Tema Mate
Senior Member
- Dec 19, 2013
- 107
- 193
Wakati hayo yakiendelea kufukuta,Chanzo cha Karibu Kabisa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu kinasema,Awali Posho za Wabunge zilikuwa laki saba 700,000/ kwa kila Mjumbe Kwa Siku.Pia mbali na laki saba hiyo,Ofisi ya Bunge wakishirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu iliadhimia kumlipa kila Mjumbe wa Bunge Maalum Fao la Kuhitimisha Bunge Maalumu Tsh.Milioni 5.
Katika Kikao Kilichofanyika Tar.13.02.2014 Ofisi ya Waziri Mkuu Jijini Dsm kikihusisha Katibu wa Bunge,Naibu Waziri wa Fedha(sera) Mh.Mwigulu pamoja na Ujumbe kutoka Ofisi ya Rais.Kwenye Kikao hicho.Mezani kulikuwa na agenda ya kuruhusu Malipo ya Posho kwa wajumbe wa Bunge Maalumu yawe tsh.700000/=
Msimamo Mkubwa Kutoka Hazina ulikuwa hazina haina fedha za Kulipa Wajumbe wa Bunge la Katiba kwa Kiwango hicho cha laki saba,Mwigulu akiwa ndiye muwakilishi kutoka hazina alisimamia kuwa "Wakati huu Nchi ikiwa na Madeni kwa Walimu,Huduma za Afya hazijaboreshwa,Miradi ya maendeleo kama barabara na Umeme bado sehemu zingine imesimama,Leo hii tutawambia nini Watanzania kwa kuwalipa watu wanaokwenda kukaa Bungeni kwa siku walipwe Laki Saba.
Hoja hiyo ya Mwigulu inadaiwa iliungwa Mkono na Ujumbe kutoka kwa Rais na hatimaye kushawishi kikao kikubaliane na malipo ya Laki tatu.
Kinachofanyika hivi sasa na tume iliyoundwa Bungeni kwaajili ya Kutafuta ufafanuzi wa ama kuongeza posho kimya kimya au kusimama na posho ya laki saba,Wajumbe wa tume wanapo mbioni kukutana na Hazina(mwigulu) kwaajili ya kuangalia uwezekano wa kuongeza Posho hizo,Japo Mwigulu kwenye kikao cha awali kwa waziri Mkuu aliapa kuto ruhusu fedha ya Wananchi kulipwa kwa watu wanaokaa tu Bungeni.
MY TAKE:Mwigulu Simamia hapo hapo,Walizani Hazina ni Uchochoro wa kukwapua Fedha za Umma.Rais atangaze wazi,Wajumbe wasiotaka Posho ya laki Tatu wajiorodheshe waondoke Bungeni,Afanye Uteuzi mwingine.