Siridhishwi na kasi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo

Siridhishwi na kasi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo

Huna unalolijua kwenye hili. Wachina waliolipwa ni mradi gani? Kinachofanyika ni kwamba miradi mikubwa ipo subjected na interest na wachina kampuni zao zinapata mikopo toka china yenye single digit interest.
Wanachofanya ni kutekeleza mradi regardless ya financial status na faida wanaipata kwenye interest za kimkataba

Sasa ukiona mradi wa wachina unaendelea na local contractor unasuasua usifikiri jamaa wamelipwa ni madeni ya kutisha
Na vile tunaelekea kwenye uchaguzi sijui watawala hapa wanachomokaje
Ni Kweli mkuu , ulicho kiandika,
 
Mkuu inaelekea huyu waziri wa Ujenzi Mh Bashungwa pale wizarani na kanyaboya tu!
Hana impact kwenye kutetea maslahi ya Taasisi kubwa kama TANROADS.
Hela ya Road Fund ipo, tunashangaa inaenda wapi?
Siyo waziri ndo tatizo, tatizo Tanroad imeharibiwa na miradi ya viwanja vya ndege TAA, wale WA TAA warudishwe huko huko maana wanakula hela za Barabara na kazi hawafanyi yaani wapo tu ofisini hawajui wafanye wapi kazi, hela zinazotumika kwa viwanja ni za Tanroads, magari Tanroads, safari zao Tanroad sasa hela inaishia kwa wafanyakazi badala ya kwenda Barabarani kwenye kazi na hawakai kwenye mikoa wapo wanazunguka tu.
 
Hao uliokutana nao siyo kwamba hawaungi mkono ununuzi wa helicopter ya Mama na ndiyo maana hawalipwi!!
Nilitaka kusema hili...WAKANDARASI WAPI hao hawajalipwa? Si waliungana kumnunulia Hangaya helikopta kwakuwa wamekuwa wanufaika wazuri wa miradi na kulipwa kwa wakati!
 
Kwa wale wanaoifahamu TANROADS kwa miongo zaidi ya miwili au mitatu, wanasema wakala huyu wa barabara yuko hoi.
TANROADS bado ina miradi mingi lakini haina fedha za kujiendesha.
Tatizo kubwa inaonekaka kwa sasa TANROADS pamoja na wizara yake ya Ujenzi si kipenzi cha serikali..

Nimekutana na makandarasi zaidi ya wawili na ni kilio bin malamiko ya kutolipwa fedha kwa wakati au hakuna kabisa.
Serikali haina hela ni kama Ime Collapse ila visingizio ni kuwa mwisho wa Mwaka wa fedha wanafunga mahesabu.
Haya ngoja tuone maana ndio mwezi huu wa mifumo kufunguka.
Tunapoelekea kuna miezi mishahara itaanza kusua sua kulipwa kwa wakati
 
Nilitaka kusema hili...WAKANDARASI WAPI hao hawajalipwa? Si waliungana kumnunulia Hangaya helikopta kwakuwa wamekuwa wanufaika wazuri wa miradi na kulipwa kwa wakati!
Siasa zile mkuu hamna lolote wakandarasi wenyewe Walishangaa kuwa ni kina nani hao walionunua helkopta.
Labda wakandarasi wa Kichina.
 
Kwa wale wanaoifahamu TANROADS kwa miongo zaidi ya miwili au mitatu, wanasema wakala huyu wa barabara yuko hoi.
TANROADS bado ina miradi mingi lakini haina fedha za kujiendesha.
Tatizo kubwa inaonekaka kwa sasa TANROADS pamoja na wizara yake ya Ujenzi si kipenzi cha serikali..

Nimekutana na makandarasi zaidi ya wawili na ni kilio bin malamiko ya kutolipwa fedha kwa wakati au hakuna kabisa.
Changamoto hii
 
Vyanzo vya mapato TANROADS nibWizara mama ya Ujenzi na Road Fund!
Pesa za Road Fund, kwa sasa zinagawanywa kwa uwiano wa 65/35 baina ya TANROADS na TARURA.
Kabla JPM hajaanzisha TARURA, mgao wote kutoka Road Fund ulikuwa wa TANROADS.
Pesa za Road Fund siyo za Miradi mipya, ni za kukarabati na kutunza (maintain) Barabara zilizopo.
Miradi yote Mipya ya Barabara inapata pesa kutoka Serikali Kuu, na pesa nyingi zilikuwa Mikopo kutoka Mabenki ya Ndani na Nje ya Nchi.
Serikali ya JPM ilibana sana matumizi yasiyo ya lazima.
Hivi sasa mpaka Wacheza Tamthilia wanatumia pesa za Walipa Kodi.
Tusishangae TANROADS wakikosa Fedha za kukamilisha Miradi ya Barabara.

Vyanzo vya mapato TANROADS nibWizara mama ya Ujenzi na Road Fund!
 
Siyo waziri ndo tatizo, tatizo Tanroad imeharibiwa na miradi ya viwanja vya ndege TAA, wale WA TAA warudishwe huko huko maana wanakula hela za Barabara na kazi hawafanyi yaani wapo tu ofisini hawajui wafanye wapi kazi, hela zinazotumika kwa viwanja ni za Tanroads, magari Tanroads, safari zao Tanroad sasa hela inaishia kwa wafanyakazi badala ya kwenda Barabarani kwenye kazi na hawakai kwenye mikoa wapo wanazunguka tu.
Kwa kweli hiyo ni point.
TANROADS wafanyekazi zenyevutaalam wao-kujenga barabara na si vinginevyo.
Lakini ukosefu wa fedha hicho ninkizungumkuti.
 
Haiwezekani labda kama Kuna Hila,unachukua fuel yote kwa Lita itakayotumika kwa namna yote hapa Tanzania unazidisha kwa kile kiwango kinachokatwa toka Kila Lita ya fuel consumed mzigo huo unaupeleka Tan road.si mabilioni hayo kama si Matrilioni,Sasa watakosa je fedha kwa mfano!
Hali ndio hiyo wako taabani Road fund imefanyiwa relocation na Mwigulu & Co wakandarasi wahajalipwa muda sasa na haijulikani lini wanalipwa. Kingine nafikiri CEO wa Tanroads na waziri wa ujenzi hawana maelewano yanayoeleweka au tuseme mmoja au wote hawatekelezi majukumu yao ipasavyo haijawahi kutokea ukame huu wakandarasi wanasita kuomba kazi kwa sasa maana hali sio nzuri kazi zinasusua sekta ya ujenzi wa barabara imesinyaa vibaya sana hizo kodi sijui zinapatikana wapi na hayo makampuni yanajiendesha vp
 
Wadau tumefuatilia.
TANROADS hawapewi hiyo fedha kama inavyostahili.
Siasa zinaua huyu wakala wa maendeleo.
Hazina nafikiri kuna shida kubwa sana kuliko tunavyofikiri maana wenyewe ndo wanapeleka mafungu kwenye hizo taasisi kingine CEO na waziri wa ujenzi hawana maelewano yanayoeleweka maana wao ndo viuongo muhimu wa wizara na taasisi sasa kama mafungu hayafiki mbona hatumuoni waziri akipaza sauti juu ya hilo. Tuliona enzi za Mfugale na mawaziri wote aliofanya nae kazi mambo yalikuwa yanaenda muswano kabisa ila sasa hovyo kabisa wanachechemea kama enzi zile za idara ya ujenzi miaka hiyo.
 
Ndio mjue yule mwehu alikuwa anadhulumu watu na plea bargain, hela za NSSF, na kuwaibia wa Bureau de change na kukopa mikopo ya kausha damu huko india na china.
Leo hii chato inapumulia machine sababu uchumi wake uliendeshwa na hela za kudhulumu wafanyabiashara
Vyanzo vya mapato Tanroads viko wazi mbona pesa hazipelekwi ipasavyo fatilia ujifunze
 
Serikali haina hela ni kama Ime Collapse ila visingizio ni kuwa mwisho wa Mwaka wa fedha wanafunga mahesabu.
Haya ngoja tuone maana ndio mwezi huu wa mifumo kufunguka.
Tunapoelekea kuna miezi mishahara itaanza kusua sua kulipwa kwa wakati
Mwigulu anakana hilo lakini muda utatueleza
 
Back
Top Bottom