo iliiomba EWURA.
Sitaki kukuchosha sana kwakuwa unaonyesha wewe umezoea kulalamika na kupotosha ukweli.
 
We ni fa.la kweli ndio mmezoea uongo kila siku kudanganya watu ...

Ndio mliwadanganya watu hivyo hivyo kwenye VAT matokeo yake bank zikaongeza makato....

Endelea kudanganya watu tu......
 
Aipitielo nayo ishakuwa dondandugu sasa! Haiponi kabisa!!!
 
Nchi zingene wamefanikiwa vipi kuwa na umeme wa uhakika?
Nchi zingine zinatumia vyanzo vingi ikiwa ni pamoja na nuclear, mkaa wa mawe, mafuta, gesi nk! Hivyo wanakuwa na ziada ya umeme!

Sisi hapa tuna umeme wa maji, gesi na mafuta lakini bado hautoshi! Kumbuka umeme wa mafuta tumetapeliwa na hivyo kuishia kuwalipa IPTL, DOWANS nk mamilioni ya fedha wasizostahili!
 
We ni fa.la kweli ndio mmezoea uongo kila siku kudanganya watu ...

Ndio mliwadanganya watu hivyo hivyo kwenye VAT matokeo yake bank zikaongeza makato....

Endelea kudanganya watu tu......

Mkuu haihitaji hasira, yaliyopelekwa ni maombi na wadau mnatakiwa KUTOA maoni EWURA sio jamii forums.

Unafahamu gharama za uzalishaji umeme kwa unit moja? Mbona zenyewe hamuongelei? Uchunguzi wa kina huwa unafanyika watu hawakurupuki
 
Hivi yule jamaa aliesema ikitoa inshu kama hii atawajibika yuko wapi?

Na alisema Serikali itauza Umeme nchi ya Ethopia Yani TZ itaanza ku export Umeme kwenye Ethopia sasa kikowapi kuanza kupandisha bei ya Umeme ?
 
Na alisema Serikali itauza Umeme nchi ya Ethopia Yani TZ itaanza ku export Umeme kwenye Ethopia sasa kikowapi kuanza kupandisha bei ya Umeme ?

(a) Miradi ya Uzalishaji umeme

Ili kukabiliana na ongezeko la mahitaji ya umeme na kukidhi mahitaji ya uchumi wa viwanda, Serikali imekamilisha ujenzi wa mitambo ya Kinyerezi I (MW 150) Mwezi Machi, 2016 na katika kipindi cha Mwaka 2016/17 ujenzi wa mitambo mipya ya Kinyerezi I Extension (MW 185) unatekelezwa kwa gharama za Dola za Marekani Milioni 188 na Kinyerezi II (MW 240) unatekelezwa kwa kiasi cha Dola za Marekani Milioni 344.

(b) Miradi ya Njia za Usafirishaji Umeme.

Ili kuenda sambamba na miradi ya kuzalisha umeme, Serikali kupitia TANESCO inatekeleza miradi kadhaa ya kusafirisha umeme. Miradi hiyo ni kama ifuatavyo:-

i. Mradi wa kusafirisha umeme wa msongo wa kilovoti 400 kutoka Iringa hadi Shinyanga (backborne) ambapo upo katika hatua za mwisho kukamilika. Mradi huu utaimarisha upatikanaji wa umeme katika maeneo ya Kanda ya Ziwa, Kati na Kaskazini. Mradi huu umekamilika kwa asilimia 98; ambapo utatekelezwa kwa kiasi cha Dola za Marekani Milioni 490;

ii. Mradi wa kusafirisha umeme kutoka Makambako hadi Songea wa msongo wa kilovoti wa 220 wenye urefu wa kilomita 250 pamoja na kusambaza umeme katika mikoa ya Njombe na Ruvuma. Kazi zinazoendelea ni ujenzi wa miundombinu ya kusambaza umeme, kwa upande wa njia ya kusafirisha umeme, kazi zinazoendelea ni usanifu wa kina (Detail Feasibility Study), uingizwaji wa vifaa vya ujenzi na uandaaji wa eneo la mradi (Site Moblization). Mradi wa kusafirisha umeme wa Makambako Songea utatekelezwa kwa kiasi cha Dola za Marekani milioni 190;

iii. Miradi wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa kilovoti 400 yenye urefu wa kilomita 1,148 kutoka Mbeya - Sumbawanga - Kigoma - Nyakanazi (North - West Transmission Line);

iv. Mradi wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa kilovoti 400 yenye urefu wa kilomita 664 kutoka Dar es Salaam - Chalinze – Tanga - Arusha (North - East Transmission Line) ambapo zaidi ya Dola za Marekani Milioni 55 zitatumika kuteleza mradi huu. Mkopo wa kiasi hicho cha fedha zimepatikana kutoka katika benki a Exim ya China. Kazi zinazoendelea kwa sasa ni kuweka mipaka kwenye njia ya kusafirisha umeme;

v. Mradi wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa kilovoti 400 kutoka Somanga fungu hadi Dar es Salaam (Kinyerezi), gharama za mradi ni Dola za Marekani milioni 150. Kwa sasa Serikali inatafuta fedha za kutekeleza mradi husika;

vi. Pia Serikali inatekeleza miradi ya Kikanda kama vile miradi ya kusafirisha umeme kutoka Zambia - Tanzania – Kenya (ZTK). Lengo la miradi hii ni kuweza kuimarisha upatikanaji wa umeme katika eneo la Afrika Mashariki pamoja na kuimarisha biashara ya kuuziana umeme.

Aidha, mradi huu unatekelezwa kwa sehemu, ambapo itajengwa njia ya kusafirisha umeme kutoka Namanga (mpakani kati ya Tanzania & Kenya) hadi Singida yenye urefu wa kilomita 414 ambapo itagharimu kiasi cha Dola za Marekeni Milioni 258 ambapo wafadhili wa mradi huo ni AfDB na JICA, njia ya kusafirisha umeme kutoka Singida hadi Iringa (mradi huu wa backborne upo katika hatua za mwisho kukamilika), njia ya kusafirisha umeme kutoka Iringa hadi Mbeya yenye urefu wa kilomita 292 pamoja na ujenzi wa substations mbili (2) (mradi utagharimu kiasi cha Dola za Marekani takribani Milioni 200), na sehemu ya mwisho ni njia ya kusafirisha umeme kutoka Mbeya hadi Tunduma yenye urefu wa kilomita 100 itagharimu Dola za Marekani 38 Milioni.

(c) Miradi ya Njia za Usambazaji umeme.

Serikali kupitia TANESCO imeendelea kutekeleza miradi kadhaa ya kuimarisha miundombinu ya kusambaza na kusafirisha umeme katika Majiji na Miji hapa nchini, ambayo ni;

i. Mradi wa kuimarisha upatikanaji wa umeme katika Jiji la Dar es Salaam ambapo ujenzi wa kituo cha kupoza umeme katikati ya Jiji upo katika hatua za mwisho za kukamimilika (Improving the Electricity Power Supply relability in City of Dar es Salaam), ambapo mradi huu unafadhaliwa na Serikali ya Finland pamoja na Serikali ya Tanzania kwa kiasi cha Euro Milioni 28.2.

ii. Pia mradi mwingine wa kuboresha miundombinu ya usambazaji umeme unaofadhaliwa na Serikali ya Japani unaendelea kutekelezwa katika Jiji Dar es Salaam. Kiasi cha Dola za Marekani Milioni 38 zitatumika kutekeleza kazi hiyo.

iii. Mradi wa Tanzania Energy Development and Access Project (TEDAP) unatekelezwa katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha na Kilimanjaro. Mradi unakusudia kuboresha na kuimarisha upatikanaji wa umeme wa uhakika katika mikoa husika . Mradi huu unahusisha ujenzi wa miundombinu ya kusambaza, kusafirisha pamoja na vituo vya kupoza umeme. Kiasi cha Dola za Marekani Milioni 26.44 zitatumika kutekeleza mradi huu pindi utakapokamilika.

Kwa kuzingatia kuwa azma ya Serikali ni kufikia uzalishaji wa umeme wa Megawati 5,000 ifikapo 2020 na Megawati 10,000 ifikapo 2025. Serikali ilianzisha mkakati maalum wa kuongeza uwekezaji katika miradi ya kuzalisha umeme ambayo inatekelezwa kwa kushirikiana na sekta binafsi kutoka ndani na nje ya nchi.

(a) Miradi ya uzalishaji ni kama ifutayo:-

i. Miradi midogo ya Nishati Jadidifu (Renewable Energy) yenye MW 16.29 imetekelezwa na sekta binafsi, miradi hiyo ni;-

· Miradi midogo ya kuzalisha umeme wa maji (Min Hydropower) ambayo ni Uwemba - MW 0.84; Mwenga MW 4; na Yori MW 0.95; na

· Miradi midogo ya kuzalisha umeme kwa kutumia tungamo taka (Biomass) ni Tanwat MW 1.5 na TPC MW 9.0.

ii. Kilwa Energy Gas Fired Plant (371.2 MW) - US$ Milioni 465,

Mwekezaji yupo katika hatua za mwisho za majadiliano ya Mikataba mbali mbali ambayo ni; Mkataba wa nyongeza wa utekelezaji (Addendum to Implementation Agreement), Mkataba wa Ubia (Shareholders Agreement), na Mkataba wa kununua gesi asilia (Direct Gas supply Agreement) ili kupata ufadhali wa mradi.

(b)Miradi ya usafirishaji umeme

Uwekezaji kwenye miundombinu ya usafirishaji wa umeme ni jukumu la Serikali na si sekta binafsi. Aidha, Sheria ya umeme ya Mwaka 2008 inaruhusu sekta binafsi kupitisha umeme kwenye miundombinu hiyo kwa kulipia Wheeling Charge na wala si kumiliki miundombinu husika.
 
unatenganisha vipi umeme wa gas na umeme wa iptl,usilete mzaha kwenye issue serious kama hii.
Nnangale IPTL ni ya mkubwa wa dunia punguza hasira,hata watoto wako wataikuta hii kitu.Kuteganisha umeme wa gas na IPTL hakukusaidii chochote.Upepo unavuma kwa wafanyakazi hewa,vyeti hewa,wanafunzi hewa n.k,umeshasikia pameguswa hapo? think big.
 
IPO siku watu wanaoishi maeneo yenye upepo mkali watajiondoa Tanesco halafu wengine tutatumia solar ndo tutakapo heshimiana.....
 
IPO siku watu wanaoishi maeneo yenye upepo mkali watajiondoa Tanesco halafu wengine tutatumia solar ndo tutakapo heshimiana.....
Wapi thubutu kutengeneza tu umeme wako ni kosa kama vijana wengine wanajua kutengeneza umeme wa choose lakini ukitengeneza unaambiwa unaihuju Tanesco.....
 
Nimeangalia comments zote nilijua issue kama hiz nitawaona wanaojidai na kujipambanua kama wazalendo yaani Lizaboni, wakudadavua, lupyee, yehodava... Lakini kwasababu ya upuuzi na uchumia tumbo hamna hata mmoja aliyekoment wala kutoa lolote.. Kweli watanzania twaongoza unafiki na siku wote tukiwa wazalendo kwenye issue sensitive zinazohusu taifa tutafika mbali sana.
 
Uwezi waona hapo hata mawaziri wanaoshinda humu na kutuambia tufanye kazi tuache kulalamika hakuna hata mmoja utamuona akichangia hapo wanapita kimya kimya
 
Nnangale IPTL ni ya mkubwa wa dunia punguza hasira,hata watoto wako wataikuta hii kitu.Kuteganisha umeme wa gas na IPTL hakukusaidii chochote.Upepo unavuma kwa wafanyakazi hewa,vyeti hewa,wanafunzi hewa n.k,umeshasikia pameguswa hapo? think big.
Wakubwa gani hao?
 
Naomba muniombee kwa mungu, je wewe unawasaidiaje hao, wakati hutaki hata kutaja jina ESCRO!!!
 
Huyu IPTL inaonekana ni mkubwa kuliko hata mteule wa marekani yaani jamaa hagusiki aisee!!!
 
Back
Top Bottom