Sisi wanawake bwana!

Sisi wanawake bwana!

mwanaume wa watu yupo njia pnda hajui amfate yupi amsikilize mama yake anayemtishia kama mimi sio mama yako ndoa iko pale pale au baba anayemwambia hakuna ndoa na mahari yetu waturudishie au amsamehe baby wake shetani wamwisho wa mwaka kampitia tu
Asimsikilize mtu.

Asepe apotee hewani na kwenye hayo mazingira kama mwezi hivi.

Wazee wa ushauri wakose wa kumpa ushauri.

Akija kurudi jambo litakua limeisha na atagundua kafanya maamuzi ya maana.
 
Tatizo huenda na huyo shemeji yake wameanza zamani na ile kufanya mazoea kwamba hakuna atakayejua, pengine na ile tufanye ya mwisho ya kuagana.. Na kwenye jambo la Mungu shetani anaweka makao hapohapo kupigia mstari ili ndoa isifanikiwe
Hilo halikua jambo la Mungu. Ni la shetani kabisa. Mungu kamsanua tu kijana wa watu kua hili ni bomu unalisuka
 
Mama mtu ni mchawi na mka mwana mtarajiwa ni mchawi wanataka wajenge kiringe vzr

Watamlefitisha
 
habari zishagaa hakuna mtu asiejua s unajua taarifa mbaya husambaa kwa haraka zaidi sasa kuna haja gani kufosi ndoa kwa scenerio kama hiyo? huku baba anataka warudishiwe mahari huku mama ansema haiwezekani ndoa ipo pale pale
Hii inamaanishi hilo ''janaume'' linalotaka kuoa linapangiwa mambo yake na wazazi!
 
Hatari sana. Hili lilimkuta jamaa yangu, alimfunia mkewe mtarajiwa siku 2 kabla ya ndoa na bado akamuoa. Hadi leo wapo wote mwaka kama wa nane
Kuna wanaume wasio na wivu. Hasa huko uswazi haya mambo ndiyo yametawala. Mpangaji wa chumba cha pili leo anafumaniwa na mke wa mpangaji wa chumba cha kwanza, unazuka ugomvi, keshokutwa unakuta uogomvi umeisha wanaongozana. Huyo jamaa yako ana moyo mgumu sana.
 
Kuna wanaume wasio na wivu. Hasa huko uswazi haya mambo ndiyo yametawala. Mpangaji wa chumba cha pili leo anafumaniwa na mke wa mpangaji wa chumba cha kwanza, unazuka ugomvi, keshokutwa unakuta uogomvi umeisha wanaongozana. Huyo jamaa yako ana moyo mgumu sana.
Huyo jamaa ni mtoto wa kishia kinoma. Kabla ya ndoa alikuwa akiishi na demu wake so dem alikuwa anaaga anaenda kwao kumbe anaenda kwa jamaa yake... Anakaa weekend
 
kunaye mtu mmoja alikua na mpenzi wake, mapenzi shatashata huku bibie akikataa wanaume waliokua wanakimbizana kuleta posa kwao kwa kisingizio ana mtu wake, kama uzuri amejaaliwa binti huyu, ni mzuri mashallah

Kaka wa watu kajitafuta kajipata, kajitutumua kwenda ukweni akapangiwa mahari tena ya bei na vitu ghali akatimiza yote mpaka tarehe ya ndoa ikapangwa, kisanga kikaja bibie kafumaniwa na mume wa nduguye tena kakiri si mara moja wala mbili shemeji anatelezesha utamu kwake.

Ujinga unaokuja ni mama wa mwanaume kushinikiza mwanae aoe hivyohivyo kisa watu wameshatoa michango na sare vitambaa wamekata hivi mama kweli unaweza kumshauri mwanao huu wazimu?
Huyo mama mwenyewe atakuwa ni mkware.
 
shida inakuja jamaa huyo ndio alikua mwanamke wake aliewekeza hisia zake kwake ni huyo huyo tangu watu tunahisi hisi mpaka ikawa dhahiri
Hili huwa linatokea. Kuna mtu wa ukoo wetu naye ilimtokea lakini yeye ilikuwa ni kwenye haya makanisa ya walokole. Jamaa alikuwa na binti hapo hapo kanisani na kanisa zima lilikuwa linajua ni wachumba wanaokaribia kufunga ndoa. Msichana akaja kufumaniwa na kiongozi wa kanisa. Mchungaji mwenye kanisa akawa anamshinikiza jamaa amuoe. Wakaweka kikao cha wazee wa kanisa wakamlisha jamaa mahubiri na umuhimu wa kusamahe, jamaa akakataa katakata na akawatukana matusi mazito. Akafikia hatua ya kusema ulokole ni upotofu na akakata mguu kanisani kabisa. Baada kabisa akaja kubadilisha mawazo na kuanza kuhudhuria tena kanisani ila mpaka sasa hajaoa na imepita miaka kama nane tangu kisa kitokee.
 
Back
Top Bottom