Sisi tuliiga wapi kuwa na vyeo vyote viwili vya Waziri Mkuu na Makamu wa Rais?

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Kwenye nchi nyingi maarufu zenye mfumo wa Urais wenye nguvu ziko hivi
1. Marekani - Haina waziri mkuu, ina makamu wa Rais

2.Ufaransa - Haina makamu wa Rais, ina Waziri Mkuu

3. Africa Kusini - Haina waziri mkuu, ina makamu wa Rais

4.Kenya - Haina waziri mkuu, ina makamu wa Rais

5.Zambia - Haina waziri mkuu, ina makamu wa Rais

6.Ghana - Haina waziri mkuu, ina Makamu wa Rais.

7. Senegal - Haina makamu wa Rais, ina Waziri Mkuu

8.Botswana - Haina waziri mkuu, ina Makamu wa Rais

9. Brazil - Haina waziri mkuu, ina Makamu wa Rais

10. Korea Kusini - Haina makamu wa Rais, ina Waziri mkuu
 
Infact,
Mataifa mengi ulimwenguni yameiga mambo mengi mazuri ya uongozi kutoka Tanzania ,

na Tanzania haina haja kabisa, kuiga chochote kutoka popote duniani kwasababu inajitosheleza vyema katika uongozi wa kisiasa, kijamii, kiuchmi kitaifa na kimataifa 🐒
 
Kwa Tanzania waziri mkuu ni kama rais kivuli wa Tanganyika. Hii ni siri tunayoijua watu wachache wakiwemo wakina mafwele.
 
Tuliiga China...yenye Rais, Makamu wa Rais na Waziri mkuu.
 
Kwani hatuwezi kubuni na watu wakaja kuiga hapa kwetu?
 
Naona anapima na kuchagua pick and choose. Kwa nini ufikiri sisi ni WA kuoga tu, kwa nini tusiigwe? Uingereza hawana Rais. Afrika ya Kusini wana Wizara ya Kuchagua Ushoga ("Freedom to choose sexual orientation", imo kwenye Katiba). Ujerumani hawana Rais, na Dubai na Saudia. Utaiga wangapi? Naomba ututafutie ni Nchi ngapi wameiga Tanzania? Umetaja Kenya, umesahau Raila alitengenezewa cheo cha Prime Minister ili kubalsnce makabila, alipopewa Uvice Pres it dent na Mwai Kibali cheo kikafutwa. Usituambie ya kuigaiga.
 
Je, Una uhakika kwamba hauugui kichaa?
 
Sisi tupo na upekee ambao ni nadra sana kwa nchi nyingine

Mambo kama Mwenge wa Uhuru,

Marais wawili ndani ya nchi moja,

Halafu cha kushangaza Waziri Mkuu hatambuliki kikatiba huko Zenji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…