Gesi kwenye AC inapotea au tuseme kuisha au kupunguza kabisa Kwa sababu ya leakage yaani kuvuja. Hata AC mpya inaweza kuisha gesi. Gesi kwenye AC inaweza kuvuja kwenye zile pipe zake, kwenye condenser ya nje na overplater yaani condenser la ndani au kwenye zile joint zake pale unapotaka kufunga zile pipe inawezekana fundi akafunga upande na gesi ikavuja na kuisha hata kama AC ni mpya. Usikubali kuongezewa gesi Kila siku Kwa kuwa tu eti fundi amekuambia, ni lazima fundi aitafute leakage aizibe ndo ajaze gesi, gesi ni bei ghali pia. Mfano Kuna watu hawajui hivyo Kila siku au siku kadhaa hujaziwa gesi, huo ni utapeli tu imagine Gesi ya bei rahisi tu kilo ni karibu 16,000 hiyo ni R22 tu, ikiwa ni R32 au R410 gesi yake Iko juu sana.Kwanini AC inaisha gesi wakati kwenye mzunguko wake hakuna uvujaji,
ges inapotea wapi?
Nahitimisha kuwa gesi kwenye AC haiishi, ikiisha jua Kuna kuvuja. Mafundi wengi huangalia condenser ya nje tu akiona shwari basi anasema haivuji ngoja tujaze gesi tu, kumbe Kuna joint lazima ziangaliwe, overplater nalo lote liangalie Hadi pipe nazo ziangaliwe, changamoto ni wamiliki wa AC nadhani wakiambiwa watoe kiasi Fulani cha pesa wanaleta tabu ndio maana mafundi wanapiga na kusepa, AC moja tu kama inavuja sehemu ndogo unaweza chukua siku nzima kugundua leakage, hivyo wabongo wengi wanadharau kazi za watu ndo maana mafundi wanawadanganya.