Spika zilikuwa siyo nzuri au more specifically Samia alipokwenda kwenye podium hawakutayarisha vizuri
Halafu nimefika pale nimeona watu wanazuiwa kupiga picha. Mtu mmoja amekamatwa na mtu kavaa kiraia,kaulizwa kwa nini unapiga picha? Akamshika ,anaanza kumkokota,aondoke naye.Akasema bado hajapiga picha. Jamaa kamnyang'anya simu akaikagua, halafu akaona kweli hajapiga picha. Akamrudishia simu yake.
Halafu walikuwa wanabishana pale. CCM wengine walikuwa wamefika mapema sana,kwa sababu zile shughuli zilianza saa moja asubuhi. Walifika mapema kwa hiyo walikuwa wanataka kuondoka. Lakini walikuwa wanazuiwa kuondoka.
Baada ya dakika kumi au kumi na tano za kumsikiliza Samia,nikaamua kuondoka,kuondoka mapema.
Nimetembea kidogo ghagla nikaona makundi makubwa ya watu wanatoka katika mkutano,wale watu waliokuwa wamezuiwa baadaye waliruhusiwa.
Nikataka kuuliza kwani Samia kamaliza kuongea? Nikaamua, probably ameamua kumaliza mapema,kwa sababu watu waliokuwa wanatoka walikuwa wengi.
Hawa watu walikuwa red hot with anger.
"Haturudi tena. Tunaenda kujiunga na Chadema" "Ujinga namna Ile halafu wanategemea mtu atampigia kura yule?"
Baadaye nimekwenda nimefika mbali kidogo nikasikia kama tangazo la kumsalza mkutano..
Nikamuuliza kijana mmoja wa Kijani, Mkutano umekwisha au vipi?
Akasema Samia yupo kule mpaka sasa ,ila sasa ndiyo anajitayarisha kuondoka."
Nikamuuliza yule kijana,huyu kijana labda ni teenager,labda ni UVCCM.,"Kwa hiyo watu wameondoka,wamemdharau Samia.?"
Akasema,"Well,er..,I wouldn't put it that way." Halafu akaenda kupanda basi la Chama.
Lakini jambo hilo tu moja nilitaka kusema. Warekebishe mic vizuri,waweke spika nzuri.
Samia ameongea,ameanza kwa kujisifu jinsi Serikali ilipoanza kazi ilikuta vyombo vingi vya habari vimefungiwa,ikavirudisha kazini vyote.