Robert Heriel Mtibeli
Platinum Member
- Mar 24, 2018
- 40,153
- 93,069
SISI CONTENT CREATORS WA JF NA MITANDAO MINGINE TUNASUBIRI KWA HAMU HAYO MABILIONI. CHONDECHONDE MAKONDA TUTAONANA WABAYA.
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.
1. Kwenye hii nchi ya Tanzania, moja ya watu wanaofanya kazi kubwa Sana kwenye jamii yetu na serikali ni Sisi Content Creators hasa wa kuandika articles(makala) mitandaoni.
2. Ingawaje hatupewi uzito lakini hakuna asiyejua mchango wetu katika nchi hii.
3. Wote ni mashahidi, Siku hizi elimu, maarifa, ujuzi, ufahamu vipo mtandaoni.
4. Mara nyingi hata viongozi wa serikali hupata mawazo mapya chanya kupitia makala zinazoandikwa huku mitandaoni.
Mnafahamu Siku hizi usomaji wa magazeti umepungua kwa kiasi kikubwa.
5. Kupitia maandishi yetu content creators WA mitandaoni tumesaidia serikali kwenye mambo ya kisera, ulinzi na usalama, kidiplomasia, utungaji wa Sheria n.k.
6. Watanzania wengi wamefaidika kijamii na kiuchumi kupitia maandishi yetu.
Mahusiano ya ndoa na familia kwa waliofanikiwa kusoma makala za mahusiano wamefaidika.
7. Maamuzi ya kutoa mapesa, mamilioni kwaajili ya Content Creators yalikuwa ni ndoto na kilio chetu kwa muda mrefu.
8. Paul Makonda wazo lako ni zuri sio kwa sababu litaninufaisha na Mimi hapana. Bali kutokana na ukweli mchungu kuwa Kuna vijana wanafanya KAZI kubwa kwenye taifa hili lakini tumekuwa kama hatuwaoni. Tena wengi wao wanafanya kizalendo.
9. Fedha hizo tunazitolea Macho.
10. Kwa mfano humu JamiiForum kuna watu wanaandika Sana. Sisi wote ni Mashahidi. Tunachukua mawazo yao.
11. Tunayatumia katika maisha yetu ya Kila Siku. Kwenye mambo yetu ya kiuchumi tunayatumia.
Kwenye mambo yetu ya ndoa na familia tunayatumia.
Tunatumia kuongeza uelewa wa dunia. Yananufaisha.
12. Lakini hatuwapi chochote. Tukienda Kanisani na misikitini tunatoa sadaka.
Popote tunapofaidika lazima tutoe shukrani. Kwa nini hawa Content Creators wakiwepo WA kuandika tusiwape hat shukrani japokuwa sio lazima!
13. Kuna MTU atasema pooh! TaikonMaster unajipigia assist. Nope! Mimi hata nisipokuwepo. Ila natamani kuona wale ninaofaidika kutoka kwao wakikua na kufanikiwa.
14. Kuna watu wanaandika jamani. Wote tumeongeza ufahamu wetu humu kwa kusoma maandiko ya watu humu au mitandao mingine.
15. Kusoma ni kuongeza ufahamu. Mtu anayesoma ni sawasawa na mtu anayetembea duniani. Lazima awe na exposure na ajue mambo mengi.
16. Maandishi ni dunia. Kila unayemuona anadunia yake. Unaposoma maandishi ya watu wengine wengi ndivyo unavyotembea katika dunia na unaongeza exposure.
17. Kuna watu kama kina MALCOM LUMUMBA Mshana Jr , Pascal Mayalla Mad Max Nguruvi3 Mzee Mwanakijiji Somebody Mama Amon sijui Dr amon kuna ChoiceVariable
Wapo wengi Sana humu. Doctor Mama Amon
18. Mitandao mingine ya Facebook wapo watu wanaandika vitu mpaka unasema yeah.
Wapeni hizo pesa.
19. Pesa zisiende tuu kwa wanaorekodi video.
20. Nakuhakikishia asilimia Tisini ya video unazoziona zinatokana na content creators wanaondika, yaani watunzi na waandishi wa makala na short stories.
21. Ninaushahidi na hili kwa sababu kwa mfano kwa upande wangu wapo content creators wakubwa wa video na wengine ni wachekeshaji WA standup comedy ambao wanachukua maudhui kutoka kwangu. Na wanasema kabisa Wana wengine wanaowaandikia na kuwabunia scene drama, na mambo ya kuigiza au kusema.
22. Zile zote za usiku wa mahaba, Movies Recaps zote mnazosikiliza na kuziona mitandaoni zinatoka kwa waandishi na watunzi.
23. Motivation speakers asimilia 90% wanasoma makala zetu ndipo wafanye kazi zao.
24. Maelezo yote hayo na mengi niliyobakiza sio kwamba kuonyesha tunastahili kuliko wengine au sisi ni Bora kuliko wengine. Hapana. Najaribu kuonyesha tija ya hawa watu na jinsi ambavyo tunatakiwa tuwatendee.
25. Kitu kimoja ambacho watunzi na waandishi wote duniani tunafanana na kuelekeana. Na hapa nazungumzia waandishi na watunzi wa kuzaliwa yaani wenye vipaji vya kuzaliwa sio kusomea.
Tuko hivi;
a) Hatuwezagi kuwa Machawa.
Duniani kote waandishi na watunzi wa kuzaliwa hatunaga hulka na tabia ya uchawa.
b) Tunakaaga upande wa Haki.
Fuatilia waandishi wenye vipaji wote hapa Tanzania na duniani kwa ujumla.
Siku zote tunapinga dhulma, uonevu.
Iko hivi huwezi ukawa na akili ya utunzi alafu ukawa ukatetea dhulma. Ukishaanza kutetea dhulma kalamu lazima ikukatae.
Utajikuta mawazo na uwezo wa akili kutunga na kuunganisha maneno vinakata automatically.
c) Waandishi na Watunzi wa kuzaliwa ni kama Manabii na mitume.
Wengi wetu ni wanahulka ya unafalsafa. Sifa hiyo hutufanya tuwe kama waalimu, mitume na manabii.
d) Waandishi tunapenda Ukweli.
Hata kama tutatumia lugha ya picha, na hadithi ya kubuni lakini tutaelezea ukweli bila kuupindisha. Iwe Ukweli uliopita, uliopo au ujao.
e) Asilimia tisini na tisa tuna AKILI. Huwezi kuta mtunzi na mwandishi wa kuzaliwa akawa na akili ndogo.
Kwa sababu kufikiri na kutafakari mambo ni moja ya nguzo zetu kuu. Sio ajabu wengi wetu tunapenda kukaa pekeetu muda mwingi.
26. Kwa kifupi hizo hela tunazihitaji. Hawa vijana wapewe ili iwatie moyo na kuwapa hamasa.
27. Nimeeleza sifa za watunzi ili mjue kabisa msijewapa hela na masharti ya uchawa au kuwazingira na kuwafunga kalamu zao.
28. Msije haribu hiyo tasnia kwa sababu hiyo ndio injini ya kutoa mawazo ndani ya nchi. Ukishapeleka rushwa huko unaua taifa kimawazo.
Watu watakuwa wanaandika vitu visivyoeleweka.
29. Mwisho kabisa, waandishi na watunzi wengi duniani hawanaga Vyama vya siasa na wengi sio wafuasi wa Dini ila wanaimani na kuamini katika HAKI na KWELI.
Kufikia hapo sina la ziada.
TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam