Sisi ni mabingwa wa kufunga AC karibu tukuhudumie

Sisi ni mabingwa wa kufunga AC karibu tukuhudumie

Air-cooler inatumia maji kupooza hewa huku AC haitumii maji kupooza hewa
Kitendo cha kutumia maji hakiwezi kusababisha Nimonia (Pneumonia)?

Nauliza maana sisi wa huku milimani kwenye baridi hayo mambo hatuna ujuzi nayo.

Na katika hizo njia mbili ipi ni bora zaidi kwenye maeneo yenye joto kubwa kama maeneo ya bonde la ufa?
 
Kitendo cha kutumia maji hakiwezi kusababisha Nimonia (Pneumonia)?

Nauliza maana sisi wa huku milimani kwenye baridi hayo mambo hatuna ujuzi nayo.

Na katika hizo njia mbili ipi ni bora zaidi kwenye maeneo yenye joto kubwa kama maeneo ya bonde la ufa?
Ac ni nzuri ila kwa sababu ya baadhi ya watu wana kipato kidogo wanaprefer air-cooler
 
Joto ni kali ila tuna-suluhisho kwa ajili yako
75FC08FB-D86A-47C4-9FEB-B8B4B443CB10.jpeg
 
Tofauti ya Inverter na Non-inveter ni ipi katika:
  • technically
  • economically
  • reliability
  • convenience
  • efficiency
  • operating costs

Nishaona hapo juu Inverter based A.C bei juu kuliko Non-Inveter. Kwanini?

Mteja akija utamshauri achukue aina gani
Kuna tofauti kuu kadhaa kati ya Inverter-based air conditioner na Non-inverter air conditioner, ambazo zinaathiri ufanisi, matumizi ya umeme, na utendaji wa jumla. Hizi ni tofauti hizo:

1. Kanuni ya Uendeshaji

  • Inverter Air Conditioner: Hii ina compressor ambayo hurekebisha kasi ya mzunguko kulingana na joto la chumba. Inapofikia joto lililowekwa, compressor hupunguza kasi bila kuzima kabisa.
  • Non-inverter Air Conditioner: Compressor ya aina hii huwaka na kuzima kikamilifu mara kwa mara ili kudhibiti joto. Haibadilishi kasi ya mzunguko wake.

2. Matumizi ya Nishati

  • Inverter AC: Inatumia nishati kwa ufanisi zaidi kwa sababu compressor inafanya kazi polepole inapofikia joto linalotakiwa, ikipunguza matumizi ya umeme.
  • Non-inverter AC: Huchukua umeme mwingi kwa sababu compressor huzima na kuwashwa tena mara kwa mara, jambo ambalo linaongeza matumizi ya nishati.

3. Gharama ya Awali

  • Inverter AC: Gharama yake ya ununuzi ni ya juu zaidi kutokana na teknolojia yake ya hali ya juu.
  • Non-inverter AC: Bei yake ya awali ni ya chini na inapatikana kwa urahisi zaidi.

4. Utendaji

  • Inverter AC: Inadumisha joto la chumba kwa uthabiti zaidi na hufanya kazi kwa utulivu bila mabadiliko makubwa ya joto.
  • Non-inverter AC: Inaweza kusababisha mabadiliko ya haraka ya joto (joto linaweza kupanda na kushuka) kwa sababu ya kuwasha na kuzima compressor.

5. Kelele

  • Inverter AC: Inatoa kelele kidogo kwa sababu compressor inafanya kazi polepole inapohitajika.
  • Non-inverter AC: Inaweza kuwa na kelele zaidi kwa sababu ya mizunguko ya kuwasha na kuzima compressor.

6. Matengenezo na Uhai

  • Inverter AC: Inahitaji matengenezo ya hali ya juu zaidi, lakini huweza kudumu kwa muda mrefu ikiwa inatunzwa vizuri.
  • Non-inverter AC: Inahitaji matengenezo rahisi, lakini compressor inaweza kuharibika haraka kutokana na kuwasha na kuzima mara kwa mara.

7. Hali ya Hewa ya Nje

  • Inverter AC: Inaweza kufanya kazi vizuri hata wakati hali ya hewa ya nje ni mbaya, kwa sababu inaweza kurekebisha nguvu ya compressor.
  • Non-inverter AC: Ufanisi wake unaweza kupungua katika hali ya hewa yenye changamoto, kwani compressor hairekebishi kasi.

Hitimisho:​

  • Kama unatafuta kifaa kinachookoa umeme na kudumisha joto la chumba kwa uthabiti, Inverter AC ni bora.
  • Ikiwa unazingatia gharama ya awali na unatumia kifaa kwa muda mfupi, basi Non-inverter AC inaweza kuwa chaguo bora.
 
AVS inafungwa kwenye AC ipi kati ya hizo aina mbili na je, kuna ulazima wa kuifunga?.
 
umesema kuna kujaza gesi kwenye AC mie nalijua ukifunga umefunga.! kwani AC inakija ikiwa tupu ila ukitaka kufunga ndio unaijaza gesi.? na hiyo gesi inatumika kwa miezi mingapi itakuwa imeisha hivyo kuhitaji kujaza tena na pia ni mda gani upite ndio uifanyie service mashine na pia utajuaje kama gesi imeisha kwenye AC.?
 
umesema kuna kujaza gesi kwenye AC mie nalijua ukifunga umefunga.! kwani AC inakija ikiwa tupu ila ukitaka kufunga ndio unaijaza gesi.? na hiyo gesi inatumika kwa miezi mingapi itakuwa imeisha hivyo kuhitaji kujaza tena na pia ni mda gani upite ndio uifanyie service mashine na pia utajuaje kama gesi imeisha kwenye AC.?
Kujaza gas ni ac ambayo ilishatumika mda
mrefu na gas inapimwa na fundi
 
Ninayo Ac aina ya Samsung 24btu. toka nimenunua sijaitumia sana kutokana na ukubwa wake na mimi sebule yangu ni ndogo sana. Ningependa kubadilisha nipate angalau 12btu. Kama kuna mtu anahitaji A/c kubwa anaweza akanipatia hiyo ndogo tufanya kubadilishana. Nilinunua bila kupata elimu ya kutosha.
 
Back
Top Bottom