Sisi tuliozaliwa familia zenye imani mchanganyiko. Hatuonagi shida hata serikali nzima iongozwe na Dini moja

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
40,153
Reaction score
93,069
Hamjambo!

Moja ya faida ya kutokea familia zenye Imani mchanganyiko. Yaani ukoo wa Baba dini hii, ukoo wa Mama dini nyingine. Au imani mchanganyiko, tamaduni mchanganyiko ni pamoja na kutokuwa mtu wa imani kali au udini.

Sisi wengine Msikitini tunaingia. Kanisani tunaingia. Usabatoni tunaingia. Ukatolikini au ulutheri tunaingia.

Hiyo sio rahisi kwa mtu aliyetokea familia yenye kabila moja pekee au dini moja pekee. Hawa hupata changamoto sana kimtazamo na kuchangamana.

Serikali yote hata iwe Waislam watupu. Kwa sisi Watibeli hatuna tatizo na hilo. Ilimradi nchi haiongozwi Kiislamu. Kuna katiba na sheria.

Suala la Dini au imani ni suala binafsi. Ni kama ushabiki wa Simba na Yanga, au Manchester na Liverpool.

Uadilifu hautokani na dini au dhehebu fulani. Kila dhehebu lina watu waadilifu na wasio waadilifu.

Sisi Watibeli hatutazami watu kwa Dini au imani zao.

Ndio maana tunauwezo wa kukosoa yoyote bila kujali dini au imani yake.
Tunauwezo wa kuikosoa dini au imani yoyote ile. Namaanisha yoyote ile.

Mimi ninasali Sabato. Mtu nikimsikia akikosoa usabato nitakachoangalia hoja zake zina mashiko kiwango gani. Sio kwamba nione ninashambuliwa.

Ndio maana kuna wakati fulani niliwahi kukosoa Kanisa la Wasabato Vikali kwa kukaa kimya kutokemea vitendo viovu vinavyohusishwa na serikali. Wao kazi kukemea wala nguruwe, wavunja Sabato, lakini huwezi sikia wakikosoa utekaji na baadhi ya matendo mabaya ya serikali. Zaidi sana utawasikia wakisifia na kuombea tuu viongozi. Hili nilishasemaga. Huo ni unafiki.

Nchi hata iongozwe na viongozi wote wawe Katoliki au Lutheran au wapagani sisi Watibeli hatuna tatizo na huwezi sikia tukilalamikia jambo hilo.

Ilimradi taratibu zifuatwe.

Haki zitendeke. Nchi isiongozwe kwa misingi ya imani fulani.
Usijeleta usabato wako kwenye mambo ya serikali hapa. Kama huli Nguruwe ni wewe na dini yako. Wengine wanakula.

Kama unafunga ramadhani ni wewe na uislam wako. Wengine siku ya ramadhani ni siku kama siku zingine. Uislam wako ubaki nyumbani kwako na mkeo huko.

Kuna ile Kasumba mbaya kwamba sijui nchi hii akitoka Rais Muislam anayefuata sijui awe mkatoliki, mara sijui Rais akiwa muislam makamu wake awe Mkatoliki na kinyume chake ni kweli. Huo utaratibu ni upuuzi. Ni dhana potofu.

Ni ukatili na dhulma.
Nchi hii sio lazima mtu awe Dini fulani ndio aiongoze. Mtu wa dini yoyote au asiye na Dini anatakiwa kuwa na Haki ya kuongoza. Ilimradi Katiba ya nchi ifuatwe.

Sisi Watibeli, Dini ni kama Club za mipira au za michezo hivi.

Dhana za kusema viongozi wa serikali kuhusishwa na udini ni potofu sana.
Kwanza hata hayo ya kuapa na Biblia sijui Quran ni mfumo wa kizamani. Haina maana yoyote ile.

Mtu aape kwa Katiba. Ashike Katiba aape nayo.
Niliwahi kuandika na nitarudia hii mada kuandika tena. Kuapa kwa kutumia Biblia au Quran ni ukoloni mamboleo.

Hivyo vitabu sio vya kwetu. Ni katiba za zamani za mataifa ya wayahudi na waarabu wa kale.

Unaposoma Biblia au Quran, hizo ni Katiba za mataifa ya kale ya mashariki ya kati. Hayana uhusiano wowote na Tanzania.

Vitabu hivyo vitumike tuu kwa hiyari ya watu binafsi kama sehemu kujifunzia lakini having ulazima wa kutumika kwenye mambo makubwa ya kimaamuzi katika nchi.
Mara bungeni, mara mahakamani, mara serikalini. Hapana!

Katiba ya nchi ndio Kitabu kitakatifu katika nchi husika. Kinatuhusu sisi wenyewe. Kinataja watu wetu wenyewe. Kinataja mipaka yetu wenyewe. Kinahusu wakati wetu sisi wenyewe. Tumekitengeneza sisi wenyewe.

Wewe uwe muislam, sijui Mkristo, sijui mbudha na mpagani. Katiba ya nchi ndio ifuatwe.

Nchi haiongozwi kwa Imani.
Viongozi wake hawatachaguliwa kwa imani zao. Katiba na sheria za nchi yetu ndio msingi.

Ndio maana yakija mambo serious hapa, unashangaa hili moja linatoka kama liislam linasema hivi. Jingine linasema hivi kama likristo.
Hawazingatii maslahi ya nchi.
Kama wangesimama kwa kufuata kitabu cha Katiba kama reference utofauti mkubwa ungepungua.

Mimi nimemaliza.

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
 
Ni kweli Tuliotoka familia zenye imani mchanganyiko hatuna shida na dini ya mtu katika nafasi yoyote.Wala hatuoni shida kuchangamana na watu wa Imani tofauti.Wengi wanaoanzisha mijadala ya udini wamelelewa familia zisizo na mchanganyiko wa Imani.
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Hata sisi wenye imani za kimila. Kama sisi wamasai huwa hatuna shida
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Ukiona milio inakuwa mingi kwenye hilo ,kinachopigiwa kelele ni maslahi ya kifedha.
Sio kwamba watu wanazipenda sana dini zao
Ila kuna ujinga kwamba viongozi wengi wakiwa wakristu au muslims basi hela nyingi na fursa nyingi zitaenda kwao.
 
Hamjambo!

Moja ya faida ya kutokea familia zenye Imani mchanganyiko. Yaani ukoo wa Baba dini hii, ukoo wa Mama dini nyingine. Au imani mchanganyiko, tamaduni mchanganyiko ni pamoja na kutokuwa mtu wa imani kali au udini.

Sisi wengine Msikitini tunaingia. Kanisani tunaingia. Usabatoni tunaingia. Ukatolikini au ulutheri tunaingia.

Hiyo sio rahisi kwa mtu aliyetokea familia yenye kabila moja pekee au dini moja pekee. Hawa hupata changamoto sana kimtazamo na kuchangamana.

Serikali yote hata iwe Waislam watupu. Kwa sisi Watibeli hatuna tatizo na hilo. Ilimradi nchi haiongozwi Kiislamu. Kuna katiba na sheria.

Suala la Dini au imani ni suala binafsi. Ni kama ushabiki wa Simba na Yanga, au Manchester na Liverpool.

Uadilifu hautokani na dini au dhehebu fulani. Kila dhehebu lina watu waadilifu na wasio waadilifu.

Sisi Watibeli hatutazami watu kwa Dini au imani zao.

Ndio maana tunauwezo wa kukosoa yoyote bila kujali dini au imani yake.
Tunauwezo wa kuikosoa dini au imani yoyote ile. Namaanisha yoyote ile.

Mimi ninasali Sabato. Mtu nikimsikia akikosoa usabato nitakachoangalia hoja zake zina mashiko kiwango gani. Sio kwamba nione ninashambuliwa.

Ndio maana kuna wakati fulani niliwahi kukosoa Kanisa la Wasabato Vikali kwa kukaa kimya kutokemea vitendo viovu vinavyohusishwa na serikali. Wao kazi kukemea wala nguruwe, wavunja Sabato, lakini huwezi sikia wakikosoa utekaji na baadhi ya matendo mabaya ya serikali. Zaidi sana utawasikia wakisifia na kuombea tuu viongozi. Hili nilishasemaga. Huo ni unafiki.

Nchi hata iongozwe na viongozi wote wawe Katoliki au Lutheran au wapagani sisi Watibeli hatuna tatizo na huwezi sikia tukilalamikia jambo hilo.

Ilimradi taratibu zifuatwe.

Haki zitendeke. Nchi isiongozwe kwa misingi ya imani fulani.
Usijeleta usabato wako kwenye mambo ya serikali hapa. Kama huli Nguruwe ni wewe na dini yako. Wengine wanakula.

Kama unafunga ramadhani ni wewe na uislam wako. Wengine siku ya ramadhani ni siku kama siku zingine. Uislam wako ubaki nyumbani kwako na mkeo huko.

Kuna ile Kasumba mbaya kwamba sijui nchi hii akitoka Rais Muislam anayefuata sijui awe mkatoliki, mara sijui Rais akiwa muislam makamu wake awe Mkatoliki na kinyume chake ni kweli. Huo utaratibu ni upuuzi. Ni dhana potofu.

Ni ukatili na dhulma.
Nchi hii sio lazima mtu awe Dini fulani ndio aiongoze. Mtu wa dini yoyote au asiye na Dini anatakiwa kuwa na Haki ya kuongoza. Ilimradi Katiba ya nchi ifuatwe.

Sisi Watibeli, Dini ni kama Club za mipira au za michezo hivi.

Dhana za kusema viongozi wa serikali kuhusishwa na udini ni potofu sana.
Kwanza hata hayo ya kuapa na Biblia sijui Quran ni mfumo wa kizamani. Haina maana yoyote ile.

Mtu aape kwa Katiba. Ashike Katiba aape nayo.
Niliwahi kuandika na nitarudia hii mada kuandika tena. Kuapa kwa kutumia Biblia au Quran ni ukoloni mamboleo.

Hivyo vitabu sio vya kwetu. Ni katiba za zamani za mataifa ya wayahudi na waarabu wa kale.

Unaposoma Biblia au Quran, hizo ni Katiba za mataifa ya kale ya mashariki ya kati. Hayana uhusiano wowote na Tanzania.

Vitabu hivyo vitumike tuu kwa hiyari ya watu binafsi kama sehemu kujifunzia lakini having ulazima wa kutumika kwenye mambo makubwa ya kimaamuzi katika nchi.
Mara bungeni, mara mahakamani, mara serikalini. Hapana!

Katiba ya nchi ndio Kitabu kitakatifu katika nchi husika. Kinatuhusu sisi wenyewe. Kinataja watu wetu wenyewe. Kinataja mipaka yetu wenyewe. Kinahusu wakati wetu sisi wenyewe. Tumekitengeneza sisi wenyewe.

Wewe uwe muislam, sijui Mkristo, sijui mbudha na mpagani. Katiba ya nchi ndio ifuatwe.

Nchi haiongozwi kwa Imani.
Viongozi wake hawatachaguliwa kwa imani zao. Katiba na sheria za nchi yetu ndio msingi.

Ndio maana yakija mambo serious hapa, unashangaa hili moja linatoka kama liislam linasema hivi. Jingine linasema hivi kama likristo.
Hawazingatii maslahi ya nchi.
Kama wangesimama kwa kufuata kitabu cha Katiba kama reference utofauti mkubwa ungepungua.

Mimi nimemaliza.

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
Wenye akili nzuri hatuna shida na dini za wengine.
Hata wale waliotangulia wenye akili nzuri waliamua serikali isiwe na dini.
Ubaguzi na upendeleo wa kidini ni kwa wajinga wachache.
Hata hivyo, hali hiyo isipodhibitiwa yaweza kuwa na madhara makubwa kwa sababu wenye akili nzuri ni wachache Sana.
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Hata mimi sioni mantiki ya dini kwenye mambo ya kitaifa na kijamii
kwanza pisi za kigalatia tunabonda sana
 
Hamjambo!

Moja ya faida ya kutokea familia zenye Imani mchanganyiko. Yaani ukoo wa Baba dini hii, ukoo wa Mama dini nyingine. Au imani mchanganyiko, tamaduni mchanganyiko ni pamoja na kutokuwa mtu wa imani kali au udini.

Sisi wengine Msikitini tunaingia. Kanisani tunaingia. Usabatoni tunaingia. Ukatolikini au ulutheri tunaingia.

Hiyo sio rahisi kwa mtu aliyetokea familia yenye kabila moja pekee au dini moja pekee. Hawa hupata changamoto sana kimtazamo na kuchangamana.

Serikali yote hata iwe Waislam watupu. Kwa sisi Watibeli hatuna tatizo na hilo. Ilimradi nchi haiongozwi Kiislamu. Kuna katiba na sheria.

Suala la Dini au imani ni suala binafsi. Ni kama ushabiki wa Simba na Yanga, au Manchester na Liverpool.

Uadilifu hautokani na dini au dhehebu fulani. Kila dhehebu lina watu waadilifu na wasio waadilifu.

Sisi Watibeli hatutazami watu kwa Dini au imani zao.

Ndio maana tunauwezo wa kukosoa yoyote bila kujali dini au imani yake.
Tunauwezo wa kuikosoa dini au imani yoyote ile. Namaanisha yoyote ile.

Mimi ninasali Sabato. Mtu nikimsikia akikosoa usabato nitakachoangalia hoja zake zina mashiko kiwango gani. Sio kwamba nione ninashambuliwa.

Ndio maana kuna wakati fulani niliwahi kukosoa Kanisa la Wasabato Vikali kwa kukaa kimya kutokemea vitendo viovu vinavyohusishwa na serikali. Wao kazi kukemea wala nguruwe, wavunja Sabato, lakini huwezi sikia wakikosoa utekaji na baadhi ya matendo mabaya ya serikali. Zaidi sana utawasikia wakisifia na kuombea tuu viongozi. Hili nilishasemaga. Huo ni unafiki.

Nchi hata iongozwe na viongozi wote wawe Katoliki au Lutheran au wapagani sisi Watibeli hatuna tatizo na huwezi sikia tukilalamikia jambo hilo.

Ilimradi taratibu zifuatwe.

Haki zitendeke. Nchi isiongozwe kwa misingi ya imani fulani.
Usijeleta usabato wako kwenye mambo ya serikali hapa. Kama huli Nguruwe ni wewe na dini yako. Wengine wanakula.

Kama unafunga ramadhani ni wewe na uislam wako. Wengine siku ya ramadhani ni siku kama siku zingine. Uislam wako ubaki nyumbani kwako na mkeo huko.

Kuna ile Kasumba mbaya kwamba sijui nchi hii akitoka Rais Muislam anayefuata sijui awe mkatoliki, mara sijui Rais akiwa muislam makamu wake awe Mkatoliki na kinyume chake ni kweli. Huo utaratibu ni upuuzi. Ni dhana potofu.

Ni ukatili na dhulma.
Nchi hii sio lazima mtu awe Dini fulani ndio aiongoze. Mtu wa dini yoyote au asiye na Dini anatakiwa kuwa na Haki ya kuongoza. Ilimradi Katiba ya nchi ifuatwe.

Sisi Watibeli, Dini ni kama Club za mipira au za michezo hivi.

Dhana za kusema viongozi wa serikali kuhusishwa na udini ni potofu sana.
Kwanza hata hayo ya kuapa na Biblia sijui Quran ni mfumo wa kizamani. Haina maana yoyote ile.

Mtu aape kwa Katiba. Ashike Katiba aape nayo.
Niliwahi kuandika na nitarudia hii mada kuandika tena. Kuapa kwa kutumia Biblia au Quran ni ukoloni mamboleo.

Hivyo vitabu sio vya kwetu. Ni katiba za zamani za mataifa ya wayahudi na waarabu wa kale.

Unaposoma Biblia au Quran, hizo ni Katiba za mataifa ya kale ya mashariki ya kati. Hayana uhusiano wowote na Tanzania.

Vitabu hivyo vitumike tuu kwa hiyari ya watu binafsi kama sehemu kujifunzia lakini having ulazima wa kutumika kwenye mambo makubwa ya kimaamuzi katika nchi.
Mara bungeni, mara mahakamani, mara serikalini. Hapana!

Katiba ya nchi ndio Kitabu kitakatifu katika nchi husika. Kinatuhusu sisi wenyewe. Kinataja watu wetu wenyewe. Kinataja mipaka yetu wenyewe. Kinahusu wakati wetu sisi wenyewe. Tumekitengeneza sisi wenyewe.

Wewe uwe muislam, sijui Mkristo, sijui mbudha na mpagani. Katiba ya nchi ndio ifuatwe.

Nchi haiongozwi kwa Imani.
Viongozi wake hawatachaguliwa kwa imani zao. Katiba na sheria za nchi yetu ndio msingi.

Ndio maana yakija mambo serious hapa, unashangaa hili moja linatoka kama liislam linasema hivi. Jingine linasema hivi kama likristo.
Hawazingatii maslahi ya nchi.
Kama wangesimama kwa kufuata kitabu cha Katiba kama reference utofauti mkubwa ungepungua.

Mimi nimemaliza.

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
Waislam wakishika nchi uchumi unavurugika kabisa. Mwinyi aliharibu sana nchi. Akaja Kikwete akavurunda ile mbaya, sasa ni Samia, yeye na marafiki zake wanajimilikisha kila kitu.

Wakristo wakishika nchi, wao ni udikteta kwa kwenda mbele. Nyerere dikteta, Mmapa dikteta na Magufuli pia. Ila wanajitahidi sana kuifanya nchi iwe na maadili,na pia wanaimarisha uchumi.

Tuchague twende na nani?
 
Back
Top Bottom