Sisi wote wageni hapa duniani, imekuaje unajiita "Life Coach"?

Sisi wote wageni hapa duniani, imekuaje unajiita "Life Coach"?

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2012
Posts
14,588
Reaction score
32,361
Wakuu kuna kitu kimekuwa kikinikera mno na kunishangaza, naona leo nikiweke hadharani. Kuna hawa viumbe wanaojiita Life Coach wamezidi kuongezeka sana town. Kimsingi ni Motivational Speakers ambao kwa sababu wanazozijua wao wameamua kujipa vyeo kwamba ni makocha wa maisha.

Najiuliza maswali mengi sana; kama sisi wote tumezaliwa na hapa duniani na kuanza kuishi tukijifunza kila siku kuhusu dunia, sasa hawa wenzetu walienda chuo gani kujifunza zaidi na kuwa mbele yetu kiasi cha kujikuta wamekuwa Life coaches?

Cha kushangaza hawa watu wamekuwa mstari wa mbele kujifanya kujua kila fani na kutoa ushauri huku wao binafsi wakiishi maisha ya kawaida na kuendelea tu kupigika kama sisi sote.

Mimi ninashauri hawa Motivational Speakers wasijiite Life Coach maana inatia hasira sana.
 
Nafikiri hao wapo kwa walio kata tamaa mkuu, kikawaida ukiwa mzima wa afya utaona mgonjwa anadeka.
 
Kama kuna need / gap basi hao ndio wanai-fill; To each their own...

Ni kama tu wewe unapoenda kwenye Imani zako mchungaji n.k. (na unapata kitu unachohitaji huko) mwisho wa siku kama it makes you sleep better at night who are we to say otherwise ?!!

Nadhani mwenye tatizo ni wewe kuingilia maisha ya watu na kupata kero kama vile umeambiwa na wewe uende cha kufanya hayo masomo wanayotoa labda uyachallenge na utayachallenge vipi wakati maisha hayana SI Unit kibaya kwako kwa mwingine ni kizuri (What is good for the goose is not necessarily good for the gander)

By the way maisha ni nini ?
 
Kwani mwamposa sio life coach lakini yeye kajiita mtume….yaani kavaa vazi la kondoo kutapeli watu hilo vp mkuu halikuumi…!!?
 
Back
Top Bottom