GE2025 Sisi tulikuwa pale tulishindwa kumsikia Samia akiongea

GE2025 Sisi tulikuwa pale tulishindwa kumsikia Samia akiongea

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Je ulikumbuka kumnusa kinywa chake kama alikuwa bwax au lah?
 
Hukumsikia alicho sema Polepole?

Huhitajiki kwenda na kiwliwili chako kupiga kura kwenye kituo. Kura yako ishapigwa kupitia NIDA.

Ningekuelewa kama unge ahidi kushiriki kuhakikisha kuwa hutumiwi kizembe kuhalalisha uchafuzi unaofanywa na hawa mashetani. Kuna njia nyingi za kukataa kuhalalisha ujambazi.
Kwa bahati sijui mbaya au nzuri mim Sina namba ya nida.....
 
Kwa hizo sera zake nilizosikia anazinadi,nimejiuliza huyu mtu amekaa ikulu miaka kibao hajui hata changamoto halisi zinazowakabili watanzania?
Machawa wanasema hana deni katika nchi kama Tanzania. Kampeni yake ingetakiwa kuwa opposite, kusema ana deni kubwa, kazi kubwa kwa dhamana aliyopewa kuwa Rais wa Tanzania.

Deni la kupigania na kulinda maslahi ya Tanzania, deni la kupigania haki kwa Watanzania wote na deni la kuleta maendeleo kama, elimu, maji, umeme, hospitali, miundombinu.

Hakuna kiongozi wa umma alipewa dhamana asiyekuwa na deni. Dhamana maana yake ni kama unadaiwa, una deni unawajibika kutimiza malengo kadhaa yaliyofanya upate dhamana.
 
Kwa bahati sijui mbaya au nzuri mim Sina namba ya nida.....
Lakini bado matokeo ya uchafuzi yatakuandama; kwa hiyo huna njia ya kuepuka; ushiriki au usishiriki, matokeo yake yanakuhusu.

Ninakubaliana na wewe, kwenda kupanga mstari ni upumbavu; na pengine tusipokubaliana ni kuwa; kubaki tu nyumbani siku hiyo bila ya kuchangia hata kiduchu kwa njia yoyote unayoona inafaa kuzuia uhalifu huo; hata kama siyo upumbavu, lakini ni wazi huo ni ujinga.

Ni hivi: hakuna binaadam yeyote asiyeogopa kudhurika. Sasa jambazi mwenye silaha akija mtaani kwenu, wewe na baadhi ya majirani mkaamua kujifungia tu ndani na kuwaachia wanaojitoa mhanga kukabiliana na jambazi; mkashindwa hata kutoboa tu gurudumu la gari la jambazi kusaidia lisiepuke kudhibitiwa na hao majirani waliojitoa mhanga; hapo inakuwa kama mpo kwenye upande wa huyo jambazi.

Tafakari sana mTanzania mwenzangu. Tupo kwenye hali isiyokuwa ya kawaida kabisa.
 
Back
Top Bottom