gstar
JF-Expert Member
- Jun 19, 2011
- 790
- 1,373
Awali ya yote, nipongeze juhudi zinazofanywa na serikali ya awamu ya sita chini ya kiongozi wake Raisi Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha kuwa anatekeleza miradi yote iliyoachwa na mtangulizi wake hayati Dk. John Pombe Magufuli, pia kuibua miradi mipya na kuitekeleza kukamilifu.
Hata hivyo, kuna hali ya kusuasua kwa utekelezaji wa miradi mingi hasa ya ujenzi wa barabara, kwamba inachukua muda mrefu kukamilika ama inakamilika ikiwa chini ya kiwango. Kuchelewa kukamilika kwa miradi kunatoa mwanya wa rushwa na kuongezeka kwa gharama za utekelezaji. Ujenzi wa barabara unapochukua muda mrefu unaweza kusababisha uharibifu ama kuchakaa kwa miundombinu hiyo kabla hata ya mradi kukabidhiwa kwa serikali matokeo yake mzabuni atapaswa kurudia ama kukarabati mradi kwa gharama nyingine zilizo nje ya gharama za wali. Tuliliona hili kwenye mradi wa Mwendokasi Mbagala.
Nataka nitolee mfano wa barabara ya mwendo kasi awamu ya tatu na nne. Awamu ya pili ni ujenzi ulio husisha barabara ya Kilwa (barabara ya Mbagala) licha ya mradi ule kusemwa kwamba umekamilika bado umeonekana una mapungufu mengi, sehemu nyingi za barabara zimeonekana nyufa baadhi ya vituo vya mwendo kasi kutokuwa na ubora stahiki, na sehemu ya kingo za barbara kubomoka kabla ya matumizi rasmi. Hata hivyo mpaka sasa mradi wa mwendokasi Mbagala haujaanza kutumika licha ya adha kubwa wanayoipata wakazi wa Mbagala kwenye swala la usafiri. Mpaka najiuliza hivi Hawa viongozi wetu wana uchungu na maisha yetu kweli?
Barabara ya Gongo la Mboto au Nyerere Road naona ujenzi wake unasuasua ni zaidi ya mwaka tangu ujenzi ulipoanza, lakini kumbuka kwamba barabara hii ndio kioo cha Tanzania, wageni wengi wanapofikia hapa nchini wakitua Airport lazima wapite katika barbara hii sasa kitendo cha kuijenga barabara hii kwa zaidi ya mwaka mmoja, licha ya kuendelea kuwapa adha ya usafiri wakazi wa Gongo la Mboto lakini pia kinaharibu taswira ya nchi yetu hasa kwa wageni wanaotutembelea mara kwa mara.
Lakini wakati barabara hiyo ikiwa bado haija kamika tayari awamu nyingine ya ujenzi imeanzishwa ni katika maeneo ya katikati ya mji yote hayo yamesha bomolewa na kazi ya ujenzi inaendelea. Ninajiuliza ikiwa kipande cha barabara ya Gongo la Mboto hakija kamilika iweje waanzishe ujenzi mpya? Nilidhani ingekuwa busara kukamilisha ujenzi wa hatua moja kabla ya kuhamia hatua nyingine na iwapo kampuni iliyopewa tenda ni moja, itakuwa ni vigumu kusimamia maeneo yote hayo yanayo endelea na ujenzi kwa wakati mmoja, inaweza kusababisha barabara hizi kujengwa chini ya kiwango kutokana na usimamizi duni na upungufu wa rasilimali za kutosha kutekelezwa mradi kwa pamoja.
Kwa ushauri wangu ningependekeza kwamba serikali kupitia kwa wizara ya ujenzi na kamati za bunge iweze kutazama ujenzi wa barabara hasa ya mradi wa mwendokasi wa Dar es Salaam ili waone ni namna gani bora inayopaswa kuchukuliwa kutekelezwa ujenzi huo bila kuathiri shughuli za kibinadamu zinazo endelea ndani ya Jiji. Pia kuangalia uwezekano wa kuharakisha ukamilishwaji wa miradi kwa wakati na kwa uharaka. Kama nchi ya China walijenga hospitali kubwa ya kutibu wagonjwa wa korona ndani ya masaa 72 iweje kipande cha barbara kisichozidi kilomita 100 kichukue muda mrefu kukamilika?
Natanguliza Shukrani zangu za dhadi.
CC. Prof. Makame Mbarawa, Kassim Majaliwa, Dr. Philip Mpango, Dr. Mwigulu Nchemba.